Our Lady of Medjugorje Messages containing 'mkae'
Total found:
2
Ujumbe, 25 Julai 2018
“
W
anangu wapendwa! Mungu aliniita ili niwaongozeni kwake, maana Yeye ndiye nguvu yenu. Kwa hiyo ninawaalika kumwomba na kumtegemea, maana Yeye ndiye kimbizo lenu kutoka kila uovu uliokaribu na kupeleka mioyo mbali kutoka neema na furaha mnakoitwa. Wanangu isheni Mbingu hapa duniani ili
mkae
vizuri na amri za Mungu ziwe mwanga katika njia yenu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwapenda nyote kwa upendo wa kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Machi 2022
“
W
anangu wapendwa! Ninasikiliza kilio chenu na maombi ya amani. Shetani amekuwa akipigania vita kwa miaka mingi. Kwa hiyo Mungu amenituma kati yenu ili niwaongoze katika njia ya utakatifu, kwa sababu ubinadamu uko kwenye njia panda. Nawaalikeni: mrudieni Mungu na amri za Mungu
mkae
vizuri hapa duniani na mtoke katika janga hili ambalo mmeingia kwa sababu humsikii Mungu anayewapenda na anayetaka kuwaokoa na kuwaongoza kuelekea maisha mapya. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose