Our Lady of Medjugorje Messages containing 'kuishi'
Total found:
31
Ujumbe, 25 Aprili 2018
“
W
anangu wapendwa, leo pia ninawaalika
kuishi
pamoja na Yesu maisha yenu mapya. Bwana Mfufuka awape nguvu ili muwe daima mashujaa katika majaribu ya maisha, na waaminifu na mdumu katika kusali, maana Yesu aliwaokoeni kwa majeraha Yake na kwa njia ya Ufufuko Wake aliwapa maisha mapya. Salini, wanangu na msipoteze matumaini. Katika mioyo yenu na ziwe furaha na amani, muwe mashahidi ya furaha ya kuwa wangu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwapenda nyote kwa upendo wangu wa kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo wa kimama ninawaalika ili kwa moyo safi na wazi, kwa imani kabisa, mpokee upendo mkubwa wa Mwanangu. Mimi ninajua ukuu wa upendo wake, mimi nilimchukua ndani yangu, Hostia moyoni, Mwanga na Upendo wa ulimwengu. Wanangu, hata kuelekea kwangu kwenu ninyi ni ishara ya upendo na ya huruma ya Baba wa Mbinguni, ni tabasamu kilichojaa upendo wa Mwanangu, ni mwaliko kwa uzima wa milele. Damu ya Mwanangu ilimwagika kwa ajili yenu kwa upendo. Ile Damu yenye thamani ni kwa wokovu wenu, kwa ajili ya uzima wa milele. Baba wa mbinguni aliumba mtu kwa ajili ya furaha ya milele. Haiwezekani ninyi kufa, ninyi mnaojua upendo wa Mwanangu, ninyi mnaomfuata. Uzima umeshinda: Mwanangu yu hai! Kwa hiyo, wanangu, mitume wa upendo wangu, sala iwaonyeshe njia, jinsi ya kueneza upendo wa Mwanangu kwa jinsi ilivyo bora zaidi. Wanangu, hata wakati mnapojaribu
kuishi
maneno ya Mwanangu, ninyi mnasali. Wakati mnapowapenda watu mnaokutana nao, mnaeneza upendo wa Mwanangu. Upendo ni neno linalofungua milango ya Uzima. Wanangu, tangu awali nimesali kwa ajili ya Kanisa. Kwa hiyo ninawaalika nanyi, mitume wa upendo wangu, kusali kwa ajili ya Kanisa na watumishi wake, kwa wale ambao Mwanangu amewaita. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, mapenzi na upendo wa Baba wa mbinguni hufanya mimi niwe katikati yenu, ili kusaidia kwa upendo wa kimama ukuaji wa imani katika mioyo yenu, ili kwamba muweze hakika kuelewa lengo la maisha ya kidunia na ukuu wa yale ya kimbingu. Wanangu, maisha ya kidunia ndiyo njia kuelekea umilele, kuelekea ukweli na uzima: kuelekea kwa Mwanangu. Kwa njia hii nataka kuwaongoza. Ninyi, wanangu, ninyi wenye sikuzote kiu ya upendo mkubwa zaidi, ukweli na imani, mjue ya kuwa moja tu ni chemchemi mnakoweza kunywa: imani katika Baba wa mbinguni, imani katika upendo wake. Mtegemee kabisa mapenzi yake wala msiogope: kila lililo bora kwa ajili yenu, kila linalowachukua kwenye uzima wa milele, mtapewa! Mtaelewa ya kuwa lengo la maisha si sikuzote kutaka na kutwaa, lakini kupenda na kutoa; mtakuwa na amani ya kweli na upendo wa kweli, mtakuwa mitume wa upendo. Kwa mfano wenu, mtawafanya wale wanangu wasiomjua Mwanangu na upendo wake watake kumjua. Wanangu, mitume wa upendo wangu, mwabuduni Mwanangu pamoja nami, na mpendeni juu ya vyote. Jaribuni sikuzote
kuishi
katika ukweli wake. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninapowatazama ninyi mnaopenda Mwanangu, furaha inajaza Moyo wangu. Ninawabariki kwa baraka ya kimama. Pamoja na baraka ya kimama ninawabariki hata wachungaji wenu: ninyi mnaotangaza maneno ya Mwanangu, mnaobariki kwa mikono yake na mnaompenda hata kuwa tayari kufanya kwa furaha kila sadaka kwa ajili yake. Ninyi mfuateni Yeye, aliyekuwa Mchungaji wa kwanza, Mmisionari wa kwanza. Wanangu, mitume wa upendo wangu,
kuishi
na kufanya kazi kwa ajili ya wengine, kwa wale wote mnaopenda kwa njia ya Mwanangu, ni furaha na faraja ya maisha ya kidunia. Ikiwa kwa njia ya sala, upendo na sadaka Ufalme wa Mungu ni katika mioyo yenu, hapo kwa ninyi maisha ni yenye furaha na matulivu. Katikati ya wale wanaompenda Mwanangu na wanaopendana kwa ajili yake, maneno si ya lazima. Kutazamana kwatosha ili kusikia maneno yasiyonenwa na hisia zisizoonyeshwa. Pale panapotawala upendo, wakati hauna maana tena. Sisi ni pamoja nanyi! Mwanangu anawajua na kuwapenda. Upendo ni kilichowaongoza kwangu na, kwa njia ya upendo huu, mimi nitakuja kwenu na nitawaambieni kazi za wokovu. Ninataka ya kuwa wana wangu wote wawe na imani na wahisi upendo wangu wa kimama unaowaongoza kwa Yesu. Kwa hiyo ninyi, wanangu, ko kote mwendako angazeni kwa upendo na kwa imani, kama mitume wa upendo. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Juni 2020
