Our Lady of Medjugorje Messages containing 'na'
Total found:
218
Ujumbe, 25 Aprili 2013
“
W
anangu wapendwa! Salini, salini, mwendelee kusali ili mioyo yenu ifungukie kupokea imani jinsi ua linavyofunguka kuelekea mianga ya joto la jua. Huo ni wakati wa neema ambao Mungu anawajalia kwa njia ya uwepo wangu, lakini ninyi mpo mbali
na
moyo wangu. Kwa hiyo nawaalikeni kwa uongofu binafsi
na
kwenye sala katika familia zenu. Maandiko matakatifu yawe daima kichocheo chenu. Nawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawaalikeni tena kupenda
na
kutohukumu. Mwanangu, kwa mapenzi ya Baba aliye mbinguni, alikuwapo pamoja nanyi ili awaonyesheni njia ya wokovu, awaokoeni si awahukumuni.
Na
ikiwa mnataka kumfuata Mwanangu, msihukumu
na
mpende, kama vile Baba aliye mbinguni anavyowapenda ninyi. Hata wakati mnapoteseka sana, au mnapojikwaa chini ya msalaba, msikate tamaa, msihukumu, bali kumbukeni kwamba mnapendwa,
na
msifuni Baba aliye mbinguni kwa upendo wake. Wanangu, msiiache njia ninayowaongozeni. Msikimbie kwenye maangamizi. Kusali
na
kufunga itawapa nguvu zaidi ili mweze kuishi kama vile baba wa Mbinguni atakavyo; ili muwe mitume wangu wa imani
na
upendo; ili maisha yenu iwe
na
baraka ya wale mnaowaona; ili muwe kitu kimoja
na
baba aliye mbinguni
na
Mwanangu. Wanangu, huu ni ukweli wa pekee, ukweli uletao wongofu wenu
na
kisha wongofu wa wengine wote wasiojua maana ya neno kupenda. Wanangu, Mwanangu aliwapeni wachungaji: muwalinde,
na
muwaombee. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Mei 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni kuwa
na
nguvu
na
imara katika imani
na
katika sala, ili sala zenu ziwe zenye nguvu za kuweza hata kufungua moyo wa Mwanangu mpendwa Yesu. Salini enyi wanangu wadogo, bila kukoma, ili moyo wenu ujifungue kwa upendo wa Mungu. Mimi nipo pamoja nanyi, nawaombea ninyi nyote nikasali kwa ajili ya uwongofu wenu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Juni 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, katika wakati huu wa wasiwasi nawaalikeni tena kutembea nyuma ya Mwanangu,
na
kumfuata. Nayajua maumivu, mateso
na
taabu zenu, lakini katika Mwanangu mtapumzika, ndani yake mtapata amani
na
wokovu. Wanangu, msisahau ya kuwa Mwanangu amewakomboa ninyi kwa msalaba wake akawajalieni kuwa tena wana wa Mungu
na
kuwafundisha kumwita tena "Baba" yenu, Mungu aliye mbinguni. Ili muwe wapenzi wa Mungu Baba, basi muwe
na
mapendo
na
msamaha, kwa kuwa Baba yenu ni upendo
na
msamaha. Salini
na
fungeni, kwa maana hii ndiyo njia ya kujua
na
kumfahamu Baba aliye mbinguni. Mtakapomjua huyo Baba, mtafahamu ya kuwa Yeye tu ni muhimu kwenu (Maria Mtakatifu amenena hayo kwa nguvu
na
amkazo sana). Mimi, nikiwa Mama, nataka wanangu wawe watu wenye umoja ambamo Neno la Mungu husikilizwa
na
kutekelezwa. Kwa hiyo, enyi wanangu, mfuateni Mwanangu, muwe kitu kimoja naye, muwe wana wa Mungu. Pendeni wachungaji wenu kama vile Mwanangu alivyowapenda alipowaita kuwatumikia ninyi. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Juni 2013
“
W
anangu wapendwa! Kwa furaha moyoni nawapendeni nyote
na
kuwaalika kuukaribia moyo wangu usio
na
ndoa, ili moyo wangu uwapeleke karibu zaidi kwa Mwanangu, Yesu Kristo, ili naye awajalieni amani yake
na
upendo wake ambavyo ni chakula kwa kila mmoja wenu. Jifungueni, wanangu, kwa kusali,
na
jifungueni kwa upendo wangu. Mimi ndimi Mama yenu nisiyeweza kuwaachieni katika mtawanyiko
na
katika dhambi peke yenu. Enyi wana, mnaalikwa kuwa wanangu, wanangu wapendwa ili niweze kwakabidhi wote kwa Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Julai 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo wa kimama nawaomba mnipe mioyo yenu ili niweze kumtolea Mwanangu, ili naye aweze kuiokoa, kuiokoa kutoka uovu wote unaowafanya daima kuwa watumwa
