Our Lady of Medjugorje Messages containing 'na'
Total found:
218
Ujumbe, 2 Juni 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kama vile katika mahali pengine nilipokuja, vivyo hivyo hapa pia nawaalika kusali. Salini kwa ajili ya wale wasiomjua Mwanangu, kwa ajili ya wale ambao hawajaujua upendo wa Mungu, dhidi ya dhambi, kwa ajili ya waliowekwa wakfu, kwa ajili ya wale ambao Mwanangu aliwaita ili wawe
na
upendo
na
roho yenye nguvu, kwa ajili yenu
na
kwa ajili ya Kanisa. Mwombeni Mwanangu,
na
upendo mnaohisi kwa ajili ya ukaribu, utawapa nguvu
na
utawatayarisha kwa matendo mema mtakayofanya kwa Jina lake. Wanangu muwe tayari. Wakati huu ni njia panda ya maisha. Kwa hiyo nawaalika tena kwa imani
na
matumaini, ninawaonyesha njia ya kushika. Hayo ni maneno ya Injili: Mitume wangu, ulimwengu unahitaji sana mikono yenu iliyoinuliwa mbinguni, kuelekea kwa Mwanangu
na
kwa Baba wa mbinguni. Ni lazima kuwa
na
unyenyekevu mwingi
na
usafi wa moyo. Mumwamini Mwanangu
na
jueni ya kuwa mnaweza kuwa bora zaidi daima. Moyo wangu wa kimama unatamani kwamba ninyi, mitume wa upendo wangu, muwe sikuzote mianga midogo ya ulimwengu. Mtie nuru pale giza inapotaka kutawala
na
kwa sala yenu
na
upendo wenu, muonyeshe sikuzote njia ya kweli, ziokoeni nafsi. Mimi nipo pamoja nanyi. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Juni 2017
“
W
anangu wapendwa! Leo nataka kuwashukuru kwa uvumilivu wenu
na
kuwaalika kujifungua kwa sala ya ndani. Wanangu, sala ni moyo wa imani
na
wa matumaini katika uzima wa milele. Kwa hiyo salini kwa moyo mpaka moyo wenu umwimbie Mungu Mwumbaji aliyewapa maisha kwa shukrani. Wanangu, Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwaletea baraka yangu ya amani ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Julai 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawashukuru kwa kuitikia miito yangu
na
kukusanyika karibu nami, Mama yenu wa mbinguni. Najua kwamba mnanifikiri kwa upendo
na
matumaini. Mimi ninawapendeni nyote kama vile anavyowapendeni Mwanangu ambaye, kwa upendo wake wenye huruma, ananituma nije kwenu, mara nyingi pia. Yeye, aliyekuwa mtu
na
aliye Mungu, Mmoja
na
Utatu; Yeye aliyeteswa kwa ajili yenu mwilini
na
nafsini. Yeye aliyejifanya Mkate ailishe nafsi zenu
na
hivyo kuziokoa. Wanangu, nawafundisha jinsi ya kustahili upendo wake, kumwelekeza mawazo yenu, kumwishi Mwanangu. Mitume wa upendo wangu, ninawafunika kwa joho langu kwa sababu, kama Mama yenu, nataka kuwalinda. Nawasihi: mwuombee ulimwengu wote: moyo wangu unateswa. Dhambi zinaongezeka, ni nyingi mno. Lakini kwa msaada wenu – mlio wanyenyekevu, wanyofu, wenye upendo, watawa
na
watakatifu – moyo wangu utashinda. Mpendeni Mwanangu kupita wote
na
ulimwengu wote kwa njia yake. Msisahau kabisa ya kuwa kila ndugu yenu ana ndani yake kitu cha thamani: nafsi. Kwa hiyo, wanangu, pendeni wale wote wasiomjua Mwanangu ili kwa njia ya maombi
na
upendo utokao katika maombi, wawe wema zaidi. Ili wema uweze kushinda ndani yao. Ili nafsi zao ziweze kuokoka
na
kupata uzima wa milele. Enyi mitume wangu, wanangu. Mwanangu aliwaambieni mpendane. Hiyo iandikwe mioyoni mwenu
na
kwa kusali jaribuni kuishi upendo huu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Julai 2017
“
W
anangu wapendwa! Muwe sala
na
kioo cha upendo wa Mungu kwa wale wote walio mbali
na
amri za Mungu. Wanangu, muwe waaminifu
na
thabiti katika wongofu
na
mjifanye kazi juu yenu wenyewe ili utakatifu wa maisha uwe kwenu jambo la ukweli. Jipeni moyo ninyi kwa ninyi mtende mema kwa njia ya kusali ili maisha yenu duniani yawe mazuri zaidi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni, kama Mama wa Yule anayewapendeni, nipo hapa pamoja nanyi niwasaidieni kumjua, kumfuata. Mwanangu amewaachieni nyayo za hatua zake, ili iwe rahisi zaidi kwenu kumfuata. Msiogope, msiwe
na
wasiwasi. Mimi nipo pamoja nanyi! Msichoke, maana sala nyingi
na
sadaka zinahitajiwa kuwasaidia wale wasiomwomba, wasiompenda
na
wasiomjua Mwanangu. Muwasaidie mkiona ndani yao ndugu zenu. Enyi mitume wa upendo wangu, sikilizeni sauti yangu ndani yenu, hisieni upendo wangu. Kwa hiyo salini: salini mkitenda, salini mkitoa. Salini kwa upendo, salini kwa matendo
na
kwa fikira, kwa jina la Mwanangu. Kadiri mtakavyotoa upendo, ndivyo mtakavyoupokea. Upendo utokao katika Upendo huangaza ulimwengu. Ukombozi ni upendo,
na
upendo hauna mwisho. Wakati Mwanangu atakapokuja tena duniani, atatafuta upendo katika mioyo yenu. Wanangu, Yeye alifanya kwa ajili yenu matendo mengi ya upendo. Ninawafundisha kuyaona, kuyaelewa
na
kumshukuru mkimpenda
na
kumsamehe sikuzote
na
tena jirani yako. Kwa kuwa kumpenda Mwanangu maana yake ni kusamehe. Mwanangu hapendwi, ikiwa hatuwezi kumsamehe jirani yetu, ikiwa hatuwezi kumwelewa jirani yetu, ikiwa tunamhukumu. Wanangu, faida gani kusali, msipopenda wala msiposamehe? Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2017
“
W
anangu wapendwa! leo ninawaalika kuwa watu wa sala. Salini mpaka hata sala itakapokuwa kwenu furaha
na
mkutano
na
Yeye aliye juu. Yeye atageuza moyo wenu nanyi mtakuwa watu wa upendo
na
wa amani. Wanangu, msisahau kwamba shetani ni mwenye nguvu
na
anataka kuwaachisha kusali. Ninyi, msisahau kwamba sala ni kifunguo cha siri cha mkutano pamoja
na
Mungu. Kwa hiyo Mimi nipo pamoja nanyi, niwaongoze. Msiache kusali. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nani angeweza kusema nanyi vizuri zaidi kuliko Mimi kuhusu upendo
na
maumivu ya mwanangu? Niliishi pamoja naye, niliteseka pamoja naye. Nikiishi maisha ya kidunia, nilionja maumivu, maana nilikuwa mama. Mwanangu alipenda michakato
na
kazi ya Baba wa Mbinguni, Mungu wa kweli;
na
, kama alivyoniambia, alikuja kusudi awakomboe ninyi. Mimi nilificha maumivu yangu kwa njia ya upendo. Bali ninyi, wanangu, ninyi mnaweka maswali mengi, hamwelewi maumivu, hamwelewi kwamba, kwa njia ya upendo wa Mungu, mnapaswa kupokea maumivu
na
kuyachukua. Kila mwanadamu, iwe kwa kiwango kikubwa au kidogo, yampasa afanye mang'amuzi. Lakini, tukiwa
na
amani rohoni
na
tukiwa
na
hali ya neema, tumaini moja lipo: ni Mwanangu, Mungu aliyezaliwa
na
Mungu. Maneno yake ni mbegu ya uzima wa milele: Yanapopandwa katika roho njema, huleta matunda mengi. Mwanangu amechukua maumivu maana amepokea juu yake dhambi zenu. Kwa hiyo ninyi, wanangu, mitume wa upendo wangu, ninyi mnaoteswa: mjue kwamba maumivu yenu yatakuwa mwanga
na
utukufu. Wanangu, wakati mnapovumilia maumivu, wakati mnapoteswa, Mbingu huingia ndani yenu, nanyi mnawapa watu wote karibu nanyi Mbingu kidogo
na
matumaini mengi. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2017
“
W
anangu wapendwa! leo ninawaalika kuwa makarimu katika kujinyima, katika kufunga
na
katika sala kwa ajili ya wale wote wanaojaribiwa, nao ni ndugu zenu kina kaka
na
kina dada.
Na
hasa ninawaomba kusali kwa ajili ya makuhani
na
kwa wote waliojiweka wakfu ili kwa ari zaidi wampende Yesu, ili Roho Mtakatifu aijaze mioyo yao kwa furaha, ili watoe ushuhuda wa Mbingu
na
mafumbo ya kimbingu. Roho nyingi ipo katika dhambi kwa sababu hakuna wale wanaojitoa sadaka
na
kusali kwa wongofu wao. Mimi nipo pamoja nanyi nikiwaombeeni ili mioyo yenu ijazwe furaha. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninaongea nanyi kama Mama, kwa maneno rahisi, lakini yamejaa wingi wa upendo
na
wa bidii kwa wanangu, ambao kwa njia ya Mwanangu wamekabidhiwa kwangu. Mwanangu, ambaye anakuja kutoka umilele
na
hata sasa, anaongea nanyi kwa maneno ya uzima
na
anapanda upendo katika mioyo wazi. Kwa hiyo nawaomba, mitume wa upendo wangu: muwe
na
mioyo iliyo wazi sikuzote kurehemu
na
kusamehe. Wasameheni sikuzote wenzenu kama Mwanangu, kwa vile hivyo amani itakuwa ndani yenu. Wanangu, lindeni nafsi yenu, maana hiyo ndiyo ukweli wa pekee ulio wenu bila shaka. Mmeanza kusahau umuhimu wa familia. Familia haipaswi kuwa mahali pa mateso
na
maumivu, bali mahali pa uelewano
na
huruma. Familia wanaojaribu kuishi kama apendavyo Mwanangu, wanaishi wakipendana. Tangu alipokuwa angali mtoto, Mwanangu aliniambia ya kuwa watu wote kwake ni ndugu zake. Kwa hiyo kumbukeni, enyi mitume wa upendo wangu, watu wote mnaowaona ni kwenu familia yenu, ndugu kama apendavyo Mwanangu. Wanangu, msipoteze muda kufikiria
na
kuhangaikia mambo yajayo. Kitu chenu kimoja cha kuhangaikia kwenu kiwe vipi kuishi vema kila dakika kadiri ya Mwanangu,
na
tazama hiyo ndiyo ni amani! Wanangu, msisahau kabisa kuwaombea wachungaji wenu. Salini ili waweze kupokea watu wote kama wanao, ili, kama apendavyo Mwanangu, wawe kwao kama baba za kiroho. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2017
“
W
anangu wapendwa! Katika kipindi hiki cha neema ninawaalika kuwa sala. Wote mna matatizo, taabu, maumivu
na
wasiwasi. Watakatifu wawe kwenu mfano
na
onyo kwa utakatifu, Mungu atakuwa karibu nanyi
na
mtakuwa wapya kwa utafiti
na
wongofu wa binafsi. Imani itakuwa kwenu tumaini,
na
furaha itazaliwa katika mioyo yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Novemba 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nikiwatazama hapa mmekusanyika kunizunguka, Mama yenu, ninaona nafsi safi nyingi. Ninawaona wanangu wengi wanaotafuta upendo
na
faraja lakini hakuna mtu anayewapa. Ninawaona hata wale wanaotenda mabaya maana hawana mifano myema, maana hawajamjua mwanangu. Mwanangu anawatuma ninyi kwangu, Mama, sawa kwa wote, niwafundisheni kupenda, ili muelewe ya kuwa ninyi ni ndugu. Ninatamani kuwasaidia. Mitume wa upendo wangu, kwa mwanangu yamtosha tamaa hai ya imani
na
upendo
na
atayakubali, lakini mnapaswa kustahili, kuwa
na
tamaa
na
mioyo wazi, Mwanangu huingia katika mioyo wazi. Mimi kama Mama ninatamani kwamba mjue Mwanangu katika kweli: Mungu aliyezaliwa
na
Mungu, kwamba mjue ukuu wa Upendo wake, ambao mnahitaji. Yeye amezichukua juu yake dhambi zenu, ameupata Ukombozi wenu,
na
badala yake anaomba mpendane ninyi kwa ninyi. Mwanangu ni upendo, Yeye anawapenda watu wote bila tofauti, watu wote wa nchi zote, wa mataifa yote. Ikiwa ninyi, wanangu, mngeishi upendo wa Mwanangu, ufalme wake ungekwisha kuwa duniani. Kwa hiyo, Mitume wa upendo wangu, salini, salini ili Mwanangu
na
upendo wake wawe ndani yenu nanyi muweze kuwa mfano wa upendo
na
muweze kuwasaidia wote wale ambao hawajamjua Mwanangu. Msisahau kamwe kwamba Mwanangu, mmoja
na
utatu, anawapendeni. Pendeni
na
wombeeni wachungaji wenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2017
“
W
anangu wapendwa! Katika kipindi hiki cha neema ninawaalika kusali. Salini
na
tafuteni amani, wanangu. Yeye aliyekuja hapa duniani awatoe amani, pasipo kuwabagua kuwa ninyi ni nani
na
ni kitu gani - Yeye, Mwanangu, ndugu yenu, kwa njia yangu anawaalika kuongoka maana pasipo Mungu hamna baadaye wala uzima wa milele. Kwa hiyo aminini, salini
na
isheni katika neema
na
mkingojea mkutano wenu wa binafsi pamoja naye. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninawaelekea ninyi kama Mama yenu, Mama wa wenye haki, Mama wa wale wanaopenda
na
kuteseka, Mama wa watakatifu. Wanangu, ninyi pia mnaweza kuwa watakatifu: ni juu yenu. Watakatifu ni wale wanaompenda Baba wa Mbinguni kupita kiasi, wale wanaompenda kupita chochote. Kwa hivyo, wanangu, jaribuni daima kuboreka. Kama ninyi mnajaribu kuwa wema, mtaweza kuwa watakatifu, hata kama hamfikiri hiyo juu yenu. Kama mnafikiri kuwa wema, ninyi sio wanyenyekevu
na
kiburi huwatenga kutoka utakatifu. Katika ulimwengu huu wa wasiwasi, umejaa vitisho, mikono yako, mitume wa upendo wangu, inapaswa kuwa imenyoshwa katika maombi
na
rehema. Kwangu, wanangu, nipeni zawadi ya Rozari, mawaridi ninayopenda sana! Mawaridi yangu ni maombi yenu msemayo kwa moyo wote,
na
sio yale msemayo kwa midomo yenu tu. Mawaridi yangu ni matendo yenu ya maombi, imani
na
upendo. Wakati alipokuwa mtoto, mwanangu aliniambia kwamba watoto wangu watakuwa wengi
na
wataniletea mawaridi mengi. Sikuelewa, sasa najua kwamba ninyi ni watoto wale, wanaoniletea mawaridi wakati mnapompenda mwanangu kupita yote, wakati mnaposali kwa moyo wote, wakati mnapowasaidia walio maskini zaidi. Hayo ndiyo mawaridi yangu! Hii ndiyo imani, inayosababisha kila kitu katika maisha kifanyike kwa upendo;
na
kiburi hakijulikani;
na
muwe tayari daima, kusamehe upesi, bila kuhukumu
na
daima mjaribu kuelewa ndugu yako. Kwa hiyo, mitume wa upendo wangu, muwaombeeni wale wasiojua kupenda, wale wasiowapenda, wale waliowatenda mabaya, wale ambao hawakujua upendo wa Mwanangu. Wanangu, ninawaomba haya, kwa sababu kumbukeni: kuomba maana yake ni kupenda
na
kusamehe. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2017
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaletea Mwanangu Yesu, ili awajalieni amani Yake
na
baraka Yake. Wanangu wapendwa, ninawaalika ninyi nyote kuishi
na
kushuhudia neema
na
zawadi mlizozipokea. Msiogope!Salini ili Roho Mtakatifu awapeni nguvu ya kuwa mashahidi wenye furaha
na
watu wa amani
na
matumaini. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, wakati duniani upendo unapopunguka, wakati njia ya wokovu haipatikani, Mimi, Mama yenu, naja kuwasaidieni kujua imani ya kweli, iliyo hai
na
ya kina,
na
kuwasaidieni kupenda kabisa. Kama Mama ninatamani mpendane, muwe wema
na
safi. Ni hamu yangu muwe wenye haki
na
mpendane. Wanangu, muwe wafurahivu rohoni, muwe safi, muwe watoto. Mwanangu alisema kwamba anapenda kukaa kati ya wenye mioyo safi, maana wenye mioyo safi ni daima vijana
na
wafurahivu. Mwanangu aliwaambieni msameheane
na
mpendane. Najua kwamba si rahisi sikuzote. Mateso husababisha kukua rohoni. Ili kukua rohoni kadiri iwezekanavyo, lazima msamehe
na
kupenda kwa dhati
na
kwa kweli. Wana wangu wengi duniani hawamjui Mwanangu, hawampendi. Lakini ninyi mnaompenda Mwanangu
na
kumchukua moyoni salini, salini,
na
mkisali mumhisi Mwanangu karibu yenu. Nafsi yenu ipumue Roho yake! Mimi nipo kati yenu
na
kuongea juu ya mambo madogo
na
makubwa. Sitachoka kuwasimulieni habari ya Mwanangu, aliye upendo wa kweli. Kwa hiyo, wanangu, nifungulieni mioyo yenu, acheni niwaongoze kama mama. Muwe mitume wa upendo wa Mwanangu
na
wangu. Kama Mama nawasihi: msisahau wale walioitwa
na
Mwanangu wawaongoze. Wachukueni moyoni
na
muwaombee. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2018
“
W
anangu wapendwa! Kipindi hiki kiwe kwenu kipindi cha sala ili Roho Mtakatifu, kwa njia ya sala, ashuke juu yenu
na
awape wongofu. Fungueni mioyo yenu
na
someni Maandiko Matakatifu ili, kwa njia ya ushahidi, ninyi pia muweze kuwa karibu zaidi
na
Mungu. Wanangu, tafuteni hasa Mungu
na
vitu vya Mungu
na
acheni duniani vile vya dunia, maana Shetani huwavuta kwa mavumbi
na
dhambi. Ninyi mnaalikwa katika njia ya utakatifu
na
mmeumbwa kwa ajili ya Mbingu. Tafuteni, kwa hiyo, Mbingu
na
vitu vya mbinguni. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninyi ambao Mwanangu anawapenda, ninyi ambao mimi ninawapenda, msiruhusu ubinafsi, kujipenda wenyewe, zitawale duniani. Msiache upendo
na
wema zifichwe. Ninyi mnaopendwa, mliojua upendo wa Mwanangu, kumbukeni ya kuwa kupendwa maana yake ni kupenda. Wanangu, muwe
na
imani! Mnapokuwa
na
imani mnafurahi
na
mkaeneza amani, nafsi yenu inaruka kwa shangwe: katika nafsi ile yumo Mwanangu. Mnapojitolea wenyewe kwa ajili ya imani, mnapojitolea wenyewe kwa ajili ya upendo, mnapowafanyia watu wengine mema, Mwanangu hutabasamu katika nafsi yenu. Mitume wa upendo wangu, mimi, kama Mama, ninawaelekea, ninawakusanya kunizunguka
na
ninataka kuwaongozeni katika njia ya upendo
na
imani, katika njia ya kufika kwenye Nuru ya ulimwengu. Nipo hapa kwa upendo
na
kwa imani, kwa maana, kwa baraka yangu ya kimama, nataka kuwapeni matumaini
na