“
W
anangu wapendwa, ninasikiliza maombi yenu na sala zenu na ninawaombea kwa mwanangu Yesu aliye njia, kweli na uzima. Wanangu, rudieni kusali na fungueni mioyo yenu katika wakati huu wa neema na shikeni njia ya wongofu. Maisha yenu yanapita na hayana maana bila Mungu. Kwa hiyo mimi ni pamoja nanyi niwaongoze kuelekea utakatifu wa maisha ili kila mmoja wenu agundue furaha ya
kuishi
. Wanangu, ninawapenda wote na kuwabariki kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2020
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati wa neema. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaalika tena, wanangu, mrudieni Mungu na kwa kusali ili sala iwe furaha kwenu. Enyi wanangu hamtakuwa na wakati ujao wala amani mpaka katika maisha yenu mtakapoanza
kuishi
maongezi ya binafsi na badiliko katika mema. Maovu yatakoma na amani itatawala katika mioyo yenu na katika ulimwengu. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombea kwa mwanangu Yesu kwa ajili ya kila mmoja wenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Mimi ni pamoja nanyi kwa muda mrefu kwa maana Mungu ni mkuu katika upendo wake na katika uwepo wangu. Wanangu, ninawaalika kurudi kwa Mungu na kwa sala. Kipimo cha
kuishi
kwenu kiwe upendo na msisahau, wanangu, kwamba maombi na kufunga hufanya miujiza ndani yenu na kuwazunguka. Yote mnayoyafanya yawe kwa ajili ya utukufu wa Mungu na hapo Mbingu itajaza moyo wenu na furaha mkahisi ya kuwa Mungu anawapenda na kunituma ili kuokoa ninyi na Dunia ambayo juu yake mnaishi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mtoto Yesu anayewaletea amani, Yule aliye wakati uliopita, wakati wa sasa na wakati ujao wa
kuishi
kwenu. Wanangu, msiruhusu imani yenu na matumaini yenu katika wakati ujao ulio bora yazimike, kwa maana ninyi mmechaguliwa kwa kuwa mashahidi wa matumaini katika kila hali. Kwa ajili hiyo mimi ni hapa pamoja na Yesu ili awabariki kwa amani yake. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2021
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huo ninawaalika kusali, kufunga na kujikana ili muweze kuwa wenye nguvu zaidi katika imani. Huu ni wakati wa mwamko na wa kuzaliwa upya. Kama vitu vya asili vinavyojitoa nanyi wanangu, fikirini juu ya mambo mliyopokea. Muwe waletaji wa amani na wa upendo wenye furaha ili
kuishi
vizuri duniani. Tamanini Mbingu kwa sababu Mbinguni hakuna wala huzuni wala machukio. Kwa hiyo, wanangu, amueni tena kuongoka, na utakatifu utawale katika maisha yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2021
“
W
anangu wapendwa! Mungu ameniruhusu kuwa pamoja nanyi leo pia kwa kuwaalika kusali na kufunga. Ishini wakati huu wa neema na muwe mashahidi wa tumaini maana, ninawaambia tena wanangu, kwa kusali na kufunga hata vita vinaweza kuisha. Wanangu, aminini na
kuishi
katika imani na kwa imani wakati huu wa neema na Moyo wangu usio na dhambi ya asili haumwachi yeyote kati yenu katika wasiwasi ikiwa ananikimbilia. Ninawaombea mbele ya Yeye aliye juu na ninasali ili amani iwepo katika mioyo yenu na kwa ajili ya tumaini katika wakati ujao. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2021
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu Yesu awapeni amani yake. Wanangu, bila amani hamna wala wakati ujao, wala baraka, kwa hiyo rudieni kusali kwa sababu tunda la sala ni furaha na imani, na bila hiyo hamwezi
kuishi
. Baraka ya leo tunayowapa, ileteni kwa jamaa zenu na tajirisheni wote wale mnaokuta ili wahisi neema ambayo mnapokea. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2