Our Lady of Medjugorje Messages containing 'kwa'
Total found:
219
Ujumbe, 25 Novemba 2019
“
W
anangu wapendwa, wakati huu uwe kwenu wakati wa sala. Bila Mungu hamwezi kuwa na amani.
Kwa
hiyo, wanangu, salini
kwa
ajili ya amani katika mioyo yenu na katika familia zenu ili Yesu aweze kuzaliwa ndani yenu na kuwapeni upendo wake na baraka yake. Ulimwengu uko katika vita
kwa
sababu mioyo imejaa machukio na wivu. Wanangu, wasiwasi unaonekana katika macho yenu
kwa
sababu hamkuruhusu Yesu kuzaliwa katika maisha yenu. Mtafuteni, ombeni na Yeye atajitoa kwenu katika yule Mtoto aliye furaha na amani. Mimi niko pamoja nanyi na ninasali pamoja nanyi. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninapowatazama ninyi mnaopenda Mwanangu, furaha inajaza Moyo wangu. Ninawabariki
kwa
baraka ya kimama. Pamoja na baraka ya kimama ninawabariki hata wachungaji wenu: ninyi mnaotangaza maneno ya Mwanangu, mnaobariki
kwa
mikono yake na mnaompenda hata kuwa tayari kufanya
kwa
furaha kila sadaka
kwa
ajili yake. Ninyi mfuateni Yeye, aliyekuwa Mchungaji wa kwanza, Mmisionari wa kwanza. Wanangu, mitume wa upendo wangu, kuishi na kufanya kazi
kwa
ajili ya wengine,
kwa
wale wote mnaopenda
kwa
njia ya Mwanangu, ni furaha na faraja ya maisha ya kidunia. Ikiwa
kwa
njia ya sala, upendo na sadaka Ufalme wa Mungu ni katika mioyo yenu, hapo
kwa
ninyi maisha ni yenye furaha na matulivu. Katikati ya wale wanaompenda Mwanangu na wanaopendana
kwa
ajili yake, maneno si ya lazima. Kutazamana kwatosha ili kusikia maneno yasiyonenwa na hisia zisizoonyeshwa. Pale panapotawala upendo, wakati hauna maana tena. Sisi ni pamoja nanyi! Mwanangu anawajua na kuwapenda. Upendo ni kilichowaongoza kwangu na,
kwa
njia ya upendo huu, mimi nitakuja kwenu na nitawaambieni kazi za wokovu. Ninataka ya kuwa wana wangu wote wawe na imani na wahisi upendo wangu wa kimama unaowaongoza
kwa
Yesu.
Kwa
hiyo ninyi, wanangu, ko kote mwendako angazeni
kwa
upendo na
kwa
imani, kama mitume wa upendo. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2019
“
W
anangu wapendwa, Nawaletea ninyi Mwanangu Yesu ili awabariki na kuwafunulia Upendo wake utokao mbinguni. Moyo wenu unatamani amani inayopungua zaidi na zaidi duniani.
Kwa
sababu hiyo watu wako mbali na Mungu, nafsi zinaumwa na zinaelekea kifo cha kiroho. Mimi nipo pamoja nanyi, wanangu, niwaongoze kwenye njia hii ya wokovu ambayo Mungu anawaiteni. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2020 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, najua kuwepo katika maisha yenu na mioyo yenu. Nahisi upendo wenu, nasikia sala zenu na kuzipeleka
kwa
Mwanangu. Lakini, wanangu, mimi nataka
kwa
njia ya upendo wa kimama, kuwepo katika maisha ya wanangu wote. Nataka kukusanya karibu yangu wanangu wangu wote, chini ya joho langu la kimama.
Kwa
hiyo ninawaalika ninyi na kuwaiteni mitume wa upendo wangu, il mnisaidie. Wanangu, Mwanangu aliyatamka maneno haya: "Baba yetu”, Baba yetu uliye popote na katika mioyo yetu,
kwa
sababu ataka kuwafundisha kusali
kwa
maneno na
kwa
hisia zenu. Ataka muwe bora zaidi kila siku, muishi upendo wenye rehema ulio sala na sadaka isiyo na mipaka
kwa
ajili ya wengine. Wanangu mpeni Mwanangu upendo
kwa
jirani; mpeni jirani wenu maneno ya faraja, ya huruma na matendo ya haki. Yote mliyoyatoa
kwa
wengine, enyi mitume wa upendo wangu, Mwanangu anayapokea kama zawadi. Nami ni pamoja nanyi
kwa
sababu Mwanangu ataka kwamba upendo wangu, ulio kama mwali wa nuru, uzihuishe nafsi zenu, uwasaidie katika kutafuta amani na uheri wa milele.
