Our Lady of Medjugorje Messages containing 'ni'
Total found:
127
Ujumbe, 25 Januari 2023
“
W
anangu wapendwa! Ombeni pamoja nami kwa ajili ya amani maana shetani anataka vita na chuki katika mioyo na mataifa. Kwa hiyo salini na, katika siku zenu, toeni sadaka kwa kufunga na kutubu ili Mungu awape amani. Wakati ujao uko kwenye njia panda kwa sababu mwanadamu wa kisasa hataki Mungu. Kwa hiyo ubinadamu unaelekea kwenye upotevu. Ninyi, wanangu,
ni
tumaini langu. Ombeni pamoja nami kwamba niliyoyaanza Fatima na hapa yatimie. Ombeni na mshuhudie amani katika mazingira yenu na muwe watu wa amani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 18 Machi 2023 - Tokeo la kila mwaka kwa Miriana Dragićević-Soldo
Mwotaji Mirjana Dragićević-Soldo alikuwa na matukio ya kila siku kutoka Juni 24, 1981 hadi Desemba 25, 1982. Katika hafla ya kutokezwa kwake kwa kila siku, akimfunulia siri ya kumi, Bikira alimfunulia kwamba atakuwa na tukio la kila mwaka mnamo Machi 18 na ndivyo ilivyokuwa katika miaka hii yote. Tukio hilo lilianza saa 1.33 jioni na kudumu hadi saa 1.39.
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika mpate kumjua Mwanangu vizuri iwezekanavyo kwa sala na rehema. Ili kwa mioyo safi na iliyo wazi mjifunze kusikiliza. Sikilizeni Mwanangu anachowaambieni ili mpate kuona tena kiroho. Kama watu wamoja wa Mungu, kwa ushirika na Mwanangu, ishuhudieni kweli kwa maisha yenu. Ombeni, wanangu, ili kwamba pamoja na Mwanangu muweze kuleta amani, furaha na upendo kwa ndugu zenu wote. Mimi
ni
pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka zangu za kimama.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika kwenye maombi ya nguvu. Umamboleo unataka kuingia katika mawazo yenu na kuwaibia furaha ya maombi na kukutana na Yesu. Kwa hiyo, wanangu wapendwa, fanyeni upya sala katika familia zenu ili moyo wangu wa kimama ufurahi kama siku za kwanza nilipowachagua ninyi na jibu lilikuwa
ni
maombi mchana na usiku na mbingu haikunyamaza bali ilitolea kwa mahali hapa neema, amani na baraka kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2023
“
W
anangu wapendwa! Pepo za uovu, chuki na wasiwasi huvuma duniani kote kuharibu maisha yote. Kwa hiyo Aliye Juu amenituma kwenu ili niwaongoze kwenye njia ya amani na ushirika na Mungu na wanadamu. Ninyi, wanangu,
ni
mikono yangu iliyopanuliwa: ombeni, mfunge na toeni sadaka kwa ajili ya amani, hazina ambayo kila moyo unatamani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu ili aijaze mioyo yenu amani kwa sababu Yeye
ni
amani. Wanangu, mtafuteni Yesu katika ukimya wa mioyo yenu ili azaliwe upya. Ulimwengu unamhitaji Yesu, hivyo wanangu, mtafuteni kwa maombi maana anajitoa kila siku kwa kila mmoja wenu.
”
Mama yetu alikuja leo akiwa amevalia mavazi ya heshima akiwa na mtoto Yesu mikononi mwake. Yesu alinyoosha mkono wake kama ishara ya baraka na Mama yetu alituombea kwa lugha ya aramaika.
Ujumbe, 25 Februari 2024
“
W
anangu wapendwa! Salini na mfanye upya moyo wenu ili lile jema mlilopanda lizae matunda ya furaha na ushirika na Mungu. Magugu yamechukua mioyo mingi na imekuwa tasa. Kwa hiyo ninyi, wanangu, muwe mwanga, upendo na mikono yangu iliyonyoshwa katika ulimwengu huu unaomtamani Mungu ambaye
ni
upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Karibuni Ujumbe, 18 Machi 2024 - Tokeo la kila mwaka kwa Miriana Dragićević-Soldo
Mwotaji Mirjana Dragićević-Soldo alikuwa na matukio ya kila siku kutoka Juni 24, 1981 hadi Desemba 25, 1982. Katika hafla ya kutokezwa kwake kwa kila siku, akimfunulia siri ya kumi, Bikira alimfunulia kwamba atakuwa na tukio la kila mwaka mnamo Machi 18 na ndivyo ilivyokuwa katika miaka hii yote. Tukio hilo lilianza saa 1.33 jioni na kudumu hadi saa 1.39.
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika mpate kumjua Mwanangu vizuri iwezekanavyo kwa sala na rehema. Ili kwa mioyo safi na iliyo wazi mjifunze kusikiliza. Sikilizeni Mwanangu anachowaambieni ili mpate kuona tena kiroho. Kama watu wamoja wa Mungu, kwa ushirika na Mwanangu, ishuhudieni kweli kwa maisha yenu. Ombeni, wanangu, ili kwamba pamoja na Mwanangu muweze kuleta amani, furaha na upendo kwa ndugu zenu wote. Mimi
ni
pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka zangu za kimama.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7