Our Lady of Medjugorje Messages containing 'huu'
Total found:
55
Ujumbe, 25 Januari 2021
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huo ninawaalika kusali, kufunga na kujikana ili muweze kuwa wenye nguvu zaidi katika imani.
Huu
ni wakati wa mwamko na wa kuzaliwa upya. Kama vitu vya asili vinavyojitoa nanyi wanangu, fikirini juu ya mambo mliyopokea. Muwe waletaji wa amani na wa upendo wenye furaha ili kuishi vizuri duniani. Tamanini Mbingu kwa sababu Mbinguni hakuna wala huzuni wala machukio. Kwa hiyo, wanangu, amueni tena kuongoka, na utakatifu utawale katika maisha yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2021
“
W
anangu wapendwa! Mungu ameniruhusu kuwa pamoja nanyi leo pia kwa kuwaalika kusali na kufunga. Ishini wakati
huu
wa neema na muwe mashahidi wa tumaini maana, ninawaambia tena wanangu, kwa kusali na kufunga hata vita vinaweza kuisha. Wanangu, aminini na kuishi katika imani na kwa imani wakati
huu
wa neema na Moyo wangu usio na dhambi ya asili haumwachi yeyote kati yenu katika wasiwasi ikiwa ananikimbilia. Ninawaombea mbele ya Yeye aliye juu na ninasali ili amani iwepo katika mioyo yenu na kwa ajili ya tumaini katika wakati ujao. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2021
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaalika kushuhudia imani yenu katika rangi za majira ya kuchipua, na iwe imani ya matumaini na ya ujasiri. Wanangu, imani yenu isitindike katika hali yoyote na hata katika wakati
huu
wa majaribio. Tembeeni kwa ujasiri pamoja na Kristo Mfufuka kuelekea Mbingu iliyo lengo lenu. Mimi ninaandamana nanyi katika mwendo
huu
wa utakatifu na kuweka ninyi nyote katika Moyo wangu Usio na dhambi ya asili. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2021
“
W
anangu wapendwa! Ninawatazama na kuwaalika: mrudieni Mungu maana Yeye ndiye upendo na kwa ajili ya upendo alinituma kwenu ili niwaongoze kwenye njia ya wongofu. Acheni dhambi na maovu, amueni kuwa watakatifu na furaha itatawala; nanyi mtakuwa mikono yangu iliyopanuliwa katika ulimwengu
huu
uliopotea. Ninatamani ya kuwa muwe sala na matumaini kwa wale ambao hawajamjua Mungu wa upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2021
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika kuwa sala kwa wale wote wasiosali. Shuhudieni, wanangu, kwa njia ya maisha yenu furaha ya kuwa wangu na Mungu atajibu sala zenu na kuwapa amani katika ulimwengu
huu
wa wasiwasi ambamo kiburi na ubinafsi hutawala. Wanangu, ninyi muwe wakarimu na upendo wa upendo wangu ili wapagani wahisi ya kuwa ninyi ni wangu na waweze kuugeukia Moyo wangu Usio na dhambi ya asili. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2021
“
W
anangu wapendwa! Niko pamoja nanyi katika wakati
huu
wa rehema na ninawaalika nyote kuwa waleta amani na upendo katika ulimwengu
huu
, ambapo, wanangu, Mungu anawaalika kupitia Kwangu kuwa sala, upendo na kielelezo cha Paradiso, hapa duniani. Mioyo yenu na ijazwe na furaha na imani katika Mungu ili, wanangu, muwe na imani kamili katika mapenzi yake matakatifu. Hii ndiyo sababu mimi niko pamoja nanyi kwa sababu Yeye, Aliye Juu, ananituma kati yenu ili kuwahimiza ninyi kuwa na matumaini na mtakuwa waleta amani katika ulimwengu
huu
wenye wasiwasi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2023
“
W
anangu wapendwa! Ongokeni na mvae mavazi ya toba na maombi ya kina ya kibinafsi na kwa unyenyekevu mwombe Aliye Juu amani. Katika wakati
huu
wa neema Shetani anataka kuwapotosha ninyi, nanyi wanangu, mwangalieni Mwanangu na kumfuata kuelekea Kalvari, kwa kujikana na kufunga. Niko pamoja nanyi kwa sababu Aliye Juu ameniruhusu niwapende ninyi na kuwaongoza kuelekea furaha ya moyo, katika imani inayokua ndani ya wale wote wanaompenda Mungu zaidi ya vitu vyote. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Machi 2023
“
W
anangu wapendwa! Wakati
huu
uwe wakati wa sala kwa ajili yenu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati
huu
wa neema, ambao Aliye Juu amenituma niwapende ninyi na kuwaongoza katika njia ya uongofu, toeni sala zenu na sadaka zenu kwa ajili ya wale wote walio mbali na wasiojua upendo wa Mungu. Ninyi, wanangu, muwe mashahidi wa upendo na amani kwa mioyo yote isiyotulia. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati
huu
wa neema ninawaalika ninyi kwenye maombi kwa moyo. Mioyo yenu, wanangu, igeuzwe kuelekea mbinguni kwa maombi, ili mioyo yenu ipate kuhisi Mungu wa upendo anayewaponya na kuwapenda kwa upendo mkuu. Mimi niko pamoja nanyi kuwaongoza kwenye njia ya uongofu wa moyo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Wakati
huu
na uunganishwe na sala kwa ajili ya amani na kwa matendo mema ili kusudi ionekane furaha ya kumngoja Mfalme wa amani mioyoni mwenu, ndani ya familia zenu na katika ulimwengu ambao hauna matumaini. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2024
“
W
anangu wapendwa! Wakati
huu
uwe wakati wa maombi.
”
Ujumbe, 25 Februari 2024
“
W
anangu wapendwa! Salini na mfanye upya moyo wenu ili lile jema mlilopanda lizae matunda ya furaha na ushirika na Mungu. Magugu yamechukua mioyo mingi na imekuwa tasa. Kwa hiyo ninyi, wanangu, muwe mwanga, upendo na mikono yangu iliyonyoshwa katika ulimwengu
huu
unaomtamani Mungu ambaye ni upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Machi 2024
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati
huu
wa neema, ombeni pamoja nami ili mema yapate kushinda ndani yenu na karibu nanyi. Hasa, wanangu, ombeni kwa umoja na Yesu katika njia yake ya msalaba. Wekeni katika maombi yenu ubinadamu
huu
unaotangatanga bila Mungu na bila upendo wake. Muwe maombi, muwe mwanga na mashahidi kwa wale wote mnaokutana nao, enyi wanangu, ili Mungu wa rehema awarehemu.. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2024
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati
huu
wa neema ninawaalika ninyi kuomba kwa moyo wenu. Wanangu, tengenezeni vikundi vya maombi ambavyo ndani yake mtahimizana kutenda mema na kukua katika furaha. Wanangu, bado mko mbali. Kwa hiyo, daima ongokeni upya na mchague njia ya utakatifu na matumaini ili Mungu awape amani kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3