Our Lady of Medjugorje Messages containing 'kumwomba'
Total found:
3
Ujumbe, 25 Februari 2017
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalika kuishi kwa kina imani yenu na
kumwomba
Aliye juu ili aiimarishe, hivyo upepo na dhoruba yasije yakaivunja. Mizizi ya imani yenu iwe sala na tumaini katika uzima wa milele. Tokea sasa, wanangu, jijengeni wenyewe, katika wakati huu wa neema ambapo Mungu anawapeni neema ili kwa njia ya kujinyima na mwito wa kuongoka muwe watu wenye imani na tumaini safi na ya kuvumilia. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawaalika kusali pasipo kuomba, bali mkitoa sadaka, mkijitolea wenyewe. Nawaalika kuleta habari ya ukweli na upendo wenye rehema. Ninamwomba Mwanangu kwa ajili yenu, kwa imani yenu, inayoendelea kupunguka katika mioyo yenu. Ninamwomba awasaidieni kwa Roho ya Mungu, kama vile mimi nami ninavyotaka kuwasaidieni kwa roho ya kimama. Wanangu, itawabidi kujiboresha! Wale tu walio safi, wanyenyekevu na wamliojaa upendo wanautegemeza ulimwengu, wanaokoa ulimwengu na wao wenyewe. Wanangu, Mwanangu ndiye moyo wa ulimwengu: lazima kumpenda na
kumwomba
, na si kumsaliti daima tena. Kwa hiyo ninyi, mitume wa upendo wangu, mstawishe imani katika mioyo ya watu kwa mfano wenu, kwa sala yenu na kwa upendo wenye rehema. Mimi nipo karibu nanyi na nitawasaidia. Salini ili wachungaji wenu wapate mwanga zaidi kadiri wawezavyo, ili waweze kuangaza wale wote wanaoishi gizani. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Julai 2018
“
W
anangu wapendwa! Mungu aliniita ili niwaongozeni kwake, maana Yeye ndiye nguvu yenu. Kwa hiyo ninawaalika
kumwomba
na kumtegemea, maana Yeye ndiye kimbizo lenu kutoka kila uovu uliokaribu na kupeleka mioyo mbali kutoka neema na furaha mnakoitwa. Wanangu isheni Mbingu hapa duniani ili mkae vizuri na amri za Mungu ziwe mwanga katika njia yenu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwapenda nyote kwa upendo wa kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose