Our Lady of Medjugorje Messages containing 'kichocheo'
Total found:
3
Ujumbe, 25 Aprili 2013
“
W
anangu wapendwa! Salini, salini, mwendelee kusali ili mioyo yenu ifungukie kupokea imani jinsi ua linavyofunguka kuelekea mianga ya joto la jua. Huo ni wakati wa neema ambao Mungu anawajalia kwa njia ya uwepo wangu, lakini ninyi mpo mbali na moyo wangu. Kwa hiyo nawaalikeni kwa uongofu binafsi na kwenye sala katika familia zenu. Maandiko matakatifu yawe daima
kichocheo
chenu. Nawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2014
“
W
anangu wapendwa! Salini katika kipindi hiki cha neema na ombeni maombezi ya Watakatifu wote ambao wapo tayari katika mwanga. Wao wawe mfano na
kichocheo
kwenu siku hata siku, katika njia ya uwongofu wenu. Wanangu, mfahamu ya kuwa maisha yenu ni mafupi na ya kupita upesi. Kwa hiyo tamanini uzima wa milele na mtayarishe mioyo yenu katika sala. Mimi nipo pamoja nanyi na ninamwomba Mwanangu kwa ajili ya kila mmoja wenu, hasa kwa wale waliojiweka wakfu kwangu na kwa Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2016
“
W
anangu wapendwa! Uwepo wangu ni zawadi ya Mungu na
kichocheo
cha uwongofu wenu. Shetani ana nguvu na anataka kutia moyoni na fikirani mwenu fujo na wasiwasi. Kwa hiyo, ninyi wanangu salini ili Roho Mtakatifu awaongoze katika njia iliyonyoka ya furaha na amani. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombea ninyi mbele ya Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose