Our Lady of Medjugorje Messages containing 'mahangaiko'
Total found:
6
Ujumbe, 2 Septemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawapendeni, ninyi nyote, watoto wangu nyote, muwe wote moyoni mwangu, ninyi nyote mmepata upendo wangu wa kimama na ninatamani kuwaongoza nyote ili mjue furaha ya Mungu. Kwa hiyo nawaalikeni: nahitaji mitume wanyenyekevu ambao, kwa moyo mkunjufu, wanapokea Neno la Mungu na ambao wako tayari kuwasaidia watu wengine ili, kwa njia ya Neno la Mungu, waelewe maana ya maisha yao. Ili muweze kufanya hayo, wanangu, yawapasa, kwa njia ya kusali na kufunga, kusikiliza kwa moyo mkunjufu na kujifunza kujidhili au kujinyenyekesha. Yawapasa kujifunza kukataa yote yanayowatenganisha na Neno la Mungu na kutamani tu yanayowakaribisha. Msiogope, mimi nipo hapa. Ninyi si peke yenu. Namwomba Roho Mtakatifu ili awafanye wapya, ili awaimarishe. Namwomba Roho Mtakatifu, ili mkisaidia wengine, muweze kujiponya nyinyi wenyewe. Naomba ili, kwa njia yake, muwe wana wa Mungu na mitume wangu.
”
Kisha kwa
mahangaiko
makubwa Bikira Maria alisema:
“
K
wa ajili ya Yesu, kwa ajili ya mwanangu, pendeni wale ambao Yeye aliwaita mkitamani baraka ya mikono ile ambayo Yeye tu ameyaweka wakfu. Msiyaruhusu maovu yatawale. Nawaalikeni tena: ni kwa njia ya wachungaji wangu tu moyo wangu utashinda. Msiyaruhusu maovu yawatenganisheni na wachungaji wenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nimekuja kwenu, katikati yenu, ili mnipe
mahangaiko
yenu, niweze kuyaleta mbele ya Mwanangu na kuwaombeeni kwake kwa manufaa yenu. Najua kuwa kila mmoja wenu ana
mahangaiko
yake, majaribu yake. Kwa hiyo kwa moyo wa kimama nawaalikeni: Njooni kwenye Meza ya Mwanangu! Yeye humega mkate kwa ajili yenu, huwapa Yeye mwenyewe. Huwapa matumaini. Anawaomba kuwa na imani zaidi, matumaini zaidi, utulivu zaidi. Anawaomba mpigane ndani yenu dhidi ya ubinafsi, hukumu na udhaifu wa kibinadamu. Kwa hiyo Mimi, kama Mama, nawaambieni: salini, maana sala huwapa nguvu ya kupigana ndani yenu. Mwanangu, alipokuwa mtoto, aliniambia mara nyingi ya kuwa wengi watanipenda na kuniita "Mama". Mimi hapa, katikati yenu, nasikia upendo na kuwashukuru! Kwa njia ya upendo huu namwomba Mwanangu ili hakuna hata mmoja wenu, wanangu, arudiye nyumbani jinsi alivyokuja. Ili mlete matumaini, rehema na upendo kadiri muwezavyo; ili muwe mitume wa upendo wangu, wanaoshuhudia kwa maisha yao kwamba Baba aliye Mbinguni ni chemchemi ya uzima si ya mauti. Wanangu wapendwa, nawaomba tena kwa moyo wa kimama: waombeeni wateule wa Mwanangu, kwa ajili ya mikono yao iliyobarikiwa, kwa ajili ya wachungaji wenu, ili waweze kumhubiri Mwanangu kwa upendo mwingi wawezavyo, na hivyo kusababisha wongofu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, maneno yangu ni manyofu lakini yamejaa upendo wa kimama na
mahangaiko
. Wanangu, juu yenu vivuli vya giza na vya udanganyifu vinaenea zaidi na zaidi, mimi ninawaiteni kuelekea mwanga na ukweli, mimi ninawaita kuelekea Mwanangu. Yeye peke yake huweza kugeuza kukata tamaa na maumivu yetu kuwa amani na utulivu, Yeye peke yake huweza kutoa matumaini katika maumivu makali sana. Mwanangu ni uzima wa ulimwengu, kwa kadiri mtakavyomjua, ndivyo mtakavyomkaribia na kumpenda maana Mwanangu ni upendo, na upendo unageuza yote. Yeye hufanya la ajabu hata neno lisilo la maana bila upendo machoni penu. Kwa hiyo nawaambieni tena ya kwamba mnapaswa kupenda sana ikiwa mnatamani kukua kiroho. Najua, enyi mitume wa upendo wangu, kwamba si rahisi sikuzote, lakini, wanangu, hata njia ngumu ni njia zinazoongoza kwenye ukuaji wa kiroho, wa kiimani na kwa Mwanangu. Wanangu, salini, mfikirie Mwanangu, nyakati zote za siku zenu inueni nafsi zenu kwake nami nitakusanya sala zenu kama maua kutoka bustani nzuri kuliko zote na kumpa Mwanangu. Muwe hakika mitume wa upendo wangu, wapeni wote upendo wa Mwanangu, muwe bustani zenye maua mazuri kuliko yote. Kwa njia ya sala saidieni wachungaji wenu ili waweze kuwa baba za kiroho waliojaa upendo kwa watu wote. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2020
“
W
anangu wapendwa, Katika kipindi hiki cha neema nataka kuona nyuso zenu zigeuke katika sala. Ninyi mmejaa
mahangaiko
ya kidunia kiasi kwamba hamuoni hata ujio wa majira ya kuchipua kwa mimea. Wanangu, mnaalikwa kwa toba na kwa sala. Kama viumbe vya asili vinapigana katika kimya kwa maisha mapya, hivyo hata ninyi mnaalikwa kujifungua katika sala kwa Mungu ambaye kwake mtapata amani na joto la jua la kipindi cha kuchanua kwa mimea katika mioyo yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2022
“
W
anangu wapendwa! Ninawatazama na ninamshukuru Mungu kwa kila mmoja wenu, kwa sababu ameniruhusu niwe nanyi tena ili kuwasihi katika utakatifu. Wanangu amani inavurugika na shetani anataka
mahangaiko
. Kwa hiyo maombi yenu yawe na nguvu zaidi ili kila roho chafu ya utengano na vita itulie. Iweni wajenzi wa amani na wachukuaji wa Aliyefufuka ndani yenu na karibu nanyi ili mema yapate kushinda katika kila mtu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2022
“
W
anangu wapendwa! Salini ili Roho Mtakatifu awaangazie kuwa watafutaji wa Mungu wenye furaha na mashahidi wa upendo usio na kikomo. Mimi niko pamoja nanyi, wanangu, na ninawaalika ninyi nyote tena: jitieni moyo na mshuhudie matendo mema ambayo Mungu anafanya ndani yenu na kupitia kwenu. Furahini katika Mungu. Mtendeeni mema jirani yenu ili mpate afya njema duniani na ombeeni amani ambayo inatishiwa kwa sababu shetani hutaka vita na
mahangaiko
. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose