Our Lady of Medjugorje Messages containing 'kujifungua'
Total found:
3
Ujumbe, 25 Juni 2017
“
W
anangu wapendwa! Leo nataka kuwashukuru kwa uvumilivu wenu na kuwaalika
kujifungua
kwa sala ya ndani. Wanangu, sala ni moyo wa imani na wa matumaini katika uzima wa milele. Kwa hiyo salini kwa moyo mpaka moyo wenu umwimbie Mungu Mwumbaji aliyewapa maisha kwa shukrani. Wanangu, Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaletea baraka yangu ya amani ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2018
“
W
anangu wapendwa! Katika kipindi hiki cha neema ninawaalika nyote
kujifungua
na kuishi amri ambazo Mungu aliwapeni ili, kwa njia ya sakramenti, ziwaongoze katika njia ya wongofu. Ulimwengu na vishawishi vya ulimwengu vinawajaribu; ninyi, wanangu, angalieni viumbe vya Mungu ambavyo katika uzuri na unyenyekevu Yeye aliwapa, na mpendeni Mungu, enyi wanangu, kuliko kila kitu naye atawaongoza katika njia ya wokovu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2020
“
W
anangu wapendwa, Katika kipindi hiki cha neema nataka kuona nyuso zenu zigeuke katika sala. Ninyi mmejaa mahangaiko ya kidunia kiasi kwamba hamuoni hata ujio wa majira ya kuchipua kwa mimea. Wanangu, mnaalikwa kwa toba na kwa sala. Kama viumbe vya asili vinapigana katika kimya kwa maisha mapya, hivyo hata ninyi mnaalikwa
kujifungua
katika sala kwa Mungu ambaye kwake mtapata amani na joto la jua la kipindi cha kuchanua kwa mimea katika mioyo yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose