Our Lady of Medjugorje Messages containing 'pamoja'
Total found:
134
Ujumbe, 2 Februari 2020 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nilichaguliwa kuwa mama wa Mungu na mama yenu, kwa maamuzi na upendo wa Bwana, lakini pia kwa mapenzi yangu, kwa upendo wangu usio na kifani kwake Baba wa mbinguni na kwa imani yangu yote Kwake. Mwili wangu ulikuwa kikombe cha Mungu Mtu. Nilikuwa mtumishi wa ukweli, wa upendo na wokovu kama vile nilivyo sasa katikati yenu, ili kuwaalika, wanangu, mitume wa upendo wangu, kuwa waletaji ukweli, ili kuwaalika, kwa njia ya utashi na upendo yenu kumwelekea Mwanangu, ili kueneza maneno Yake, maneno ya wokovu na kuyaonyesha, kwa vitendo vyenu, kwa wale wote ambao hawajamjua mwanangu na upendo Wake. Nguvu mtaipata katika Ekaristi: Mwanangu awalisheni kwa mwili Wake na kuwaimarisha kwa damu Yake. Wanangu, wekeni mikono yenu
pamoja
kwa sala na tazameni kuelekea msalaba kwa ukimya. Kwa jinsi hii mtapata imani ili muweze kuieneza, mtapata ukweli ili muweze kuupambanua, mtapata upendo ili muweze kuelewa namna ya kupenda kwa uhakika. Wanangu, mitume wa upendo wangu, wekeni mikono yenu
pamoja
kwa sala na tazameni kuelekea msalaba: katika msalaba tu kuna wokovu. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Machi 2020 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, upendo wenu safi na wa kweli unavuta Moyo wangu wa kimama. Imani yenu na usadiki wenu katika Baba wa mbinguni ni mawaridi yenye harufu nzuri mnayonitolea: shada la mawaridi mazuri sana, lililotengenezwa kwa sala zenu, kwa matendo ya rehema na ya upendo. Mitume wa upendo wangu, ninyi mnaojaribu kumfuata Mwanangu pasipo unafiki na kwa moyo safi, ninyi ambao pasipo unafiki mnampenda, muwe ninyi wenyewe kusaidia: muwe mfano kwa wale ambao hawajajua upendo wa Mwanangu. Lakini, wanangu, siyo kwa maneno tu, bali hata kwa matendo na hisia safi, ambayo kwa njia yake mnamtukuza Baba wa mbinguni. Mitume wa upendo wangu, ni wakati wa kukesha na ninawaombeni upendo; na msihukumu mtu yeyote, kwa maana Baba wa mbinguni atahukumu wote. Ninawaombeni mpende, na mueneze ukweli, kwa maana ukweli ni wa kale: Ukweli siyo mpya, Ukweli ni wa milele, Ukweli ndiyo ukweli! Ukweli unatolea ushuhuda wa umilele wa Mungu. Bebeni mwanga wa Mwanangu na mpasue giza ambalo linataka kuwakandamiza zaidi na zaidi. Msiwe na hofu: kwa ajili ya neema na upendo wa Mwanangu, mimi nipo
pamoja
nanyi! Ninawashukuru. ”
”
Ujumbe, 25 Machi 2020
“
W
anangu wapendwa, katika miaka hii yote mimi nipo
pamoja
nanyi ili kuwaongoza kwenye njia ya wokovu. Rudieni kwa Mwanangu, rudieni katika sala na mfungo. Wanangu, mwachieni Mungu aongee na mioyo yenu kwa sababu shetani anatawala na anatamani kuangamiza maisha yenu na dunia mnamotembelea. Muwe na ujasiri na amueni kuwa watakatifu. Mtaona wongofu katika mioyo yenu na katika familia zenu, sala itasikilizwa, Mungu atayapokea maombi yenu na kuwapa amani. Mimi nipo
pamoja
nanyi na kuwabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2020
“
W
anangu wapendwa, wakati huu uwe kwenu himizo kwa wongofu wenu binafsi. Wanangu, ombeni katika upweke Roho Mtakatifu ili iwaimarishe katika imani na katika kumsadiki Mungu ili kuweza kuwa mashahidi wa upendo ambao Mungu anawapa kupitia uwepo wangu. Wanangu, msiruhusu majaribu yafanye mioyo yenu kuwa migumu na sala kuwa kama jangwa. Muwe mwangi wa upendo wa Mungu na mshuhudieni Yesu Aliyefufuka kwa njia ya maisha yenu. Mimi nipo
pamoja
nanyi na ninawapenda nyote kwa upendo wangu wa kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu”.
