Our Lady of Medjugorje Messages containing 'na'
Total found:
218
Ujumbe, 2 Aprili 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa njia ya upendo mkubwa wa Baba wa Mbinguni, mimi ni pamoja nanyi kama Mama yenu nanyi ni pamoja nami kama wanangu, kama mitume wa upendo wangu ambao ninakusanya daima karibu nami. Wanangu, ninyi ni wale ambao, mkisali, yawapasa kujitolea kabisa kwa Mwanangu, ili kwamba si ninyi tena mnaoishi, bali ni Mwanangu ndani yenu; ili wale wote wasiomjua wamwone ndani yenu
na
watake kumjua. Salini ili waone ndani yenu unyenyekevu thabiti
na
wema, utayari kuwatumikia wengine; waone kwamba mnaishi kwa moyo wito wenu duniani, mkishirikiana
na
Mwanangu. Waone ndani yenu upole, rehema
na
upendo kuelekea Mwanangu, kama vile kuelekea ndugu
na
dada zenu. Enyi mitume wa upendo wangu, hamna budi kusali sana
na
kutakasa mioyo yenu, ili ninyi muwe wale wa kwanza waendao katika njia ya Mwanangu; ili ninyi muwe wale wenye haki wanaoungana
na
haki ya Mwanangu. Wanangu, kama mitume wangu lazima muungane
na
ushirika utokao katika Mwanangu, ili wanangu wasiomjua Mwanangu watambue ushirika wa upendo
na
watake kutembea katika njia ya uzima, njia ya umoja
na
Mwanangu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2018
“
W
anangu wapendwa, leo pia ninawaalika kuishi pamoja
na
Yesu maisha yenu mapya. Bwana Mfufuka awape nguvu ili muwe daima mashujaa katika majaribu ya maisha,
na
waaminifu
na
mdumu katika kusali, maana Yesu aliwaokoeni kwa majeraha Yake
na
kwa njia ya Ufufuko Wake aliwapa maisha mapya. Salini, wanangu
na
msipoteze matumaini. Katika mioyo yenu
na
ziwe furaha
na
amani, muwe mashahidi ya furaha ya kuwa wangu. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwapenda nyote kwa upendo wangu wa kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Mwanangu, aliye mwanga wa upendo, yote aliyoyafanya
na
anayoyafanya hufanya kwa ajili ya upendo. Vivyo hivyo nanyi, wanangu, mnapoishi katika upendo, mnapompenda jirani yenu
na
mnapofanya mapenzi yake. Enyi mitume wa upendo wangu, jifanyeni wadogo! Mfungulieni Mwanangu mioyo yenu safi, ili Yeye aweze kutenda kazi kwa njia yenu. Kwa msaada wa imani, mjijazie upendo. Lakini, wanangu, msisahau ya kuwa Ekaristi ndiyo kiini cha imani. Yeye ndiye Mwanangu anayewalisheni kwa Mwili wake
na
kuwaimarisheni kwa Damu yake. Yeye ndiye ajabu ya upendo: Mwanangu ajaye tena mwenye uhai ili kuzifufua nafsi. Wanangu, mkiishi katika upendo, ninyi mnafanya mapenzi ya Mwanangu naye huishi ndani yenu. Wanangu, matakwa yangu ya kimama ni kwamba mpendeni zaidi
na
zaidi, maana Yeye anawapenda kwa upendo wake. Anawapa upendo wake ili muweze kuueneza kwa watu wote kandokando yenu. Kwa njia ya upendo wake, kama mama mimi nipo pamoja nanyi kuwaambieni maneno ya upendo
na
matumaini, kuwaambieni maneno ya milele
na
ya kushinda wakati
na
mauti, kuwaalikeni kuwa mitume wangu wa upendo. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Mei 2018
“
W
anangu wapendwa, katika wakati huo wa wasiwasi ninawaalika kumwamini zaidi Mungu aliye Baba yenu mbinguni
na
anayenituma kuwaongozeni kwake. Ninyi, mfungulieni mioyo yenu kwa zawadi ambazo Yeye ataka kuwapeni
na
katika kimya ya moyo wenu mwabuduni Mwanangu, aliyetolea maisha Yake ili muishi katika milele anakotaka kuwaongoza. Matumaini yenu
na
yawe furaha ya kukutana
na
Yule Aliye juu katika maisha ya kila siku. Kwa hiyo ninawaalika: msiache sala maana sala hutenda miujiza. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Juni 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika kupokea kwa unyofu wa moyo maneno yangu, ninayowaambieni kama Mama ili muende katika njia ya mwanga kamili, wa usafi, wa upendo wa pekee wa Mwanangu, mtu
na
Mungu. Raha, mwanga usioelezeka kwa maneno ya kibinadamu utaingia nafsini mwenu,
na
mtashikwa
na
amani
na
upendo wa Mwanangu. Ninataka hayo kwa wanangu wote. Kwa hiyo ninyi, mitume wa upendo wangu, ninyi mnaojua kupenda
na
kusamehe, ninyi msiohukumu, ninyi ambao mimi ninahimiza, muwe mfano kwa wale wote wasiokwenda katika njia ya mwanga
na
upendo au waliotengana nayo. Kwa njia ya maisha yenu waonyesheni ukweli, waonyesheni upendo, maana upendo hushinda matatizo yote,
na
wanangu wote wana kiu ya upendo. Ushirika wenu wa upendo ni zawadi kwa Mwanangu
na
kwangu. Lakini, wanangu, kumbukeni ya kuwa kupenda maana yake ni kupenda mwenzako
na
kutakia wongofu wa nafsi yake. Ninapowatazama mmekusanyika karibu nami, moyo wangu unahuzunika kwa sababu ninaona upendo haba wa kidugu, upendo wenye huruma. Wanangu, Ekaristi, Mwanangu hai katikati yenu,
na
maneno yake yatawasaidia kuelewa. Neno lake, kweli, ni uhai, Neno lake huburudisha nafsi, Neno lake huwajulisha upendo. Wanangu wapenzi, ninawaombeni tena, kama Mama apendaye wana wake: wapendeni wachungaji wenu, waombeeni… Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Juni 2018
“
W
anangu wapendwa! Hii ni siku ambayo Bwana amenipa kwa kumshukuru kwa kila mmoja wenu, kwa wale walioongoka
na
waliokubali habari zangu
na
walioshika njia ya wongofu
na
ya utakatifu. Wanangu, furahini, maana Mungu ni mwenye rehema
na
anawapenda wote kwa Upendo wake mkubwa sana
na
kuwaongoza kuelekea njia ya wokovu kwa msaada wa kuja kwangu hapa. Mimi ninawapenda wote
na
ninawapa mwanangu ili Yeye awape amani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Julai 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Mimi ni Mama wa ninyi nyote
na
kwa hiyo msiogope kwa sababu mimi ninasikia sala zenu, najua kwamba mnanitafuta
na
kwa hiyo ninamwomba Mwanangu kwa ajili yenu; Mwanangu ambaye yu katika mwuungo pamoja
na
Baba wa mbinguni
na
pamoja
na
Roho Mfariji, Mwanangu anayewaongoza roho katika Ufalme alikotoka, ambao ni Ufalme wa amani
na
wa mwanga. Wanangu, mmepewa uhuru wa kuchagua, kwa hiyo mimi kama Mama ninawasihi mchague uhuru kwa mema,
na
kwa moyo safi
na
mnyofu mnaelewa, ingawa pengine hamwelewi maneno yote, ndani yenu mng'amue ukweli ni nini. Wanangu, msipoteze ukweli
na
maisha ya kweli kwa kufuata maneno ya uongo. Kwa njia ya maisha ya kweli Ufalme wa mbinguni huingia katika mioyo yenu, ni Ufalme wa upendo, wa amani
na
wa maelewano. Katika Ufalme ule, wanangu, hautakuwa
na
ubinafsi wa kuwaondoa kutoka kwa Mwanangu, kutakuwa
na
upendo
na
maelewano
na
jirani yako. Kwa hiyo kumbukeni, ninawaambieni tena, kusali maana yake ni kuwapenda wengine, kumpenda jirani yako, kujitoa kwa ajili yao; pendeni
na
toeni kwa jina la Mwanangu, hapo Yeye atatenda kazi ndani yenu
na
kwa ajili yenu. Wanangu, fikirini daima juu ya Mwanangu, mpendeni bila kipimo
na
hapo mtakuwa
na
maisha ya kweli, yatakayokuwa ya milele. Nawashukuru enyi Mitume wa upendo wangu!
