Our Lady of Medjugorje Messages containing 'na'
Total found:
218
Ujumbe, 25 Agosti 2016
“
W
anangu wapendwa! Leo nataka kushirikiana pamoja nanyi furaha ya mbinguni. Ninyi wanangu fungueni mlango wa moyo ili katika moyo wenu matumaini, amani
na
mapendo ambazo Mungu peke yake anaweza kutoa ziweze kukua. Wanangu, mnapenda mno dunia
na
mambo ya dunia, kwa hiyo Shetani huwatikisa kama upepo ufanyavyo
na
mawimbi ya bahari. Kwa hiyo mnyororo wa maisha yenu uwe sala ya moyo
na
kumwabudu Mwanangu Yesu. Kwake mtolee maisha yenu yajayo ili muwe ndani Yake furaha
na
mfano kwa watu wengine kwa njia ya matendo yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kulingana
na
mapenzi ya Mwanangu
na
upendo wangu wa kimama naja kwenu, wanangu, hasa kwa wale ambao hawajajua bado upendo wa Mwanangu. Ninakuja kwenu mnaonifikiria, mnaoomba msaada wangu. Ninawapa upendo wangu wa kimama
na
kuwaletea baraka ya Mwanangu. Mnayo mioyo safi
na
wazi? Mnaona dalili za uwepo wangu
na
upendo wangu? Wanangu, katika maisha yenu ya dunia igieni moyo
na
mfano wangu. Maisha yangu yalikuwa maumivu, ukimya, imani
na
matumaini pasipo mipaka katika Baba wa Mbinguni. Hakuna kitu cha bahati: si maumivu, si furaha, si mateso, si upendo. Hizo zote ni neema ambazo Mwanangu anawapeni
na
zinazowaongoza kwenye uzima wa milele. Mwanangu anawaomba mapendo
na
sala ndani yake. Kupenda
na
kusali ndani yake maana yake — kama Mama nataka kuwafundisha — ni kusali katika ukimya wa nafsi zenu, si kusema kwa midomo tu. Ni tendo dogo zuri litendwalo kwa jina la Mwanangu; ni uvumilivu, rehema, upokeaji wa maumivu
na
kujitolea kwa ajili ya wengine. Wanangu, Mwanangu huwatazama. Ombeni ili ninyi pia muuone uso wake,
na
ili uso huo uweze kufunuliwa kwenu. Wanangu, mimi nawafunulia ukweli halisi wa pekee. Salini kwa kuyaelewa
na
kuweza kueneza mapendo
na
matumaini, kwa kuweza kuwa mitume wa upendo wangu. Moyo wangu wa kimama hupenda hasa wachungaji. Iombeeni mikono yao iliyobarikiwa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2016
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalika kusali. Sala
na
iwe maisha kwenu. Hivyo tu moyo wenu utajaa amani
na
furaha. Mungu atakuwa karibu nanyi, nanyi mtamhisi moyoni mwenu kama rafiki. Mtaongea naye kama
na
mmoja mjuaye
na
, wanangu, mtaona hitaji la kutoa ushuhuda maana Yesu atakuwa moyoni mwenu
na
ninyi mtaambatana naye. Mimi ni pamoja nanyi
na
kuwapenda nyote kwa upendo wangu wa kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Roho Mtakatifu, kwa njia ya Baba wa Mbinguni, amenifanya Mama: Mama wa Yesu
na
, kwa hiyo, Mama yenu vilivile. Kwa hiyo nawajilia niwasikilize, niwafungulie mikono yangu ya kimama, niwapeni Moyo wangu
na
kuwaalika kukaa pamoja nami, kwa maana kutoka juu ya msalaba Mwanangu amenikabidhi ninyi. Kwa bahati mbaya wanangu wengi hawakujua upendo wa Mwanangu, wengi hawataka kumjua. Loo, wanangu, mabaya mengi yatoka kwa wale ambao hawana budi ya kuona
na
kuelewa ili kuamini! Kwa hiyo, wanangu, mitume wangu, katika kimya ya moyo wenu sikilizeni sauti ya Mwanangu, ili moyo wenu uwe makazi yake wala usiwe giza
na
huzuni, bali uangaziwe
na
mwanga wa Mwanangu. Tafuteni matumaini kwa imani, maana imani ni maisha ya roho. Ninawaalika tena: salini! Salini ili kuishi imani katika unyenyekevu, katika amani ya kiroho
na
mkiangaziwa
na
mwanga. Wanangu, msijaribu kuelewa yote mara moja, maana Mimi nami sikuelewa yote mara moja, lakini niliyaamini maneno ya kimungu aliyoyasema Mwanangu, Yeye aliyekuwa mwanga wa kwanza
na
mwanzo wa Ukombozi. Enyi mitume wa moyo wangu, ninyi mnaosali, mnaojitolea, mnaopenda wala msiohukumu: ninyi nendeni mkaeneze ukweli, maneno ya Mwanangu, Injili. Ninyi kweli, ni Injili iliyo hai, ninyi ni miali ya mwanga wa Mwanangu. Mwanangu
na
mimi tutakuwa karibu nanyi, tutawatia moyo
na
kuwajaribu. Wanangu, ombeeni daima
na
hasa baraka ya wale ambao Mwanangu amebariki mikono yao, yaani Wachungaji wenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2016
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalika: ombeni amani! Acheni ubinafsi
na
ishini ujumbe ninaowapa. Bila hizo ujumbe hamwezi kubadili maisha yenu. Mkiwa watu wa sala mtakuwa
na
amani. Mkiishi katika amani mtaona hitaji la kutoa ushuhuda maana mtamtambua Mungu mnayemhisi sasa kama yu mbali. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini,
na
mkamwache Mungu aingie mioyoni mwenu. Rudieni kufunga
na
kuungama, ili muweze kushinda uovu ulio ndani yenu
na
kandokando yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Novemba 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kuja
na
kujifunua kwangu kwenu ni furaha kubwa ya Moyo wangu wa kimama. Ni zawadi ya Mwanangu kwa ajili yenu
na
ya wale watakaokuja. Kama Mama nawaalika: mpendeni Mwanangu kuliko yote! Ili kumpenda kwa moyo wote, yawapaswa kumjua: Mtamjua kwa kusali: Salini kwa moyo
na
hisia zenu. Kusali maana yake ni kutafakari upendo wake
na
kujitolea kwake. Kusali maana yake ni kupenda, kutoa, kuteseka
na
kutolea sadaka. Nawaalika ninyi, wanangu, kuwa mitume ya sala
na
upendo. Wanangu, ni wakati wa kukesha. Katika kesha hii nawaalika kusali, kupenda
na
kutumaini. Maadamu Mwanangu ataangalia mioyo yenu, Moyo wangu wa kimama unatamani kwamba Yeye aone ndani ya mioyo yenu tumaini timilifu
na
upendo. Upendo wa mitume wangu wote pamoja utaishi, utashinda
na
utafunua maovu. Wanangu, mimi nilikuwa kalisi ya Mtu - Mungu, nilikuwa chombo cha Mungu. Kwa hiyo nawaalika ninyi, mitume wangu, kuwa kalisi ya upendo mnyofu
na
safi wa Mwanangu. Nawalika kuwa chombo ambacho kwa njia yake wote wasiojua upendo wa Mungu, wasiopenda kamwe, wataelewa, wataupokea
na
wakaokolewa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2016
“
W
anangu wapendwa! Leo pia nawaalika kurudi katika sala. Katika wakati huu wa neema, Mungu amenijalia kuwaongoza kuelekea utakatifu
na
maisha ya unyofu, ili katika mambo madogo muweze kumtambua Mungu Mwumbaji, kumpenda
na
ili maisha yenu yawe shukrani kwa Mungu Mkuu kwa yote aliyowajalia. Wanangu, maisha yenu yawe zawadi kwa wengine katika upendo naye Mungu atawabariki. Nanyi, mumshuhudie bila kutafuata faida, kwa ajili ya upendo kwa Mungu. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwaombea ninyi nyote mbele ya Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Moyo wangu wa kimama unalia machozi ninapoyaona yale wanayoyafanya wanangu. Dhambi zinaongezeka, usafi wa moyo unaendelea kupoteza umuhimu wake. Mwanangu amesahauliwa
na
upendo kwake unaendelea kupunguka
na
wanangu wanateswa. Kwa hiyo, wanangu, mitume wa moyo wangu, iteni jina la Mwanangu kwa nafsi
na
kwa moyo: Yeye atakuwa
na
maneno ya mwanga kwenu. Naye atajionyesha kwenu, anashiriki Mkate pamoja nanyi
na
anawapa maneno ya upendo, ili myageuze kuwa matendo ya huruma
na
muwe hivyo mashahidi ya ukweli. Kwa hiyo, wanangu, msiogope! Acheni Mwanangu awe ndani yenu. Yeye atawatumia ninyi ili kuzitibu nafsi zinazojeruhiwa
na
kuziongoka zile zinazopotea. Kwa hiyo, wanangu, rudieni kusali Rozari. Mwisali kwa roho ya ukarimu, ya sadaka
na
ya huruma. Salini si kwa maneno tu, ila kwa matendo ya huruma. Salini kwa upendo kwa watu wote. Mwanangu amekuza kimaadili upendo kwa njia ya sadaka yake. Kwa hiyo isheni pamoja naye mpate nguvu
na
matumaini, mpate upendo ulio uhai wa kuongoza kwenye uzima wa milele. Kwa njia ya upendo wa Mungu mimi nami ni pamoja nanyi,
na
nitawaongoza kwa upendo wa kimama. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2016 - Tokeo la Yakobo Kolo la kila mwaka
Katika tokeo la mwisho wa kila siku la tarehe 12 Septemba 1998 Mama Maria alimwambia Yakobo ya kuwa ataona tokeo lake mara moja kila mwaka, tarehe 25 Desemba, siku ya Kristmasi. Hivyo ikatokea
na
mwaka huu. Mama Maria ametokea pamoja
na
Mtoto Yesu mikononi mwake. Tokeo likaanza saa nane adhuhuri
na
dakika ishirini
na
kudumu dakika kumi. Yakobo, baadaye, akatoa ujumbe ufuatao:
“
W
anangu wapendwa, Leo katika siku hii ya neema nawaalika hasa kusali kwa ajili ya amani. Wanangu, nimekuja hapa kama Malkia wa Amani
na
mara nyingi nimewaalika kusali kwa ajili ya amani. Lakini wanangu, mioyo yenu imefadhaika. Dhambi inawazuia kufunguliwa kabisa kwa neema
na
amani ambayo Mungu ataka kuwapeni. Ili kuishi amani, wanangu, yawapasa kuwa kwanza
na
amani mioyoni mwenu
na
kujiachia kabisa kwa Mungu
na
mapenzi Yake. Msitafute amani
na
furaha katika mambo ya dunia hii maana haya yote hupita. Muelekee rehema ya kweli, amani itokayo kwa Mungu tu
na
hivyo mioyo wenu hivyo tu itajaa furaha ya kweli; hivyo tu mtaweza kuwa mashahidi wa amani katika dunia hii ya hofu. Mimi ni mama yenu
na
ninawaombea kila mmoja wenu mbele ya Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2016
“
W
anangu wapendwa! Kwa furaha kubwa leo nawaletea Mwanangu Yesu ili Yeye awapeni amani Yake. Wanangu, fungueni mioyo yenu
na
muwe wafurahivu, ili muweze kuipokea. Mbingu ni pamoja nanyi
na
zinapambana kwa ajili ya amani mioyoni mwenu, katika jamaa
na
ulimwenguni
na
ninyi, wanangu, msaidieni kwa sala zenu ili iwe hivyo. Ninawabariki pamoja
na
Mwanangu Yesu
na
kuwaomba msikose matumaini,
na
mtazamo wenu
na
moyo wenu yaelekee daima mbinguni
na
uzima wa milele. Hivyo mtafunguliwa kwa Mungu
na
mipango Yake. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Mwanangu alikuwa chemchemi ya upendo
na
mwanga alipoongea
na
watu wa mataifa yote. Mitume wangu, fuateni mwanga wake, si rahisi, yawapasa kuwa wadogo, yawapasa kuwa wadogo kuliko wengine wote
na
kwa msaada wa imani kujazwa
na
upendo wake. Hakuna mtu duniani, pasipo imani, awezaye kuwa
na
uzoefu wa mwujiza. Mimi nipo pamoja nanyi, ninajionyesha kwa matokeo hayo, kwa maneno hayo, nataka kuwashuhudia upendo wangu
na
utunzaji wangu wa kimama. Wanangu, msipoteze wakati mkiweka maswali ambayo hamtapata kamwe majibu, maisha yenu duniani yatakapomalizika Baba wa Mbinguni atawajibu. Mjue daima ya kuwa Mungu hujua yote, Mungu huona, Mungu hupenda. Mwanangu mpenzi sana huangaza maisha
na
kupasua giza. Upendo wa kimama unaonileta kwenu hauelezeki, umefichwa lakini ni halisi, ninawaonyesheni hisia zangu, upendo, hisani
na
ukarimu wangu wa kimama. Kutoka kwenu, mitume wangu, ninatafuta sala zenu: mawaridi yaliyo matendo ya upendo, hizo ndizo kwa moyo wangu wa kimama sala za kunipendeza sana, haya ninayaletea Mwanangu aliyezaliwa kwa ajili yenu. Yeye anawatazama ninyi
na
kuwasikia. Sisi tupo kila siku karibu nanyi kwa upendo wenu ambao huita, huunga, huongoa, hutia moyo
na
kujaza. Kwa hiyo mitume wangu pendaneni daima, lakini hasa mpende Mwanangu, hii ni njia ya pekee ya wokovu kuelekea uzima wa milele, hiyo ni sala ya kunipendeza ambayo kama harufu nzuri ajabu ya mawaridi, hujaa moyo wangu. Ombeni daima, waombeeni wachungaji wenu ili wapate nguvu ya kuwa mwanga wa Mwanangu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2017
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalika kusali kwa ajili ya amani. Amani katika mioyo ya wanadamu, amani katika familia
na
amani duniani. Shetani ana nguvu
na
anataka ninyi nyote kuwa wapinzani wa Mungu, kuwarudisha katika yote yaliyo ya kibinadamu
na
kuteketeza katika mioyo yote hisia zinazowaongoza kwa Mungu
na
mambo ya Mungu. Ninyi, wanangu, salini
na
mpambane
na
uyakinifu, shauku ya mambo ya kisasa
na
ubinafsi ambayo malimwengu huwatolea. Wanangu, kateni shauri ya kuwa watakatifu
na
mimi, pamoja
na
Mwanangu Yesu, nitawaombeeni. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninyi mnaojaribu kumtolea Mwanangu kila siku ya maisha yenu, ninyi mnaojaribu kuishi pamoja naye, ninyi mnaosali
na
kujitolea, ninyi ni matumaini katika ulimwengu huu wenye udhia. Ninyi ni miali ya mwanga wa Mwanangu, Injili iliyo hai,
na
ninyi ni mitume wangu wapenzi wa upendo. Mwanangu ni pamoja nanyi. Vili vile, lakini, Yeye anawangojea kwa uvumilivu wale wasiomjua. Kwa hiyo ninyi, mitume wa upendo wangu, salini kwa moyo
na
onyesheni kwa matendo upendo wa Mwanangu. Kwenu ninyi hiyo ni matumaini ya pekee,
na
njia ya pekee kuelekea uzima wa milele. Mimi, kama Mama, ni hapa pamoja nanyi. Sala zenu mnazoniomba ni kwangu mawaridi ya upendo mazuri kuliko yote, Siwezi kutokuwapo pale ninapohisi harufu ya mawaridi. Kuna matumaini! Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2017
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalika kuishi kwa kina imani yenu
na
kumwomba Aliye juu ili aiimarishe, hivyo upepo
na
dhoruba yasije yakaivunja. Mizizi ya imani yenu iwe sala
na
tumaini katika uzima wa milele. Tokea sasa, wanangu, jijengeni wenyewe, katika wakati huu wa neema ambapo Mungu anawapeni neema ili kwa njia ya kujinyima
na
mwito wa kuongoka muwe watu wenye imani
na
tumaini safi
na
ya kuvumilia. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo wa kimama naja kuwasaidieni kuwa
na
upendo zaidi, maana yake imani zaidi. Naja kuwasaidieni kuishi kwa upendo maneno ya Mwanangu, ili ulimwengu uwe tofauti. Kwa sababu hiyo nawakusanya, mitume wa mapendo yangu, karibu nami. Niangalieni kwa upendo, ongeeni nami kama vile
na
Mama kuhusu mateso yenu, maumivu yenu, furaha zenu. Ombeni ili nisali Mwanangu kwa ajili yenu. Mwanangu ni mwenye rehema
na
haki. Moyo wangu wa kimama ungependa ninyi pia muwe hivyo. Moyo wangu wa kimama ungependa ya kuwa ninyi, mitume wa mapendo yangu, mngeongea kwa maisha yetu juu ya Mwanangu
na
juu yangu pamoja
na
watu wote walio karibu nanyi, ili ulimwengu uwe tofauti, ili wairudie imani
na
tumaini. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini kwa moyo. Salini kwa upendo, salini kwa matendo mema. Salini ili wote wamjue Mwanangu, ili ulimwengu ugeuke, ulimwengu uokoke. Ishini kwa upendo maneno ya Mwanangu. Msihukumu, lakini mpendaneni, ili Moyo wangu uweze kushinda. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Machi 2017
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema nawaalika nyote kufungua mioyo yenu kwa huruma ya Mungu ili kwa ajili ya sala, toba
na
maamuzi kwa ajili ya utakatifu muanze maisha mapya. Majira haya ya kuchipua yanawaita, katika mawazo yenu
na
mioyo yenu, kuishi maisha mapya, kujifanya upya. Kwa hiyo, wanangu, mimi nipo pamoja nanyi niwasaidie ili mkatakati wa kukata shauri muweze kusema NDIYO kwa Mungu
na
amri za Mungu. Ninyi si peke yenu, mimi nipo pamoja nanyi kwa njia ya neema ambayo Yeye Aliye juu hunijalia kwa ajili yenu
na
kwa uzao wenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Aprili 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, mitume wa upendo wangu, inawapasa ninyi kuujulisha upendo wa Mwanangu kwa wale wote ambao hawakumjua. Inawapasa ninyi, mianga midogo ya ulimwengu, ambao mimi ninaifunza kwa upendo wa kimama ili ing'ae waziwazi kwa mwangaza kamili. Sala itawasaidia, maana sala huwaokoa ninyi, sala huuokoa ulimwengu. Kwa hiyo, wanangu, salini kwa maneno, kwa moyo, kwa upendo wenye huruma
na
kwa sadaka. Mwanangu aliwaonyesha njia: Yeye aliyejimwilisha
na
kunifanya kuwa kalisi ya kwanza; Yeye ambaye kwa sadaka yake isiyo
na
kifani aliwaonyesha kama inavyopaswa kupenda. Kwa hiyo, wanangu, msiogope kusema kweli. Msiogope kujigeuza wenyewe
na
ulimwengu ili kueneza mapendo, mkitenda kila jinsi kusudi Mwanangu aweze kujulikana
na
kupendwa kwa kuwapenda wengine kwa ajili yake. Mimi, kama mama, nipo daima pamoja nanyi. Namwomba Mwanangu awasaidie ili katika maisha yenu upendo utawale: upendo uishio, upendo uvutao, upendo utoao uzima. Huo ndio upendo ninaowafundisha, upendo safi. Inawapasa ninyi, mitume wangu, kuutambua, kuuishi, kuueneza. Waombeeni wachungaji wenu kwa moyo, ili waweze kumshuhudia Mwanangu kwa upendo. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2017
“
W
anangu wapendwa! Pendeni, salini
na
shuhudieni uwepo wangu kwa ajili ya wale wote walio mbali. Kwa njia ya ushuhuda wenu
na
mfano wenu mnaweza kuvuta mioyo iliyo mbali
na
Mungu
na
neema yake. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kukuombeeni kila mmoja wenu ili kwa upendo
na
uhodari muweze kushuhudia
na
kuwahimiza wale wote walio mbali
na
Moyo wangu usio
na
doa. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawaalika kusali pasipo kuomba, bali mkitoa sadaka, mkijitolea wenyewe. Nawaalika kuleta habari ya ukweli
na
upendo wenye rehema. Ninamwomba Mwanangu kwa ajili yenu, kwa imani yenu, inayoendelea kupunguka katika mioyo yenu. Ninamwomba awasaidieni kwa Roho ya Mungu, kama vile mimi nami ninavyotaka kuwasaidieni kwa roho ya kimama. Wanangu, itawabidi kujiboresha! Wale tu walio safi, wanyenyekevu
na
wamliojaa upendo wanautegemeza ulimwengu, wanaokoa ulimwengu
na
wao wenyewe. Wanangu, Mwanangu ndiye moyo wa ulimwengu: lazima kumpenda
na
kumwomba,
na
si kumsaliti daima tena. Kwa hiyo ninyi, mitume wa upendo wangu, mstawishe imani katika mioyo ya watu kwa mfano wenu, kwa sala yenu
na
kwa upendo wenye rehema. Mimi nipo karibu nanyi
na
nitawasaidia. Salini ili wachungaji wenu wapate mwanga zaidi kadiri wawezavyo, ili waweze kuangaza wale wote wanaoishi gizani. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Mei 2017
“
W
anangu wapendwa! Yeye Aliye juu ameniruhusu kuwaalikeni tena kwa uongofu. Wanangu, fungueni mioyo yenu kwa neema ambayo wote mnaalikwa. Muwe mashahidi wa amani
na
wa upendo katika ulimwengu huu wa wasiwasi. Maisha yenu hapa duniani ni ya mpito. Salini ili kwa njia ya sala muweze kutamani mbingu
na
mambo ya mbinguni
na
mioyo yenu itaona yote kwa njia tofauti. Ninyi si peke yenu, Mimi nipo pamoja nanyi
na
ninawaombeeni kwa Mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
Next>>