Our Lady of Medjugorje Messages containing 'na'
Total found:
218
Ujumbe, 25 Novemba 2019
“
W
anangu wapendwa, wakati huu uwe kwenu wakati wa sala. Bila Mungu hamwezi kuwa
na
amani. Kwa hiyo, wanangu, salini kwa ajili ya amani katika mioyo yenu
na
katika familia zenu ili Yesu aweze kuzaliwa ndani yenu
na
kuwapeni upendo wake
na
baraka yake. Ulimwengu uko katika vita kwa sababu mioyo imejaa machukio
na
wivu. Wanangu, wasiwasi unaonekana katika macho yenu kwa sababu hamkuruhusu Yesu kuzaliwa katika maisha yenu. Mtafuteni, ombeni
na
Yeye atajitoa kwenu katika yule Mtoto aliye furaha
na
amani. Mimi niko pamoja nanyi
na
ninasali pamoja nanyi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninapowatazama ninyi mnaopenda Mwanangu, furaha inajaza Moyo wangu. Ninawabariki kwa baraka ya kimama. Pamoja
na
baraka ya kimama ninawabariki hata wachungaji wenu: ninyi mnaotangaza maneno ya Mwanangu, mnaobariki kwa mikono yake
na
mnaompenda hata kuwa tayari kufanya kwa furaha kila sadaka kwa ajili yake. Ninyi mfuateni Yeye, aliyekuwa Mchungaji wa kwanza, Mmisionari wa kwanza. Wanangu, mitume wa upendo wangu, kuishi
na
kufanya kazi kwa ajili ya wengine, kwa wale wote mnaopenda kwa njia ya Mwanangu, ni furaha
na
faraja ya maisha ya kidunia. Ikiwa kwa njia ya sala, upendo
na
sadaka Ufalme wa Mungu ni katika mioyo yenu, hapo kwa ninyi maisha ni yenye furaha
na
matulivu. Katikati ya wale wanaompenda Mwanangu
na
wanaopendana kwa ajili yake, maneno si ya lazima. Kutazamana kwatosha ili kusikia maneno yasiyonenwa
na
hisia zisizoonyeshwa. Pale panapotawala upendo, wakati hauna maana tena. Sisi ni pamoja nanyi! Mwanangu anawajua
na
kuwapenda. Upendo ni kilichowaongoza kwangu
na
, kwa njia ya upendo huu, mimi nitakuja kwenu
na
nitawaambieni kazi za wokovu. Ninataka ya kuwa wana wangu wote wawe
na
imani
na
wahisi upendo wangu wa kimama unaowaongoza kwa Yesu. Kwa hiyo ninyi, wanangu, ko kote mwendako angazeni kwa upendo
na
kwa imani, kama mitume wa upendo. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2019
“
W
anangu wapendwa, Nawaletea ninyi Mwanangu Yesu ili awabariki
na
kuwafunulia Upendo wake utokao mbinguni. Moyo wenu unatamani amani inayopungua zaidi
na
zaidi duniani. Kwa sababu hiyo watu wako mbali
na
Mungu, nafsi zinaumwa
na
zinaelekea kifo cha kiroho. Mimi nipo pamoja nanyi, wanangu, niwaongoze kwenye njia hii ya wokovu ambayo Mungu anawaiteni. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2020 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, najua kuwepo katika maisha yenu
na
mioyo yenu. Nahisi upendo wenu, nasikia sala zenu
na
kuzipeleka kwa Mwanangu. Lakini, wanangu, mimi nataka kwa njia ya upendo wa kimama, kuwepo katika maisha ya wanangu wote. Nataka kukusanya karibu yangu wanangu wangu wote, chini ya joho langu la kimama. Kwa hiyo ninawaalika ninyi
na
kuwaiteni mitume wa upendo wangu, il mnisaidie. Wanangu, Mwanangu aliyatamka maneno haya: "Baba yetu”, Baba yetu uliye popote
na
katika mioyo yetu, kwa sababu ataka kuwafundisha kusali kwa maneno
na
kwa hisia zenu. Ataka muwe bora zaidi kila siku, muishi upendo wenye rehema ulio sala
na
sadaka isiyo
na
mipaka kwa ajili ya wengine. Wanangu mpeni Mwanangu upendo kwa jirani; mpeni jirani wenu maneno ya faraja, ya huruma
na
matendo ya haki. Yote mliyoyatoa kwa wengine, enyi mitume wa upendo wangu, Mwanangu anayapokea kama zawadi. Nami ni pamoja nanyi kwa sababu Mwanangu ataka kwamba upendo wangu, ulio kama mwali wa nuru, uzihuishe nafsi zenu, uwasaidie katika kutafuta amani
na
uheri wa milele. Kwa hiyo, wanangu, pendaneni,
na
muunganishwe kwa njia ya Mwanangu, ili muwe wana wa Mungu ambao wote pamoja kwa moyo uliojaa, wazi
na
safi mkisema kwa pamoja “Baba yetu” pasipo kuogopa! Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2020
“
W
anangu wapendwa, Leo ninawaalika kusali tena zaidi ili msikie katika mioyo yenu utakatifu wa msamaha. Katika familia lazima kuwepo utakatifu kwa sababu enyi wanangu, ulimwengu hauna wakati ujao bila upendo
na
utakatifu, kwa sababu katika utakatifu
na
katika furaha ninyi mjitolee kwa Mungu Mwumbaji anayewapendeni kwa upendo mkubwa sana. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2020 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nilichaguliwa kuwa mama wa Mungu
na
mama yenu, kwa maamuzi
na
upendo wa Bwana, lakini pia kwa mapenzi yangu, kwa upendo wangu usio
na
kifani kwake Baba wa mbinguni
na
kwa imani yangu yote Kwake. Mwili wangu ulikuwa kikombe cha Mungu Mtu. Nilikuwa mtumishi wa ukweli, wa upendo
na
wokovu kama vile nilivyo sasa katikati yenu, ili kuwaalika, wanangu, mitume wa upendo wangu, kuwa waletaji ukweli, ili kuwaalika, kwa njia ya utashi
na
upendo yenu kumwelekea Mwanangu, ili kueneza maneno Yake, maneno ya wokovu
na
kuyaonyesha, kwa vitendo vyenu, kwa wale wote ambao hawajamjua mwanangu
na
upendo Wake. Nguvu mtaipata katika Ekaristi: Mwanangu awalisheni kwa mwili Wake
na
kuwaimarisha kwa damu Yake. Wanangu, wekeni mikono yenu pamoja kwa sala
na
tazameni kuelekea msalaba kwa ukimya. Kwa jinsi hii mtapata imani ili muweze kuieneza, mtapata ukweli ili muweze kuupambanua, mtapata upendo ili muweze kuelewa namna ya kupenda kwa uhakika. Wanangu, mitume wa upendo wangu, wekeni mikono yenu pamoja kwa sala
na
tazameni kuelekea msalaba: katika msalaba tu kuna wokovu. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2020
“
W
anangu wapendwa, Katika kipindi hiki cha neema nataka kuona nyuso zenu zigeuke katika sala. Ninyi mmejaa mahangaiko ya kidunia kiasi kwamba hamuoni hata ujio wa majira ya kuchipua kwa mimea. Wanangu, mnaalikwa kwa toba
na
kwa sala. Kama viumbe vya asili vinapigana katika kimya kwa maisha mapya, hivyo hata ninyi mnaalikwa kujifungua katika sala kwa Mungu ambaye kwake mtapata amani
na
joto la jua la kipindi cha kuchanua kwa mimea katika mioyo yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2020 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, upendo wenu safi
na
wa kweli unavuta Moyo wangu wa kimama. Imani yenu
na
usadiki wenu katika Baba wa mbinguni ni mawaridi yenye harufu nzuri mnayonitolea: shada la mawaridi mazuri sana, lililotengenezwa kwa sala zenu, kwa matendo ya rehema
na
ya upendo. Mitume wa upendo wangu, ninyi mnaojaribu kumfuata Mwanangu pasipo unafiki
na
kwa moyo safi, ninyi ambao pasipo unafiki mnampenda, muwe ninyi wenyewe kusaidia: muwe mfano kwa wale ambao hawajajua upendo wa Mwanangu. Lakini, wanangu, siyo kwa maneno tu, bali hata kwa matendo
na
hisia safi, ambayo kwa njia yake mnamtukuza Baba wa mbinguni. Mitume wa upendo wangu, ni wakati wa kukesha
na
ninawaombeni upendo;
na
msihukumu mtu yeyote, kwa maana Baba wa mbinguni atahukumu wote. Ninawaombeni mpende,
na
mueneze ukweli, kwa maana ukweli ni wa kale: Ukweli siyo mpya, Ukweli ni wa milele, Ukweli ndiyo ukweli! Ukweli unatolea ushuhuda wa umilele wa Mungu. Bebeni mwanga wa Mwanangu
na
mpasue giza ambalo linataka kuwakandamiza zaidi
na
zaidi. Msiwe
na
hofu: kwa ajili ya neema
na
upendo wa Mwanangu, mimi nipo pamoja nanyi! Ninawashukuru. ”
”
Ujumbe, 25 Machi 2020
“
W
anangu wapendwa, katika miaka hii yote mimi nipo pamoja nanyi ili kuwaongoza kwenye njia ya wokovu. Rudieni kwa Mwanangu, rudieni katika sala
na
mfungo. Wanangu, mwachieni Mungu aongee
na
mioyo yenu kwa sababu shetani anatawala
na
anatamani kuangamiza maisha yenu
na
dunia mnamotembelea. Muwe
na
ujasiri
na
amueni kuwa watakatifu. Mtaona wongofu katika mioyo yenu
na
katika familia zenu, sala itasikilizwa, Mungu atayapokea maombi yenu
na
kuwapa amani. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2020
“
W
anangu wapendwa, wakati huu uwe kwenu himizo kwa wongofu wenu binafsi. Wanangu, ombeni katika upweke Roho Mtakatifu ili iwaimarishe katika imani
na
katika kumsadiki Mungu ili kuweza kuwa mashahidi wa upendo ambao Mungu anawapa kupitia uwepo wangu. Wanangu, msiruhusu majaribu yafanye mioyo yenu kuwa migumu
na
sala kuwa kama jangwa. Muwe mwangi wa upendo wa Mungu
na
mshuhudieni Yesu Aliyefufuka kwa njia ya maisha yenu. Mimi nipo pamoja nanyi
na
ninawapenda nyote kwa upendo wangu wa kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu”.
”
Ujumbe, 25 Mei 2020
“
W
anangu wapendwa, Salini pamoja Nami kwa maisha mapya ya ninyi nyote. Wanangu, katika mioyo yenu mnajua ni nini lazima kibadilike: rudini kwa Mungu
na
kwa Amri Zake ili Roho Mtakatifu aweze kugeuza maisha yenu
na
uso wa dunia hii, inayohitaji kufanywa upya katika Roho. Wanangu, muwe sala kwa wale wote wasiosali, muwe furaha kwa wale wote wasioona njia ya kutokea, muwe waletaji mwanga katika giza za wakati huu wa wasiwasi. Salini
na
ombeni msaada
na
ulinzi wa watakatifu ili ninyi pia muweze kutamani mbingu
na
mambo halisi ya kimbingu. Mimi nipo pamoja nanyi nikiwalinda
na
kuwabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2020
“
W
anangu wapendwa, ninasikiliza maombi yenu
na
sala zenu
na
ninawaombea kwa mwanangu Yesu aliye njia, kweli
na
uzima. Wanangu, rudieni kusali
na
fungueni mioyo yenu katika wakati huu wa neema
na
shikeni njia ya wongofu. Maisha yenu yanapita
na
hayana maana bila Mungu. Kwa hiyo mimi ni pamoja nanyi niwaongoze kuelekea utakatifu wa maisha ili kila mmoja wenu agundue furaha ya kuishi. Wanangu, ninawapenda wote
na
kuwabariki kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2020
“
W
anangu wapendwa, Katika wakati huu wa wasiwasi ambapo ibilisi anavuna nafsi ili kuwavuta kwake, niwaalika kwa sala ya kudumu ili katika sala mtambue Mungu wa upendo
na
wa matumaini. Wanangu, shikeni msalaba katika mikono yenu.
Na
uwatie moyo kwa kuwa upendo unashinda sikuzote hasa sasa ambapo msalaba
na
imani yamekataliwa. Ninyi muwe mwangwi
na
mfano kwa njia ya maisha yenu ya kuwa imani
na
matumaini bado hai
na
ulimwengu mpya wa amani unawezekana. Mimi nipo pamoja nanyi
na
ninawaombea mbele ya mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2020
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati wa neema. Mimi nipo pamoja nanyi
na
kuwaalika tena, wanangu, mrudieni Mungu
na
kwa kusali ili sala iwe furaha kwenu. Enyi wanangu hamtakuwa
na
wakati ujao wala amani mpaka katika maisha yenu mtakapoanza kuishi maongezi ya binafsi
na
badiliko katika mema. Maovu yatakoma
na
amani itatawala katika mioyo yenu
na
katika ulimwengu. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini. Mimi nipo pamoja nanyi
na
ninawaombea kwa mwanangu Yesu kwa ajili ya kila mmoja wenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Mimi ni pamoja nanyi kwa muda mrefu kwa maana Mungu ni mkuu katika upendo wake
na
katika uwepo wangu. Wanangu, ninawaalika kurudi kwa Mungu
na
kwa sala. Kipimo cha kuishi kwenu kiwe upendo
na
msisahau, wanangu, kwamba maombi
na
kufunga hufanya miujiza ndani yenu
na
kuwazunguka. Yote mnayoyafanya yawe kwa ajili ya utukufu wa Mungu
na
hapo Mbingu itajaza moyo wenu
na
furaha mkahisi ya kuwa Mungu anawapenda
na
kunituma ili kuokoa ninyi
na
Dunia ambayo juu yake mnaishi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2020
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu ninawaita kumrudia Mungu
na
sala. Waiteni watakatifu wote wawasaidie ili wawe mfano
na
msaada kwenu. Shetani ni mwenye nguvu
na
anapigania kuivutia kwake mioyo mingi zaidi awezavyo. Anataka vita
na
chuki. Kwa sababu hiyo Mimi ni pamoja nanyi muda mrefu ili niwaongoze kwenye njia ya wokovu, kwa Yule aliye njia, kweli
na
uzima. Wanangu, rudini kwa upendo kumwelekea Mungu naye atakuwa nguvu yenu
na
kimbilio lenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Huu ni wakati wa upendo, wa uchangamfu, wa sala
na
wa furaha. Salini, wanangu, ili Mtoto Yesu azaliwe katika mioyo yenu. Fungueni mioyo yenu kwa Yesu anayejitoa kwa kila mmoja wenu. Mungu amenialika ili mimi niwe furaha
na
matumaini katika wakati huu nami ninawaambia: bila Mtoto Yesu hamna wala huruma wala hisia ya Mbingu, zinazofichika katika yule Mtoto mchanga. Kwa hiyo, wanangu, fanyeni kazi juu ya nafsi zenu wenyewe. Mkisoma Maandiko Matakatifu, mtagundua kuzaliwa kwa Yesu
na
furaha kama ile ya siku za kwanza ya matokeo ya Medjugorje iliyotolea kwa ubinadamu. Historia itakuwa ukweli, ambao hata leo unajirudia ndani yenu
na
kuwazunguka. Fanyeni kazi
na
jengeni amani kwa njia ya sakramenti ya Kitubio. Jipatanisheni
na
Mungu, wanangu,
na
mtaona miujiza inawazunguka. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mtoto Yesu anayewaletea amani, Yule aliye wakati uliopita, wakati wa sasa
na
wakati ujao wa kuishi kwenu. Wanangu, msiruhusu imani yenu
na
matumaini yenu katika wakati ujao ulio bora yazimike, kwa maana ninyi mmechaguliwa kwa kuwa mashahidi wa matumaini katika kila hali. Kwa ajili hiyo mimi ni hapa pamoja
na
Yesu ili awabariki kwa amani yake. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2021
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huo ninawaalika kusali, kufunga
na
kujikana ili muweze kuwa wenye nguvu zaidi katika imani. Huu ni wakati wa mwamko
na
wa kuzaliwa upya. Kama vitu vya asili vinavyojitoa nanyi wanangu, fikirini juu ya mambo mliyopokea. Muwe waletaji wa amani
na
wa upendo wenye furaha ili kuishi vizuri duniani. Tamanini Mbingu kwa sababu Mbinguni hakuna wala huzuni wala machukio. Kwa hiyo, wanangu, amueni tena kuongoka,
na
utakatifu utawale katika maisha yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2021
“
W
anangu wapendwa! Mungu ameniruhusu kuwa pamoja nanyi leo pia kwa kuwaalika kusali
na
kufunga. Ishini wakati huu wa neema
na
muwe mashahidi wa tumaini maana, ninawaambia tena wanangu, kwa kusali
na
kufunga hata vita vinaweza kuisha. Wanangu, aminini
na
kuishi katika imani
na
kwa imani wakati huu wa neema
na
Moyo wangu usio
na
dhambi ya asili haumwachi yeyote kati yenu katika wasiwasi ikiwa ananikimbilia. Ninawaombea mbele ya Yeye aliye juu
na
ninasali ili amani iwepo katika mioyo yenu
na
kwa ajili ya tumaini katika wakati ujao. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
Next>>