Our Lady of Medjugorje Messages containing 'makusudi'
Total found:
2
Ujumbe, 25 Septemba 2019
“
W
anangu wapendwa, Leo ninawaalika kusali kwa ajili ya
makusudi
yangu ili niweze kuwasaidia. Wanangu, salini Rosari mkitafakari mafumbo ya Rosari maana hata ninyi katika maisha yenu mnapitia furaha na maumivu. Kwa njia hii mtageuza mafumbo katika maisha yenu maana maisha ni fumbo hadi mtakapoyaweka katika mikono ya Mungu. Hivyo mtakuwa na mang'amuzi ya imani kama Petro aliyemkuta Yesu na Roho Mtakatifu aliyoijaza roho yake. Hata ninyi, wanangu, mnaalikwa kushuhudia mkiishi upendo ambao kwao siku kwa siku Mungu anawajaza kwa njia ya uwepo wangu. Kwa hiyo, wanangu, muwe wazi na salini kwa moyo katika imani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2022
“
W
anangu wapendwa! Ninafurahi pamoja nanyi na kuwashukuru kwa kila sadaka na sala ambayo mlitolea kwa
makusudi
yangu. Wanangu, msisahau ya kuwa ninyi ni muhimu katika mpango wangu wa wokovu wa wanadamu. Rudeni kwa Mungu na kwa sala ili Roho Mtakatifu atende kazi ndani yenu na kupitia ninyi. Wanangu, Mimi ni pamoja nanyi hata katika siku hizi ambapo shetani anapiga kwa vita na kwa machukio. Utengano ni wenye nguvu na maovu yatenda kazi katika mwanadamu kama hajatenda bado mpaka leo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose