Our Lady of Medjugorje Messages containing 'kwa'
Total found:
219
Ujumbe, 2 Januari 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nipo hapa katikati yenu kama Mama atakaye kuwasaidia kuujua ukweli. Nilipokuwa nikiishi maisha kama yenu duniani, nilikuwa nikijua ukweli na
kwa
hivyo kuwa na kipande cha Mbinguni duniani.
Kwa
hiyo, wanangu, nataka ninyi pia muwe washiriki wa hali hivyo. Baba wa Mbinguni ataka mioyo minyofu, ijaayo ujuzi wa ukweli: Ataka muwapende wote mnaokutana nao, maana mimi pia nampenda Mwanangu katika ninyi nyote. Huo ndio mwanzo wa ujuzi wa ukweli. Mtapewa kweli nyingi za uongo. Mtazitambua
kwa
mioyo iliyotakaswa
kwa
kufunga, kusali,
kwa
kufanya toba pamoja na kuishika Injili: Huo ndiyo ukweli wa pekee, nao ni ule ambao Mwanangu aliwaachieni. Msiufanyie utafiti mwingi sana: mnaombwa kuupenda na kuutoa, kama vile nilivyofanya mimi pia. Wanangu, mkipenda, mioyo yenu itakuwa maskani ya Mwanangu na yangu, na maneno ya Mwanangu yatakuwa mwongozo wa maisha yenu. Wanangu, nitawatumia, ninyi mitume wa upendo, kusaidia wanangu wote kuujua ukweli. Wanangu, mimi nimeliombea sikuzote Kanisa la Mwanangu,
kwa
hiyo nawasihi ninyi pia kufanya vile vile. Salini ili wachungaji wenu waangazwe
kwa
upendo wa Mwanangu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2015
“
W
anangu wapendwa! Hata leo ninawaalika: ishini katika sala mwito wenu. Leo, kama bado haijatokea awali, Shetani atamani kumfunga pumzi binadamu na roho yake
kwa
njia ya upepo wake unaoambukiza chukio na hofu. Katika mioyo mingi hakuna furaha
kwa
sababu hakuna Mungu wala sala. Uadui na vita zinaongezeka siku hata siku. Ninawaalika, wanangu, anzisheni upya
kwa
ari mwelekeo wa kutafuta utakatifu na upendo
kwa
maana nimekuja katikati yenu
kwa
ajili hiyo. Tuwe upendo na msamaha
kwa
wale wote wanaofahamu na kutaka kupenda
kwa
mapendo ya kibinadamu tu wala siyo
kwa
ule upendo mkubwa sana wa kimungu ambao Mungu anatualikia. Wanangu, matumaini ya kesho iliyo bora zaidi yawe daima mioyoni mwenu. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nipo hapa katikati yenu. Ninawatazama, ninawapa tabasamu na kuwapenda kama mama peke yake awezavyo kufanya.
Kwa
neema ya Roho Mtakatifu ajaye
kwa
njia ya usafi wangu, ninaona mioyo yenu na kuitolea
kwa
Mwanangu. Tangu muda mrefu nawaombeni muwe mitume wangu, na kusali
kwa
ajili ya wale wasioujua upendo wa Mungu. Naomba sala inayotokana na upendo, sala itoayo matunda na sadaka. Msipotee muda kutaka kuelewa kama mnastahili kuwa mitume wangu, Baba aliye Mbinguni atahukumu wote, lakini ninyi mpendeni na msikilizeni. Najua ya kuwa mambo hayo yote yanawafadhaisha, hata ujio wangu katikati yenu, lakini upokeeni
kwa
furaha na salini ili muelewe kwamba mnastahili kufanya kazi
kwa
ajili ya ufalme wa mbingu. Upendo wangu ni juu yenu. Salini ili upendo wangu udumu ndani ya kila moyo,
kwa
maana upendo huo unaosamehe ujitolea bila kukata tamaa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2015
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika nyote: salini zaidi na muongee kidogo. Katika kusali tafuteni mapenzi ya Mungu na yaishini kadiri ya amri ambazo Mungu anawaalika kuziishi. Mimi nipo pamoja nanyi na kusali pamoja nanyi. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninyi ni nguvu yangu. Ninyi, mitume wangu, ambao,
kwa
upendo wenu, unyenyekevu na sala ya kimya kimya, mnamwezesha Mwanangu ajulikane. Ninyi mnaishi ndani yangu. Ninyi mnanibeba mioyoni mwenu. Ninyi mnajua ya kuwa mna Mama awapendaye na aliyekuja kuwaletea upendo. Nawatazama katika Baba wa Mbinguni, natazama fikira zenu, maumivu yenu, mateso yenu na kuyaleta
kwa
Mwanangu. Msiogope! Msipoteze matumaini, maana Mwanangu humsikiliza Mama yake. Yeye hupenda tangu alipozaliwa, na ndio furaha yangu ya kuwa wanangu wote wajue upendo huo; na wote wale ambao,
kwa
sababu ya maumivu yao na kutoelewa kwao, walimwacha waweze kurudi kwake, na wote wao wasiomjua wamjue.
Kwa
sababu hiyo ninyi hapa ni mitume wangu, nami pia pamoja nanyi kama Mama yenu. Salini ili kuwa imara katika imani, maana upendo na rehema hutoka katika imani imara.
Kwa
njia ya upendo na rehema mtawasaidia wale wote wasiofahamu ya kuwa wanachagua giza badala ya nuru. Salini
kwa
ajili ya wachungaji wenu, maana wao ni nguvu ya Kanisa ambayo Mwanangu aliwaachieni.
Kwa
njia ya Mwanangu wao ni wachungaji wa roho. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Machi 2015
“
W
anangu wapendwa! Hata leo pia Yeye Aliye Juu ameniruhusu kuwa pamoja nanyi na kuwaongoza katika njia ya uwongofu. Mioyo mingi imejifunga
kwa
neema wala haitaki kusikiliza mwaliko wangu. Ninyi wanangu salini na pambaneni na kishawishi na mipango yote ya uovu ambayo anayowapatia shetani
kwa
njia ya mambo ya kisasa. Muwe hodari katika kusali na mkishika msalaba mikononi salini ili maovu yasiwatumie wala kuwashinda. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombea. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Aprili 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nimewachagua ninyi, mitume wangu,
kwa
maana kila mmoja wenu huchukua ndani yake jambo njema. Ninyi mnaweza kunisaidia ili ule upendo ambao kwao Mwanangu amekufa, na kufufuka baadaye, ushinde tena.
Kwa
hiyo nawaalika, mitume wangu, kujaribu kuona katika kila kiumbe cha Mungu, katika wanangu wote, kitu chema na kujitahidi kuwaelewa. Wanangu, ninyi nyote ni kaka na dada
kwa
njia ya huyo Roho Mtakatifu. Ninyi mliojaa upendo
kwa
ajili ya Mwanangu, mnaweza kuwaeleza wote ambao hawajui cho chote kuhusu upendo huo, yote mnayoyafahamu. Ninyi mmejua upendo wa Mwanangu, mnaelewa ufufuko wake, na mnamgeuzia macho
kwa
furaha. Haja yangu ya kimama ni kwamba wanangu wote waungane katika upendo wa Yesu.
Kwa
hiyo nawaalika, mitume wangu, kuishi
kwa
furaha Ekaristi maana, katika Ekaristi, mwanangu anajitoa
kwa
ajili yenu tena na tena, na
kwa
mfano wake, anawaonyesha namna ya kutoa upendo na sadaka
kwa
jirani. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2015
“
W
anangu wapendwa! Mimi nipo pamoja nanyi hata leo niwaongozeni kwenye wokovu. Moyo wenu una wasiwasi maana roho yenu ni dhaifu na imechoka
kwa
mambo yote ya dunia. Ninyi wanangu, ombeni Roho Mtakatifu awageuze na kuwajaza nguvu yake ya imani na tumaini ili muweze kuwa imara katika kupambana kwenu na maovu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombea kwenye Mwanangu Yesu. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, fungueni mioyo yenu mkajaribu kuhisi jinsi ninavyowapenda na kutaka mpendeni Mwanangu. Nataka mpende zaidi
kwa
kuwa haiwezekani kumjua pasipo kumpenda, maana Yeye ndiye upendo. Wanangu, mimi nawajueni: najua maumivu yenu na mateso yenu maana niliyaishi. Nafurahi pamoja nanyi
kwa
furaha zenu. Nalia machozi pamoja nanyi katika maumivu yenu. Sitawaacheni kamwe. Nitaongea nanyi daima
kwa
upole wa kimama na, kama mama, nahitaji mioyo yenu ifumbuliwe, ili
kwa
hekima na unyofu mueneze upendo wa Mwanangu. Nawahitaji ninyi mfumbuliwe na kuwa wepesi kupokea mema na huruma. Nahitaji muungano wenu na Mwanangu,
kwa
maana nataka mpate kufanikiwa na kumsaidia kuleta heri
kwa
wanangu wote. Mitume wangu, nawahitaji, ili muwaonyeshe wote ukweli wa Mungu, ili moyo wangu, ulioteswa na kuteswa hata leo kupita kiasi, uweze kushinda katika upendo. Salini
kwa
ajili ya utakatifu wa wachungaji wenu, ili katika jina la Mwanangu, waweze kutenda maajabu, maana utakatifu hutenda maajabu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Mei 2015
“
W
anangu wapendwa! Hata leo mimi nipo pamoja nanyi na
kwa
furaha nawaalikeni nyote: salini na aminini nguvu ya sala. Fungueni mioyo yenu, wanangu, ili Mungu awajaze upendo wake, nanyi mtakuwa furaha ya watu wengine. Ushahidi wenu utakuwa na nguvu na lote mfanyalo litaendana na mapenzi ya Mungu. Mimi nipo pamoja nanyi, nikisali
kwa
ajili yenu na
kwa
ajili ya wokovu wenu hata mtakapomweka Mungu mahali pa kwanza. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Juni 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nataka kufanya kazi
kwa
njia yenu, wanangu, mitume wangu, ili mwishowe niweze kukusanya wanangu wote pale ambapo pameandaliwa tayari
kwa
ajili ya furaha yenu. Nawaombea, kusudi
kwa
matendo yenu muweze kugeuza, kwani muda umefika
kwa
matendo ya kweli,
kwa
ajili ya Mwanangu. Upendo wangu utafanya kazi ndani mwenu, nitawatumia ninyi. Muwe na imani nami, kwani yote ninayotamani, ninayatamani
kwa
ajili yenu, wema wa milele, ulioumbwa
kwa
njia ya Baba wa Mbinguni. Ninyi, wanangu, mitume wangu, muishi maisha ya duniani pamoja na wanangu ambao hawafahamu upendo wa Mwanangu, wale ambao hawaniiti mama. Lakini msiogope kushuhudia ukweli,
kwa
maana ikiwa ninyi hamtaogopa na kushuhudia ukweli
kwa
uhodari, ukweli utashinda kimuujiza. Kumbukeni: nguvu iko katika upendo. Wanangu, upendo ndio kutubu, kusamehe, kusali, kujitoa sadaka na rehema, maana mkijua kupenda
kwa
matendo mtawabadilisha na wengine, mtawezesha mwanga wa Mwanangu uingie katika mioyo yao. Nawashukuru. Muwaombee wachungaji wenu, wao ni mali ya Mwanangu. Yeye aliwaita. Salini ili wawe siku zote na nguvu na uhodari wa kung'aa
kwa
nuru ya Mwanangu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Juni 2015
“
W
anangu wapendwa! Hata leo Yeye Aliye Juu ananipa neema ya kuweza kuwapenda na kuwaalika muweze kuongoka. Wanangu, Mungu awe kesho yenu, vita, wasiwasi, huzuni yasiwatawale, ila furaha na amani zitawale mioyoni mwa watu wote, na mjue kuwa pasipo Mungu hamtapata kamwe amani.
Kwa
hiyo, wanangu, mrudieni Mungu na sala ili mioyo yenu iimbe
kwa
furaha. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawapenda
kwa
upendo usio na kipimo. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Julai 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawaalika kueneza imani katika Mwanangu, imani yenu. Ninyi wanangu, mlioangazwa na Roho Mtakatifu, mitume wangu, itangazeni imani
kwa
watu wengine, yaani
kwa
wasiosadiki, wasioijua na wasiotaka kuijua.
Kwa
sababu hiyo yawapasa kusali sana
kwa
ajili ya zawadi ya upendo, maana upendo ndio alama maalum ya imani ya kweli, na ninyi mtakuwa mitume wa upendo wangu. Upendo hufanya upya daima maumivu na furaha ya Ekaristi, hufanya upya maumivu ya Mateso ya Mwanangu, aliyewaonyesha upendo usio na kifani; hufanya upya furaha ya tendo la kuwaachia Mwili wake na Damu yake
kwa
ajili ya kuwalisha na hivyo kuwa kitu kimoja nanyi. Nikiwaangalia
kwa
wema nahisi upendo pasipo kiasi, ulioniimarisha katika hamu yangu ya kuwaongoza katika imani thabiti. Imani thabiti itawapa furaha na uchangamfu duniani, na mwishowe kuwaunganisha na Mwanangu. Hiyo ndiyo hamu yake.
Kwa
hiyo mwishi katika Yeye, na katika upendo, isheni katika nuru iliyowaangaza daima katika Ekaristi. Nawaombeni kusali sana
kwa
wachungaji wenu, kusali ili kupata upendo mkubwa
kwa
ajili yao,
kwa
maana Mwanangu aliwapeni ili waweze kuwalisha
kwa
Mwili wake na kuwafundisha upendo.
Kwa
hiyo wapendeni ninyi pia! Lakini, wanangu, kumbukeni: upendo maana yake ni kuvumilia na kutoa na kutohukumu kamwe. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Julai 2015
“
W
anangu wapendwa, hata leo
kwa
furaha nipo pamoja nanyi na ninawaalika wote, wanangu, salini, salini, salini, ili muweze kuelewa upendo nilio nao kwenu. Upendo wangu una nguvu kuliko uovu,
kwa
hiyo wanangu mjongeeni Mungu ili muweze kuonja furaha yangu
kwa
Mungu. Pasipo Mungu, wanangu, hamtakuwa na wakati ujao, wala tumaini, wala wokovu,
kwa
hiyo acheni uovu na chagueni wema: Mimi nipo pamoja nanyi na pamoja nanyi namwomba Mungu
kwa
mahitaji yenu yote. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, mimi, kama Mama apendaye wanawe, natambua jinsi ulivyo mgumu muda huu mnaouishi. Naona mateso yenu, lakini jueni kwamba hamko peke yenu: Mwanangu yu pamoja nanyi! Yeye yupo popote, asiyeonekana, lakini mtaweza kumwona ikiwa mtamwishi. Yeye ndiye nuru inayoangaza roho yenu na kuleta amani. Yeye ndiye Kanisa, mnalopaswa kulipenda, kuliombea na kulilinda daima: si
kwa
maneno tu, bali
kwa
matendo ya upendo. Wanangu, fanyeni yote ili Mwanangu ajulikane
kwa
watu wote, na aweze kupendwa,
kwa
maana ukweli ni katika Mwanangu, aliyezaliwa na Mungu, Mwana wa Mungu. Msipoteze muda
kwa
kufikiri mno; mtajitenganisha na ukweli. Pokeeni Neno lake
kwa
moyo mnyofu na kuliishi. Mkiishi Neno lake, mtasali. Mkiishi Neno lake, mtapenda
kwa
upendo wenye huruma, na mtapendana.
Kwa
kadiri mtakavyokuwa na upendo hivyo ndivyo mtakavyokuwa mbali na kifo.
Kwa
wale watakaoishi na kulipenda Neno la Mwanangu, kifo kitakuwa uhai kwao. Nawashukuru! Salini
kwa
ajili ya kuweza kuona Mwanangu katika wachungaji wenu. Salini
kwa
ajili ya kuweza kumkumbatia katika wao.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2015
“
W
anangu wapendwa, hata leo ninawaalika: muwe sala. Sala iwe mabawa
kwa
ajili ya mkutano kati yenu na Mungu. Ulimwengu upo katika wakati wa kujaribiwa,
kwa
maana umemsahau na kumwacha Mungu.
