Our Lady of Medjugorje Messages containing 'na'
Total found:
218
Ujumbe, 2 Novemba 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nataka kuongea nanyi tena juu ya upendo. Nimewakusanya kunizunguka kwa Jina la Mwanangu, kwa kadiri ya mapenzi yake. Nataka imani yenu iwe thabiti
na
iwe inatokana
na
mapendo, kwa maana wanangu wale wanaoelewa upendo wa Mwanangu
na
kuufuata, huishi katika mapendo
na
matumaini. Wamejua upendo wa Mungu. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini ili muweze kupenda zaidi muwezavyo
na
kutenda matendo ya upendo. Kwa maana, imani peke yake, pasipo upendo wala matendo ya upendo, si neno ninaloomba kwenu. Wanangu, ule ni utovu wa imani, ni kujisifu mwenyewe. Mwanangu hutaka imani
na
matendo, upendo
na
wema. Mimi ninasali, lakini nawaombeni pia kusali
na
kuishi upendo, kwa maana nataka ya kuwa Mwanangu, atakapoona mioyo ya wanangu wote, aweze kuona ndani yake upendo
na
wema, sio chukio
na
ubaridi. Wanangu, mitume ya upendo wangu, msipoteze tumaini, msikate tamaa: ninyi mnaweza kufanya! Mimi ninawapeni moyo
na
kuwabariki, maana yote yaliyopo duniani hapa - ambayo kwa bahati mbaya wanangu wengi huweka mahali pa kwanza - yatatoweka
na
upendo
na
matendo ya upendo tu zitabaki, nazo zitawafungulia malango ya Ufalme wa Mbinguni. Nitawangojea karibu
na
malango hayo, karibu
na
malango hayo nataka kuwangojea
na
kuwakumbatia wanangu wote. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2015
“
W
anangu wapendwa, leo ninawaalika nyote: salini kwa ajili ya nia zangu. Amani ipo hatarini kwa hiyo wanangu, salini
na
muwe waletaji wa amani
na
matumani katika ulimwengu huu wa wasiwasi ambamo shetani anashambulia
na
kuleta majaribu ya kila aina. Wanangu muwe thabiti katika sala
na
imara katika imani. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwaombea ninyi nyote mbele ya Mwanangu, Yesu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, mimi ni sikuzote pamoja nanyi, kwa maana Mwanangu alinikabidhi ninyi. Nanyi, wanangu, mnanihitaji mimi, mnitafute, mnijie
na
mfurahishe Moyo wangu wa kimama. Mimi ninawapenda
na
nitawapenda ninyi mnaoteseka
na
kutolea mateso yenu kwa ajili ya Mwanangu
na
kwa ajili yangu. Upendo wangu hutafuta upendo wa wanangu wote
na
wanangu wote hutafuta upendo wangu. Kwa njia ya upendo Yesu hutafuta ushirika kati ya Mbingu
na
dunia, kati ya Baba wa mbinguni
na
ninyi, wanangu, Kanisa lake. Kwa hiyo lazima kusali sana, kusali
na
kulipenda Kanisa ambalo ninyi ni wake. Sasa Kanisa linateseka
na
kuhitaji mitume ambao, wakipenda ushirika, wanaposhuhudia
na
kutoa, waonyeshe njia za Mungu. Kanisa linahitaji mitume ambao, wakiishi Ekaristi kwa moyo, watende matendo makuu. Kanisa linawahitaji ninyi, mitume wangu wa upendo. Wanangu, Kanisa limeteswa
na
kusalitiwa tangu siku zake za awali, lakini linazidi kukua siku hata siku. Kanisa halitaharibiki, kwa maana Mwanangu alilipa moyo: Ekaristi. Nuru ya ufufuo wake imeng’aa
na
itang’aa juu yake. Kwa hiyo msiogope! Waombeeni wachungaji wenu, ili wawe
na
nguvu
na
upendo kwa kuwa madaraja ya wokovu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2015 - Tokeo la Yakov
“
W
anangu wapendwa, miaka hii yote ambapo Mungu ananijalia kuwepo pamoja nanyi ni ishara ya upendo mwingi sana wa Mungu kwa kila mmoja wenu
na
ishara ya jinsi alivyowapenda. Wanangu, Yeye Aliye Juu amewapeni neema nyingi
na
anataka kuwapa neema nyingi zaidi. Lakini, wanangu, mioyo yenu imefungwa, inaishi katika hofu
na
hayaruhusu upendo wa Yesu
na
amani yake yapate nafasi katika mioyo yenu
na
kutawala maisha yenu. Kuishi pasipo Mungu ni kuishi gizani wala kutoujua kamwe upendo wa Baba
na
ulinzi wake kwa kila mmoja wenu. Kwa hiyo wanangu, leo hasa mwombeni Yesu ili tangu leo maisha yenu yapate kuzaliwa upya katika Mungu,
na
maisha yenu iwe nuru itokayo kwenu. Namna hii mtakuwa mashahidi wa uwepo wa Mungu ulimwenguni hasa kwa kila mtu aishiye gizani. Wanangu, nawapenda
na
kuwaombeeni kila siku kwake Yeye Aliye Juu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2015
“
W
anangu wapendwa, Leo pia nawaletea Mwanangu Yesu katika mikono yangu,
na
kwa mikono hiyo nawapeni amani Yake
na
hamu ya Mbinguni. Ninasali pamoja nanyi kwa ajili ya amani
na
ninawaalika muwe amani. Nawabariki wote kwa baraka yangu ya kimama
na
ya amani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kama Mama nafurahi ya kuwa katikati yenu, kwa maana nataka kuongea nanyi tena kuhusu maneno ya Mwanangu
na
upendo wake. Natumaini mtanipokea kwa upendo, maana maneno ya Mwanangu
na
upendo wake ni nuru
na
tumaini la pekee katika giza la siku hizi. Huu ni ukweli wa pekee, nanyi mtakaoupokea
na
kuuishi, mtakuwa
na
mioyo safi
na
minyenyekevu. Mwanangu hupenda mioyo safi
na
minyenyekevu. Mioyo safi
na
minyenyekevu inahuisha maneno ya Mwanangu: inayaishi, inayaeneza
na
kufanya hata wote wayasikie. Maneno ya Mwanangu yanaamsha maisha ya wale wanaoyasikiliza, maneno ya Mwanangu hurudisha upendo
na
matumaini. Kwa hiyo, mitume wangu wapenzi, wanangu, isheni maneno ya Mwanangu. Pendaneni kama Yeye alivyowapenda. Pendaneni katika jina lake
na
kumbukumbu lake. Kanisa huendelea
na
kukua kwa ajili ya wale wanaosikiliza maneno ya Mwanangu, kwa sababu ya wanaohuzunika
na
kuteseka kimyakimya katika tumaini la kukombolewa milele. Kwa hiyo wanangu wapendwa, maneno ya Mwanangu
na
upendo wake yawe wazo la kwanza
na
la mwisho la siku yenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2016
“
W
anangu wapendwa, hata leo nawaalika kusali. Pasipo sala hamwezi kuishi maana sala ndiyo mnyororo unaowawezesha kumkaribia Mungu. Kwa hiyo wanangu, kwa unyenyekevu wa moyo mrudieni Mungu
na
Amri zake ili muweze kusema kwa moyo wote: kama mbinguni lifanyike hata duniani. Wanangu, ninyi ni huru kuamua katika uhuru kuwa wa Mungu ama dhidi yake. Tazameni kama shetani anavyotaka kuwaingiza katika dhambi
na
utumwa. Kwa hiyo, wanangu, rudini kwa Moyo Wangu ili Mimi niweze kuwaongoza kwa Mwanangu Yesu aliye Njia,
na
Ukweli
na
Uzima. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nimewaalika
na
ninawaalika tena kumjua Mwanangu, kuujua ukweli. Mimi nipo pamoja nanyi
na
ninasali ili mfanikiwe. Wanangu, yawapasa kusali sana ili kupata upendo
na
uvumilivu mwingi kadiri muwezavyo, ili kuweza kuvumilia sadaka
na
kuwa maskini rohoni. Mwanangu, kwa njia ya Roho Mtakatifu, yu sikuzote pamoja nanyi. Kanisa lake huzaliwa katika kila moyo unaomjua. Salini ili muweze kumjua Mwanangu, salini ili roho yenu iwe kitu kimoja pamoja naye. Hiyo ndiyo sala
na
huo ndio upendo wa kuwavutia wengine
na
kuwafanyeni kuwa mitume wangu. Ninawatazama kwa upendo, kwa upendo wa kimama. Ninawajua, najua maumivu yenu
na
mateso yenu, kwa maana Mimi nami niliteswa kimya. Imani yangu ilinipa upendo
na
tumaini. Ninawaambieni tena: Ufufuo wa Mwanangu
na
Kupokewa kwangu mbinguni ni tumaini
na
