Our Lady of Medjugorje Messages containing 'mwanangu'
Total found:
127
Ujumbe, 25 Julai 2022
“
W
anangu wapendwa! Niko pamoja nanyi kuwaongoza katika njia ya uongofu kwa sababu, wanangu, kwa maisha yenu mnaweza kuleta nafsi nyingi karibu na
Mwanangu
. Iweni mashahidi wenye furaha wa Neno la Mungu na wa upendo, mkiwa na matumaini ndani ya mioyo yenu yashindayo uovu wote. Mwasamehe wanaowadhuru na tembeeni katika njia ya utakatifu. Ninawaongoza kwa
Mwanangu
ili Yeye awe njia, ukweli na uzima kwenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2022
“
W
anangu wapendwa! Mungu ananiruhusu niwe pamoja nanyi na kuwaongoza kwenye njia ya amani ili kupitia amani ya kibinafsi, muweze kujenga amani duniani. Nipo pamoja nanyi na ninawaombea kwa
Mwanangu
Yesu ili awape imani thabiti na tumaini ya maisha bora ya baadaye ninayotaka kujenga pamoja nanyi. Ninyi, jipeni moyo na msiogope maana Mungu yu pamoja nanyi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2022
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaletea
Mwanangu
Yesu ili muwe amani yake na kielelezo cha utulivu na furaha ya Mbinguni. Salini, wanangu, ili muwe wazi kukaribisha amani, kwa sababu mioyo mingi imefungwa kupokea wito ya nuru ibadiliyo mioyo. Niko pamoja nanyi na ninawaombea mjifungue kumkaribisha Mfalme wa Amani anayeijaza mioyo yenu joto na baraka. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2023
“
W
anangu wapendwa! Ongokeni na mvae mavazi ya toba na maombi ya kina ya kibinafsi na kwa unyenyekevu mwombe Aliye Juu amani. Katika wakati huu wa neema Shetani anataka kuwapotosha ninyi, nanyi wanangu, mwangalieni
Mwanangu
na kumfuata kuelekea Kalvari, kwa kujikana na kufunga. Niko pamoja nanyi kwa sababu Aliye Juu ameniruhusu niwapende ninyi na kuwaongoza kuelekea furaha ya moyo, katika imani inayokua ndani ya wale wote wanaompenda Mungu zaidi ya vitu vyote. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 18 Machi 2023 - Tokeo la kila mwaka kwa Miriana Dragićević-Soldo
Mwotaji Mirjana Dragićević-Soldo alikuwa na matukio ya kila siku kutoka Juni 24, 1981 hadi Desemba 25, 1982. Katika hafla ya kutokezwa kwake kwa kila siku, akimfunulia siri ya kumi, Bikira alimfunulia kwamba atakuwa na tukio la kila mwaka mnamo Machi 18 na ndivyo ilivyokuwa katika miaka hii yote. Tukio hilo lilianza saa 1.33 jioni na kudumu hadi saa 1.39.
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika mpate kumjua
Mwanangu
vizuri iwezekanavyo kwa sala na rehema. Ili kwa mioyo safi na iliyo wazi mjifunze kusikiliza. Sikilizeni
Mwanangu
anachowaambieni ili mpate kuona tena kiroho. Kama watu wamoja wa Mungu, kwa ushirika na
Mwanangu
, ishuhudieni kweli kwa maisha yenu. Ombeni, wanangu, ili kwamba pamoja na
Mwanangu
muweze kuleta amani, furaha na upendo kwa ndugu zenu wote. Mimi ni pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka zangu za kimama.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea
Mwanangu
ili aijaze mioyo yenu amani kwa sababu Yeye ni amani. Wanangu, mtafuteni Yesu katika ukimya wa mioyo yenu ili azaliwe upya. Ulimwengu unamhitaji Yesu, hivyo wanangu, mtafuteni kwa maombi maana anajitoa kila siku kwa kila mmoja wenu.
”
Mama yetu alikuja leo akiwa amevalia mavazi ya heshima akiwa na mtoto Yesu mikononi mwake. Yesu alinyoosha mkono wake kama ishara ya baraka na Mama yetu alituombea kwa lugha ya aramaika.
Karibuni Ujumbe, 18 Machi 2024 - Tokeo la kila mwaka kwa Miriana Dragićević-Soldo
Mwotaji Mirjana Dragićević-Soldo alikuwa na matukio ya kila siku kutoka Juni 24, 1981 hadi Desemba 25, 1982. Katika hafla ya kutokezwa kwake kwa kila siku, akimfunulia siri ya kumi, Bikira alimfunulia kwamba atakuwa na tukio la kila mwaka mnamo Machi 18 na ndivyo ilivyokuwa katika miaka hii yote. Tukio hilo lilianza saa 1.33 jioni na kudumu hadi saa 1.39.
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika mpate kumjua
Mwanangu
vizuri iwezekanavyo kwa sala na rehema. Ili kwa mioyo safi na iliyo wazi mjifunze kusikiliza. Sikilizeni
Mwanangu
anachowaambieni ili mpate kuona tena kiroho. Kama watu wamoja wa Mungu, kwa ushirika na
Mwanangu
, ishuhudieni kweli kwa maisha yenu. Ombeni, wanangu, ili kwamba pamoja na
Mwanangu
muweze kuleta amani, furaha na upendo kwa ndugu zenu wote. Mimi ni pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka zangu za kimama.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7