Our Lady of Medjugorje Messages containing 'kimbilio'
Total found:
3
Ujumbe, 25 Julai 2019
“
W
anangu wapendwa, mwaliko wangu kwenu ni sala. Sala iwe kwenu furaha na taji la kuwaunganisha na Mungu. Wanangu, majaribu yatakuja nanyi hamtakuwa na nguvu na dhambi itatawala lakini mkiwa wangu, mtashinda maana
kimbilio
lenu litakuwa Moyo wa Mwanangu Yesu. Kwa hiyo wanangu, rudieni sala ili sala iwe maisha kwenu, mchana na usiku. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2020
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu ninawaita kumrudia Mungu na sala. Waiteni watakatifu wote wawasaidie ili wawe mfano na msaada kwenu. Shetani ni mwenye nguvu na anapigania kuivutia kwake mioyo mingi zaidi awezavyo. Anataka vita na chuki. Kwa sababu hiyo Mimi ni pamoja nanyi muda mrefu ili niwaongoze kwenye njia ya wokovu, kwa Yule aliye njia, kweli na uzima. Wanangu, rudini kwa upendo kumwelekea Mungu naye atakuwa nguvu yenu na
kimbilio
lenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2023
“
W
anangu wapendwa! Aliye Juu ameniruhusu niwe miongoni mwenu, niwaombee, niwe Mama yenu na
kimbilio
lenu. Ninawaalika wanangu, mrudieni Mungu na kwenye maombi na Mungu atawabariki kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose