Our Lady of Medjugorje Messages containing 'ipo'
Total found:
2
Ujumbe, 25 Novemba 2015
“
W
anangu wapendwa, leo ninawaalika nyote: salini kwa ajili ya nia zangu. Amani
ipo
hatarini kwa hiyo wanangu, salini na muwe waletaji wa amani na matumani katika ulimwengu huu wa wasiwasi ambamo shetani anashambulia na kuleta majaribu ya kila aina. Wanangu muwe thabiti katika sala na imara katika imani. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombea ninyi nyote mbele ya Mwanangu, Yesu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2017
“
W
anangu wapendwa! leo ninawaalika kuwa makarimu katika kujinyima, katika kufunga na katika sala kwa ajili ya wale wote wanaojaribiwa, nao ni ndugu zenu kina kaka na kina dada. Na hasa ninawaomba kusali kwa ajili ya makuhani na kwa wote waliojiweka wakfu ili kwa ari zaidi wampende Yesu, ili Roho Mtakatifu aijaze mioyo yao kwa furaha, ili watoe ushuhuda wa Mbingu na mafumbo ya kimbingu. Roho nyingi
ipo
katika dhambi kwa sababu hakuna wale wanaojitoa sadaka na kusali kwa wongofu wao. Mimi nipo pamoja nanyi nikiwaombeeni ili mioyo yenu ijazwe furaha. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose