Our Lady of Medjugorje Messages containing 'kwa'
Total found:
219
Ujumbe, 2 Juni 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kama vile katika mahali pengine nilipokuja, vivyo hivyo hapa pia nawaalika kusali. Salini
kwa
ajili ya wale wasiomjua Mwanangu,
kwa
ajili ya wale ambao hawajaujua upendo wa Mungu, dhidi ya dhambi,
kwa
ajili ya waliowekwa wakfu,
kwa
ajili ya wale ambao Mwanangu aliwaita ili wawe na upendo na roho yenye nguvu,
kwa
ajili yenu na
kwa
ajili ya Kanisa. Mwombeni Mwanangu, na upendo mnaohisi
kwa
ajili ya ukaribu, utawapa nguvu na utawatayarisha
kwa
matendo mema mtakayofanya
kwa
Jina lake. Wanangu muwe tayari. Wakati huu ni njia panda ya maisha.
Kwa
hiyo nawaalika tena
kwa
imani na matumaini, ninawaonyesha njia ya kushika. Hayo ni maneno ya Injili: Mitume wangu, ulimwengu unahitaji sana mikono yenu iliyoinuliwa mbinguni, kuelekea
kwa
Mwanangu na
kwa
Baba wa mbinguni. Ni lazima kuwa na unyenyekevu mwingi na usafi wa moyo. Mumwamini Mwanangu na jueni ya kuwa mnaweza kuwa bora zaidi daima. Moyo wangu wa kimama unatamani kwamba ninyi, mitume wa upendo wangu, muwe sikuzote mianga midogo ya ulimwengu. Mtie nuru pale giza inapotaka kutawala na
kwa
sala yenu na upendo wenu, muonyeshe sikuzote njia ya kweli, ziokoeni nafsi. Mimi nipo pamoja nanyi. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Juni 2017
“
W
anangu wapendwa! Leo nataka kuwashukuru
kwa
uvumilivu wenu na kuwaalika kujifungua
kwa
sala ya ndani. Wanangu, sala ni moyo wa imani na wa matumaini katika uzima wa milele.
Kwa
hiyo salini
kwa
moyo mpaka moyo wenu umwimbie Mungu Mwumbaji aliyewapa maisha
kwa
shukrani. Wanangu, Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaletea baraka yangu ya amani ya kimama. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Julai 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawashukuru
kwa
kuitikia miito yangu na kukusanyika karibu nami, Mama yenu wa mbinguni. Najua kwamba mnanifikiri
kwa
upendo na matumaini. Mimi ninawapendeni nyote kama vile anavyowapendeni Mwanangu ambaye,
kwa
upendo wake wenye huruma, ananituma nije kwenu, mara nyingi pia. Yeye, aliyekuwa mtu na aliye Mungu, Mmoja na Utatu; Yeye aliyeteswa
kwa
ajili yenu mwilini na nafsini. Yeye aliyejifanya Mkate ailishe nafsi zenu na hivyo kuziokoa. Wanangu, nawafundisha jinsi ya kustahili upendo wake, kumwelekeza mawazo yenu, kumwishi Mwanangu. Mitume wa upendo wangu, ninawafunika
kwa
joho langu
kwa
sababu, kama Mama yenu, nataka kuwalinda. Nawasihi: mwuombee ulimwengu wote: moyo wangu unateswa. Dhambi zinaongezeka, ni nyingi mno. Lakini
kwa
msaada wenu – mlio wanyenyekevu, wanyofu, wenye upendo, watawa na watakatifu – moyo wangu utashinda. Mpendeni Mwanangu kupita wote na ulimwengu wote
kwa
njia yake. Msisahau kabisa ya kuwa kila ndugu yenu ana ndani yake kitu cha thamani: nafsi.
Kwa
hiyo, wanangu, pendeni wale wote wasiomjua Mwanangu ili
kwa
njia ya maombi na upendo utokao katika maombi, wawe wema zaidi. Ili wema uweze kushinda ndani yao. Ili nafsi zao ziweze kuokoka na kupata uzima wa milele. Enyi mitume wangu, wanangu. Mwanangu aliwaambieni mpendane. Hiyo iandikwe mioyoni mwenu na
kwa
kusali jaribuni kuishi upendo huu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Julai 2017
“
W
anangu wapendwa! Muwe sala na kioo cha upendo wa Mungu
kwa
wale wote walio mbali na amri za Mungu. Wanangu, muwe waaminifu na thabiti katika wongofu na mjifanye kazi juu yenu wenyewe ili utakatifu wa maisha uwe kwenu jambo la ukweli. Jipeni moyo ninyi
kwa
ninyi mtende mema
kwa
njia ya kusali ili maisha yenu duniani yawe mazuri zaidi. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa,
kwa
mapenzi ya Baba wa mbinguni, kama Mama wa Yule anayewapendeni, nipo hapa pamoja nanyi niwasaidieni kumjua, kumfuata. Mwanangu amewaachieni nyayo za hatua zake, ili iwe rahisi zaidi kwenu kumfuata. Msiogope, msiwe na wasiwasi. Mimi nipo pamoja nanyi! Msichoke, maana sala nyingi na sadaka zinahitajiwa kuwasaidia wale wasiomwomba, wasiompenda na wasiomjua Mwanangu. Muwasaidie mkiona ndani yao ndugu zenu. Enyi mitume wa upendo wangu, sikilizeni sauti yangu ndani yenu, hisieni upendo wangu.
Kwa
hiyo salini: salini mkitenda, salini mkitoa. Salini
kwa
upendo, salini
kwa
matendo na
kwa
fikira,
kwa
jina la Mwanangu. Kadiri mtakavyotoa upendo, ndivyo mtakavyoupokea. Upendo utokao katika Upendo huangaza ulimwengu. Ukombozi ni upendo, na upendo hauna mwisho. Wakati Mwanangu atakapokuja tena duniani, atatafuta upendo katika mioyo yenu. Wanangu, Yeye alifanya
kwa
ajili yenu matendo mengi ya upendo. Ninawafundisha kuyaona, kuyaelewa na kumshukuru mkimpenda na kumsamehe sikuzote na tena jirani yako.
Kwa
kuwa kumpenda Mwanangu maana yake ni kusamehe. Mwanangu hapendwi, ikiwa hatuwezi kumsamehe jirani yetu, ikiwa hatuwezi kumwelewa jirani yetu, ikiwa tunamhukumu. Wanangu, faida gani kusali, msipopenda wala msiposamehe? Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2017
“
W
anangu wapendwa! leo ninawaalika kuwa watu wa sala. Salini mpaka hata sala itakapokuwa kwenu furaha na mkutano na Yeye aliye juu. Yeye atageuza moyo wenu nanyi mtakuwa watu wa upendo na wa amani. Wanangu, msisahau kwamba shetani ni mwenye nguvu na anataka kuwaachisha kusali. Ninyi, msisahau kwamba sala ni kifunguo cha siri cha mkutano pamoja na Mungu.
Kwa
hiyo Mimi nipo pamoja nanyi, niwaongoze. Msiache kusali. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nani angeweza kusema nanyi vizuri zaidi kuliko Mimi kuhusu upendo na maumivu ya mwanangu? Niliishi pamoja naye, niliteseka pamoja naye. Nikiishi maisha ya kidunia, nilionja maumivu, maana nilikuwa mama. Mwanangu alipenda michakato na kazi ya Baba wa Mbinguni, Mungu wa kweli; na, kama alivyoniambia, alikuja kusudi awakomboe ninyi. Mimi nilificha maumivu yangu
kwa
njia ya upendo. Bali ninyi, wanangu, ninyi mnaweka maswali mengi, hamwelewi maumivu, hamwelewi kwamba,
kwa
njia ya upendo wa Mungu, mnapaswa kupokea maumivu na kuyachukua. Kila mwanadamu, iwe
kwa
kiwango kikubwa au kidogo, yampasa afanye mang'amuzi. Lakini, tukiwa na amani rohoni na tukiwa na hali ya neema, tumaini moja lipo: ni Mwanangu, Mungu aliyezaliwa na Mungu. Maneno yake ni mbegu ya uzima wa milele: Yanapopandwa katika roho njema, huleta matunda mengi. Mwanangu amechukua maumivu maana amepokea juu yake dhambi zenu.
Kwa
hiyo ninyi, wanangu, mitume wa upendo wangu, ninyi mnaoteswa: mjue kwamba maumivu yenu yatakuwa mwanga na utukufu. Wanangu, wakati mnapovumilia maumivu, wakati mnapoteswa, Mbingu huingia ndani yenu, nanyi mnawapa watu wote karibu nanyi Mbingu kidogo na matumaini mengi. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2017
“
W
anangu wapendwa! leo ninawaalika kuwa makarimu katika kujinyima, katika kufunga na katika sala
kwa
ajili ya wale wote wanaojaribiwa, nao ni ndugu zenu kina kaka na kina dada. Na hasa ninawaomba kusali
kwa
ajili ya makuhani na
kwa
wote waliojiweka wakfu ili
kwa
ari zaidi wampende Yesu, ili Roho Mtakatifu aijaze mioyo yao
kwa
furaha, ili watoe ushuhuda wa Mbingu na mafumbo ya kimbingu. Roho nyingi ipo katika dhambi
kwa
sababu hakuna wale wanaojitoa sadaka na kusali
kwa
wongofu wao. Mimi nipo pamoja nanyi nikiwaombeeni ili mioyo yenu ijazwe furaha. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninaongea nanyi kama Mama,
kwa
maneno rahisi, lakini yamejaa wingi wa upendo na wa bidii
kwa
wanangu, ambao
kwa
njia ya Mwanangu wamekabidhiwa kwangu. Mwanangu, ambaye anakuja kutoka umilele na hata sasa, anaongea nanyi
kwa
maneno ya uzima na anapanda upendo katika mioyo wazi.
Kwa
hiyo nawaomba, mitume wa upendo wangu: muwe na mioyo iliyo wazi sikuzote kurehemu na kusamehe. Wasameheni sikuzote wenzenu kama Mwanangu,
kwa
vile hivyo amani itakuwa ndani yenu. Wanangu, lindeni nafsi yenu, maana hiyo ndiyo ukweli wa pekee ulio wenu bila shaka. Mmeanza kusahau umuhimu wa familia. Familia haipaswi kuwa mahali pa mateso na maumivu, bali mahali pa uelewano na huruma. Familia wanaojaribu kuishi kama apendavyo Mwanangu, wanaishi wakipendana. Tangu alipokuwa angali mtoto, Mwanangu aliniambia ya kuwa watu wote kwake ni ndugu zake.
Kwa
hiyo kumbukeni, enyi mitume wa upendo wangu, watu wote mnaowaona ni kwenu familia yenu, ndugu kama apendavyo Mwanangu. Wanangu, msipoteze muda kufikiria na kuhangaikia mambo yajayo. Kitu chenu kimoja cha kuhangaikia kwenu kiwe vipi kuishi vema kila dakika kadiri ya Mwanangu, na tazama hiyo ndiyo ni amani! Wanangu, msisahau kabisa kuwaombea wachungaji wenu. Salini ili waweze kupokea watu wote kama wanao, ili, kama apendavyo Mwanangu, wawe kwao kama baba za kiroho. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2017
“
W
anangu wapendwa! Katika kipindi hiki cha neema ninawaalika kuwa sala. Wote mna matatizo, taabu, maumivu na wasiwasi. Watakatifu wawe kwenu mfano na onyo
kwa
utakatifu, Mungu atakuwa karibu nanyi na mtakuwa wapya
kwa
utafiti na wongofu wa binafsi. Imani itakuwa kwenu tumaini, na furaha itazaliwa katika mioyo yenu. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Novemba 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nikiwatazama hapa mmekusanyika kunizunguka, Mama yenu, ninaona nafsi safi nyingi. Ninawaona wanangu wengi wanaotafuta upendo na faraja lakini hakuna mtu anayewapa. Ninawaona hata wale wanaotenda mabaya maana hawana mifano myema, maana hawajamjua mwanangu. Mwanangu anawatuma ninyi kwangu, Mama, sawa
kwa
wote, niwafundisheni kupenda, ili muelewe ya kuwa ninyi ni ndugu. Ninatamani kuwasaidia. Mitume wa upendo wangu,
kwa
mwanangu yamtosha tamaa hai ya imani na upendo na atayakubali, lakini mnapaswa kustahili, kuwa na tamaa na mioyo wazi, Mwanangu huingia katika mioyo wazi. Mimi kama Mama ninatamani kwamba mjue Mwanangu katika kweli: Mungu aliyezaliwa na Mungu, kwamba mjue ukuu wa Upendo wake, ambao mnahitaji. Yeye amezichukua juu yake dhambi zenu, ameupata Ukombozi wenu, na badala yake anaomba mpendane ninyi
kwa
ninyi. Mwanangu ni upendo, Yeye anawapenda watu wote bila tofauti, watu wote wa nchi zote, wa mataifa yote. Ikiwa ninyi, wanangu, mngeishi upendo wa Mwanangu, ufalme wake ungekwisha kuwa duniani.
Kwa
hiyo, Mitume wa upendo wangu, salini, salini ili Mwanangu na upendo wake wawe ndani yenu nanyi muweze kuwa mfano wa upendo na muweze kuwasaidia wote wale ambao hawajamjua Mwanangu. Msisahau kamwe kwamba Mwanangu, mmoja na utatu, anawapendeni. Pendeni na wombeeni wachungaji wenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2017
“
W
anangu wapendwa! Katika kipindi hiki cha neema ninawaalika kusali. Salini na tafuteni amani, wanangu. Yeye aliyekuja hapa duniani awatoe amani, pasipo kuwabagua kuwa ninyi ni nani na ni kitu gani - Yeye, Mwanangu, ndugu yenu,
kwa
njia yangu anawaalika kuongoka maana pasipo Mungu hamna baadaye wala uzima wa milele.
Kwa
hiyo aminini, salini na isheni katika neema na mkingojea mkutano wenu wa binafsi pamoja naye. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninawaelekea ninyi kama Mama yenu, Mama wa wenye haki, Mama wa wale wanaopenda na kuteseka, Mama wa watakatifu. Wanangu, ninyi pia mnaweza kuwa watakatifu: ni juu yenu. Watakatifu ni wale wanaompenda Baba wa Mbinguni kupita kiasi, wale wanaompenda kupita chochote.
Kwa
hivyo, wanangu, jaribuni daima kuboreka. Kama ninyi mnajaribu kuwa wema, mtaweza kuwa watakatifu, hata kama hamfikiri hiyo juu yenu. Kama mnafikiri kuwa wema, ninyi sio wanyenyekevu na kiburi huwatenga kutoka utakatifu. Katika ulimwengu huu wa wasiwasi, umejaa vitisho, mikono yako, mitume wa upendo wangu, inapaswa kuwa imenyoshwa katika maombi na rehema. Kwangu, wanangu, nipeni zawadi ya Rozari, mawaridi ninayopenda sana! Mawaridi yangu ni maombi yenu msemayo
kwa
moyo wote, na sio yale msemayo
kwa
midomo yenu tu. Mawaridi yangu ni matendo yenu ya maombi, imani na upendo. Wakati alipokuwa mtoto, mwanangu aliniambia kwamba watoto wangu watakuwa wengi na wataniletea mawaridi mengi. Sikuelewa, sasa najua kwamba ninyi ni watoto wale, wanaoniletea mawaridi wakati mnapompenda mwanangu kupita yote, wakati mnaposali
kwa
moyo wote, wakati mnapowasaidia walio maskini zaidi. Hayo ndiyo mawaridi yangu! Hii ndiyo imani, inayosababisha kila kitu katika maisha kifanyike
kwa
upendo; na kiburi hakijulikani; na muwe tayari daima, kusamehe upesi, bila kuhukumu na daima mjaribu kuelewa ndugu yako.
Kwa
hiyo, mitume wa upendo wangu, muwaombeeni wale wasiojua kupenda, wale wasiowapenda, wale waliowatenda mabaya, wale ambao hawakujua upendo wa Mwanangu. Wanangu, ninawaomba haya,
kwa
sababu kumbukeni: kuomba maana yake ni kupenda na kusamehe. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2017
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaletea Mwanangu Yesu, ili awajalieni amani Yake na baraka Yake. Wanangu wapendwa, ninawaalika ninyi nyote kuishi na kushuhudia neema na zawadi mlizozipokea. Msiogope!Salini ili Roho Mtakatifu awapeni nguvu ya kuwa mashahidi wenye furaha na watu wa amani na matumaini. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, wakati duniani upendo unapopunguka, wakati njia ya wokovu haipatikani, Mimi, Mama yenu, naja kuwasaidieni kujua imani ya kweli, iliyo hai na ya kina, na kuwasaidieni kupenda kabisa. Kama Mama ninatamani mpendane, muwe wema na safi. Ni hamu yangu muwe wenye haki na mpendane. Wanangu, muwe wafurahivu rohoni, muwe safi, muwe watoto. Mwanangu alisema kwamba anapenda kukaa kati ya wenye mioyo safi, maana wenye mioyo safi ni daima vijana na wafurahivu. Mwanangu aliwaambieni msameheane na mpendane. Najua kwamba si rahisi sikuzote. Mateso husababisha kukua rohoni. Ili kukua rohoni kadiri iwezekanavyo, lazima msamehe na kupenda
kwa
dhati na
kwa
kweli. Wana wangu wengi duniani hawamjui Mwanangu, hawampendi. Lakini ninyi mnaompenda Mwanangu na kumchukua moyoni salini, salini, na mkisali mumhisi Mwanangu karibu yenu. Nafsi yenu ipumue Roho yake! Mimi nipo kati yenu na kuongea juu ya mambo madogo na makubwa. Sitachoka kuwasimulieni habari ya Mwanangu, aliye upendo wa kweli.
Kwa
hiyo, wanangu, nifungulieni mioyo yenu, acheni niwaongoze kama mama. Muwe mitume wa upendo wa Mwanangu na wangu. Kama Mama nawasihi: msisahau wale walioitwa na Mwanangu wawaongoze. Wachukueni moyoni na muwaombee. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2018
“
W
anangu wapendwa! Kipindi hiki kiwe kwenu kipindi cha sala ili Roho Mtakatifu,
kwa
njia ya sala, ashuke juu yenu na awape wongofu. Fungueni mioyo yenu na someni Maandiko Matakatifu ili,
kwa
njia ya ushahidi, ninyi pia muweze kuwa karibu zaidi na Mungu. Wanangu, tafuteni hasa Mungu na vitu vya Mungu na acheni duniani vile vya dunia, maana Shetani huwavuta
kwa
mavumbi na dhambi. Ninyi mnaalikwa katika njia ya utakatifu na mmeumbwa
kwa
ajili ya Mbingu. Tafuteni,
kwa
hiyo, Mbingu na vitu vya mbinguni. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninyi ambao Mwanangu anawapenda, ninyi ambao mimi ninawapenda, msiruhusu ubinafsi, kujipenda wenyewe, zitawale duniani. Msiache upendo na wema zifichwe. Ninyi mnaopendwa, mliojua upendo wa Mwanangu, kumbukeni ya kuwa kupendwa maana yake ni kupenda. Wanangu, muwe na imani! Mnapokuwa na imani mnafurahi na mkaeneza amani, nafsi yenu inaruka
kwa
shangwe: katika nafsi ile yumo Mwanangu. Mnapojitolea wenyewe
kwa
ajili ya imani, mnapojitolea wenyewe
kwa
ajili ya upendo, mnapowafanyia watu wengine mema, Mwanangu hutabasamu katika nafsi yenu. Mitume wa upendo wangu, mimi, kama Mama, ninawaelekea, ninawakusanya kunizunguka na ninataka kuwaongozeni katika njia ya upendo na imani, katika njia ya kufika kwenye Nuru ya ulimwengu. Nipo hapa
kwa
upendo na
kwa
imani,
kwa
maana,
kwa
baraka yangu ya kimama, nataka kuwapeni matumaini na nguvu katika mwendo wenu,
kwa
sababu njia ya kuongoza
kwa
Mwanangu si rahisi: imejaa matendo ya kujinyima, ya kujitolea, ya kujidhabihu, ya kusamehe na ya upendo, upendo mwingi. Njia ile, lakini, hupata amani na furaha. Wanangu, msisadiki sauti za uongo zinazosemesha
kwa
maneno yasiyo na ukweli, mwanga usio wa ukweli. Ninyi wanangu rudini
kwa
Maandiko! Ninawaangalieni
kwa
upendo kupita kiasi na,
kwa
neema ya Mungu, ninajidhihirisha kwenu. Wanangu, njoni pamoja nami, nafsi yenu iruke
kwa
shangwe! Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2018
“
W
anangu wapendwa! Katika kipindi hiki cha neema ninawaalika nyote kujifungua na kuishi amri ambazo Mungu aliwapeni ili,
kwa
njia ya sakramenti, ziwaongoze katika njia ya wongofu. Ulimwengu na vishawishi vya ulimwengu vinawajaribu; ninyi, wanangu, angalieni viumbe vya Mungu ambavyo katika uzuri na unyenyekevu Yeye aliwapa, na mpendeni Mungu, enyi wanangu, kuliko kila kitu naye atawaongoza katika njia ya wokovu. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Baba wa Mbinguni amenifanyia makuu, jinsi anavyowafanyia wale wote wanaompenda sana na
kwa
wema na uaminifu na wanaomtumikia
kwa
ibada. Wanangu, Baba wa Mbinguni anawapenda na
kwa
ajili ya upendo wake mimi nipo hapa pamoja nanyi. Ninasema nanyi:
kwa
nini hamtaki kuona ishara? Pamoja naye yote ni rahisi zaidi: hata mateso, tunayoishi pamoja naye, ni mepesi zaidi, maana kuna imani. Imani husaidia mateso, na maumivu pasipo imani huongoza katika kukata tamaa. Mateso tunayoyaishi na kuyatolea
kwa
Mungu, huinua mtu. Je, Mwanangu hakuukomboa ulimwengu
kwa
njia ya mateso yake makali? Mimi, kama mama yake, katika maumivu na mateso nilikaa pamoja naye, kama vile ninavyokaa pamoja nanyi. Wanangu, mimi nipo pamoja nanyi katika maisha: katika maumivu na mateso, katika furaha na upendo.
Kwa
hiyo muwe na matumaini: matumaini ndiyo yanayotuwezesha kuelewa ya kuwa hapa, kwenye mateso, ni uhai. Wanangu, mimi nasema nanyi; sauti yangu inasema na nafsi yenu, Moyo wangu unasema na moyo wenu: Enyi, mitume wa upendo wangu, Moyo wangu wa kimama jinsi gani unavyowapenda. Mambo haya nataka kuwafundisha. Jinsi gani Moyo wangu unataka muwe wakamilifu, lakini mtakuwa hivyo tu wakati nafsi, mwili na upendo yatakapoungana ndani yenu. Kama wanangu nawaombeni: salini sana
kwa
ajili ya Kanisa na
kwa
wahudumu wake,
kwa
wachungaji wenu, ili Kanisa liwe kama Mwanangu anavyolitaka: safi kama maji ya chemchemi na limejaa upendo. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Machi 2018
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika kukaa pamoja nami katika kusali, wakati huu wa neema, ambapo giza linapigana na mwagaza. Wanangu, salini, muungame dhambi zenu mkaanzishe maisha mapya katika neema. Kateni shauri
kwa
Mungu naye atawaongoza kuelekea utakatifu na msalaba utakuwa kwenu ishara ya ushindi na matumaini. Mjivunie kubatizwa na mshukuruni moyoni mwenu kushika mpango wa Mungu. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
Next>>