Our Lady of Medjugorje Messages containing 'mtakuwa'
Total found:
22
Ujumbe, 25 Mei 2021
“
W
anangu wapendwa! Ninawatazama na kuwaalika: mrudieni Mungu maana Yeye ndiye upendo na kwa ajili ya upendo alinituma kwenu ili niwaongoze kwenye njia ya wongofu. Acheni dhambi na maovu, amueni kuwa watakatifu na furaha itatawala; nanyi
mtakuwa
mikono yangu iliyopanuliwa katika ulimwengu huu uliopotea. Ninatamani ya kuwa muwe sala na matumaini kwa wale ambao hawajamjua Mungu wa upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2021
“
W
anangu wapendwa! Niko pamoja nanyi katika wakati huu wa rehema na ninawaalika nyote kuwa waleta amani na upendo katika ulimwengu huu, ambapo, wanangu, Mungu anawaalika kupitia Kwangu kuwa sala, upendo na kielelezo cha Paradiso, hapa duniani. Mioyo yenu na ijazwe na furaha na imani katika Mungu ili, wanangu, muwe na imani kamili katika mapenzi yake matakatifu. Hii ndiyo sababu mimi niko pamoja nanyi kwa sababu Yeye, Aliye Juu, ananituma kati yenu ili kuwahimiza ninyi kuwa na matumaini na
mtakuwa
waleta amani katika ulimwengu huu wenye wasiwasi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2