Our Lady of Medjugorje Messages containing 'mmejaa'
Total found:
2
Ujumbe, 25 Desemba 2018 - Tokeo la mwaka la Yakobo
Katika tokeo la mwisho la kila siku tarehe 12 Septemba 1998 Bikira Maria alimwambia Yakobo Kolo ya kuwa ataona tokeo mara moja kila mwaka, tarehe 25 Decemba, siku ya Noeli. Hivyo kumekuwa na tokea hata mwaka huu. Tokeo limeanza saa 7 na dakika 38 na likadumu dakika 9. Bikira Maria amekuja pamoja na Mtoto Yesu mikononi mwake. Bikira Maria kwa njia ya Yakobo alipitisha ujumbe huu:
“
W
anangu wapendwa, katika siku hii ya neema ninawaalika kupenda. Wanangu, Mungu anawapenda kupita kiasi na kwa hiyo wanangu,
mmejaa
imani, bila kutazama nyuma na bila hofu mwachieni kabisa mioyo yenu ili Mungu aijaze kwa upendo wake. Msiwe na hofu kuamini upendo Wake na rehema Yake maana upendo Wake ni mwenye nguvu kuliko kila udhaifu wenu na hofu. Kwa hiyo, wanangu,
mmejaa
upendo katika mioyo yenu mwamini Yesu na mseme Ndiyo yenu maana Yeye ni njia ya pekee ya kuwaongoza kwa Baba wa milele.
”
Ujumbe, 25 Februari 2020
“
W
anangu wapendwa, Katika kipindi hiki cha neema nataka kuona nyuso zenu zigeuke katika sala. Ninyi
mmejaa
mahangaiko ya kidunia kiasi kwamba hamuoni hata ujio wa majira ya kuchipua kwa mimea. Wanangu, mnaalikwa kwa toba na kwa sala. Kama viumbe vya asili vinapigana katika kimya kwa maisha mapya, hivyo hata ninyi mnaalikwa kujifungua katika sala kwa Mungu ambaye kwake mtapata amani na joto la jua la kipindi cha kuchanua kwa mimea katika mioyo yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose