Error Error(s) before html tag encountered

 

Karibuni Ujumbe, 25 Juni 2024

Wanangu wapendwa! Nafurahi pamoja nanyi na namshukuru Mungu kwa kunijalia kuwa nanyi ili kuwaongoza na kuwapenda. Wanangu, amani iko hatarini na familia inashambuliwa. Ninawaalika, wanangu, rudi kwenye sala ya familia. Wekeni Maandiko Matakatifu mahali panapoonekana na msome kila siku. Mpendeni Mungu kuliko vitu vyote ili muwe salama duniani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu”.