“Wanangu wapendwa! Kwa furaha moyoni nawaalika wote kuishi imani yenu na kuishuhudia kwa moyo na mfano kwa kila namna. Ee wanangu, kateni shauri kuacha kabisa dhambi na vishawishi vyake; mioyo yenu ijae furaha na upendo kwa utakatifu. Mimi, wanangu, nawapenda na ninaambatana nanyi. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu. ”