Our Lady of Medjugorje Messages containing 'neema'
Total found:
55
Ujumbe, 25 Aprili 2019
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati wa
neema
, wakati wa rehema kwa kila mmoja wenu. Wanangu, msiruhusu upepo wa chukio na hofu utawale ndani yenu na karibu nanyi. Ninyi, wanangu, mmealikwa kuwa upendo na sala. Ibilisi ataka hofu na fujo lakini ninyi, wanangu, muwe furaha ya Yesu Mfufuka ambaye amekufa na kufufuka kwa ajili ya kila mmoja wenu. Yeye ameshinda kifo kwa kuwapeni uzima, uzima wa milele. Kwa hiyo, wanangu, mshuhudieni na muwe wenye fahari kwa kufufuliwa katika Yeye. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2019
“
W
anangu wapendwa, Fanyeni kazi na shuhudieni kwa upendo Ufalme wa Mbinguni ili muweze kuwa hamjambo hapa duniani. Wanangu, Mungu atabariki mara mia zaidi juhudi yenu na mtakuwa mashahidi katikati ya watu, roho za wale wasioamini zitahisi
neema
ya wongofu na Mbingu itazipokea taabu zenu na sadaka zenu. Wanangu, shuhudieni kwa tasbihi mkononi ili muwe wangu na kateni shauri kuwa watakatifu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Salini kila siku Tasbihi, taji lile la maua linaloniungana moja kwa moja kama Mama kwa maumivu yenu, mateso, mahitaji na matumaini. Mitume wa upendo wangu, Mimi nipo pamoja nanyi kwa njia ya
neema
na upendo wa Mwanangu, nanyi ninawaombeni sala. Sala zenu zinahitajika sana ulimwenguni, ili roho ziongoke! Fungueni wazi kwa imani timilifu mioyo yenu kwa Mwanangu, na yeye ataandika ndani yao muhtasari wa Neno lake, yaani upendo. Ishini muungano usiotenganika na Moyo Mtakatifu sana wa Mwanangu! Wanangu, kama Mama nawaambieni ya kwamba hakuna wakati wa kupoteza ili kupiga magoti mbele ya Mwanangu, kumkiri kama Mungu wenu, aliye kitovu cha maisha yenu. Mtoeni karama, zile anazozipenda zaidi, yaani upendo kwa jirani yako, rehema na mioyo safi. Mitume wa upendo wangu, wanangu wengi bado hawajamkiri Mwanangu kama Mungu wao, bado hawajajua upendo wake. Lakini ninyi, kwa njia ya sala yenu inayosema kwa moyo safi na wazi, pamoja na karama mnazotoa kwa Mwanangu, mtasababisha kwamba hata mioyo migumu zaidi ifunguke. Mitume wa upendo wangu, nguvu ya sala inayosemwa kutokana na moyo, ya sala yenye nguvu na iliyojaa upendo, hugeuza ulimwengu. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini! Mimi nipo pamoja nanyi.. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2020
“
W
anangu wapendwa, Katika kipindi hiki cha
neema
nataka kuona nyuso zenu zigeuke katika sala. Ninyi mmejaa mahangaiko ya kidunia kiasi kwamba hamuoni hata ujio wa majira ya kuchipua kwa mimea. Wanangu, mnaalikwa kwa toba na kwa sala. Kama viumbe vya asili vinapigana katika kimya kwa maisha mapya, hivyo hata ninyi mnaalikwa kujifungua katika sala kwa Mungu ambaye kwake mtapata amani na joto la jua la kipindi cha kuchanua kwa mimea katika mioyo yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2020 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, upendo wenu safi na wa kweli unavuta Moyo wangu wa kimama. Imani yenu na usadiki wenu katika Baba wa mbinguni ni mawaridi yenye harufu nzuri mnayonitolea: shada la mawaridi mazuri sana, lililotengenezwa kwa sala zenu, kwa matendo ya rehema na ya upendo. Mitume wa upendo wangu, ninyi mnaojaribu kumfuata Mwanangu pasipo unafiki na kwa moyo safi, ninyi ambao pasipo unafiki mnampenda, muwe ninyi wenyewe kusaidia: muwe mfano kwa wale ambao hawajajua upendo wa Mwanangu. Lakini, wanangu, siyo kwa maneno tu, bali hata kwa matendo na hisia safi, ambayo kwa njia yake mnamtukuza Baba wa mbinguni. Mitume wa upendo wangu, ni wakati wa kukesha na ninawaombeni upendo; na msihukumu mtu yeyote, kwa maana Baba wa mbinguni atahukumu wote. Ninawaombeni mpende, na mueneze ukweli, kwa maana ukweli ni wa kale: Ukweli siyo mpya, Ukweli ni wa milele, Ukweli ndiyo ukweli! Ukweli unatolea ushuhuda wa umilele wa Mungu. Bebeni mwanga wa Mwanangu na mpasue giza ambalo linataka kuwakandamiza zaidi na zaidi. Msiwe na hofu: kwa ajili ya
neema
na upendo wa Mwanangu, mimi nipo pamoja nanyi! Ninawashukuru. ”
”
Ujumbe, 25 Juni 2020
“
W
anangu wapendwa, ninasikiliza maombi yenu na sala zenu na ninawaombea kwa mwanangu Yesu aliye njia, kweli na uzima. Wanangu, rudieni kusali na fungueni mioyo yenu katika wakati huu wa
neema
na shikeni njia ya wongofu. Maisha yenu yanapita na hayana maana bila Mungu. Kwa hiyo mimi ni pamoja nanyi niwaongoze kuelekea utakatifu wa maisha ili kila mmoja wenu agundue furaha ya kuishi. Wanangu, ninawapenda wote na kuwabariki kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2020
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati wa
neema
. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaalika tena, wanangu, mrudieni Mungu na kwa kusali ili sala iwe furaha kwenu. Enyi wanangu hamtakuwa na wakati ujao wala amani mpaka katika maisha yenu mtakapoanza kuishi maongezi ya binafsi na badiliko katika mema. Maovu yatakoma na amani itatawala katika mioyo yenu na katika ulimwengu. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombea kwa mwanangu Yesu kwa ajili ya kila mmoja wenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2021
“
W
anangu wapendwa! Mungu ameniruhusu kuwa pamoja nanyi leo pia kwa kuwaalika kusali na kufunga. Ishini wakati huu wa
neema
na muwe mashahidi wa tumaini maana, ninawaambia tena wanangu, kwa kusali na kufunga hata vita vinaweza kuisha. Wanangu, aminini na kuishi katika imani na kwa imani wakati huu wa
neema
na Moyo wangu usio na dhambi ya asili haumwachi yeyote kati yenu katika wasiwasi ikiwa ananikimbilia. Ninawaombea mbele ya Yeye aliye juu na ninasali ili amani iwepo katika mioyo yenu na kwa ajili ya tumaini katika wakati ujao. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2021
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu Yesu awapeni amani yake. Wanangu, bila amani hamna wala wakati ujao, wala baraka, kwa hiyo rudieni kusali kwa sababu tunda la sala ni furaha na imani, na bila hiyo hamwezi kuishi. Baraka ya leo tunayowapa, ileteni kwa jamaa zenu na tajirisheni wote wale mnaokuta ili wahisi
neema
ambayo mnapokea. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2023
“
W
anangu wapendwa! Ongokeni na mvae mavazi ya toba na maombi ya kina ya kibinafsi na kwa unyenyekevu mwombe Aliye Juu amani. Katika wakati huu wa
neema
Shetani anataka kuwapotosha ninyi, nanyi wanangu, mwangalieni Mwanangu na kumfuata kuelekea Kalvari, kwa kujikana na kufunga. Niko pamoja nanyi kwa sababu Aliye Juu ameniruhusu niwapende ninyi na kuwaongoza kuelekea furaha ya moyo, katika imani inayokua ndani ya wale wote wanaompenda Mungu zaidi ya vitu vyote. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa
neema
, ambao Aliye Juu amenituma niwapende ninyi na kuwaongoza katika njia ya uongofu, toeni sala zenu na sadaka zenu kwa ajili ya wale wote walio mbali na wasiojua upendo wa Mungu. Ninyi, wanangu, muwe mashahidi wa upendo na amani kwa mioyo yote isiyotulia. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa
neema
ninawaalika ninyi kwenye maombi kwa moyo. Mioyo yenu, wanangu, igeuzwe kuelekea mbinguni kwa maombi, ili mioyo yenu ipate kuhisi Mungu wa upendo anayewaponya na kuwapenda kwa upendo mkuu. Mimi niko pamoja nanyi kuwaongoza kwenye njia ya uongofu wa moyo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika kwenye maombi ya nguvu. Umamboleo unataka kuingia katika mawazo yenu na kuwaibia furaha ya maombi na kukutana na Yesu. Kwa hiyo, wanangu wapendwa, fanyeni upya sala katika familia zenu ili moyo wangu wa kimama ufurahi kama siku za kwanza nilipowachagua ninyi na jibu lilikuwa ni maombi mchana na usiku na mbingu haikunyamaza bali ilitolea kwa mahali hapa
neema
, amani na baraka kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Machi 2024
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa
neema
, ombeni pamoja nami ili mema yapate kushinda ndani yenu na karibu nanyi. Hasa, wanangu, ombeni kwa umoja na Yesu katika njia yake ya msalaba. Wekeni katika maombi yenu ubinadamu huu unaotangatanga bila Mungu na bila upendo wake. Muwe maombi, muwe mwanga na mashahidi kwa wale wote mnaokutana nao, enyi wanangu, ili Mungu wa rehema awarehemu.. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2024
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa
neema
ninawaalika ninyi kuomba kwa moyo wenu. Wanangu, tengenezeni vikundi vya maombi ambavyo ndani yake mtahimizana kutenda mema na kukua katika furaha. Wanangu, bado mko mbali. Kwa hiyo, daima ongokeni upya na mchague njia ya utakatifu na matumaini ili Mungu awape amani kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3