nguvu katika mwendo wenu, kwa sababu njia ya kuongoza kwa Mwanangu si rahisi: imejaa matendo ya kujinyima, ya kujitolea, ya kujidhabihu, ya kusamehe
na
ya upendo, upendo mwingi. Njia ile, lakini, hupata amani
na
furaha. Wanangu, msisadiki sauti za uongo zinazosemesha kwa maneno yasiyo
na
ukweli, mwanga usio wa ukweli. Ninyi wanangu rudini kwa Maandiko! Ninawaangalieni kwa upendo kupita kiasi
na
, kwa neema ya Mungu, ninajidhihirisha kwenu. Wanangu, njoni pamoja nami, nafsi yenu iruke kwa shangwe! Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2018
“
W
anangu wapendwa! Katika kipindi hiki cha neema ninawaalika nyote kujifungua
na
kuishi amri ambazo Mungu aliwapeni ili, kwa njia ya sakramenti, ziwaongoze katika njia ya wongofu. Ulimwengu
na
vishawishi vya ulimwengu vinawajaribu; ninyi, wanangu, angalieni viumbe vya Mungu ambavyo katika uzuri
na
unyenyekevu Yeye aliwapa,
na
mpendeni Mungu, enyi wanangu, kuliko kila kitu naye atawaongoza katika njia ya wokovu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Baba wa Mbinguni amenifanyia makuu, jinsi anavyowafanyia wale wote wanaompenda sana
na
kwa wema
na
uaminifu
na
wanaomtumikia kwa ibada. Wanangu, Baba wa Mbinguni anawapenda
na
kwa ajili ya upendo wake mimi nipo hapa pamoja nanyi. Ninasema nanyi: kwa nini hamtaki kuona ishara? Pamoja naye yote ni rahisi zaidi: hata mateso, tunayoishi pamoja naye, ni mepesi zaidi, maana kuna imani. Imani husaidia mateso,
na
maumivu pasipo imani huongoza katika kukata tamaa. Mateso tunayoyaishi
na
kuyatolea kwa Mungu, huinua mtu. Je, Mwanangu hakuukomboa ulimwengu kwa njia ya mateso yake makali? Mimi, kama mama yake, katika maumivu
na
mateso nilikaa pamoja naye, kama vile ninavyokaa pamoja nanyi. Wanangu, mimi nipo pamoja nanyi katika maisha: katika maumivu
na
mateso, katika furaha
na
upendo. Kwa hiyo muwe
na
matumaini: matumaini ndiyo yanayotuwezesha kuelewa ya kuwa hapa, kwenye mateso, ni uhai. Wanangu, mimi nasema nanyi; sauti yangu inasema
na
nafsi yenu, Moyo wangu unasema
na
moyo wenu: Enyi, mitume wa upendo wangu, Moyo wangu wa kimama jinsi gani unavyowapenda. Mambo haya nataka kuwafundisha. Jinsi gani Moyo wangu unataka muwe wakamilifu, lakini mtakuwa hivyo tu wakati nafsi, mwili
na
upendo yatakapoungana ndani yenu. Kama wanangu nawaombeni: salini sana kwa ajili ya Kanisa
na
kwa wahudumu wake, kwa wachungaji wenu, ili Kanisa liwe kama Mwanangu anavyolitaka: safi kama maji ya chemchemi
na
limejaa upendo. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Machi 2018
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika kukaa pamoja nami katika kusali, wakati huu wa neema, ambapo giza linapigana
na
mwagaza. Wanangu, salini, muungame dhambi zenu mkaanzishe maisha mapya katika neema. Kateni shauri kwa Mungu naye atawaongoza kuelekea utakatifu
na
msalaba utakuwa kwenu ishara ya ushindi
na
matumaini. Mjivunie kubatizwa
na
mshukuruni moyoni mwenu kushika mpango wa Mungu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
Next>>