Our Lady of Medjugorje Messages containing 'ili'
Total found:
169
Ujumbe, 25 Septemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika kwenye maombi ya nguvu. Umamboleo unataka kuingia katika mawazo yenu na kuwaibia furaha ya maombi na kukutana na Yesu. Kwa hiyo, wanangu wapendwa, fanyeni upya sala katika familia zenu
ili
moyo wangu wa kimama ufurahi kama siku za kwanza nilipowachagua ninyi na jibu lilikuwa ni maombi mchana na usiku na mbingu haikunyamaza bali ilitolea kwa mahali hapa neema, amani na baraka kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2023
“
W
anangu wapendwa! Pepo za uovu, chuki na wasiwasi huvuma duniani kote kuharibu maisha yote. Kwa hiyo Aliye Juu amenituma kwenu
ili
niwaongoze kwenye njia ya amani na ushirika na Mungu na wanadamu. Ninyi, wanangu, ni mikono yangu iliyopanuliwa: ombeni, mfunge na toeni sadaka kwa ajili ya amani, hazina ambayo kila moyo unatamani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu na uunganishwe na sala kwa ajili ya amani na kwa matendo mema
ili
kusudi ionekane furaha ya kumngoja Mfalme wa amani mioyoni mwenu, ndani ya familia zenu na katika ulimwengu ambao hauna matumaini. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu
ili
aijaze mioyo yenu amani kwa sababu Yeye ni amani. Wanangu, mtafuteni Yesu katika ukimya wa mioyo yenu
ili
azaliwe upya. Ulimwengu unamhitaji Yesu, hivyo wanangu, mtafuteni kwa maombi maana anajitoa kila siku kwa kila mmoja wenu.
”
Mama yetu alikuja leo akiwa amevalia mavazi ya heshima akiwa na mtoto Yesu mikononi mwake. Yesu alinyoosha mkono wake kama ishara ya baraka na Mama yetu alituombea kwa lugha ya aramaika.
Ujumbe, 25 Februari 2024
“
W
anangu wapendwa! Salini na mfanye upya moyo wenu
ili
lile jema mlilopanda lizae matunda ya furaha na ushirika na Mungu. Magugu yamechukua mioyo mingi na imekuwa tasa. Kwa hiyo ninyi, wanangu, muwe mwanga, upendo na mikono yangu iliyonyoshwa katika ulimwengu huu unaomtamani Mungu ambaye ni upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Karibuni Ujumbe, 18 Machi 2024 - Tokeo la kila mwaka kwa Miriana Dragićević-Soldo
Mwotaji Mirjana Dragićević-Soldo alikuwa na matukio ya kila siku kutoka Juni 24, 1981 hadi Desemba 25, 1982. Katika hafla ya kutokezwa kwake kwa kila siku, akimfunulia siri ya kumi, Bikira alimfunulia kwamba atakuwa na tukio la kila mwaka mnamo Machi 18 na ndivyo ilivyokuwa katika miaka hii yote. Tukio hilo lilianza saa 1.33 jioni na kudumu hadi saa 1.39.
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika mpate kumjua Mwanangu vizuri iwezekanavyo kwa sala na rehema.
Ili
kwa mioyo safi na iliyo wazi mjifunze kusikiliza. Sikilizeni Mwanangu anachowaambieni
ili
mpate kuona tena kiroho. Kama watu wamoja wa Mungu, kwa ushirika na Mwanangu, ishuhudieni kweli kwa maisha yenu. Ombeni, wanangu,
ili
kwamba pamoja na Mwanangu muweze kuleta amani, furaha na upendo kwa ndugu zenu wote. Mimi ni pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka zangu za kimama.
”
Ujumbe, 25 Machi 2024
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema, ombeni pamoja nami
ili
mema yapate kushinda ndani yenu na karibu nanyi. Hasa, wanangu, ombeni kwa umoja na Yesu katika njia yake ya msalaba. Wekeni katika maombi yenu ubinadamu huu unaotangatanga bila Mungu na bila upendo wake. Muwe maombi, muwe mwanga na mashahidi kwa wale wote mnaokutana nao, enyi wanangu,
ili
Mungu wa rehema awarehemu.. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2024
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika ninyi kuomba kwa moyo wenu. Wanangu, tengenezeni vikundi vya maombi ambavyo ndani yake mtahimizana kutenda mema na kukua katika furaha. Wanangu, bado mko mbali. Kwa hiyo, daima ongokeni upya na mchague njia ya utakatifu na matumaini
ili
Mungu awape amani kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Karibuni Ujumbe, 25 Juni 2024
“
W
anangu wapendwa! Nafurahi pamoja nanyi na namshukuru Mungu kwa kunijalia kuwa nanyi
ili
kuwaongoza na kuwapenda. Wanangu, amani iko hatarini na familia inashambuliwa. Ninawaalika, wanangu, rudi kwenye sala ya familia. Wekeni Maandiko Matakatifu mahali panapoonekana na msome kila siku. Mpendeni Mungu kuliko vitu vyote
ili
muwe salama duniani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu”.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9