upendo kwa ajili yenu. Kwa hiyo, wanangu, salini ili kujua ukweli, ili kupata imani thabiti, ya kuongoza mioyo yenu
na
kuweza kugeuza mateso yenu
na
maumivu yenu kuwa upendo
na
tumaini. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2016
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema nawaalikeni nyote kuongoka. Wanangu, mnapenda kidogo,
na
bado mnasali kidogo. Mmepotea wala hamjui lengo lenu ni nini. Chukueni msalaba wenu, mwangalieni Yesu mumfuate. Yeye anajitoa kwenu hata kufa msalabani maana anawapenda. Wanangu, nawaalikeni kurudia kusali kwa moyo kwa maana katika sala mnaweza kupata matumaini
na
maana ya uwepo wenu. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwaombea. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ujio wangu kwenu ni zawadi ya Baba wa Mbinguni kwa ajili yenu. Kwa njia ya upendo wake ninakuja kuwasaidieni kupata njia inayowangoza kwenye ukweli,
na
kupata njia inayowaongoza kwa Mwanangu. Ninakuja kuwathibitishia ukweli. Nataka kuwakumbushia maneno ya Mwanangu. Yeye aliyatamka maneno ya wokovu kwa ulimwengu wote, maneno ya upendo kwa watu wote, ule upendo aliouonyesha kwa kujitolea kwake sadaka. Lakini hata leo wanangu wengi hawamjui, hawataki kumjua, hawamjali. Kwa sababu ya kutokujali kwao, moyo wangu unateseka kwa uchungu. Mwanangu amekuwa daima katika Baba. Alipozaliwa duniani, ametuletea Umungu, wakati kutoka kwangu ameuchukua ubinadamu. Kwa njia yake Neno limefika katikati yetu. Kwa njia yake Mwanga, ambao hupenyeza mioyoni, huiangaza, huijaza upendo
na
faraja, umeingia ulimwenguni. Wanangu, wanaweza kumwona Mwanangu wale wote wanaompenda, kwa kuwa uso wake huonekana kwa njia ya mioyo inayojaa mapendo kumwelekea Yeye. Kwa hiyo, wanangu, mitume wangu, mnisikilize! Acheni uovu
na
ubinafsi. Msiishi tu kwa ajili ya vitu vya ulimwengu, vinavyoharibika. Mpendeni Mwanangu
na
muwawezeshe wengine kuutambua uso kwa njia ya mapendo mliyo nayo kwake. Mimi nitawasaidia kumjua zaidi. Mimi nitawaeleza kuhusu Yeye. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Machi 2016
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaletea upendo wangu. Mungu ameniruhusu kuwapenda ninyi
na
kwa upendo nawaalika mwongoke. Wanangu, ninyi ni maskini katika upendo,
na
wala hamjaelewa bado ya kuwa Mwanangu Yesu ametolea maisha Yake ili awaokoeni
na
kuwapa uzima wa milele. Kwa hiyo salini wanangu, salini ili muweze kuelewa katika sala upendo wa Mungu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Aprili 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, msiwe
na
mioyo migumu, iliyofungwa
na
iliyojaa hofu. Pokeeni upendo wangu wa kimama uiangaze
na
kuijaza mioyo yenu upendo
na
matumaini, ili, kama Mama, niyalainishe maumivu yenu: ninayajua,
na
nimeyaonja. Maumivu huinua nayo ni sala kuu kuliko zote. Mwanangu huwapenda hasa wanaopokea maumivu. Alinituma Mimi niyalainishe
na
kuwaletea matumaini. Mumwamini Yeye. Najua kuwa ni vigumu kwenu, maana mnaona giza linalozidi kuongeza karibu yenu pande zote. Wanangu, giza mtalivunja kwa njia ya sala
na
upendo. Yule anayesali
na
kupenda haogopi, ana matumaini
na
upendo wenye huruma: Anaona mwanga,
na
anamwona Mwanangu. Kama mitume wangu nawaalika mjaribu kuwa mfano wa upendo wenye huruma
na
wenye matumaini. Salini sikuzote tena kwa ajili ya kupata upendo mwingi kadiri muwezavyo, maana upendo huleta mwanga unaovunja kila giza,
na
humleta Mwanangu. Msiogope, ninyi si peke yenu: Mimi nipo pamoja nanyi! Ninawasihi waombeeni wachungaji wenu, ili wawe