”
Ujumbe, 25 Mei 2020
“
W
anangu wapendwa, Salini
pamoja
Nami kwa maisha mapya ya ninyi nyote. Wanangu, katika mioyo yenu mnajua ni nini lazima kibadilike: rudini kwa Mungu na kwa Amri Zake ili Roho Mtakatifu aweze kugeuza maisha yenu na uso wa dunia hii, inayohitaji kufanywa upya katika Roho. Wanangu, muwe sala kwa wale wote wasiosali, muwe furaha kwa wale wote wasioona njia ya kutokea, muwe waletaji mwanga katika giza za wakati huu wa wasiwasi. Salini na ombeni msaada na ulinzi wa watakatifu ili ninyi pia muweze kutamani mbingu na mambo halisi ya kimbingu. Mimi nipo
pamoja
nanyi nikiwalinda na kuwabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2020
“
W
anangu wapendwa, ninasikiliza maombi yenu na sala zenu na ninawaombea kwa mwanangu Yesu aliye njia, kweli na uzima. Wanangu, rudieni kusali na fungueni mioyo yenu katika wakati huu wa neema na shikeni njia ya wongofu. Maisha yenu yanapita na hayana maana bila Mungu. Kwa hiyo mimi ni
pamoja
nanyi niwaongoze kuelekea utakatifu wa maisha ili kila mmoja wenu agundue furaha ya kuishi. Wanangu, ninawapenda wote na kuwabariki kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2020
“
W
anangu wapendwa, Katika wakati huu wa wasiwasi ambapo ibilisi anavuna nafsi ili kuwavuta kwake, niwaalika kwa sala ya kudumu ili katika sala mtambue Mungu wa upendo na wa matumaini. Wanangu, shikeni msalaba katika mikono yenu. Na uwatie moyo kwa kuwa upendo unashinda sikuzote hasa sasa ambapo msalaba na imani yamekataliwa. Ninyi muwe mwangwi na mfano kwa njia ya maisha yenu ya kuwa imani na matumaini bado hai na ulimwengu mpya wa amani unawezekana. Mimi nipo
pamoja
nanyi na ninawaombea mbele ya mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2020
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati wa neema. Mimi nipo
pamoja
nanyi na kuwaalika tena, wanangu, mrudieni Mungu na kwa kusali ili sala iwe furaha kwenu. Enyi wanangu hamtakuwa na wakati ujao wala amani mpaka katika maisha yenu mtakapoanza kuishi maongezi ya binafsi na badiliko katika mema. Maovu yatakoma na amani itatawala katika mioyo yenu na katika ulimwengu. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini. Mimi nipo
pamoja
nanyi na ninawaombea kwa mwanangu Yesu kwa ajili ya kila mmoja wenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Mimi ni
pamoja
nanyi kwa muda mrefu kwa maana Mungu ni mkuu katika upendo wake na katika uwepo wangu. Wanangu, ninawaalika kurudi kwa Mungu na kwa sala. Kipimo cha kuishi kwenu kiwe upendo na msisahau, wanangu, kwamba maombi na kufunga hufanya miujiza ndani yenu na kuwazunguka. Yote mnayoyafanya yawe kwa ajili ya utukufu wa Mungu na hapo Mbingu itajaza moyo wenu na furaha mkahisi ya kuwa Mungu anawapenda na kunituma ili kuokoa ninyi na Dunia ambayo juu yake mnaishi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2020
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu ninawaita kumrudia Mungu na sala. Waiteni watakatifu wote wawasaidie ili wawe mfano na msaada kwenu. Shetani ni mwenye nguvu na anapigania kuivutia kwake mioyo mingi zaidi awezavyo. Anataka vita na chuki. Kwa sababu hiyo Mimi ni
