Our Lady of Medjugorje Messages containing 'kuhisi'
Total found:
4
Ujumbe, 25 Februari 2014
“
W
anangu wapendwa! Mnaona, mnasikia na
kuhisi
kwamba katika mioyo ya watu wengi hakuna Mungu. Hawamtaki kwa maana wapo mbali na sala na hawana amani mioyoni. Ninyi, wanangu, salini, na isheni kadiri ya amri za Mungu. Muwe sala, enyi mlioitikia "naam" tangu mwanzo wa mwaliko wangu. Mshuhudieni Mungu na mtambue uwepo wangu wala msisahau, wanangu, ya kuwa mimi ni pamoja nanyi na ninawapenda. Siku hata siku nawachukua kwa Mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, fungueni mioyo yenu mkajaribu
kuhisi
jinsi ninavyowapenda na kutaka mpendeni Mwanangu. Nataka mpende zaidi kwa kuwa haiwezekani kumjua pasipo kumpenda, maana Yeye ndiye upendo. Wanangu, mimi nawajueni: najua maumivu yenu na mateso yenu maana niliyaishi. Nafurahi pamoja nanyi kwa furaha zenu. Nalia machozi pamoja nanyi katika maumivu yenu. Sitawaacheni kamwe. Nitaongea nanyi daima kwa upole wa kimama na, kama mama, nahitaji mioyo yenu ifumbuliwe, ili kwa hekima na unyofu mueneze upendo wa Mwanangu. Nawahitaji ninyi mfumbuliwe na kuwa wepesi kupokea mema na huruma. Nahitaji muungano wenu na Mwanangu, kwa maana nataka mpate kufanikiwa na kumsaidia kuleta heri kwa wanangu wote. Mitume wangu, nawahitaji, ili muwaonyeshe wote ukweli wa Mungu, ili moyo wangu, ulioteswa na kuteswa hata leo kupita kiasi, uweze kushinda katika upendo. Salini kwa ajili ya utakatifu wa wachungaji wenu, ili katika jina la Mwanangu, waweze kutenda maajabu, maana utakatifu hutenda maajabu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Mei 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika ninyi mwende katika mazingira ya asili na kusali ili kwamba Aliye Juu Sana aseme na moyo wenu na kwamba muweze
kuhisi
uwezo wa Roho Mtakatifu kushuhudia upendo ambao Mungu anao kwa kila kiumbe. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika ninyi kwenye maombi kwa moyo. Mioyo yenu, wanangu, igeuzwe kuelekea mbinguni kwa maombi, ili mioyo yenu ipate
kuhisi
Mungu wa upendo anayewaponya na kuwapenda kwa upendo mkuu. Mimi niko pamoja nanyi kuwaongoza kwenye njia ya uongofu wa moyo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose