Our Lady of Medjugorje Messages containing 'mungu'
Total found:
144
Ujumbe, 25 Aprili 2013
“
W
anangu wapendwa! Salini, salini, mwendelee kusali ili mioyo yenu ifungukie kupokea imani jinsi ua linavyofunguka kuelekea mianga ya joto la jua. Huo ni wakati wa neema ambao
Mungu
anawajalia kwa njia ya uwepo wangu, lakini ninyi mpo mbali na moyo wangu. Kwa hiyo nawaalikeni kwa uongofu binafsi na kwenye sala katika familia zenu. Maandiko matakatifu yawe daima kichocheo chenu. Nawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni kuwa na nguvu na imara katika imani na katika sala, ili sala zenu ziwe zenye nguvu za kuweza hata kufungua moyo wa Mwanangu mpendwa Yesu. Salini enyi wanangu wadogo, bila kukoma, ili moyo wenu ujifungue kwa upendo wa
Mungu
. Mimi nipo pamoja nanyi, nawaombea ninyi nyote nikasali kwa ajili ya uwongofu wenu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Juni 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, katika wakati huu wa wasiwasi nawaalikeni tena kutembea nyuma ya Mwanangu, na kumfuata. Nayajua maumivu, mateso na taabu zenu, lakini katika Mwanangu mtapumzika, ndani yake mtapata amani na wokovu. Wanangu, msisahau ya kuwa Mwanangu amewakomboa ninyi kwa msalaba wake akawajalieni kuwa tena wana wa
Mungu
na kuwafundisha kumwita tena "Baba" yenu,
Mungu
aliye mbinguni. Ili muwe wapenzi wa
Mungu
Baba, basi muwe na mapendo na msamaha, kwa kuwa Baba yenu ni upendo na msamaha. Salini na fungeni, kwa maana hii ndiyo njia ya kujua na kumfahamu Baba aliye mbinguni. Mtakapomjua huyo Baba, mtafahamu ya kuwa Yeye tu ni muhimu kwenu (Maria Mtakatifu amenena hayo kwa nguvu na amkazo sana). Mimi, nikiwa Mama, nataka wanangu wawe watu wenye umoja ambamo Neno la
Mungu
husikilizwa na kutekelezwa. Kwa hiyo, enyi wanangu, mfuateni Mwanangu, muwe kitu kimoja naye, muwe wana wa
Mungu
. Pendeni wachungaji wenu kama vile Mwanangu alivyowapenda alipowaita kuwatumikia ninyi. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 2 Julai 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo wa kimama nawaomba mnipe mioyo yenu ili niweze kumtolea Mwanangu, ili naye aweze kuiokoa, kuiokoa kutoka uovu wote unaowafanya daima kuwa watumwa na unaowafanya kuwa mbali na ule Wema wa pekee, yaani Mtoto wangu, anayewaokoa kutoka yote yale yanayowaongoza kwenye njia ya uovu na kuwaondolea amani. Mimi natamani kuwaongoza kwenye uhuru wa ahadi za Mtoto wangu, kwa kuwa natamani hapa yatimizwe hasa hasa mapenzi ya
Mungu
, ili kwa kupatanishwa na Baba wa Mbinguni, kufunga na kusali, waweze kuzaliwa mitume wa mapendo ya
Mungu
, yaani mitume watakaoeneza kwa mapendo na uhuru, Mapendo ya
Mungu
kwa watoto wangu wote, mitume watakaoeneza mapendo aminifu kwa Baba wa Mbinguni na hivyo kufungua milango ya mbingu. Watoto wapenzi, toeni furaha ya mapendo yenu na mshikamano wenu kwa wachungaji wenu kama vile Mtoto wangu alivyowaomba wao kutoa furaha hiyo. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawapendeni, ninyi nyote, watoto wangu nyote, muwe wote moyoni mwangu, ninyi nyote mmepata upendo wangu wa kimama na ninatamani kuwaongoza nyote ili mjue furaha ya
Mungu
. Kwa hiyo nawaalikeni: nahitaji mitume wanyenyekevu ambao, kwa moyo mkunjufu, wanapokea Neno la
Mungu
na ambao wako tayari kuwasaidia watu wengine ili, kwa njia ya Neno la
Mungu
, waelewe maana ya maisha yao. Ili muweze kufanya hayo, wanangu, yawapasa, kwa njia ya kusali na kufunga, kusikiliza kwa moyo mkunjufu na kujifunza kujidhili au kujinyenyekesha. Yawapasa kujifunza kukataa yote yanayowatenganisha na Neno la
Mungu
na kutamani tu yanayowakaribisha. Msiogope, mimi nipo hapa. Ninyi si peke yenu. Namwomba Roho Mtakatifu ili awafanye wapya, ili awaimarishe. Namwomba Roho Mtakatifu, ili mkisaidia wengine, muweze kujiponya nyinyi wenyewe. Naomba ili, kwa njia yake, muwe wana wa
Mungu
na mitume wangu.