Kwa
hiyo, wanangu, pendaneni, na muunganishwe
kwa
njia ya Mwanangu, ili muwe wana wa Mungu ambao wote pamoja
kwa
moyo uliojaa, wazi na safi mkisema
kwa
pamoja “Baba yetu” pasipo kuogopa! Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2020
“
W
anangu wapendwa, Leo ninawaalika kusali tena zaidi ili msikie katika mioyo yenu utakatifu wa msamaha. Katika familia lazima kuwepo utakatifu
kwa
sababu enyi wanangu, ulimwengu hauna wakati ujao bila upendo na utakatifu,
kwa
sababu katika utakatifu na katika furaha ninyi mjitolee
kwa
Mungu Mwumbaji anayewapendeni
kwa
upendo mkubwa sana. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2020 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nilichaguliwa kuwa mama wa Mungu na mama yenu,
kwa
maamuzi na upendo wa Bwana, lakini pia
kwa
mapenzi yangu,
kwa
upendo wangu usio na kifani kwake Baba wa mbinguni na
kwa
imani yangu yote Kwake. Mwili wangu ulikuwa kikombe cha Mungu Mtu. Nilikuwa mtumishi wa ukweli, wa upendo na wokovu kama vile nilivyo sasa katikati yenu, ili kuwaalika, wanangu, mitume wa upendo wangu, kuwa waletaji ukweli, ili kuwaalika,
kwa
njia ya utashi na upendo yenu kumwelekea Mwanangu, ili kueneza maneno Yake, maneno ya wokovu na kuyaonyesha,
kwa
vitendo vyenu,
kwa
wale wote ambao hawajamjua mwanangu na upendo Wake. Nguvu mtaipata katika Ekaristi: Mwanangu awalisheni
kwa
mwili Wake na kuwaimarisha
kwa
damu Yake. Wanangu, wekeni mikono yenu pamoja
kwa
sala na tazameni kuelekea msalaba
kwa
ukimya.
Kwa
jinsi hii mtapata imani ili muweze kuieneza, mtapata ukweli ili muweze kuupambanua, mtapata upendo ili muweze kuelewa namna ya kupenda
kwa
uhakika. Wanangu, mitume wa upendo wangu, wekeni mikono yenu pamoja
kwa
sala na tazameni kuelekea msalaba: katika msalaba tu kuna wokovu. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2020
“
W
anangu wapendwa, Katika kipindi hiki cha neema nataka kuona nyuso zenu zigeuke katika sala. Ninyi mmejaa mahangaiko ya kidunia kiasi kwamba hamuoni hata ujio wa majira ya kuchipua
kwa
mimea. Wanangu, mnaalikwa
kwa
toba na
kwa
sala. Kama viumbe vya asili vinapigana katika kimya
kwa
maisha mapya, hivyo hata ninyi mnaalikwa kujifungua katika sala
kwa
Mungu ambaye kwake mtapata amani na joto la jua la kipindi cha kuchanua
kwa
mimea katika mioyo yenu. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2020 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, upendo wenu safi na wa kweli unavuta Moyo wangu wa kimama. Imani yenu na usadiki wenu katika Baba wa mbinguni ni mawaridi yenye harufu nzuri mnayonitolea: shada la mawaridi mazuri sana, lililotengenezwa
kwa
sala zenu,
kwa
matendo ya rehema na ya upendo. Mitume wa upendo wangu, ninyi mnaojaribu kumfuata Mwanangu pasipo unafiki na
kwa
moyo safi, ninyi ambao pasipo unafiki mnampenda, muwe ninyi wenyewe kusaidia: muwe mfano
kwa
wale ambao hawajajua upendo wa Mwanangu. Lakini, wanangu, siyo
kwa
maneno tu, bali hata
kwa
matendo na hisia safi, ambayo
kwa
njia yake mnamtukuza Baba wa mbinguni. Mitume wa upendo wangu, ni wakati wa kukesha na ninawaombeni upendo; na msihukumu mtu yeyote,
kwa
maana Baba wa mbinguni atahukumu wote. Ninawaombeni mpende, na mueneze ukweli,
kwa
maana ukweli ni wa kale: Ukweli siyo mpya, Ukweli ni wa milele, Ukweli ndiyo ukweli! Ukweli unatolea ushuhuda wa umilele wa Mungu. Bebeni mwanga wa Mwanangu na mpasue giza ambalo linataka kuwakandamiza zaidi na zaidi. Msiwe na hofu:
kwa
ajili ya neema na upendo wa Mwanangu, mimi nipo pamoja nanyi! Ninawashukuru. ”
”
Ujumbe, 25 Machi 2020
“
W
anangu wapendwa, katika miaka hii yote mimi nipo pamoja nanyi ili kuwaongoza kwenye njia ya wokovu. Rudieni
kwa
Mwanangu, rudieni katika sala na mfungo. Wanangu, mwachieni Mungu aongee na mioyo yenu
kwa
sababu shetani anatawala na anatamani kuangamiza maisha yenu na dunia mnamotembelea. Muwe na ujasiri na amueni kuwa watakatifu. Mtaona wongofu katika mioyo yenu na katika familia zenu, sala itasikilizwa, Mungu atayapokea maombi yenu na kuwapa amani. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwabariki nyote
kwa
baraka yangu ya kimama. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2020
“
W
anangu wapendwa, wakati huu uwe kwenu himizo
kwa
wongofu wenu binafsi. Wanangu, ombeni katika upweke Roho Mtakatifu ili iwaimarishe katika imani na katika kumsadiki Mungu ili kuweza kuwa mashahidi wa upendo ambao Mungu anawapa kupitia uwepo wangu. Wanangu, msiruhusu majaribu yafanye mioyo yenu kuwa migumu na sala kuwa kama jangwa. Muwe mwangi wa upendo wa Mungu na mshuhudieni Yesu Aliyefufuka
kwa
njia ya maisha yenu. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawapenda nyote
kwa
upendo wangu wa kimama. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu”.
”
Ujumbe, 25 Mei 2020
“
W
anangu wapendwa, Salini pamoja Nami
kwa
maisha mapya ya ninyi nyote. Wanangu, katika mioyo yenu mnajua ni nini lazima kibadilike: rudini
kwa
Mungu na
kwa
Amri Zake ili Roho Mtakatifu aweze kugeuza maisha yenu na uso wa dunia hii, inayohitaji kufanywa upya katika Roho. Wanangu, muwe sala
kwa
wale wote wasiosali, muwe furaha
kwa
wale wote wasioona njia ya kutokea, muwe waletaji mwanga katika giza za wakati huu wa wasiwasi. Salini na ombeni msaada na ulinzi wa watakatifu ili ninyi pia muweze kutamani mbingu na mambo halisi ya kimbingu. Mimi nipo pamoja nanyi nikiwalinda na kuwabariki nyote
kwa
baraka yangu ya kimama. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2020
“
W
anangu wapendwa, ninasikiliza maombi yenu na sala zenu na ninawaombea
kwa
mwanangu Yesu aliye njia, kweli na uzima. Wanangu, rudieni kusali na fungueni mioyo yenu katika wakati huu wa neema na shikeni njia ya wongofu. Maisha yenu yanapita na hayana maana bila Mungu.
Kwa
hiyo mimi ni pamoja nanyi niwaongoze kuelekea utakatifu wa maisha ili kila mmoja wenu agundue furaha ya kuishi. Wanangu, ninawapenda wote na kuwabariki
kwa
baraka yangu ya kimama. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2020
“
W
anangu wapendwa, Katika wakati huu wa wasiwasi ambapo ibilisi anavuna nafsi ili kuwavuta kwake, niwaalika
kwa
sala ya kudumu ili katika sala mtambue Mungu wa upendo na wa matumaini. Wanangu, shikeni msalaba katika mikono yenu. Na uwatie moyo
kwa
kuwa upendo unashinda sikuzote hasa sasa ambapo msalaba na imani yamekataliwa. Ninyi muwe mwangwi na mfano
kwa
njia ya maisha yenu ya kuwa imani na matumaini bado hai na ulimwengu mpya wa amani unawezekana. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombea mbele ya mwanangu Yesu. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2020
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati wa neema. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaalika tena, wanangu, mrudieni Mungu na
kwa
kusali ili sala iwe furaha kwenu. Enyi wanangu hamtakuwa na wakati ujao wala amani mpaka katika maisha yenu mtakapoanza kuishi maongezi ya binafsi na badiliko katika mema. Maovu yatakoma na amani itatawala katika mioyo yenu na katika ulimwengu.
