Our Lady of Medjugorje Messages containing 'na'
Total found:
218
Ujumbe, 2 Januari 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nipo hapa katikati yenu kama Mama atakaye kuwasaidia kuujua ukweli. Nilipokuwa nikiishi maisha kama yenu duniani, nilikuwa nikijua ukweli
na
kwa hivyo kuwa
na
kipande cha Mbinguni duniani. Kwa hiyo, wanangu, nataka ninyi pia muwe washiriki wa hali hivyo. Baba wa Mbinguni ataka mioyo minyofu, ijaayo ujuzi wa ukweli: Ataka muwapende wote mnaokutana nao, maana mimi pia nampenda Mwanangu katika ninyi nyote. Huo ndio mwanzo wa ujuzi wa ukweli. Mtapewa kweli nyingi za uongo. Mtazitambua kwa mioyo iliyotakaswa kwa kufunga, kusali, kwa kufanya toba pamoja
na
kuishika Injili: Huo ndiyo ukweli wa pekee, nao ni ule ambao Mwanangu aliwaachieni. Msiufanyie utafiti mwingi sana: mnaombwa kuupenda
na
kuutoa, kama vile nilivyofanya mimi pia. Wanangu, mkipenda, mioyo yenu itakuwa maskani ya Mwanangu
na
yangu,
na
maneno ya Mwanangu yatakuwa mwongozo wa maisha yenu. Wanangu, nitawatumia, ninyi mitume wa upendo, kusaidia wanangu wote kuujua ukweli. Wanangu, mimi nimeliombea sikuzote Kanisa la Mwanangu, kwa hiyo nawasihi ninyi pia kufanya vile vile. Salini ili wachungaji wenu waangazwe kwa upendo wa Mwanangu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2015
“
W
anangu wapendwa! Hata leo ninawaalika: ishini katika sala mwito wenu. Leo, kama bado haijatokea awali, Shetani atamani kumfunga pumzi binadamu
na
roho yake kwa njia ya upepo wake unaoambukiza chukio
na
hofu. Katika mioyo mingi hakuna furaha kwa sababu hakuna Mungu wala sala. Uadui
na
vita zinaongezeka siku hata siku. Ninawaalika, wanangu, anzisheni upya kwa ari mwelekeo wa kutafuta utakatifu
na
upendo kwa maana nimekuja katikati yenu kwa ajili hiyo. Tuwe upendo
na
msamaha kwa wale wote wanaofahamu
na
kutaka kupenda kwa mapendo ya kibinadamu tu wala siyo kwa ule upendo mkubwa sana wa kimungu ambao Mungu anatualikia. Wanangu, matumaini ya kesho iliyo bora zaidi yawe daima mioyoni mwenu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nipo hapa katikati yenu. Ninawatazama, ninawapa tabasamu
na
kuwapenda kama mama peke yake awezavyo kufanya. Kwa neema ya Roho Mtakatifu ajaye kwa njia ya usafi wangu, ninaona mioyo yenu
na
kuitolea kwa Mwanangu. Tangu muda mrefu nawaombeni muwe mitume wangu,
na
kusali kwa ajili ya wale wasioujua upendo wa Mungu. Naomba sala inayotokana
na
upendo, sala itoayo matunda
na
sadaka. Msipotee muda kutaka kuelewa kama mnastahili kuwa mitume wangu, Baba aliye Mbinguni atahukumu wote, lakini ninyi mpendeni
na
msikilizeni. Najua ya kuwa mambo hayo yote yanawafadhaisha, hata ujio wangu katikati yenu, lakini upokeeni kwa furaha
na
salini ili muelewe kwamba mnastahili kufanya kazi kwa ajili ya ufalme wa mbingu. Upendo wangu ni juu yenu. Salini ili upendo wangu udumu ndani ya kila moyo, kwa maana upendo huo unaosamehe ujitolea bila kukata tamaa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2015
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika nyote: salini zaidi
na
muongee kidogo. Katika kusali tafuteni mapenzi ya Mungu
na
yaishini kadiri ya amri ambazo Mungu anawaalika kuziishi. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kusali pamoja nanyi. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninyi ni nguvu yangu. Ninyi, mitume wangu, ambao, kwa upendo wenu, unyenyekevu
na
sala ya kimya kimya, mnamwezesha Mwanangu ajulikane. Ninyi mnaishi ndani yangu. Ninyi mnanibeba mioyoni mwenu. Ninyi mnajua ya kuwa mna Mama awapendaye
na
aliyekuja kuwaletea upendo. Nawatazama katika Baba wa Mbinguni, natazama fikira zenu, maumivu yenu, mateso yenu
na
kuyaleta kwa Mwanangu. Msiogope! Msipoteze matumaini, maana Mwanangu humsikiliza Mama yake. Yeye hupenda tangu alipozaliwa,
na
ndio furaha yangu ya kuwa wanangu wote wajue upendo huo;
na
wote wale ambao, kwa sababu ya maumivu yao
na
kutoelewa kwao, walimwacha waweze kurudi kwake,
na
wote wao wasiomjua wamjue. Kwa sababu hiyo ninyi hapa ni mitume wangu, nami pia pamoja nanyi kama Mama yenu. Salini ili kuwa imara katika imani, maana upendo
na
rehema hutoka katika imani imara. Kwa njia ya upendo
na
rehema mtawasaidia wale wote wasiofahamu ya kuwa wanachagua giza badala ya nuru. Salini kwa ajili ya wachungaji wenu, maana wao ni nguvu ya Kanisa ambayo Mwanangu aliwaachieni. Kwa njia ya Mwanangu wao ni wachungaji wa roho. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Machi 2015
“
W
anangu wapendwa! Hata leo pia Yeye Aliye Juu ameniruhusu kuwa pamoja nanyi
na
kuwaongoza katika njia ya uwongofu. Mioyo mingi imejifunga kwa neema wala haitaki kusikiliza mwaliko wangu. Ninyi wanangu salini
na
pambaneni
na
kishawishi
na
mipango yote ya uovu ambayo anayowapatia shetani kwa njia ya mambo ya kisasa. Muwe hodari katika kusali
na
mkishika msalaba mikononi salini ili maovu yasiwatumie wala kuwashinda. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwaombea. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Aprili 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nimewachagua ninyi, mitume wangu, kwa maana kila mmoja wenu huchukua ndani yake jambo njema. Ninyi mnaweza kunisaidia ili ule upendo ambao kwao Mwanangu amekufa,
na
kufufuka baadaye, ushinde tena. Kwa hiyo nawaalika, mitume wangu, kujaribu kuona katika kila kiumbe cha Mungu, katika wanangu wote, kitu chema
na
kujitahidi kuwaelewa. Wanangu, ninyi nyote ni kaka
na
dada kwa njia ya huyo Roho Mtakatifu. Ninyi mliojaa upendo kwa ajili ya Mwanangu, mnaweza kuwaeleza wote ambao hawajui cho chote kuhusu upendo huo, yote mnayoyafahamu. Ninyi mmejua upendo wa Mwanangu, mnaelewa ufufuko wake,
na
mnamgeuzia macho kwa furaha. Haja yangu ya kimama ni kwamba wanangu wote waungane katika upendo wa Yesu. Kwa hiyo nawaalika, mitume wangu, kuishi kwa furaha Ekaristi maana, katika Ekaristi, mwanangu anajitoa kwa ajili yenu tena
na
tena,
na
kwa mfano wake, anawaonyesha namna ya kutoa upendo
na
sadaka kwa jirani. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2015
“
W
anangu wapendwa! Mimi nipo pamoja nanyi hata leo niwaongozeni kwenye wokovu. Moyo wenu una wasiwasi maana roho yenu ni dhaifu
na
imechoka kwa mambo yote ya dunia. Ninyi wanangu, ombeni Roho Mtakatifu awageuze
na
kuwajaza nguvu yake ya imani
na
tumaini ili muweze kuwa imara katika kupambana kwenu
na
maovu. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwaombea kwenye Mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, fungueni mioyo yenu mkajaribu kuhisi jinsi ninavyowapenda
na
kutaka mpendeni Mwanangu. Nataka mpende zaidi kwa kuwa haiwezekani kumjua pasipo kumpenda, maana Yeye ndiye upendo. Wanangu, mimi nawajueni: najua maumivu yenu
na
mateso yenu maana niliyaishi. Nafurahi pamoja nanyi kwa furaha zenu. Nalia machozi pamoja nanyi katika maumivu yenu. Sitawaacheni kamwe. Nitaongea nanyi daima kwa upole wa kimama
na
, kama mama, nahitaji mioyo yenu ifumbuliwe, ili kwa hekima
na
unyofu mueneze upendo wa Mwanangu. Nawahitaji ninyi mfumbuliwe
na
kuwa wepesi kupokea mema
na
huruma. Nahitaji muungano wenu
na
Mwanangu, kwa maana nataka mpate kufanikiwa
na
kumsaidia kuleta heri kwa wanangu wote. Mitume wangu, nawahitaji, ili muwaonyeshe wote ukweli wa Mungu, ili moyo wangu, ulioteswa
na
kuteswa hata leo kupita kiasi, uweze kushinda katika upendo. Salini kwa ajili ya utakatifu wa wachungaji wenu, ili katika jina la Mwanangu, waweze kutenda maajabu, maana utakatifu hutenda maajabu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Mei 2015
“
W
anangu wapendwa! Hata leo mimi nipo pamoja nanyi
na
kwa furaha nawaalikeni nyote: salini
na
aminini nguvu ya sala. Fungueni mioyo yenu, wanangu, ili Mungu awajaze upendo wake, nanyi mtakuwa furaha ya watu wengine. Ushahidi wenu utakuwa
na
nguvu
na
lote mfanyalo litaendana
na
mapenzi ya Mungu. Mimi nipo pamoja nanyi, nikisali kwa ajili yenu
na
kwa ajili ya wokovu wenu hata mtakapomweka Mungu mahali pa kwanza. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Juni 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nataka kufanya kazi kwa njia yenu, wanangu, mitume wangu, ili mwishowe niweze kukusanya wanangu wote pale ambapo pameandaliwa tayari kwa ajili ya furaha yenu. Nawaombea, kusudi kwa matendo yenu muweze kugeuza, kwani muda umefika kwa matendo ya kweli, kwa ajili ya Mwanangu. Upendo wangu utafanya kazi ndani mwenu, nitawatumia ninyi. Muwe
na
imani nami, kwani yote ninayotamani, ninayatamani kwa ajili yenu, wema wa milele, ulioumbwa kwa njia ya Baba wa Mbinguni. Ninyi, wanangu, mitume wangu, muishi maisha ya duniani pamoja
na
wanangu ambao hawafahamu upendo wa Mwanangu, wale ambao hawaniiti mama. Lakini msiogope kushuhudia ukweli, kwa maana ikiwa ninyi hamtaogopa
na
kushuhudia ukweli kwa uhodari, ukweli utashinda kimuujiza. Kumbukeni: nguvu iko katika upendo. Wanangu, upendo ndio kutubu, kusamehe, kusali, kujitoa sadaka
na
rehema, maana mkijua kupenda kwa matendo mtawabadilisha
na
wengine, mtawezesha mwanga wa Mwanangu uingie katika mioyo yao. Nawashukuru. Muwaombee wachungaji wenu, wao ni mali ya Mwanangu. Yeye aliwaita. Salini ili wawe siku zote
na
nguvu
na
uhodari wa kung'aa kwa nuru ya Mwanangu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Juni 2015
“
W
anangu wapendwa! Hata leo Yeye Aliye Juu ananipa neema ya kuweza kuwapenda
na
kuwaalika muweze kuongoka. Wanangu, Mungu awe kesho yenu, vita, wasiwasi, huzuni yasiwatawale, ila furaha
na
amani zitawale mioyoni mwa watu wote,
na
mjue kuwa pasipo Mungu hamtapata kamwe amani. Kwa hiyo, wanangu, mrudieni Mungu
na
sala ili mioyo yenu iimbe kwa furaha. Mimi nipo pamoja nanyi
na
ninawapenda kwa upendo usio
na
kipimo. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Julai 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawaalika kueneza imani katika Mwanangu, imani yenu. Ninyi wanangu, mlioangazwa
na
Roho Mtakatifu, mitume wangu, itangazeni imani kwa watu wengine, yaani kwa wasiosadiki, wasioijua
na
wasiotaka kuijua. Kwa sababu hiyo yawapasa kusali sana kwa ajili ya zawadi ya upendo, maana upendo ndio alama maalum ya imani ya kweli,
na
ninyi mtakuwa mitume wa upendo wangu. Upendo hufanya upya daima maumivu
na
furaha ya Ekaristi, hufanya upya maumivu ya Mateso ya Mwanangu, aliyewaonyesha upendo usio
na
kifani; hufanya upya furaha ya tendo la kuwaachia Mwili wake
na
Damu yake kwa ajili ya kuwalisha
na
hivyo kuwa kitu kimoja nanyi. Nikiwaangalia kwa wema nahisi upendo pasipo kiasi, ulioniimarisha katika hamu yangu ya kuwaongoza katika imani thabiti. Imani thabiti itawapa furaha
na
uchangamfu duniani,
na
mwishowe kuwaunganisha
na
Mwanangu. Hiyo ndiyo hamu yake. Kwa hiyo mwishi katika Yeye,
na
katika upendo, isheni katika nuru iliyowaangaza daima katika Ekaristi. Nawaombeni kusali sana kwa wachungaji wenu, kusali ili kupata upendo mkubwa kwa ajili yao, kwa maana Mwanangu aliwapeni ili waweze kuwalisha kwa Mwili wake
na
kuwafundisha upendo. Kwa hiyo wapendeni ninyi pia! Lakini, wanangu, kumbukeni: upendo maana yake ni kuvumilia
na
kutoa
na
kutohukumu kamwe. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Julai 2015
“
W
anangu wapendwa, hata leo kwa furaha nipo pamoja nanyi
na
ninawaalika wote, wanangu, salini, salini, salini, ili muweze kuelewa upendo nilio nao kwenu. Upendo wangu una nguvu kuliko uovu, kwa hiyo wanangu mjongeeni Mungu ili muweze kuonja furaha yangu kwa Mungu. Pasipo Mungu, wanangu, hamtakuwa
na
wakati ujao, wala tumaini, wala wokovu, kwa hiyo acheni uovu
na
chagueni wema: Mimi nipo pamoja nanyi
na
pamoja nanyi namwomba Mungu kwa mahitaji yenu yote. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, mimi, kama Mama apendaye wanawe, natambua jinsi ulivyo mgumu muda huu mnaouishi. Naona mateso yenu, lakini jueni kwamba hamko peke yenu: Mwanangu yu pamoja nanyi! Yeye yupo popote, asiyeonekana, lakini mtaweza kumwona ikiwa mtamwishi. Yeye ndiye nuru inayoangaza roho yenu
na
kuleta amani. Yeye ndiye Kanisa, mnalopaswa kulipenda, kuliombea
na
kulilinda daima: si kwa maneno tu, bali kwa matendo ya upendo. Wanangu, fanyeni yote ili Mwanangu ajulikane kwa watu wote,
na
aweze kupendwa, kwa maana ukweli ni katika Mwanangu, aliyezaliwa
na
Mungu, Mwana wa Mungu. Msipoteze muda kwa kufikiri mno; mtajitenganisha
na
ukweli. Pokeeni Neno lake kwa moyo mnyofu
na
kuliishi. Mkiishi Neno lake, mtasali. Mkiishi Neno lake, mtapenda kwa upendo wenye huruma,
na
mtapendana. Kwa kadiri mtakavyokuwa
na
upendo hivyo ndivyo mtakavyokuwa mbali
na
kifo. Kwa wale watakaoishi
na
kulipenda Neno la Mwanangu, kifo kitakuwa uhai kwao. Nawashukuru! Salini kwa ajili ya kuweza kuona Mwanangu katika wachungaji wenu. Salini kwa ajili ya kuweza kumkumbatia katika wao.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2015
“
W
anangu wapendwa, hata leo ninawaalika: muwe sala. Sala iwe mabawa kwa ajili ya mkutano kati yenu
na
Mungu. Ulimwengu upo katika wakati wa kujaribiwa, kwa maana umemsahau
na
kumwacha Mungu. Kwa hiyo wanangu, muwe wale wanaomtafuta
na
kupenda Mungu kuliko yote. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwaongoza kwa Mwanangu, lakini ninyi hamna budi kunena "NDIYO" yenu katika uhuru wa wana wa Mungu. Nawaombeeni