”
Kisha kwa mahangaiko makubwa Bikira Maria alisema:
“
K
wa ajili ya Yesu, kwa ajili ya mwanangu, pendeni wale ambao Yeye aliwaita mkitamani baraka ya mikono ile ambayo Yeye tu ameyaweka wakfu. Msiyaruhusu maovu yatawale. Nawaalikeni tena: ni kwa njia ya wachungaji wangu tu moyo wangu utashinda. Msiyaruhusu maovu yawatenganisheni na wachungaji wenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa! nawapendeni kwa upendo wa kimama, na kwa subira ya kimama nangojea upendo wenu na ushirikiano wenu. Nasali ili muwe jumuiya ya wana wa
Mungu
na wanangu. Nasali ili muweze kuwa jumuiya inayojihuisha kwa furaha na imani na upendo wa Mwanangu. Wanangu, nawakusanya kama mitume wangu na nitawafundisha jinsi ya kuwajulisha wengine upendo wa Mwanangu, na jinsi ya kuwafikishia habari njema, ambaye ni Mwanangu. Nipeni mioyo yenu iliyo wazi na iliyosafishwa, nami nitaijaza upendo wa Mwanangu. Upendo wake utaipa maisha yenu maana nami nitatembea pamoja nanyi. Nitakuwa pamoja nanyi hata tumfikie Baba wa Mbinguni. Wanangu, wataokoka tu wale ambao watatembea kwa upendo na imani kumwelekea Baba wa Mbinguni. Msiogope, nipo pamoja nanyi! Muwaamini wachungaji wenu kama Mwanangu alivyowaamini wakati alipowachagua, na muwaombee ili waweze kupata nguvu na upendo wa kuwaongozeni. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni mjifungulie kwa sali. Sala itasababisha miujiza ndani yenu na kwa njia yenu. Kwa hiyo, enyi wanangu, kwa moyo mkunjufu mtafuteni Yeye Aliye Juu ili awapeni nguvu ya kuwa wana wa
Mungu
, na yule Shetani asiwatikiseni kama matawi yatikiswavyo na upepo. Kateni shauri tena, wanangu, kwa
Mungu
na tafuteni tu mapenzi yake, hapo mtapata furaha na amani. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni nyote kusali. Fungueni kwa kina mlango wa mioyo yenu, enyi wanangu, kwa sala, sala ya moyo na hivyo Yeye Aliye Juu ataweza kufanya kazi katika uhuru wenu na kuanzisha uongofu wenu. Hivyo imani yenu itakuwa imara kiasi cha kuweza kusema kwa moyo wenu wote: "
Mungu
wangu na yote yangu". Halafu mtaweza kuelewa, wanangu, ya kuwa duniani hapa yote hupita. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo wa kimama na uvumilivu wa kimama naona kutangatanga kwenu na kuendelea kupotea kwenu. Kwa sababu hiyo mimi nipo pamoja nanyi. Nataka kwanza kabisa kuwasaidieni kupata kujijua ninyi wenyewe, ili baadaye muweze kuelewa na kutambua yote yanayowazuia kujua bila unafiki na kwa moyo wote upendo wa Baba wa Mbinguni. Wanangu, Baba hujulikana kwa njia ya msalaba: kwa hiyo msikatae msalaba: kwa msaada wangu, mkafanye bidii kuuelewa na kuupokea. Mtakapoweza kuupokea msalaba, mtaelewa pia upendo wa Baba wa Mbinguni. Mtatembea pamoja na Mwanangu na mimi. Mtajipambanua na wale ambao hawakujua upendo wa Baba wa Mbinguni, kujitofautisha na wale wanaomsikiliza lakini hawamwelewi, na wale wasioenda pamoja naye, na wasiomjua. Mimi nataka ninyi mjue ukweli wa Mwanangu na muwe mitume wangu; ili, kama wana wa
Mungu
, muwe na mawazo yaliyo juu ya mawazo ya kibinadamu na siku zote na katika yote mkatafute kila mara mawazo ya
Mungu
. Wanangu, salini na fungeni ili muweze kuelewa yote ninayowaombeni. Muombee wachungaji wenu mkatamani kujua, mkishirikiana nao, upendo wa Baba wa Mbinguni. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2013
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mfalme wa amani ili Yeye awapatie amani Yake. Ninyi, wanangu, salini, salini, salini. Matunda ya sala yatajionyesha kwenye nyuso za watu waliojitoa kwa
Mungu
na Ufalme wake. Mimi pamoja na mwanangu Yesu tunawabariki nyote kwa baraka ya amani. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Ili mpate kuwa mitume wangu na kuweza kusaidia wale walioko katika giza, ili waweze kuujua mwanga wa upendo wa Mwanangu, mnapaswa kuwa na moyo safi na mnyenyekevu. Hamwezi kusaidia ili Mwanangu azaliwe na kutawala mioyoni mwa wale wasiomjua, iwapo Yeye hatawali moyoni mwenu. Mimi nipo pamoja nanyi, natembea pamoja nanyi kama mama, nabisha hodi katika moyo wenu, usioweza kufunguka bila ya kuwa mnyenyekevu. Mimi nasali, lakini salini nanyi pia, wanangu wapendwa, ili muweze kumfungulia Mwanangu moyo wenu safi na mnyenyekevu na hivyo kuweza kupokea vipaji nilivyowaahidi. Hapo ndipo mtakapoongozwa kwa upendo na nguvu za Mwanangu, hapo ndipo mtakuwa mitume wangu, ambao wanaweza kueneza kwa walio karibu yao matunda ya upendo wa
Mungu
. Kutokana na ninyi na kwa njia yenu Mwanangu atafanya kazi, maana mtakuwa na Yeye kitu kimoja. Moyo wangu wa kimama unatamani muungano wa wanangu wote, kwa njia ya Mwanangu. Kwa upendo mkuu nawabariki na kuwaombea wateule wa Mwanangu, wachungaji wenu, Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2014
“
W
anangu wapendwa! Salini, salini, salini ili mionzi ya sala yenu iwaguse watu wote mnaokutana nao. Wekeni Biblia Takatifu mahali pa kuonekana katika familia zenu, mkaisome ili maneno ya amani yatiririke ndani ya mioyo yenu. Nasali pamoja nanyi na kwa ajili yenu, wanangu, ili siku hata siku mzidi kuyapokea mapenzi ya
Mungu
. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Kwa upendo wa kimama nataka kuwafundisha uadilifu, natamani kwamba katika kutenda kwenu kazi kama mitume wangu muwe wenye haki, maamuzi na hasa waadilifu. Natamani kwamba, kwa neema ya
Mungu
, muweze kupokea Baraka ya
Mungu
. Natamani, kwa njia ya kufunga na kusali, muweze kupata kutoka kwa Baba wa Mbinguni ujuzi, uhalali, utakatifu wa kimungu. Kwa ulinzi wa Mwanangu na wangu mtakuwa mitume wangu, ambao wanaweza kueneza neno la
Mungu
kwa wote wasiolijua, na mtaweza kushinda mapingamizi mtakayokutana nayo njiani. Wanangu, kwa njia ya baraka neema itawashukia, nanyi mtaweza kuilinda neema hiyo kwa kufunga na kusali, kwa kujitakasa na kujipatanisha. Mtakuwa na utendaji fanisi ninaohitaji kutoka kwenu. Waombeeni wachungaji wenu ili mionzi ya neema ya
Mungu
iangaze njia yao. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2014
“
W
anangu wapendwa! Mnaona, mnasikia na kuhisi kwamba katika mioyo ya watu wengi hakuna
Mungu
. Hawamtaki kwa maana wapo mbali na sala na hawana amani mioyoni. Ninyi, wanangu, salini, na isheni kadiri ya amri za
Mungu
. Muwe sala, enyi mlioitikia "naam" tangu mwanzo wa mwaliko wangu. Mshuhudieni
Mungu
na mtambue uwepo wangu wala msisahau, wanangu, ya kuwa mimi ni pamoja nanyi na ninawapenda. Siku hata siku nawachukua kwa Mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Machi 2014
“
W
anangu wapendwa! Nawaalikeni tena: anzeni kupambana na dhambi kama vile katika siku za mwanzo, nendeni kuungama dhambi zenu na kateni shauri ya kuwa watakatifu. Kwa njia yenu upendo wa
Mungu
utaenea ulimwenguni na amani itatawala mioyoni mwenu na baraka ya
Mungu
itawajaza. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombeeni mbele ya Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Aprili 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Kwa upendo wa kimama nataka kuwasaidia ili maisha yenu ya kusali na kutubu iwe juhudi ya kweli ya kumjongea Mwanangu na nuru yake ya kimungu, ili muweze kutengana na dhambi. Kila sala, kila Misa na kila mfungo ni juhudi ya kumjongea Mwanangu, msukumo kwa utukufu wake na kuepukana na dhambi. Ni njia ya muungano mpya wa Baba mwema na wanao. Kwa hiyo, wanangu wapendwa, kwa unyofu wa moyo uliojaa upendo mliite jina la Baba wa Mbinguni, ili awatie nuru ya Roho Mtakatifu. Kwa njia ya Roho Mtakatifu mtakuwa chemchemi ya upendo wa
Mungu
: kwenye chemchemi hiyo wale wote wasiomjua Mwanangu watakunywa, wote wenye kiu ya upendo na amani ya Mwanangu. Nawashukuru! Salini kwa ajili ya wachungaji wenu. Mimi nawaombee na nataka waonje siku zote baraka ya mikono yangu na tegemeo la Moyo wangu wa kimama.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2014
“
W
anangu wapendwa! Fungueni mioyo yenu kwa neema ambayo
Mungu
anawapa kwa njia yangu kama vile ua linalojifungua kwa miali ya joto la jua. Muwe sala na upendo kwa wale wote walio mbali na
Mungu
na upendo Wake. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombea nyote kwa Mwanangu Yesu na ninawapenda kwa upendo usio na mipaka. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2014
“
W
anangu wapendwa! Salini na mfahamu ya kwamba pasipo
Mungu
ninyi ni mavumbi. Kwa hiyo geuzeni fikira zenu na mioyo yenu kwa
Mungu
na kwa sala. Tegemeeni upendo Wake. Katika Roho ya
Mungu
ninyi nyote mnaalikwa kuwa mashahidi. Ninyi mna thamani mbele ya
Mungu
, nami nawaalika, wanangu, kuwa watakatifu, ili mweze kupata uzima wa milele. Kwa hiyo mfahamu ya kwamba maisha haya hupita. Nawapendeni na kuwaalika kwa maisha mapya ya kutubu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Juni 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Nawaalika na kupokea ninyi nyote kama wanangu. Ninasali ili mnipokee na kunipenda kama Mama yenu. Nimewaunga ninyi nyote katika moyo wangu, nimeshuka katikati yenu na kuwabariki. Najua kwamba mnataka kwangu faraja na tumaini, kwa sababu nawapenda na kuwaombea. Nawaomba kujiunga nami katika Mwanangu na kuwa mitume wangu. Ili muweze kutenda hivyo nawaalika tena kupenda. Hakuna upendo pasipo sala, hakuna sala pasipo msamaha, maana upendo ni sala, na msamaha ni upendo. Wanangu,
Mungu
aliwaumba ili mpende, pendeni ili muweze kusamehe! Kila sala itokayo katika upendo huwaunganisha na Mwanangu na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu awaangaze na kuwafanya mitume wangu: mitume ambao, kila watendalo, watalifanya kwa jina la Bwana. Wao watasali kwa matendo na siyo kwa maneno tu, kwa maana wanampenda Mwanangu na kufahamu njia ya ukweli iongozayo kwenye uzima wa milele. Waombeeni wachungaji wenu, ili waweze kuwaongoza daima kwa moyo safi katika njia ya ukweli na upendo, ndiyo njia ya Mwanangu. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Juni 2014
“
W
anangu wapendwa! Yeye Aliye Juu ananipa neema ya kuweza kuwa tena pamoja nanyi na kuwaongoza katika sala kuelekea njia ya amani. Mioyo yenu na roho zenu zina kiu ya amani na upendo, ya
Mungu
na ya furaha yake. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini na katika sala mtapata hekima ya kuishi. Nawabarikieni na kukuombeeni mbele ya Mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
1
2
3
4
5
6
7
8
Next>>