Kwa
hiyo, wanangu, salini, salini, salini. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombea
kwa
mwanangu Yesu
kwa
ajili ya kila mmoja wenu. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Mimi ni pamoja nanyi
kwa
muda mrefu
kwa
maana Mungu ni mkuu katika upendo wake na katika uwepo wangu. Wanangu, ninawaalika kurudi
kwa
Mungu na
kwa
sala. Kipimo cha kuishi kwenu kiwe upendo na msisahau, wanangu, kwamba maombi na kufunga hufanya miujiza ndani yenu na kuwazunguka. Yote mnayoyafanya yawe
kwa
ajili ya utukufu wa Mungu na hapo Mbingu itajaza moyo wenu na furaha mkahisi ya kuwa Mungu anawapenda na kunituma ili kuokoa ninyi na Dunia ambayo juu yake mnaishi. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2020
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu ninawaita kumrudia Mungu na sala. Waiteni watakatifu wote wawasaidie ili wawe mfano na msaada kwenu. Shetani ni mwenye nguvu na anapigania kuivutia kwake mioyo mingi zaidi awezavyo. Anataka vita na chuki.
Kwa
sababu hiyo Mimi ni pamoja nanyi muda mrefu ili niwaongoze kwenye njia ya wokovu,
kwa
Yule aliye njia, kweli na uzima. Wanangu, rudini
kwa
upendo kumwelekea Mungu naye atakuwa nguvu yenu na kimbilio lenu. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Huu ni wakati wa upendo, wa uchangamfu, wa sala na wa furaha. Salini, wanangu, ili Mtoto Yesu azaliwe katika mioyo yenu. Fungueni mioyo yenu
kwa
Yesu anayejitoa
kwa
kila mmoja wenu. Mungu amenialika ili mimi niwe furaha na matumaini katika wakati huu nami ninawaambia: bila Mtoto Yesu hamna wala huruma wala hisia ya Mbingu, zinazofichika katika yule Mtoto mchanga.
Kwa
hiyo, wanangu, fanyeni kazi juu ya nafsi zenu wenyewe. Mkisoma Maandiko Matakatifu, mtagundua kuzaliwa
kwa
Yesu na furaha kama ile ya siku za kwanza ya matokeo ya Medjugorje iliyotolea
kwa
ubinadamu. Historia itakuwa ukweli, ambao hata leo unajirudia ndani yenu na kuwazunguka. Fanyeni kazi na jengeni amani
kwa
njia ya sakramenti ya Kitubio. Jipatanisheni na Mungu, wanangu, na mtaona miujiza inawazunguka. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mtoto Yesu anayewaletea amani, Yule aliye wakati uliopita, wakati wa sasa na wakati ujao wa kuishi kwenu. Wanangu, msiruhusu imani yenu na matumaini yenu katika wakati ujao ulio bora yazimike,
kwa
maana ninyi mmechaguliwa
kwa
kuwa mashahidi wa matumaini katika kila hali.
Kwa
ajili hiyo mimi ni hapa pamoja na Yesu ili awabariki
kwa
amani yake. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2021
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huo ninawaalika kusali, kufunga na kujikana ili muweze kuwa wenye nguvu zaidi katika imani. Huu ni wakati wa mwamko na wa kuzaliwa upya. Kama vitu vya asili vinavyojitoa nanyi wanangu, fikirini juu ya mambo mliyopokea. Muwe waletaji wa amani na wa upendo wenye furaha ili kuishi vizuri duniani. Tamanini Mbingu
kwa
sababu Mbinguni hakuna wala huzuni wala machukio.
Kwa
hiyo, wanangu, amueni tena kuongoka, na utakatifu utawale katika maisha yenu. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2021
“
W
anangu wapendwa! Mungu ameniruhusu kuwa pamoja nanyi leo pia
kwa
kuwaalika kusali na kufunga. Ishini wakati huu wa neema na muwe mashahidi wa tumaini maana, ninawaambia tena wanangu,
kwa
kusali na kufunga hata vita vinaweza kuisha. Wanangu, aminini na kuishi katika imani na
kwa
imani wakati huu wa neema na Moyo wangu usio na dhambi ya asili haumwachi yeyote kati yenu katika wasiwasi ikiwa ananikimbilia. Ninawaombea mbele ya Yeye aliye juu na ninasali ili amani iwepo katika mioyo yenu na
kwa
ajili ya tumaini katika wakati ujao. Asanteni
kwa
kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
Next>>