na
upendo kila wakati
na
wawe
na
matendo ya upendo kwa Mwanangu, kwa njia yake
na
kwa kumkumbuka Yeye. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2016
“
W
anangu wapendwa! Moyo wangu usio
na
doa unatoka damu nikiwaangalieni katika dhambi
na
mazoea mabaya. Nawaalika: mrudieni Mungu
na
salini ili mpate kufanikiwa duniani. Mungu anawaalika kwa njia yangu ili mioyo yenu iwe tumaini
na
furaha kwa wale wote walio mbali. Ombi langu liwe kwenu manukato kwa nafsi
na
moyo ili mtukuze Mungu Mwumbaji anayewapenda
na
kuwaalika kwa mambo ya milele. Wanangu, maisha ni mafupi, mtumie nafasi hii kwa ajili ya kutenda mema. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Moyo wangu wa kimama hutaka wongofu wenu mnyofu
na
ya kuwa muwe
na
imani thabiti, ili muweze kuwatangazia watu wote wanaowazunguka upendo
na
amani. Lakini, wanangu, msisahau: kila mmoja wenu mbele ya Baba aliye Mbinguni ni ulimwengu wa pekee! Kwa hiyo nguvu ya Roho Mtakatifu isiyo kifani iweze kutenda kazi ndani mwenu! Muwe wanangu safi kwa kiroho. Katika karama ya kiroho kuna uzuri. Yote yaliyo ya kiroho ni hai
na
nzuri ajabu. Msisahau ya kuwa katika Ekaristi, iliyo moyo wa imani, Mwanangu yu daima pamoja nanyi. Yeye anawajia
na
pamoja nanyi humega mkate maana, Mwanangu, kwa ajili yenu amekufa, amefufuka akaja tena. Haya maneno yangu ni ya muhimu kwa maana ni ukweli,
na
ukweli haubadiliki: lakini wanangu wengi hawayatambui. Wanangu, maneno yangu si mazee wala mapya, ni ya milele. Kwa hiyo nawaalika ninyi, wanangu, kuangalia alama za nyakati,
na
"kukusanya misalaba yaliyovunjika"
na
kuwa mitume wa Ufunuo. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Mei 2016
“
W
anangu wapendwa! Uwepo wangu ni zawadi ya Mungu
na
kichocheo cha uwongofu wenu. Shetani ana nguvu
na
anataka kutia moyoni
na
fikirani mwenu fujo
na
wasiwasi. Kwa hiyo, ninyi wanangu salini ili Roho Mtakatifu awaongoze katika njia iliyonyoka ya furaha
na
amani. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwaombea ninyi mbele ya Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Juni 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kama Mama wa Kanisa, kama Mama yenu, ninatabasamu nikiwaona kunijia, kukusanyika kandokando yangu
na
kunitafuta. Ujio wangu katikati yenu ni onyesho la kadiri Mbingu inavyowapenda. Ujio wangu unawaonyesha njia ya kuelekea kwenye uzima wa milele, kuelekea wokovu. Mitume wangu, ninyi mnaojaribu kuwa
na
moyo safi
na
Mwanangu ndani yake, ninyi mpo katika njia njema. Ninyi mnamtafuta Mwanangu, mnatafuta njia njema. Yeye aliacha dalili nyingi za upendo wake. Ameacha tumaini. Ni rahisi kumpata, ikiwa mpo tayari kujitolea
na
kutubu, ikiwa mtakuwa
na
uvumilivu, rehema
na
upendo kwa jirani. Wanangu wengi hawaoni wala hawasikii maana hawataki. Hawapokei maneno
na
matendo yangu, lakini Mwanangu, kwa njia yangu, anawaalika wote. Roho yake huangaza wote katika mwanga wa Baba wa Mbinguni, katika ushirika kati ya Mbingu
na
dunia, katika upendano; maana upendo huita upendo
na
kutenda ili matendo yawe muhimu kuliko maneno. Kwa hiyo, mitume wangu, mliombee Kanisa lenu, lipende
na
tendeni matendo ya upendo. Ingawa limesalitiwa
na
kujeruhiwa, lipo hapa kwa sababu hutoka kwa Baba wa Mbinguni. Muwaombeeni wachungaji wenu, ili kuona ndani yao ukuu wa upendo wa Mwanangu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Juni 2016
“
W