Kwa
hiyo wanangu, muwe wale wanaomtafuta na kupenda Mungu kuliko yote. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaongoza
kwa
Mwanangu, lakini ninyi hamna budi kunena "NDIYO" yenu katika uhuru wa wana wa Mungu. Nawaombeeni na kuwapenda, wanangu,
kwa
upendo usio na mwisho. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, wapendwa mitume wangu wa upendo, waletaji wangu wa ukweli, ninawaalika tena na ninawakusanya karibu nami ili mnisaidie, ili muwasaidie wanangu wote wenye kiu ya upendo na ukweli, wenye kiu ya Mwanangu. Mimi ndimi neema ya Baba wa Mbinguni iliyotumwa kuwasaidieni kuishi neno la Mwanangu. Pendaneni. Nimeyaishi maisha yenu duniani. Najua kwamba si kitu rahisi kila mara lakini, mkipendana, mtasali
kwa
moyo, mtafikia vilele vya maisha ya roho, na njia ya kwenda mbinguni itafunguliwa mbele yenu. Pale nawangojea mimi, Mama yenu,
kwa
maana mimi nipo pale. Muwe waaminifu
kwa
Mwanangu na muwafundishe wengine uaminifu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwasaidia. Nitawafundisha imani, ili muweze kuwafikishia wengine
kwa
njia sahihi. Nitawafundisha ukweli, ili muweze kuufahamu. Nitawafundisha upendo, ili mjue upendo wa kweli ni kitu gani. Wanangu, Mwanangu atafanya yote ili aongee
kwa
njia ya maneno na matendo yenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2015
“
W
anangu wapendwa, hata leo ninamwomba Roho Mtakatifu ili ajaze mioyo yenu
kwa
imani thabiti. Sala na imani zitajaza mioyo yenu
kwa
upendo na furaha, nanyi mtakuwa ishara
kwa
wale walio mbali na Mungu. Wanangu, mpeane moyo wenyewe
kwa
wenyewe ili kufanya sala ya moyo, ili sala iweze kujaza maisha yenu na ninyi, wanangu, kila siku muwe mashahidi wa utumishi:
kwa
Mungu katika kuabudu na
kwa
majirani zenu katika mahitaji yao. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombea ninyi nyote. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nipo hapa katikati yenu kuwatieni moyo, kuwajaza
kwa
upendo wangu, kuwaalika tena kuwa mashahidi wa upendo wa Mwanangu. Wanangu wengi hawana tumaini, hawana amani, hawana upendo. Wao wanatafuta Mwanangu lakini hawajui jinsi wala wapi ya kumpata. Mwanangu awafungulia mikono Yake, nanyi wasaidieni ili waje mikononi Mwake. Wanangu,
kwa
hiyo ni lazima msali
kwa
upendo, lazima msali sana, sana, ili kupata upendo zaidi na zaidi,
kwa
maana upendo hushinda mauti na hudumisha maisha. Watume wa upendo wangu, wanangu wenye moyo mnyofu na safi, jiungeni zaidi na zaidi katika kusali. Mnatengana sana! Jipeni moyo katika kukua kiroho, kama vile Mimi ninawapeni moyo. Ninawaangalia na nipo karibu nanyi kila mnaponifikiria. Waombeeni wachungaji wenu, wale walioacha yote
kwa
ajili ya Mwanangu. Wapendeni na waombeeni, Baba wa Mbinguni husikiliza sala zenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2015
“
W
anangu wapendwa, sala yangu hata leo ni
kwa
ajili yenu nyote, hasa
kwa
wale walio na mioyo migumu kuitikia wito wangu. Mnaishi katika siku za neema wala hamtambui fadhili ambazo Mungu anawapeni
kwa
njia ya uwepo wangu. Wanangu, amueni hata leo kuwa watakatifu na jifunzeni kutokana na mifano ya watakatifu wa siku hizi na mtatambua ya kuwa utakatifu ni ukweli uliopo
kwa
ajili yenu nyote. Wanangu, furahini katika upendo
kwa
maana machoni pa Mungu ninyi ni wa pekee na hakuna atakayechukua nafasi ya mwingine,
kwa
maana ninyi ni furaha ya Mungu duniani hapa. Mshuhudieni amani, sala na upendo. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
Next>>