na
kuwapenda, wanangu, kwa upendo usio
na
mwisho. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, wapendwa mitume wangu wa upendo, waletaji wangu wa ukweli, ninawaalika tena
na
ninawakusanya karibu nami ili mnisaidie, ili muwasaidie wanangu wote wenye kiu ya upendo
na
ukweli, wenye kiu ya Mwanangu. Mimi ndimi neema ya Baba wa Mbinguni iliyotumwa kuwasaidieni kuishi neno la Mwanangu. Pendaneni. Nimeyaishi maisha yenu duniani. Najua kwamba si kitu rahisi kila mara lakini, mkipendana, mtasali kwa moyo, mtafikia vilele vya maisha ya roho,
na
njia ya kwenda mbinguni itafunguliwa mbele yenu. Pale nawangojea mimi, Mama yenu, kwa maana mimi nipo pale. Muwe waaminifu kwa Mwanangu
na
muwafundishe wengine uaminifu. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwasaidia. Nitawafundisha imani, ili muweze kuwafikishia wengine kwa njia sahihi. Nitawafundisha ukweli, ili muweze kuufahamu. Nitawafundisha upendo, ili mjue upendo wa kweli ni kitu gani. Wanangu, Mwanangu atafanya yote ili aongee kwa njia ya maneno
na
matendo yenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2015
“
W
anangu wapendwa, hata leo ninamwomba Roho Mtakatifu ili ajaze mioyo yenu kwa imani thabiti. Sala
na
imani zitajaza mioyo yenu kwa upendo
na
furaha, nanyi mtakuwa ishara kwa wale walio mbali
na
Mungu. Wanangu, mpeane moyo wenyewe kwa wenyewe ili kufanya sala ya moyo, ili sala iweze kujaza maisha yenu
na
ninyi, wanangu, kila siku muwe mashahidi wa utumishi: kwa Mungu katika kuabudu
na
kwa majirani zenu katika mahitaji yao. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwaombea ninyi nyote. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nipo hapa katikati yenu kuwatieni moyo, kuwajaza kwa upendo wangu, kuwaalika tena kuwa mashahidi wa upendo wa Mwanangu. Wanangu wengi hawana tumaini, hawana amani, hawana upendo. Wao wanatafuta Mwanangu lakini hawajui jinsi wala wapi ya kumpata. Mwanangu awafungulia mikono Yake, nanyi wasaidieni ili waje mikononi Mwake. Wanangu, kwa hiyo ni lazima msali kwa upendo, lazima msali sana, sana, ili kupata upendo zaidi
na
zaidi, kwa maana upendo hushinda mauti
na
hudumisha maisha. Watume wa upendo wangu, wanangu wenye moyo mnyofu
na
safi, jiungeni zaidi
na
zaidi katika kusali. Mnatengana sana! Jipeni moyo katika kukua kiroho, kama vile Mimi ninawapeni moyo. Ninawaangalia
na
nipo karibu nanyi kila mnaponifikiria. Waombeeni wachungaji wenu, wale walioacha yote kwa ajili ya Mwanangu. Wapendeni
na
waombeeni, Baba wa Mbinguni husikiliza sala zenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2015
“
W
anangu wapendwa, sala yangu hata leo ni kwa ajili yenu nyote, hasa kwa wale walio
na
mioyo migumu kuitikia wito wangu. Mnaishi katika siku za neema wala hamtambui fadhili ambazo Mungu anawapeni kwa njia ya uwepo wangu. Wanangu, amueni hata leo kuwa watakatifu
na
jifunzeni kutokana
na
mifano ya watakatifu wa siku hizi
na
mtatambua ya kuwa utakatifu ni ukweli uliopo kwa ajili yenu nyote. Wanangu, furahini katika upendo kwa maana machoni pa Mungu ninyi ni wa pekee
na
hakuna atakayechukua nafasi ya mwingine, kwa maana ninyi ni furaha ya Mungu duniani hapa. Mshuhudieni amani, sala
na
upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
Next>>