Our Lady of Medjugorje Messages containing 'matakatifu'
Total found:
5
Ujumbe, 25 Aprili 2013
“
W
anangu wapendwa! Salini, salini, mwendelee kusali ili mioyo yenu ifungukie kupokea imani jinsi ua linavyofunguka kuelekea mianga ya joto la jua. Huo ni wakati wa neema ambao Mungu anawajalia kwa njia ya uwepo wangu, lakini ninyi mpo mbali na moyo wangu. Kwa hiyo nawaalikeni kwa uongofu binafsi na kwenye sala katika familia zenu. Maandiko
matakatifu
yawe daima kichocheo chenu. Nawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2018
“
W
anangu wapendwa! Kipindi hiki kiwe kwenu kipindi cha sala ili Roho Mtakatifu, kwa njia ya sala, ashuke juu yenu na awape wongofu. Fungueni mioyo yenu na someni Maandiko
Matakatifu
ili, kwa njia ya ushahidi, ninyi pia muweze kuwa karibu zaidi na Mungu. Wanangu, tafuteni hasa Mungu na vitu vya Mungu na acheni duniani vile vya dunia, maana Shetani huwavuta kwa mavumbi na dhambi. Ninyi mnaalikwa katika njia ya utakatifu na mmeumbwa kwa ajili ya Mbingu. Tafuteni, kwa hiyo, Mbingu na vitu vya mbinguni. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Huu ni wakati wa upendo, wa uchangamfu, wa sala na wa furaha. Salini, wanangu, ili Mtoto Yesu azaliwe katika mioyo yenu. Fungueni mioyo yenu kwa Yesu anayejitoa kwa kila mmoja wenu. Mungu amenialika ili mimi niwe furaha na matumaini katika wakati huu nami ninawaambia: bila Mtoto Yesu hamna wala huruma wala hisia ya Mbingu, zinazofichika katika yule Mtoto mchanga. Kwa hiyo, wanangu, fanyeni kazi juu ya nafsi zenu wenyewe. Mkisoma Maandiko
Matakatifu
, mtagundua kuzaliwa kwa Yesu na furaha kama ile ya siku za kwanza ya matokeo ya Medjugorje iliyotolea kwa ubinadamu. Historia itakuwa ukweli, ambao hata leo unajirudia ndani yenu na kuwazunguka. Fanyeni kazi na jengeni amani kwa njia ya sakramenti ya Kitubio. Jipatanisheni na Mungu, wanangu, na mtaona miujiza inawazunguka. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2021
“
W
anangu wapendwa! Niko pamoja nanyi katika wakati huu wa rehema na ninawaalika nyote kuwa waleta amani na upendo katika ulimwengu huu, ambapo, wanangu, Mungu anawaalika kupitia Kwangu kuwa sala, upendo na kielelezo cha Paradiso, hapa duniani. Mioyo yenu na ijazwe na furaha na imani katika Mungu ili, wanangu, muwe na imani kamili katika mapenzi yake
matakatifu
. Hii ndiyo sababu mimi niko pamoja nanyi kwa sababu Yeye, Aliye Juu, ananituma kati yenu ili kuwahimiza ninyi kuwa na matumaini na mtakuwa waleta amani katika ulimwengu huu wenye wasiwasi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Karibuni Ujumbe, 25 Juni 2024
“
W
anangu wapendwa! Nafurahi pamoja nanyi na namshukuru Mungu kwa kunijalia kuwa nanyi ili kuwaongoza na kuwapenda. Wanangu, amani iko hatarini na familia inashambuliwa. Ninawaalika, wanangu, rudi kwenye sala ya familia. Wekeni Maandiko
Matakatifu
mahali panapoonekana na msome kila siku. Mpendeni Mungu kuliko vitu vyote ili muwe salama duniani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu”.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose