Our Lady of Medjugorje Messages containing 'mungu'
Total found:
144
Ujumbe, 25 Novemba 2021
“
W
anangu wapendwa! Niko pamoja nanyi katika wakati huu wa rehema na ninawaalika nyote kuwa waleta amani na upendo katika ulimwengu huu, ambapo, wanangu,
Mungu
anawaalika kupitia Kwangu kuwa sala, upendo na kielelezo cha Paradiso, hapa duniani. Mioyo yenu na ijazwe na furaha na imani katika
Mungu
ili, wanangu, muwe na imani kamili katika mapenzi yake matakatifu. Hii ndiyo sababu mimi niko pamoja nanyi kwa sababu Yeye, Aliye Juu, ananituma kati yenu ili kuwahimiza ninyi kuwa na matumaini na mtakuwa waleta amani katika ulimwengu huu wenye wasiwasi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2022
“
W
anangu wapendwa! Nipo pamoja nanyi na tusali pamoja. Wanangu nisaidieni kwa maombi ili shetani asishinde. Nguvu yake ya mauti, chuki na woga imeitembelea Dunia. Kwa hiyo wanangu, mrudieni
Mungu
katika maombi na katika kufunga na kuwanyima kwa ajili ya wote waliokanyagwa, maskini na wasio na sauti katika dunia hii pasipo
Mungu
. Watoto wadogo, msipomrudia
Mungu
na amri zake, hamna wakati ujao. Kwa hiyo amenituma kwenu ili niwaongoze. Leo ninawaalika mrudi kwenye sala ya kibinafsi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Machi 2022
“
W
anangu wapendwa! Ninasikiliza kilio chenu na maombi ya amani. Shetani amekuwa akipigania vita kwa miaka mingi. Kwa hiyo
Mungu
amenituma kati yenu ili niwaongoze katika njia ya utakatifu, kwa sababu ubinadamu uko kwenye njia panda. Nawaalikeni: mrudieni
Mungu
na amri za
Mungu
mkae vizuri hapa duniani na mtoke katika janga hili ambalo mmeingia kwa sababu humsikii
Mungu
anayewapenda na anayetaka kuwaokoa na kuwaongoza kuelekea maisha mapya. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2022
“
W
anangu wapendwa! Ninawatazama na ninamshukuru
Mungu
kwa kila mmoja wenu, kwa sababu ameniruhusu niwe nanyi tena ili kuwasihi katika utakatifu. Wanangu amani inavurugika na shetani anataka mahangaiko. Kwa hiyo maombi yenu yawe na nguvu zaidi ili kila roho chafu ya utengano na vita itulie. Iweni wajenzi wa amani na wachukuaji wa Aliyefufuka ndani yenu na karibu nanyi ili mema yapate kushinda katika kila mtu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2022
“
W
anangu wapendwa! Ninafurahi pamoja nanyi na kuwashukuru kwa kila sadaka na sala ambayo mlitolea kwa makusudi yangu. Wanangu, msisahau ya kuwa ninyi ni muhimu katika mpango wangu wa wokovu wa wanadamu. Rudeni kwa
Mungu
na kwa sala ili Roho Mtakatifu atende kazi ndani yenu na kupitia ninyi. Wanangu, Mimi ni pamoja nanyi hata katika siku hizi ambapo shetani anapiga kwa vita na kwa machukio. Utengano ni wenye nguvu na maovu yatenda kazi katika mwanadamu kama hajatenda bado mpaka leo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2022
“
W
anangu wapendwa! Niko pamoja nanyi kuwaongoza katika njia ya uongofu kwa sababu, wanangu, kwa maisha yenu mnaweza kuleta nafsi nyingi karibu na Mwanangu. Iweni mashahidi wenye furaha wa Neno la
Mungu
na wa upendo, mkiwa na matumaini ndani ya mioyo yenu yashindayo uovu wote. Mwasamehe wanaowadhuru na tembeeni katika njia ya utakatifu. Ninawaongoza kwa Mwanangu ili Yeye awe njia, ukweli na uzima kwenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2022
“
W
anangu wapendwa!
Mungu
ananiruhusu niwe pamoja nanyi na kuwaongoza kwenye njia ya amani ili kupitia amani ya kibinafsi, muweze kujenga amani duniani. Nipo pamoja nanyi na ninawaombea kwa Mwanangu Yesu ili awape imani thabiti na tumaini ya maisha bora ya baadaye ninayotaka kujenga pamoja nanyi. Ninyi, jipeni moyo na msiogope maana
Mungu
yu pamoja nanyi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2022
“
W
anangu wapendwa! Salini ili Roho Mtakatifu awaangazie kuwa watafutaji wa
Mungu
wenye furaha na mashahidi wa upendo usio na kikomo. Mimi niko pamoja nanyi, wanangu, na ninawaalika ninyi nyote tena: jitieni moyo na mshuhudie matendo mema ambayo
Mungu
anafanya ndani yenu na kupitia kwenu. Furahini katika
Mungu
. Mtendeeni mema jirani yenu ili mpate afya njema duniani na ombeeni amani ambayo inatishiwa kwa sababu shetani hutaka vita na mahangaiko. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2022
“
W
anangu wapendwa! Aliye juu aliniruhusu niwe pamoja nanyi; kuwa furaha kwenu na njia katika matumaini kwa sababu ubinadamu umeamua kifo. Kwa hiyo amenituma niwaelekeze kwamba bila
Mungu
hamna wakati ujao. Wanangu, muwe vyombo vya upendo kwa wale wote ambao hawajamjua
Mungu
wa upendo. Kwa furaha toeni ushuhuda wa imani yenu na msipoteze matumaini katika mabadiliko ya moyo wa mwanadamu. Niko pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka yangu ya mama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2022
“
W
anangu wapendwa! Aliye juu amenituma kwenu ili niwafundishe jinsi ya kuomba. Sala hufungua mioyo na kutoa tumaini; imani huzaliwa na kuimarishwa. Wanangu, nawaiteni kwa upendo: mrudieni
Mungu
kwa maana
Mungu
ni upendo wenu na tumaini lenu. Msipoamua kwa ajili ya
Mungu
hamna mustakabali na kwa hiyo niko pamoja nanyi kuwaongoza ili muamue uongofu na uzima na sio kifo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2023
“
W
anangu wapendwa! Ombeni pamoja nami kwa ajili ya amani maana shetani anataka vita na chuki katika mioyo na mataifa. Kwa hiyo salini na, katika siku zenu, toeni sadaka kwa kufunga na kutubu ili
Mungu
awape amani. Wakati ujao uko kwenye njia panda kwa sababu mwanadamu wa kisasa hataki
Mungu
. Kwa hiyo ubinadamu unaelekea kwenye upotevu. Ninyi, wanangu, ni tumaini langu. Ombeni pamoja nami kwamba niliyoyaanza Fatima na hapa yatimie. Ombeni na mshuhudie amani katika mazingira yenu na muwe watu wa amani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2023
“
W
anangu wapendwa! Ongokeni na mvae mavazi ya toba na maombi ya kina ya kibinafsi na kwa unyenyekevu mwombe Aliye Juu amani. Katika wakati huu wa neema Shetani anataka kuwapotosha ninyi, nanyi wanangu, mwangalieni Mwanangu na kumfuata kuelekea Kalvari, kwa kujikana na kufunga. Niko pamoja nanyi kwa sababu Aliye Juu ameniruhusu niwapende ninyi na kuwaongoza kuelekea furaha ya moyo, katika imani inayokua ndani ya wale wote wanaompenda
Mungu
zaidi ya vitu vyote. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 18 Machi 2023 - Tokeo la kila mwaka kwa Miriana Dragićević-Soldo
Mwotaji Mirjana Dragićević-Soldo alikuwa na matukio ya kila siku kutoka Juni 24, 1981 hadi Desemba 25, 1982. Katika hafla ya kutokezwa kwake kwa kila siku, akimfunulia siri ya kumi, Bikira alimfunulia kwamba atakuwa na tukio la kila mwaka mnamo Machi 18 na ndivyo ilivyokuwa katika miaka hii yote. Tukio hilo lilianza saa 1.33 jioni na kudumu hadi saa 1.39.
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika mpate kumjua Mwanangu vizuri iwezekanavyo kwa sala na rehema. Ili kwa mioyo safi na iliyo wazi mjifunze kusikiliza. Sikilizeni Mwanangu anachowaambieni ili mpate kuona tena kiroho. Kama watu wamoja wa
Mungu
, kwa ushirika na Mwanangu, ishuhudieni kweli kwa maisha yenu. Ombeni, wanangu, ili kwamba pamoja na Mwanangu muweze kuleta amani, furaha na upendo kwa ndugu zenu wote. Mimi ni pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka zangu za kimama.
”
Ujumbe, 25 Mei 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika ninyi mwende katika mazingira ya asili na kusali ili kwamba Aliye Juu Sana aseme na moyo wenu na kwamba muweze kuhisi uwezo wa Roho Mtakatifu kushuhudia upendo ambao
Mungu
anao kwa kila kiumbe. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2023
“
W
anangu wapendwa! Aliye Juu ameniruhusu niwe miongoni mwenu, niwaombee, niwe Mama yenu na kimbilio lenu. Ninawaalika wanangu, mrudieni
Mungu
na kwenye maombi na
Mungu
atawabariki kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema, ambao Aliye Juu amenituma niwapende ninyi na kuwaongoza katika njia ya uongofu, toeni sala zenu na sadaka zenu kwa ajili ya wale wote walio mbali na wasiojua upendo wa
Mungu
. Ninyi, wanangu, muwe mashahidi wa upendo na amani kwa mioyo yote isiyotulia. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika ninyi kwenye maombi kwa moyo. Mioyo yenu, wanangu, igeuzwe kuelekea mbinguni kwa maombi, ili mioyo yenu ipate kuhisi
Mungu
wa upendo anayewaponya na kuwapenda kwa upendo mkuu. Mimi niko pamoja nanyi kuwaongoza kwenye njia ya uongofu wa moyo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2023
“
W
anangu wapendwa! Pepo za uovu, chuki na wasiwasi huvuma duniani kote kuharibu maisha yote. Kwa hiyo Aliye Juu amenituma kwenu ili niwaongoze kwenye njia ya amani na ushirika na
Mungu
na wanadamu. Ninyi, wanangu, ni mikono yangu iliyopanuliwa: ombeni, mfunge na toeni sadaka kwa ajili ya amani, hazina ambayo kila moyo unatamani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2024
“
W
anangu wapendwa! Salini na mfanye upya moyo wenu ili lile jema mlilopanda lizae matunda ya furaha na ushirika na
Mungu
. Magugu yamechukua mioyo mingi na imekuwa tasa. Kwa hiyo ninyi, wanangu, muwe mwanga, upendo na mikono yangu iliyonyoshwa katika ulimwengu huu unaomtamani
Mungu
ambaye ni upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Karibuni Ujumbe, 18 Machi 2024 - Tokeo la kila mwaka kwa Miriana Dragićević-Soldo
Mwotaji Mirjana Dragićević-Soldo alikuwa na matukio ya kila siku kutoka Juni 24, 1981 hadi Desemba 25, 1982. Katika hafla ya kutokezwa kwake kwa kila siku, akimfunulia siri ya kumi, Bikira alimfunulia kwamba atakuwa na tukio la kila mwaka mnamo Machi 18 na ndivyo ilivyokuwa katika miaka hii yote. Tukio hilo lilianza saa 1.33 jioni na kudumu hadi saa 1.39.
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika mpate kumjua Mwanangu vizuri iwezekanavyo kwa sala na rehema. Ili kwa mioyo safi na iliyo wazi mjifunze kusikiliza. Sikilizeni Mwanangu anachowaambieni ili mpate kuona tena kiroho. Kama watu wamoja wa
Mungu
, kwa ushirika na Mwanangu, ishuhudieni kweli kwa maisha yenu. Ombeni, wanangu, ili kwamba pamoja na Mwanangu muweze kuleta amani, furaha na upendo kwa ndugu zenu wote. Mimi ni pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka zangu za kimama.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
Next>>