Our Lady of Medjugorje Messages containing 'mimi'
Total found:
129
Ujumbe, 25 Aprili 2021
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaalika kushuhudia imani yenu katika rangi za majira ya kuchipua, na iwe imani ya matumaini na ya ujasiri. Wanangu, imani yenu isitindike katika hali yoyote na hata katika wakati huu wa majaribio. Tembeeni kwa ujasiri pamoja na Kristo Mfufuka kuelekea Mbingu iliyo lengo lenu.
Mimi
ninaandamana nanyi katika mwendo huu wa utakatifu na kuweka ninyi nyote katika Moyo wangu Usio na dhambi ya asili. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2021
“
W
anangu wapendwa! Kwa furaha ninawaalika ninyi nyote, wanangu, mlioitikia wito wangu, kuwa furaha na amani. Kwa maisha yenu shuhudieni Mbingu ninayowaletea. Ni saa, wanangu, ya kuwa wonyesho wa upendo wangu kwa wote wale ambao hawapendi na mioyo yao imeshindwa na machukio. Msisahau:
mimi
ni pamoja nanyi na ninawaombea ninyi nyote karibu na mwanangu Yesu ili awapeni amani yake. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2021
“
W
anangu wapendwa! Niko pamoja nanyi katika wakati huu wa rehema na ninawaalika nyote kuwa waleta amani na upendo katika ulimwengu huu, ambapo, wanangu, Mungu anawaalika kupitia Kwangu kuwa sala, upendo na kielelezo cha Paradiso, hapa duniani. Mioyo yenu na ijazwe na furaha na imani katika Mungu ili, wanangu, muwe na imani kamili katika mapenzi yake matakatifu. Hii ndiyo sababu
mimi
niko pamoja nanyi kwa sababu Yeye, Aliye Juu, ananituma kati yenu ili kuwahimiza ninyi kuwa na matumaini na mtakuwa waleta amani katika ulimwengu huu wenye wasiwasi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2022
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaalika kurudia sala zenu za binafsi. Wanangu, msisahau ya kuwa shetani ni mwenye nguvu na hutaka kuvuta nafsi nyingi iwezekanavyo kwake. Kwa hivyo, ninyi kesheni katika sala na muwe na azimio katika kutenda mema.
Mimi
niko pamoja nanyi na ninawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2022
“
W
anangu wapendwa! Ninafurahi pamoja nanyi na kuwashukuru kwa kila sadaka na sala ambayo mlitolea kwa makusudi yangu. Wanangu, msisahau ya kuwa ninyi ni muhimu katika mpango wangu wa wokovu wa wanadamu. Rudeni kwa Mungu na kwa sala ili Roho Mtakatifu atende kazi ndani yenu na kupitia ninyi. Wanangu,
Mimi
ni pamoja nanyi hata katika siku hizi ambapo shetani anapiga kwa vita na kwa machukio. Utengano ni wenye nguvu na maovu yatenda kazi katika mwanadamu kama hajatenda bado mpaka leo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2022
“
W
anangu wapendwa! Salini ili Roho Mtakatifu awaangazie kuwa watafutaji wa Mungu wenye furaha na mashahidi wa upendo usio na kikomo.
Mimi
niko pamoja nanyi, wanangu, na ninawaalika ninyi nyote tena: jitieni moyo na mshuhudie matendo mema ambayo Mungu anafanya ndani yenu na kupitia kwenu. Furahini katika Mungu. Mtendeeni mema jirani yenu ili mpate afya njema duniani na ombeeni amani ambayo inatishiwa kwa sababu shetani hutaka vita na mahangaiko. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 18 Machi 2023 - Tokeo la kila mwaka kwa Miriana Dragićević-Soldo
Mwotaji Mirjana Dragićević-Soldo alikuwa na matukio ya kila siku kutoka Juni 24, 1981 hadi Desemba 25, 1982. Katika hafla ya kutokezwa kwake kwa kila siku, akimfunulia siri ya kumi, Bikira alimfunulia kwamba atakuwa na tukio la kila mwaka mnamo Machi 18 na ndivyo ilivyokuwa katika miaka hii yote. Tukio hilo lilianza saa 1.33 jioni na kudumu hadi saa 1.39.
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika mpate kumjua Mwanangu vizuri iwezekanavyo kwa sala na rehema. Ili kwa mioyo safi na iliyo wazi mjifunze kusikiliza. Sikilizeni Mwanangu anachowaambieni ili mpate kuona tena kiroho. Kama watu wamoja wa Mungu, kwa ushirika na Mwanangu, ishuhudieni kweli kwa maisha yenu. Ombeni, wanangu, ili kwamba pamoja na Mwanangu muweze kuleta amani, furaha na upendo kwa ndugu zenu wote.
Mimi
ni pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka zangu za kimama.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika ninyi kwenye maombi kwa moyo. Mioyo yenu, wanangu, igeuzwe kuelekea mbinguni kwa maombi, ili mioyo yenu ipate kuhisi Mungu wa upendo anayewaponya na kuwapenda kwa upendo mkuu.
Mimi
niko pamoja nanyi kuwaongoza kwenye njia ya uongofu wa moyo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Karibuni Ujumbe, 18 Machi 2024 - Tokeo la kila mwaka kwa Miriana Dragićević-Soldo
Mwotaji Mirjana Dragićević-Soldo alikuwa na matukio ya kila siku kutoka Juni 24, 1981 hadi Desemba 25, 1982. Katika hafla ya kutokezwa kwake kwa kila siku, akimfunulia siri ya kumi, Bikira alimfunulia kwamba atakuwa na tukio la kila mwaka mnamo Machi 18 na ndivyo ilivyokuwa katika miaka hii yote. Tukio hilo lilianza saa 1.33 jioni na kudumu hadi saa 1.39.
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika mpate kumjua Mwanangu vizuri iwezekanavyo kwa sala na rehema. Ili kwa mioyo safi na iliyo wazi mjifunze kusikiliza. Sikilizeni Mwanangu anachowaambieni ili mpate kuona tena kiroho. Kama watu wamoja wa Mungu, kwa ushirika na Mwanangu, ishuhudieni kweli kwa maisha yenu. Ombeni, wanangu, ili kwamba pamoja na Mwanangu muweze kuleta amani, furaha na upendo kwa ndugu zenu wote.
Mimi
ni pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka zangu za kimama.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7