na
unaowafanya kuwa mbali
na
ule Wema wa pekee, yaani Mtoto wangu, anayewaokoa kutoka yote yale yanayowaongoza kwenye njia ya uovu
na
kuwaondolea amani. Mimi natamani kuwaongoza kwenye uhuru wa ahadi za Mtoto wangu, kwa kuwa natamani hapa yatimizwe hasa hasa mapenzi ya Mungu, ili kwa kupatanishwa
na
Baba wa Mbinguni, kufunga
na
kusali, waweze kuzaliwa mitume wa mapendo ya Mungu, yaani mitume watakaoeneza kwa mapendo
na
uhuru, Mapendo ya Mungu kwa watoto wangu wote, mitume watakaoeneza mapendo aminifu kwa Baba wa Mbinguni
na
hivyo kufungua milango ya mbingu. Watoto wapenzi, toeni furaha ya mapendo yenu
na
mshikamano wenu kwa wachungaji wenu kama vile Mtoto wangu alivyowaomba wao kutoa furaha hiyo. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Julai 2013
“
W
anangu wapendwa! Kwa furaha moyoni nawaalika wote kuishi imani yenu
na
kuishuhudia kwa moyo
na
mfano kwa kila namna. Ee wanangu, kateni shauri kuacha kabisa dhambi
na
vishawishi vyake; mioyo yenu ijae furaha
na
upendo kwa utakatifu. Mimi, wanangu, nawapenda
na
ninaambatana nanyi. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, tafadhali muelewe, muwe tayari wote, kwa matumaini makuu, kufungua mioyo yenu; hivyo mngeelewa yote, mngeelewa kwa upendo gani nawaiteni, kwa upendo gani nataka kuwageuza, ili kuwafurahisha, kwa upendo gani nataka kuwafanya wafuasi wa Mwanangu
na
kuwapa amani katika ukamilifu wa Mwanangu. Mngeelewa ukuu wa moyo wangu wa kimama, kwa hiyo, wanangu, salini, maana kwa njia ya kusali tu imani yenu hukua
na
upendo wenu huzaliwa, upendo ambao utapunguza uzito wa msalaba kwa maana hamtakuwa peke yenu kuubeba. Katika umoja
na
Mwanangu, tukuzeni jina la Baba wa Mbinguni. Salini, salini mpate tuzo la upendo, maana upendo ni ukweli wa pekee, upendo husamehe yote, hutumikia wote
na
kuwaona wote kama ndugu. Enyi wanangu, mitume wangu, udhamini ambao Baba wa Mbinguni amewawekeni, kwa njia yangu, mtumishi Wake, ni kitu kikubwa, ili kusaidia wale wasiomjua, kusudi zapatanishwe naye, kusudi wamfuate, kwa hiyo nawafundisheni kupenda, maana mkiwa
na
upendo tu mnaweza kumjibu. Nawaalikeni tena: pendeni wachungaji wenu, salini ili katika wakati huu wa shida jina la Mwanangu atukuzwe kwa njia ya mwongozo wao. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo pia Yeye Aliye Juu anijalia neema ya kuwa pamoja nanyi
na
kuwaongoza mpate kutubu. Siku hata siku Mimi napanda mbegu
na
kuwaalika kutubu ili muweze kuwa sala, amani, upendo
na
ngano ambayo ikifa huzaa mara mia. Sipendi, wanangu wapendwa, mpate kujuta kwa yote mliyoweza kufanya wala hamkufanya. Kwa hiyo, enyi wanangu, tena kwa moyo wa furaha semeni: “ Nataka kuwa ishara kwa watu wengine”. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawapendeni, ninyi nyote, watoto wangu nyote, muwe wote moyoni mwangu, ninyi nyote mmepata upendo wangu wa kimama
na
ninatamani kuwaongoza nyote ili mjue furaha ya Mungu. Kwa hiyo nawaalikeni: nahitaji mitume wanyenyekevu ambao, kwa moyo mkunjufu, wanapokea Neno la Mungu
na
ambao wako tayari kuwasaidia watu wengine ili, kwa njia ya Neno la Mungu, waelewe maana ya maisha yao. Ili muweze kufanya hayo, wanangu, yawapasa, kwa njia ya kusali
na
kufunga, kusikiliza kwa moyo mkunjufu
na
kujifunza kujidhili au kujinyenyekesha. Yawapasa kujifunza kukataa yote yanayowatenganisha
na
Neno la Mungu
na
kutamani tu yanayowakaribisha. Msiogope, mimi nipo hapa. Ninyi si peke yenu. Namwomba Roho Mtakatifu ili awafanye wapya, ili awaimarishe. Namwomba Roho Mtakatifu, ili mkisaidia wengine, muweze kujiponya nyinyi wenyewe. Naomba ili, kwa njia yake, muwe wana wa Mungu
na
mitume wangu.
”
Kisha kwa mahangaiko makubwa Bikira Maria alisema:
“
K
wa ajili ya Yesu, kwa ajili ya mwanangu, pendeni wale ambao Yeye aliwaita mkitamani baraka ya mikono ile ambayo Yeye tu ameyaweka wakfu. Msiyaruhusu maovu yatawale. Nawaalikeni tena: ni kwa njia ya wachungaji wangu tu moyo wangu utashinda. Msiyaruhusu maovu yawatenganisheni
na
wachungaji wenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo pia nawaalikeni kusali. Uhusiano wenu
na
kusali uwe wa kila siku. Sala inasababisha miujiza ndani yenu
na
kwa njia yenu,
na
kwa hiyo, enyi wanangu, sala basi iwe ni furaha yenu. Hivyo uhusiano wenu
na
maisha utakuwa wa kina
na
wazi zaidi, pia mtaelewa kwamba maisha ni zawadi kwa kila mmoja wenu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa! nawapendeni kwa upendo wa kimama,
na
kwa subira ya kimama nangojea upendo wenu
na
ushirikiano wenu. Nasali ili muwe jumuiya ya wana wa Mungu
na
wanangu. Nasali ili muweze kuwa jumuiya inayojihuisha kwa furaha
na
imani
na
upendo wa Mwanangu. Wanangu, nawakusanya kama mitume wangu
na
nitawafundisha jinsi ya kuwajulisha wengine upendo wa Mwanangu,
na
jinsi ya kuwafikishia habari njema, ambaye ni Mwanangu. Nipeni mioyo yenu iliyo wazi
na
iliyosafishwa, nami nitaijaza upendo wa Mwanangu. Upendo wake utaipa maisha yenu maana nami nitatembea pamoja nanyi. Nitakuwa pamoja nanyi hata tumfikie Baba wa Mbinguni. Wanangu, wataokoka tu wale ambao watatembea kwa upendo
na
imani kumwelekea Baba wa Mbinguni. Msiogope, nipo pamoja nanyi! Muwaamini wachungaji wenu kama Mwanangu alivyowaamini wakati alipowachagua,
na
muwaombee ili waweze kupata nguvu
na
upendo wa kuwaongozeni. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni mjifungulie kwa sali. Sala itasababisha miujiza ndani yenu
na
kwa njia yenu. Kwa hiyo, enyi wanangu, kwa moyo mkunjufu mtafuteni Yeye Aliye Juu ili awapeni nguvu ya kuwa wana wa Mungu,
na
yule Shetani asiwatikiseni kama matawi yatikiswavyo
na
upepo. Kateni shauri tena, wanangu, kwa Mungu
na
tafuteni tu mapenzi yake, hapo mtapata furaha
na
amani. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Novemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa moyo wa kimama nawaalikeni tena kupenda, kusali bila kukata tamaa kwa zawadi ya upendo, kumpenda Baba wa Mbinguni zaidi ya yote. Mtakapompenda Yeye, mtajipenda wenyewe
na
jirani zenu. Mambo hayo hayawezi kutengana. Baba wa Mbinguni yumo katika kila mtu, hupenda kila mtu
na
kumwita kila mtu kwa jina lake. Kwa hiyo, wanangu, kwa njia ya kusali sikilizeni atakalo Baba wa Mbinguni. Ongeeni
na
Yeye. Muwe
na
uhusiano wa binafsi pamoja
na
Baba, atakayeufanya mkubwa zaidi uhusiano wake nanyi, jumuhiya ya wanangu, mitume wangu. Kama Mama napenda kwamba, kwa njia ya upendo kumwelekea Baba wa Mbinguni, inukeni juu ya ubatili wa malimwengu
na
muwasaidie wengine kujua
na
kumjongea polepole Baba wa Mbinguni. Wanangu, salini, salini, salini kwa zawadi ya upendo, kwa sababu upendo ndiye Mwanangu. Muwaombee wachungaji wenu, ili wawapende ninyi siku zote, kama vile Mwanangu alivyowapenda ninyi
na
kuonyesha akitoa maisha yake kwa wokovu wenu. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni nyote kusali. Fungueni kwa kina mlango wa mioyo yenu, enyi wanangu, kwa sala, sala ya moyo
na
hivyo Yeye Aliye Juu ataweza kufanya kazi katika uhuru wenu
na
kuanzisha uongofu wenu. Hivyo imani yenu itakuwa imara kiasi cha kuweza kusema kwa moyo wenu wote: "Mungu wangu
na
yote yangu". Halafu mtaweza kuelewa, wanangu, ya kuwa duniani hapa yote hupita. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo wa kimama
na
uvumilivu wa kimama naona kutangatanga kwenu
na
kuendelea kupotea kwenu. Kwa sababu hiyo mimi nipo pamoja nanyi. Nataka kwanza kabisa kuwasaidieni kupata kujijua ninyi wenyewe, ili baadaye muweze kuelewa
na
kutambua yote yanayowazuia kujua bila unafiki
na
kwa moyo wote upendo wa Baba wa Mbinguni. Wanangu, Baba hujulikana kwa njia ya msalaba: kwa hiyo msikatae msalaba: kwa msaada wangu, mkafanye bidii kuuelewa
na
kuupokea. Mtakapoweza kuupokea msalaba, mtaelewa pia upendo wa Baba wa Mbinguni. Mtatembea pamoja
na
Mwanangu
na
mimi. Mtajipambanua
na
wale ambao hawakujua upendo wa Baba wa Mbinguni, kujitofautisha
na
wale wanaomsikiliza lakini hawamwelewi,
na
wale wasioenda pamoja naye,
na
wasiomjua. Mimi nataka ninyi mjue ukweli wa Mwanangu
na
muwe mitume wangu; ili, kama wana wa Mungu, muwe
na
mawazo yaliyo juu ya mawazo ya kibinadamu
na
siku zote
na
katika yote mkatafute kila mara mawazo ya Mungu. Wanangu, salini
na
fungeni ili muweze kuelewa yote ninayowaombeni. Muombee wachungaji wenu mkatamani kujua, mkishirikiana nao, upendo wa Baba wa Mbinguni. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2013
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mfalme wa amani ili Yeye awapatie amani Yake. Ninyi, wanangu, salini, salini, salini. Matunda ya sala yatajionyesha kwenye nyuso za watu waliojitoa kwa Mungu
na
Ufalme wake. Mimi pamoja
na
mwanangu Yesu tunawabariki nyote kwa baraka ya amani. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Ili mpate kuwa mitume wangu
na
kuweza kusaidia wale walioko katika giza, ili waweze kuujua mwanga wa upendo wa Mwanangu, mnapaswa kuwa
na
moyo safi
na
mnyenyekevu. Hamwezi kusaidia ili Mwanangu azaliwe
na
kutawala mioyoni mwa wale wasiomjua, iwapo Yeye hatawali moyoni mwenu. Mimi nipo pamoja nanyi, natembea pamoja nanyi kama mama, nabisha hodi katika moyo wenu, usioweza kufunguka bila ya kuwa mnyenyekevu. Mimi nasali, lakini salini nanyi pia, wanangu wapendwa, ili muweze kumfungulia Mwanangu moyo wenu safi
na
mnyenyekevu
na
hivyo kuweza kupokea vipaji nilivyowaahidi. Hapo ndipo mtakapoongozwa kwa upendo
na
nguvu za Mwanangu, hapo ndipo mtakuwa mitume wangu, ambao wanaweza kueneza kwa walio karibu yao matunda ya upendo wa Mungu. Kutokana
na
ninyi
na
kwa njia yenu Mwanangu atafanya kazi, maana mtakuwa
na
Yeye kitu kimoja. Moyo wangu wa kimama unatamani muungano wa wanangu wote, kwa njia ya Mwanangu. Kwa upendo mkuu nawabariki
na
kuwaombea wateule wa Mwanangu, wachungaji wenu, Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2014
“
W
anangu wapendwa! Salini, salini, salini ili mionzi ya sala yenu iwaguse watu wote mnaokutana nao. Wekeni Biblia Takatifu mahali pa kuonekana katika familia zenu, mkaisome ili maneno ya amani yatiririke ndani ya mioyo yenu. Nasali pamoja nanyi
na
kwa ajili yenu, wanangu, ili siku hata siku mzidi kuyapokea mapenzi ya Mungu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Kwa upendo wa kimama nataka kuwafundisha uadilifu, natamani kwamba katika kutenda kwenu kazi kama mitume wangu muwe wenye haki, maamuzi
na
hasa waadilifu. Natamani kwamba, kwa neema ya Mungu, muweze kupokea Baraka ya Mungu. Natamani, kwa njia ya kufunga
na
kusali, muweze kupata kutoka kwa Baba wa Mbinguni ujuzi, uhalali, utakatifu wa kimungu. Kwa ulinzi wa Mwanangu
na
wangu mtakuwa mitume wangu, ambao wanaweza kueneza neno la Mungu kwa wote wasiolijua,
na
mtaweza kushinda mapingamizi mtakayokutana nayo njiani. Wanangu, kwa njia ya baraka neema itawashukia, nanyi mtaweza kuilinda neema hiyo kwa kufunga
na
kusali, kwa kujitakasa
na
kujipatanisha. Mtakuwa
na
utendaji fanisi ninaohitaji kutoka kwenu. Waombeeni wachungaji wenu ili mionzi ya neema ya Mungu iangaze njia yao. Nawashukuru.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
Next>>