Our Lady of Medjugorje Messages containing 'hamjui'
Total found:
3
Ujumbe, 25 Julai 2014
“
W
anangu wapendwa! Ninyi
hamjui
neema ya namna gani mnayoishi katika wakati huu ambapo Yeye Aliye Juu awapeni ishara ili mjifungue na kutubu. Mwelekeeni Mungu na kusali; sala itawale katika mioyo yenu, familia na jamaa zenu ili Roho Mtakatifu awaongoze na kuhimiza kila siku mjifungue kufanya mapenzi ya Mungu na mpango wake kwa kila mmoja wenu. Mimi nipo pamoja nanyi, na nawaombeeni pamoja na malaika na watakatifu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, mimi, Mama yenu, naja tena katikati yenu kwa upendo usio na mwisho, kutoka upendo usio na kipimo wa Baba wa Mbinguni asiye na mwisho. Na, nikitazama mioyoni mwenu, naona ya kuwa wengi wenu wanipokea kama Mama na, kwa moyo thabiti na safi, wataka kuwa mitume wangu. Lakini Mimi ni Mama pia wa ninyi ambao hamnipokei na, katika ugumu wa moyo wenu, hamtaki kujua upendo wa Mwanangu.
Hamjui
jinsi moyo wangu ulivyoteseka na jinsi nilivyowaombeeni Mwanangu. Namwomba aponye roho yenu, kwa maana najua Yeye ana uwezo wa kuwaponya. Namwomba awaangaze kwa mwujiza wa mwanga wa Roho Mtakatifu, ili mwache kumsaliti, kumtukana na kumwumiza siku zote kwa kuendelea. Nasali kwa Moyo wote ili muweze kuelewa ya kuwa Mwanangu tu ni wokovu na mwanga wa ulimwengu. Nanyi, wanangu, mitume wangu wapenzi, mbebeni daima Mwanangu katika moyo na fikira zenu. Hivyo ninyi mtakuwa mnabeba Upendo. Wale wote wasiomjua watamtambua katika upendo wenu. Mimi nipo sikuzote karibu yenu. Nipo hasa karibu na wachungaji wenu, kwa sababu Mwanangu aliwaita kuwaongozeni katika njia kuelekea milele. Nawashukuru, mitume wangu, kwa sadaka na upendo wenu!
”
Ujumbe, 25 Februari 2016
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema nawaalikeni nyote kuongoka. Wanangu, mnapenda kidogo, na bado mnasali kidogo. Mmepotea wala
hamjui
lengo lenu ni nini. Chukueni msalaba wenu, mwangalieni Yesu mumfuate. Yeye anajitoa kwenu hata kufa msalabani maana anawapenda. Wanangu, nawaalikeni kurudia kusali kwa moyo kwa maana katika sala mnaweza kupata matumaini na maana ya uwepo wenu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombea. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose