Our Lady of Medjugorje Messages containing 'na'
Total found:
218
Ujumbe, 25 Februari 2014
“
W
anangu wapendwa! Mnaona, mnasikia
na
kuhisi kwamba katika mioyo ya watu wengi hakuna Mungu. Hawamtaki kwa maana wapo mbali
na
sala
na
hawana amani mioyoni. Ninyi, wanangu, salini,
na
isheni kadiri ya amri za Mungu. Muwe sala, enyi mlioitikia "naam" tangu mwanzo wa mwaliko wangu. Mshuhudieni Mungu
na
mtambue uwepo wangu wala msisahau, wanangu, ya kuwa mimi ni pamoja nanyi
na
ninawapenda. Siku hata siku nawachukua kwa Mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Naja kwenu kama Mama
na
ninatamani kuwa kwangu kama Mama mtapata maskani, faraja
na
mapumziko. Kwa hiyo, wanangu, mitume wa upendo wangu, salini! Salini kwa moyo mkunjufu, utii
na
uaminifu kamili kwa Baba wa Mbinguni. Muwe
na
uaminifu, kama vile mimi pia nilivyokuwa mwaminifu nilipoambiwa ya kuwa nitachukua baraka za ahadi. Basi kutoka mioyo yenu yafike siku zote midomoni mwenu maneno haya "Utakalo lifanyike". Kwa hiyo muwe
na
uaminifu
na
salini, ili mimi niweze kuwaombeeni kwa Bwana, ili awape Baraka ya Mbinguni
na
kuwajaza Roho Mtakatifu. Hapo mtaweza kuwasaidia wale wote wasiomjua Bwana. Ninyi, mitume wa upendo wangu, mtawasaidia kumwita "Baba" kwa uaminifu wote. Salini kwa ajili ya wachungaji wenu
na
mujiaminishe katika mikono yao iliyobarikiwa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Machi 2014
“
W
anangu wapendwa! Nawaalikeni tena: anzeni kupambana
na
dhambi kama vile katika siku za mwanzo, nendeni kuungama dhambi zenu
na
kateni shauri ya kuwa watakatifu. Kwa njia yenu upendo wa Mungu utaenea ulimwenguni
na
amani itatawala mioyoni mwenu
na
baraka ya Mungu itawajaza. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwaombeeni mbele ya Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Aprili 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Kwa upendo wa kimama nataka kuwasaidia ili maisha yenu ya kusali
na
kutubu iwe juhudi ya kweli ya kumjongea Mwanangu
na
nuru yake ya kimungu, ili muweze kutengana
na
dhambi. Kila sala, kila Misa
na
kila mfungo ni juhudi ya kumjongea Mwanangu, msukumo kwa utukufu wake
na
kuepukana
na
dhambi. Ni njia ya muungano mpya wa Baba mwema
na
wanao. Kwa hiyo, wanangu wapendwa, kwa unyofu wa moyo uliojaa upendo mliite jina la Baba wa Mbinguni, ili awatie nuru ya Roho Mtakatifu. Kwa njia ya Roho Mtakatifu mtakuwa chemchemi ya upendo wa Mungu: kwenye chemchemi hiyo wale wote wasiomjua Mwanangu watakunywa, wote wenye kiu ya upendo
na
amani ya Mwanangu. Nawashukuru! Salini kwa ajili ya wachungaji wenu. Mimi nawaombee
na
nataka waonje siku zote baraka ya mikono yangu
na
tegemeo la Moyo wangu wa kimama.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2014
“
W
anangu wapendwa! Fungueni mioyo yenu kwa neema ambayo Mungu anawapa kwa njia yangu kama vile ua linalojifungua kwa miali ya joto la jua. Muwe sala
na
upendo kwa wale wote walio mbali
na
Mungu
na
upendo Wake. Mimi nipo pamoja nanyi
na
ninawaombea nyote kwa Mwanangu Yesu
na
ninawapenda kwa upendo usio
na
mipaka. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Mimi, Mama yenu, nipo pamoja nanyi kwa ajili yenu, kwa mahitaji yenu
na
mafundisho yenu binafsi. Baba wa Mbinguni amewapa uhuru wa kuamua peke yenu
na
kujua peke yenu. Mimi nataka kuwasaidieni. Nataka kuwa Mama kwenu, mwalimu wa ukweli, ili kwa unyofu wa moyo wazi mjue usafi usio
na
mwisho,
na
mwanga utokao kwa hiyo ukweli ili kutawanya giza, yaani mwanga uletao tumaini. Mimi, wanangu, naelewa maumivu yenu
na
mateso yenu. Nani aweza kuwaelewa zaidi kuliko Mama mmoja! Lakini enyi wanangu? Mjue kuwa idadi ya wanaonielewa
na
kunifuata ni ndogo. Pia ni kubwa idadi ya waliopotea, hao ambao hawajajua ukweli ulio katika Mwanangu. Kwa hiyo, enyi mitume wangu, salini
na
tendeni kazi. Mbebe mwanga, msipoteze tumaini. Mimi nipo nanyi
na
hasa pamoja
na
wachungaji wenu. Nawapenda
na
kuwalinda kwa Moyo wa kimama, ili kusudi wao wanawaongozeni Paradisini alikowaahidia Mwanangu. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Mei 2014
“
W
anangu wapendwa! Salini
na
mfahamu ya kwamba pasipo Mungu ninyi ni mavumbi. Kwa hiyo geuzeni fikira zenu
na
mioyo yenu kwa Mungu
na
kwa sala. Tegemeeni upendo Wake. Katika Roho ya Mungu ninyi nyote mnaalikwa kuwa mashahidi. Ninyi mna thamani mbele ya Mungu, nami nawaalika, wanangu, kuwa watakatifu, ili mweze kupata uzima wa milele. Kwa hiyo mfahamu ya kwamba maisha haya hupita. Nawapendeni
na
kuwaalika kwa maisha mapya ya kutubu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Juni 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Nawaalika
na
kupokea ninyi nyote kama wanangu. Ninasali ili mnipokee
na
kunipenda kama Mama yenu. Nimewaunga ninyi nyote katika moyo wangu, nimeshuka katikati yenu
na
kuwabariki. Najua kwamba mnataka kwangu faraja
na
tumaini, kwa sababu nawapenda
na
kuwaombea. Nawaomba kujiunga nami katika Mwanangu
na
kuwa mitume wangu. Ili muweze kutenda hivyo nawaalika tena kupenda. Hakuna upendo pasipo sala, hakuna sala pasipo msamaha, maana upendo ni sala,
na
msamaha ni upendo. Wanangu, Mungu aliwaumba ili mpende, pendeni ili muweze kusamehe! Kila sala itokayo katika upendo huwaunganisha
na
Mwanangu
na
Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu awaangaze
na
kuwafanya mitume wangu: mitume ambao, kila watendalo, watalifanya kwa jina la Bwana. Wao watasali kwa matendo
na
siyo kwa maneno tu, kwa maana wanampenda Mwanangu
na
kufahamu njia ya ukweli iongozayo kwenye uzima wa milele. Waombeeni wachungaji wenu, ili waweze kuwaongoza daima kwa moyo safi katika njia ya ukweli
na
upendo, ndiyo njia ya Mwanangu. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Juni 2014
“
W
anangu wapendwa! Yeye Aliye Juu ananipa neema ya kuweza kuwa tena pamoja nanyi
na
kuwaongoza katika sala kuelekea njia ya amani. Mioyo yenu
na
roho zenu zina kiu ya amani
na
upendo, ya Mungu
na
ya furaha yake. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini
na
katika sala mtapata hekima ya kuishi. Nawabarikieni
na
kukuombeeni mbele ya Mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Julai 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Mimi Mama yenu, ninyi mliokusanyika hapa
na
Mama wa ulimwengu mzima, nawabariki kwa baraka ya kimama
na
kuwaalika kuanza safari katika njia ya unyenyekevu. Njia hiyo inawaongoza katika ujuzi wa upendo wa Mwanangu. Mwanangu ni Mwenye uwezo. Yeye yumo katika kila kitu. Kama ninyi, wanangu, hamelewi hayo, basi mtambue kuwa katika roho yenu giza
na
upofu zinatawala. Unyenyekevu tu huweza kuwaponya. Wanangu, mimi nilikuwa nimeishi daima kwa unyenyekevu, kwa uhodari
na
kwa matumaini. Nilijua, nilikuwa nimeelewa ya kuwa Mungu yu ndani yetu
na
sisi ndani ya Mungu. Nawaombeni kuelewa vile vile. Nataka ninyi nyote muwe pamoja nami katika umilele, maana ninyi ni sehemu yangu. Katika njia yenu nitawasaidia. Upendo wangu utawafunika kama joho
na
kuwafanya ninyi mitume wa mwanga wangu, wa mwanga wa Mungu. Kwa upendo utokao katika unyenyekevu, mtaleta mwanga palipotawala giza
na
upofu. Mtaleta Mwanangu, aliye mwanga wa ulimwengu. Mimi ni sikuzote kando ya wachungaji wenu
na
kusali ili wawe siku zote kwenu mfano wa unyenyekevu. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Julai 2014
“
W
anangu wapendwa! Ninyi hamjui neema ya namna gani mnayoishi katika wakati huu ambapo Yeye Aliye Juu awapeni ishara ili mjifungue
na
kutubu. Mwelekeeni Mungu
na
kusali; sala itawale katika mioyo yenu, familia
na
jamaa zenu ili Roho Mtakatifu awaongoze
na
kuhimiza kila siku mjifungue kufanya mapenzi ya Mungu
na
mpango wake kwa kila mmoja wenu. Mimi nipo pamoja nanyi,
na
nawaombeeni pamoja
na
malaika
na
watakatifu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Sababu ya kukaa kwangu pamoja nanyi, utume wangu, ni kuwasaidieni ili wema ushinde, hata kama kwa sasa haya yaonekana ni kitu kigumu sana. Najua kwamba mambo mengi hamyaelewi, kama vile sikuelewa mengi ambayo Mwanangu alinifundisha akiwa alipokua pamoja nami, lakini mimi nilimsadiki
na
kumfuata. Haya nawaombea ninyi pia, kunisadiki
na
kunifuata, lakini, wanangu, kunifuata maana yake ni kupenda mwanangu kuliko wote, kumpenda katika kila mtu pasipo ubaguzi. Ili kuweza kufanya haya yote nawaalikeni tena kujinyima, kusali
na
kufunga. Nawaalikeni ili maisha ya roho yenu yawe ni Ekaristi. Nawaalikeni muwe mitume wangu wa mwanga, ambao wataueneza upendo
na
rehema ulimwenguni. Wanangu, maisha yenu ni mpigo tu wa moyo mbele ya uzima wa milele. Mtakapokuwa mbele ya Mwanangu, Yeye ataona katika mioyo yenu kiasi cha upendo mliokuwa nao. Ili kuweza kueneza kwa njia ya haki upendo nitamwomba Mwanangu kusudi kwa njia ya upendo awapeni umoja kati yenu
na
umoja kati yenu
na
wachungaji wenu. Mwanangu daima anajitoa upya kwa njia yao
na
anafanya mioyo yenu mipya. Msisahau hilo. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Agosti 2014
“
W
anangu wapendwa! Salini kwa nia zangu maana Shetani ataka kuangamiza mpango wangu nilio nao hapa
na
kuwaibia amani: Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini ili Mungu aweze kutenda kazi kwa njia ya kila mmoja wenu. Mioyo yenu iwe wazi kupokea mapenzi ya Mungu. Mimi nawapendeni
na
kubariki kwa baraka ya kimama. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, mimi, Mama yenu, naja tena katikati yenu kwa upendo usio
na
mwisho, kutoka upendo usio
na
kipimo wa Baba wa Mbinguni asiye
na
mwisho.
Na
, nikitazama mioyoni mwenu, naona ya kuwa wengi wenu wanipokea kama Mama
na
, kwa moyo thabiti
na
safi, wataka kuwa mitume wangu. Lakini Mimi ni Mama pia wa ninyi ambao hamnipokei
na
, katika ugumu wa moyo wenu, hamtaki kujua upendo wa Mwanangu. Hamjui jinsi moyo wangu ulivyoteseka
na
jinsi nilivyowaombeeni Mwanangu. Namwomba aponye roho yenu, kwa maana najua Yeye ana uwezo wa kuwaponya. Namwomba awaangaze kwa mwujiza wa mwanga wa Roho Mtakatifu, ili mwache kumsaliti, kumtukana
na
kumwumiza siku zote kwa kuendelea. Nasali kwa Moyo wote ili muweze kuelewa ya kuwa Mwanangu tu ni wokovu
na
mwanga wa ulimwengu. Nanyi, wanangu, mitume wangu wapenzi, mbebeni daima Mwanangu katika moyo
na
fikira zenu. Hivyo ninyi mtakuwa mnabeba Upendo. Wale wote wasiomjua watamtambua katika upendo wenu. Mimi nipo sikuzote karibu yenu. Nipo hasa karibu
na
wachungaji wenu, kwa sababu Mwanangu aliwaita kuwaongozeni katika njia kuelekea milele. Nawashukuru, mitume wangu, kwa sadaka
na
upendo wenu!
”
Ujumbe, 25 Septemba 2014
“
W
anangu wapendwa! Leo pia nawaalika ili ninyi muwe kama nyota ambazo kwa mwangaza wake zinatoa nuru
na
uzuri kwa watu ili wafurahishwe. Wanangu, ninyi pia muwe nuru, uzuri, furaha
na
amani
na
hasa sala kwa wale wote walio mbali
na
upendo wangu
na
upendo wa Mwanangu Yesu. Wanangu, ishuhudieni imani yenu
na
sala yenu katika furaha, katika furaha iliyo mioyoni mwenu
na
salini kwa ajili ya amani iliyo thawabu bora ya Mungu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo wa kimama nawaombeni: pendaneni! mioyoni mwenu muwe kama Mwanangu alitaka tangu awali: kwanza kabisa kumpenda Baba wa Mbinguni
na
kuwa
na
upendo kwa jirani yenu, kuliko yote yaliyopo hapa duniani. Wanangu wapendwa, hamtambui dalili za nyakati hizi? Hamtambui ya kuwa yote yanayotokea kando kando yenu, hutokea kwa sababu hakuna upendo? Fahamuni kwamba wokovu hupatikana katika thamani za kweli, pokeeni uweza wa Baba wa Mbinguni, mpendeni
na
kumheshimu. Fuateni njia ya Mwanangu. Ninyi, wanangu, mitume wangu wapenzi, mnakusanyika siku zote daima kunizunguka maana mna kiu, mna kiu ya amani, ya upendo
na
ya furaha. Kateni kiu yenu katika mikono yangu! Mikono yangu yawatolea Mwanangu, aliye chemchemi ya maji safi. Yeye atafufua imani yenu
na
kusafisha mioyo yenu, kwa sababu Mwanangu hupenda kwa moyo safi
na
mioyo iliyo safi humpenda Mwanangu. Mioyo safi tu ndiyo minyenyekevu
na
yenye imani thabiti. Wanangu, nawaombeni ya kuwa
na
mioyo ya namna hii! Mwanangu aliniambia ya kuwa Mimi ni Mama wa ulimwengu wote: nawaombeni ninyi, mnaonipokea kama Mama, ili kwa maisha yenu, sala
na
sadaka nisaidieni ili wanangu wote wanipokee kama Mama, niweze kuwaongoza kwenye chemchemi ya maji safi. Nawashukuru! Wanangu wapenzi, wachungaji wenu wanapowatolea mwili wa Mwanangu, mshukuruni Mwanangu daima moyoni mwenu kwa sadaka yake
na
kwa wachungaji anayewajalia siku zote.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2014
“
W
anangu wapendwa! Salini katika kipindi hiki cha neema
na
ombeni maombezi ya Watakatifu wote ambao wapo tayari katika mwanga. Wao wawe mfano
na
kichocheo kwenu siku hata siku, katika njia ya uwongofu wenu. Wanangu, mfahamu ya kuwa maisha yenu ni mafupi
na
ya kupita upesi. Kwa hiyo tamanini uzima wa milele
na
mtayarishe mioyo yenu katika sala. Mimi nipo pamoja nanyi
na
ninamwomba Mwanangu kwa ajili ya kila mmoja wenu, hasa kwa wale waliojiweka wakfu kwangu
na
kwa Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Novemba 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, mimi nipo pamoja nanyi kwa baraka ya Mwanangu, pamoja nanyi mnaonipenda
na
mnaotafuta kunifuata. Mimi natamani kuwa pia pamoja nanyi ambao hamtaki kunipokea. Kwenu nyote nafungua moyo wangu wote wa mapendo
na
kuwabariki kwa mikono yangu ya kimama. Mimi ni Mama ninayewaelewa: nilikuwa nimeishi maisha yenu
na
kujaribu mateso
na
furaha yenu. Ninyi mnaoishi katika mateso, mnafahamu maumivu yangu
na
mateso yangu kwa ajili ya wale wanangu wasiokubali kuangazwa
na
mwanga wa Mwanangu, kwa wale wanangu wanaoishi gizani. Kwa hiyo nawahitaji ninyi, ninyi mlioangazwa
na
mwanga
na
kuufahamu ukweli. Nawaalika kumwabudu Mwanangu, ili moyo wenu ukue
na
kuyafikia kweli maisha ya kiroho. Basi mitume wangu, natumaini mtaweza kunisaidia. Kunisaidia maana yake ni kuwaombea wale ambao hawajajua upendo wa Mwanangu. Mkiwaombea, mtamwonyesha Mwanangu ya kuwa mnampenda
na
kumfuata. Mwanangu aliniahidi kwamba uovu hautashinda kamwe, kwa sababu hapo mpo ninyi, roho za wenye haki: ninyi mnaojaribu kusali sala zenu kwa moyo wote; ninyi mnaotolea maumivu
na
mateso yenu kwa Mwanangu; ninyi mnaofahamu ya kuwa maisha ni kufumba
na
kufumbua tu; ninyi mnaotamani Ufalme wa mbinguni. Hayo yote huwafanya muwe mitume wangu
na
kuwaongoza kwenye shangwe ya Moyo wangu. Kwa hiyo wanangu, takaseni mioyo yenu mkamwabudu Mwanangu. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Novemba 2014
“
W
anangu wapendwa! Leo kwa namna ya pekee nawaalikeni msali. Salini, wanangu, ili muweze kutambua ninyi ni akina nani
na
ni wapi mnayopaswa kwenda. Muwe watangazaji wa Habari Njema
na
watu wa matumaini. Muwe upendo kwa wale wote wasio
na
upendo. Wanangu, mtakuwa yote
na
kuyatimiza yote iwapo tu mkisali
na
mkiwa tayari kupokea mapenzi ya Mungu, Mungu ambaye anatamani kuwaongoza katika maisha ya uzima wa milele. Mimi nipo pamoja nanyi
na
siku hata siku ninawaombeeni kwa Mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, zingatieni akilini, kwa maana nawaambia: upendo utashinda! Najua ya kuwa wengi wenu wanapoteza matumaini kwa kuwa wanaona wamezungukwa
na
mateso, maumivu, husuda
na
wivu, hata hivyo mimi ni Mama yenu. Mimi nipo katika Ufalme, lakini hata hapa nipo pamoja nanyi. Mwanangu ananituma tena ili niwasaidieni, kwa hiyo msipoteze matumaini ila nifuateni, kwa maana ushindi wa Moyo wangu ni kwa jina la Mungu. Mwanangu mpendwa anawafikiria, kama alivyofanya siku zote: mwaminini
na
mwishi kama Yeye! Yeye ni uzima wa ulimwengu. Wanangu, kumwishi Mwanangu maana yake ni kuishi Injili. Si kitu rahisi. Ni jambo linalodai upendo, rehema
na
sadaka. Hayo huwatakasa
na
kufungua Ufalme: Sala nyofu, isiyo maneno bali itokayo moyoni, itawasaidieni. Vivyo hivyo kufunga, maana hayo huleta ongezeko la upendo, rehema
na
sadaka. Kwa hiyo msipoteze matumaini, ila nifuateni. Nawaomba tena msali kwa ajili ya wachungaji wenu, ili wamtazame daima Mwanangu, aliyekuwa Mchungaji wa kwanza wa ulimwengu,
na
ambaye familia yake ilikuwa ulimwengu wote. Nawashukuru!
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
Next>>