”
Ujumbe, 25 Julai 2018
“
W
anangu wapendwa! Mungu aliniita ili niwaongozeni kwake, maana Yeye ndiye nguvu yenu. Kwa hiyo ninawaalika kumwomba
na
kumtegemea, maana Yeye ndiye kimbizo lenu kutoka kila uovu uliokaribu
na
kupeleka mioyo mbali kutoka neema
na
furaha mnakoitwa. Wanangu isheni Mbingu hapa duniani ili mkae vizuri
na
amri za Mungu ziwe mwanga katika njia yenu. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwapenda nyote kwa upendo wa kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo wa kimama ninawaalika kuifunua mioyo kwa imani, kuifunua mioyo kwa Mwanangu, ili katika mioyo yenu upendo kwa Mwanangu uimbe. Hakika, kutoka upendo huo tu, amani huingia nafsini. Wanangu, najua kwamba mna wema, najua kwamba mna upendo, upendo wenye rehema. Wanangu wangu wengi, lakini, wana moyo uliofungwa. Wanadhani kuweza kutenda pasipo kumwelekezea mawazo yao Baba wa mbinguni anayeangaza, pasipo kumwelekezea Mwanangu aliye daima pamoja nanyi katika Ekaristi
na
ataka kuwasikiliza. Wanangu, mbona hamzungumzi naye? Maisha ya kila mmoja wenu ni muhimu
na
ya thamani, maana ni zawadi ya Baba wa mbinguni kwa umilele. Kwa hiyo msisahau kamwe kumshukuru. Zungumzeni naye! Najua, enyi wanangu, ya kuwa mambo yatakayokuja hayajulikani kwenu lakini, mambo yenu ya mbele yatakapotokea, mtapata majibu yote. Upendo wangu wa kimama unataka muwe tayari. Wanangu, kwa maisha yenu wekeni katika mioyo ya watu mnaokutana hisia za amani, za mema, za upendo
na
msamaha. Kwa ajili ya sala, sikilizeni yanayowaambieni Mwanangu
na
tendeni namna hiyo. Ninawaalika tena kuwaombea wachungaji wenu, wale ambao Mwanangu aliwaita. Kumbukeni ya kuwa wanahitaji sala
na
upendo. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2018
“
W
anangu wapendwa! Huu ndio wakati wa neema. Wanangu, salini zaidi, semeni kidogo mkamwache Mungu awaongoze katika njia ya kutubu. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwapenda kwa upendo wa kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, maneno yangu ni manyofu lakini yamejaa upendo wa kimama
na
mahangaiko. Wanangu, juu yenu vivuli vya giza
na
vya udanganyifu vinaenea zaidi
na
zaidi, mimi ninawaiteni kuelekea mwanga
na
ukweli, mimi ninawaita kuelekea Mwanangu. Yeye peke yake huweza kugeuza kukata tamaa
na
maumivu yetu kuwa amani
na
utulivu, Yeye peke yake huweza kutoa matumaini katika maumivu makali sana. Mwanangu ni uzima wa ulimwengu, kwa kadiri mtakavyomjua, ndivyo mtakavyomkaribia
na
kumpenda maana Mwanangu ni upendo,
na
upendo unageuza yote. Yeye hufanya la ajabu hata neno lisilo la maana bila upendo machoni penu. Kwa hiyo nawaambieni tena ya kwamba mnapaswa kupenda sana ikiwa mnatamani kukua kiroho. Najua, enyi mitume wa upendo wangu, kwamba si rahisi sikuzote, lakini, wanangu, hata njia ngumu ni njia zinazoongoza kwenye ukuaji wa kiroho, wa kiimani
na
kwa Mwanangu. Wanangu, salini, mfikirie Mwanangu, nyakati zote za siku zenu inueni nafsi zenu kwake nami nitakusanya sala zenu kama maua kutoka bustani nzuri kuliko zote
na
kumpa Mwanangu. Muwe hakika mitume wa upendo wangu, wapeni wote upendo wa Mwanangu, muwe bustani zenye maua mazuri kuliko yote. Kwa njia ya sala saidieni wachungaji wenu ili waweze kuwa baba za kiroho waliojaa upendo kwa watu wote. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2018
“
W
anangu wapendwa! Hata viumbe vinawapa ishara za upendo wake Mungu kwa njia ya matunda vinayowapa. Nanyi, pia kupitia ujio wangu, mmepokea wingi wa zawadi
na
matunda. Wanangu, kadiri mlivyoitikia mwaliko wangu, Mungu anajua. Mimi ninawaalika: hamkuchelewa, kateni shauri kuwa watakatifu
na
kwa maisha ya pamoja
na
Mungu katika neema
na
katika amani! Mungu atawabariki
na
kuwapa mara mia zaidi, ikiwa mnamtumaini. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu, ninawaomba kuwa hodari wala kutowayawaya, maana hata mema madogo zaidi, ishara ya upendo mdogo zaidi hushinda maovu yanayoonekana zaidi
na
zaidi. Wanangu nisikilizeni ili mema yashinde, ili muweze kujua upendo wa Mwanangu ulio furaha mkubwa zaidi kuliko zote. Mikono ya mwanangu inawakumbatia, Yeye, apendaye nafsi, Yeye ambaye amejitolea kwa ajili yenu
na
kunajitolea sikuzote tena katika Ekaristi, Yeye aliye
na
maneno ya Uzima wa milele; kujua upendo wake, kufuata hatua zake, maana yake ni kuwa
na
mali ya kiroho. Huo ni utajiri unaojaza hisia iliyo njema,
na
unaoona upendo
na
mema popote. Mitume wa upendo wangu, wanangu, muwe kama mionzi ya jua ambayo kwa joto la upendo wa Mwanangu inawapasha joto wote wale wanaoizunguka. Wanangu, ulimwengu unahitaji mitume wa upendo, ulimwengu unahitaji sala nyingi, lakini sala zinazosaliwa kwa moyo
na
roho, si kwa midomo tu. Wanangu, muwe
na
hamu ya utakatifu mkiwa
na
unyenyekevu unaomwezesha Mwanangu kufanya kazi kwa njia yenu, kama Yeye apendavyo. Wanangu, sala zenu, fikira zenu
na
matendo yenu, haya yote yawafungulia ama kuwafungia mlango wa Ufalme wa Mbinguni. Mwanangu aliwaonyesha njia
na
kuwapa tumaini, mimi ninawafariji
na
kuwapa moyo maana, wanangu, mimi nilijua maumivu, lakini nilikuwa
na
imani
na
tumaini, sasa nimepata thawabu ya uzima katika Ufalme wa Mwanangu. Kwa hiyo, nisikilizeni, jipeni moyo, msiwayawaye. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2018
“
W
anangu wapendwa! Ninyi mna neema kubwa ya kuitwa kwa maisha mapya kwa njia ya ujumbe ninaowapeni. Wanangu, huu ni wakati wa neema, wakati
na
wiko kwa wongofu wenu
na
kwa vizazi vya wakati ujao. Kwa hiyo ninawaalika, wanangu, kusali zaidi
na
kumfunulia Mwanangu Yesu moyo wenu. Mimi nipo pamoja nanyi, ninawapenda wote
na
kubariki kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Novemba 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu, Moyo wangu wa kimama unateseka wakati ninapotazama wanangu wasiopenda ukweli, wanaouficha; wakati ninapotazama wanangu wasiosali kwa moyo wala kwa matendo. Nimesikitika wakati ninapomwambia Mwanangu ya kuwa wana wangu wengi hawana imani tena, ya kuwa hawamjui Yeye, Mwanangu. Kwa hiyo ninawaalika, mitume wa upendo wangu: mjaribu kutazama mpaka ndani ya mioyo ya watu,
na
kule bila shaka mtapata hazina ndogo iliyofichwa. Kutazama hivyo ni rehema ya Baba wa mbinguni. Kutafuta mema hata palipo maovu makubwa zaidi, kutafuta kuwaelewana wala kutohukumiana: hilo ni neno ambalo Mwanangu anawaombeni. Nami, kama Mama, ninawaalika kumsikiliza. Wanangu, roho ni yenye nguvu kuliko mwili
na
, ikichukuliwa
na
upendo
na
matendo hushinda vikwazo vyote. Msisahau: Mwanangu aliwapendeni
na
anawapenda. Upendo wake ni pamoja nanyi
na
ndani yenu, wakati mpo kitu kimoja pamoja naye. Yeye ni mwanga wa ulimwengu,
na
hakuna mtu wala kitu kiwezacho kumsimamisha katika utukufu wa mwisho. Kwa hiyo, mitume wa upendo wangu, msiwe
na
hofu ya kushuhudia ukweli! Ushuhudieni kwa hamu, kwa matendo, kwa upendo, kwa sadaka yenu, lakini hasa kwa unyenyekevu. Shuhudieni ukweli kwa wale ambao hawajajua Mwanangu. Mimi nitakuwa karibu nanyi, mimi nitawatia moyo. Shuhudieni upendo usioishi tena, maana huja kutoka Baba wa mbinguni ambaye ni wa milele
na
anawatolea wana wangu wote umilele. Roho wa Mwanangu itakuwa karibu nanyi. Ninawaalika tena, wanangu: muwaombee wachungaji wenu, ombeni ili upendo wa Mwanangu uweze kuwaongoza. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2018
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati wa neema
na
sala, wakati wa kungojea
na
wa majitoleo. Mungu anajitolea kwenu ili mumpende juu ya kila jambo. Kwa hiyo, wanangu, fumbueni mioyo yenu
na
jamaa zenu ili kungojea huko kugeuke kuwa sala
na
upendo
na
hasa majitoleo. Mimi nipo pamoja nanyi, wanangu,
na
ninawasihi msiache mema maana matunda yaonekana, yasikika,
na
yafika mbali. Kwa hiyo adui amekasirika
na
anafanya kila njia kuwaondoa ninyi katika sala. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2018 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu, Wakati mnaponijia kama Mama kwa moyo safi
na
wazi, mjue ya kuwa ninawasikiliza, ninawatia moyo, ninawafariji
na
hasa ninawaombeeni kwa Mwanangu. Najua ya kuwa mnataka kuwa
na
imani thabiti
na
kuionyesha kwa njia inayofaa. Neno analotaka Mwanangu kutoka kwenu ni imani ya kweli, thabiti
na
kubwa. Hivyo kila njia mnavyoielezea ni ya kufaa. Imani ni fumbo la ajabu tunalohifadhi moyoni. Inakaa baina ya Baba wa Mbinguni
na
wana wake wote. Hutambulika kwa matunda
na
kwa upendo ambao sisi tunao kwa viumbe vyote vya Mungu. Enyi mitume wa upendo wangu, wanangu, mtumaini Mwanangu! Saidieni ili wanangu wote wajue upendo wake. Ninyi ni matumaini yangu, ninyi mnaojitahidi kupenda Mwanangu pasipo unafiki. Kwa jina la upendo, kwa wokovu wenu, kulingana
na
mapenzi ya Baba wa Mbinguni
na
kwa njia ya Mwanangu, nipo hapa katikati yenu. Mitume wa upendo wangu, kwa njia ya sala
na
sadaka mioyo yenu iangazwe
na
upendo
na
mwanga wa Mwanangu. Mwanga ule
na
upendo ule uangaze wote wale mnaokutana
na
uwarudishe kwa Mwanangu! Mimi nipo nanyi. Hasa nipo pamoja
na
wachungaji wenu: kwa upendo wangu wa kimama ninawaangaza
na
kuwatia moyo, ili, kwa njia ya mikono iliyobarikiwa
na
Mwanangu, wabariki ulimwengu mzima. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2018 - Tokeo la mwaka la Yakobo
Katika tokeo la mwisho la kila siku tarehe 12 Septemba 1998 Bikira Maria alimwambia Yakobo Kolo ya kuwa ataona tokeo mara moja kila mwaka, tarehe 25 Decemba, siku ya Noeli. Hivyo kumekuwa
na
tokea hata mwaka huu. Tokeo limeanza saa 7
na
dakika 38
na
likadumu dakika 9. Bikira Maria amekuja pamoja
na
Mtoto Yesu mikononi mwake. Bikira Maria kwa njia ya Yakobo alipitisha ujumbe huu:
“
W
anangu wapendwa, katika siku hii ya neema ninawaalika kupenda. Wanangu, Mungu anawapenda kupita kiasi
na
kwa hiyo wanangu, mmejaa imani, bila kutazama nyuma
na
bila hofu mwachieni kabisa mioyo yenu ili Mungu aijaze kwa upendo wake. Msiwe
na
hofu kuamini upendo Wake
na
rehema Yake maana upendo Wake ni mwenye nguvu kuliko kila udhaifu wenu
na
hofu. Kwa hiyo, wanangu, mmejaa upendo katika mioyo yenu mwamini Yesu
na
mseme Ndiyo yenu maana Yeye ni njia ya pekee ya kuwaongoza kwa Baba wa milele.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2018
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu Yesu ambaye ni Mfalme wa amani. Yeye anawapa amani, basi amani hii isiwe yenu tu, wanangu, lakini wapelekeeni
na
wengine katika furaha
na
unyenyekevu. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwaombeeni katika wakati huu wa neema ambayo Mungu anataka kuwapa. Uwepo wangu ni ishara ya upendo, wakati nipo hapa pamoja nanyi niwalinde
na
kuwaongoza kuelekea umilele. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, inasikitisha kwamba katikati yenu, wanangu, yapo mashindano mengi, chuki, masilahi yenu wenyewe
na
ubinafsi. Wanangu, hivi kwa urahisi mnamsahau Mwanangu, maneno Yake
na
upendo Wake. Imani inazimika katika roho nyingi
na
mioyo imetekwa
na
vitu vya ulimwenguni. Lakini moyo wangu wa kimama unajua ya kuwa katikati yenu kuna wale wanaoamini
na
kupenda, wale ambao wanajaribu kumkaribia Mwanangu zaidi
na
zaidi, ambao wanamtafuta bila kuchoka
na
namna hii, wananitafuta hata mimi. Hawa ndio wanyenyekevu
na
wapole ambao, pamoja
na
maumivu
na
mateso wanayoyachukua katika kimya, pamoja
na
tumaini lao
na
hasa pamoja
na
imani yao, ni mitume wa upendo wangu. Wanangu, mitume wa upendo wangu, ninawafundisha ya kuwa Mwanangu hatafuti sala tu pasipo kuchoka bali hata matendo
na
hisia. Salini ili katika sala mpate kuzidi katika imani
na
katika upendo. Mpendane wenyewe kwa wenyewe: hilo ndilo analotaka Yeye, hiyo ndiyo ni njia ya uzima wa milele. Wanangu, msisahau ya kuwa Mwanangu ameleta mwanga kwa ulimwengu huu. Ameuleta kwa wale ambao walitaka kuuona
na
kuupokea. Hawa muwe ninyi, maana huu ndio mwanga wa ukweli, wa amani
na
wa upendo. Mimi ninawaongoza kama mama kumwabudu Mwanangu, kumpenda pamoja nami. Fikira zenu, maneno
na
matendo yenu yamwelekee Mwanangu, yawe katika jina Lake: hapo tu moyo wangu utajazwa. Nawashukuru.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
Next>>