Our Lady of Medjugorje Messages containing 'ninyi'
Total found:
124
Ujumbe, 25 Oktoba 2023
“
W
anangu wapendwa! Pepo za uovu, chuki na wasiwasi huvuma duniani kote kuharibu maisha yote. Kwa hiyo Aliye Juu amenituma kwenu ili niwaongoze kwenye njia ya amani na ushirika na Mungu na wanadamu.
Ninyi
, wanangu, ni mikono yangu iliyopanuliwa: ombeni, mfunge na toeni sadaka kwa ajili ya amani, hazina ambayo kila moyo unatamani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2024
“
W
anangu wapendwa! Salini na mfanye upya moyo wenu ili lile jema mlilopanda lizae matunda ya furaha na ushirika na Mungu. Magugu yamechukua mioyo mingi na imekuwa tasa. Kwa hiyo
ninyi
, wanangu, muwe mwanga, upendo na mikono yangu iliyonyoshwa katika ulimwengu huu unaomtamani Mungu ambaye ni upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2024
“
W
anangu wapendwa! Nipo pamoja nanyi kuwaambia kuwa nawapenda na ninawasihi sana muombe maana shetani ana nguvu na kila siku nguvu zake zinazidi kuimarika kupitia wale waliochagua kifo na chuki.
Ninyi
, wanangu, muwe maombi na mikono yangu ya upendo iwanyooshee wote walio gizani na kuitafuta nuru ya Mungu wetu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2024
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika
ninyi
kuomba kwa moyo wenu. Wanangu, tengenezeni vikundi vya maombi ambavyo ndani yake mtahimizana kutenda mema na kukua katika furaha. Wanangu, bado mko mbali. Kwa hiyo, daima ongokeni upya na mchague njia ya utakatifu na matumaini ili Mungu awape amani kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7