anangu wapendwa! Mshukuruni Mungu kwa zawadi ya kuwepo kwangu pamoja nanyi. Salini, wanangu, mkaishi amri za Mungu mweze kuwa
na
heri duniani. Leo, katika siku hii ya neema nataka kuwapeni baraka yangu ya kimama ya amani
na
ya upendo wangu. Ninawaombeeni kwa Mwanangu
na
kuwaalika kudumu katika sala ili pamoja nanyi niweze kutimiza mipango yangu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Julai 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, uwepo wangu halisi
na
wa uhai katikati yenu uwafanye kuwa wenye furaha kwani huo ni upendo mkuu wa Mwanangu. Yeye ananituma katikati yenu ili, kwa upendo wa kimama, Mimi niwaimarishe; ili muelewe kwamba maumivu
na
furaha, mateso
na
mapendo husaidia nafsi yenu kuishi kwa bidii zaidi; ili niwaalike tena kuadhimisha Moyo wa Yesu, moyo wa imani: Ekaristi. Mwanangu, siku kwa siku, hurudi hai katikati yenu: huwarudia, hata kama hakuwaacha kamwe. Wakati mmoja wenu, wanangu, anamrudia, Moyo wangu wa kimama hushtuka kwa furaha. Kwa hiyo Wanangu, irudieni Ekaristi, mrudieni Mwanangu. Njia ya kumrudia Mwanangu ni ngumu
na
imejaa kujinyima lakini mwishowe, kuna mwanga siku zote. Naelewa maumivu yenu
na
mateso yenu,
na
kwa upendo wa kimama, ninapangusa machozi yenu. Mtumainini Mwanangu, kwa maana Yeye atawafanyieni neno msilojua hata kuomba. Ninyi, wanangu, fikirieni nafsi yenu tu, kwani nafsi ni kitu cha pekee mliyo nayo duniani. Chafu ama safi, mtaichukua mbele ya Baba aliye Mbinguni. Kumbukeni: imani katika upendo wa Mwanangu hulipwa siku zote. Nawaambieni kuwaombea hasa wale ambao Mwanangu aliwaita kuishi wakimfuata
na
kulipenda kundi lao. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Julai 2016
“
W
anangu wapendwa! Ninawaangalia
na
ninawaona mmepotea, hamna wala sala wala furaha ndani ya mioyo yenu. Rudini, wanangu, kusali
na
wekeni Mungu katika mahali pa kwanza
na
si mtu. Msipoteze tumaini ninalowaletea. Wanangu, wakati huu uwe kwenu kila siku kumtafuta Mungu katika kimya ya moyo wenu
na
salini, salini, salini mpaka sala iwe furaha kwenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nimekuja kwenu, katikati yenu, ili mnipe mahangaiko yenu, niweze kuyaleta mbele ya Mwanangu
na
kuwaombeeni kwake kwa manufaa yenu. Najua kuwa kila mmoja wenu ana mahangaiko yake, majaribu yake. Kwa hiyo kwa moyo wa kimama nawaalikeni: Njooni kwenye Meza ya Mwanangu! Yeye humega mkate kwa ajili yenu, huwapa Yeye mwenyewe. Huwapa matumaini. Anawaomba kuwa
na
imani zaidi, matumaini zaidi, utulivu zaidi. Anawaomba mpigane ndani yenu dhidi ya ubinafsi, hukumu
na
udhaifu wa kibinadamu. Kwa hiyo Mimi, kama Mama, nawaambieni: salini, maana sala huwapa nguvu ya kupigana ndani yenu. Mwanangu, alipokuwa mtoto, aliniambia mara nyingi ya kuwa wengi watanipenda
na
kuniita "Mama". Mimi hapa, katikati yenu, nasikia upendo
na
kuwashukuru! Kwa njia ya upendo huu namwomba Mwanangu ili hakuna hata mmoja wenu, wanangu, arudiye nyumbani jinsi alivyokuja. Ili mlete matumaini, rehema
na
upendo kadiri muwezavyo; ili muwe mitume wa upendo wangu, wanaoshuhudia kwa maisha yao kwamba Baba aliye Mbinguni ni chemchemi ya uzima si ya mauti. Wanangu wapendwa, nawaomba tena kwa moyo wa kimama: waombeeni wateule wa Mwanangu, kwa ajili ya mikono yao iliyobarikiwa, kwa ajili ya wachungaji wenu, ili waweze kumhubiri Mwanangu kwa upendo mwingi wawezavyo,
na
hivyo kusababisha wongofu. Nawashukuru.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
Next>>