pamoja
nanyi muda mrefu ili niwaongoze kwenye njia ya wokovu, kwa Yule aliye njia, kweli na uzima. Wanangu, rudini kwa upendo kumwelekea Mungu naye atakuwa nguvu yenu na kimbilio lenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mtoto Yesu anayewaletea amani, Yule aliye wakati uliopita, wakati wa sasa na wakati ujao wa kuishi kwenu. Wanangu, msiruhusu imani yenu na matumaini yenu katika wakati ujao ulio bora yazimike, kwa maana ninyi mmechaguliwa kwa kuwa mashahidi wa matumaini katika kila hali. Kwa ajili hiyo mimi ni hapa
pamoja
na Yesu ili awabariki kwa amani yake. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2021
“
W
anangu wapendwa! Mungu ameniruhusu kuwa
pamoja
nanyi leo pia kwa kuwaalika kusali na kufunga. Ishini wakati huu wa neema na muwe mashahidi wa tumaini maana, ninawaambia tena wanangu, kwa kusali na kufunga hata vita vinaweza kuisha. Wanangu, aminini na kuishi katika imani na kwa imani wakati huu wa neema na Moyo wangu usio na dhambi ya asili haumwachi yeyote kati yenu katika wasiwasi ikiwa ananikimbilia. Ninawaombea mbele ya Yeye aliye juu na ninasali ili amani iwepo katika mioyo yenu na kwa ajili ya tumaini katika wakati ujao. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Machi 2021
“
W
anangu wapendwa! Hata leo mimi ni
pamoja
nanyi ili kuwaambieni: wanangu, yule anayesali hana hofu ya wakati ujao wala hapotezi tumaini. Mmechaguliwa kwa kuleta furaha na amani, kwa maana ni wangu. Nimekuja hapa
pamoja
na jina: Malkia wa Amani kwa sababu ibilisi anataka kuleta wasiwasi na vita, anataka kuijaza mioyo yenu kwa hofu ya wakati ujao na wakati ujao ni wa Mungu. Kwa hiyo muwe wanyenyekevu, salini na acheni yote katika mikono ya Yeye aliye Juu aliyewaumba. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2021
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaalika kushuhudia imani yenu katika rangi za majira ya kuchipua, na iwe imani ya matumaini na ya ujasiri. Wanangu, imani yenu isitindike katika hali yoyote na hata katika wakati huu wa majaribio. Tembeeni kwa ujasiri
pamoja
na Kristo Mfufuka kuelekea Mbingu iliyo lengo lenu. Mimi ninaandamana nanyi katika mwendo huu wa utakatifu na kuweka ninyi nyote katika Moyo wangu Usio na dhambi ya asili. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2021
“
W
anangu wapendwa! Kwa furaha ninawaalika ninyi nyote, wanangu, mlioitikia wito wangu, kuwa furaha na amani. Kwa maisha yenu shuhudieni Mbingu ninayowaletea. Ni saa, wanangu, ya kuwa wonyesho wa upendo wangu kwa wote wale ambao hawapendi na mioyo yao imeshindwa na machukio. Msisahau: mimi ni
pamoja
nanyi na ninawaombea ninyi nyote karibu na mwanangu Yesu ili awapeni amani yake. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2021
“
W
anangu wapendwa! Ombeni, shuhudieni na mfurahi
pamoja
nami kwa sababu Mwenyezi Aliye Juu ananituma tena kuwaongoza katika njia ya utakatifu. Mjitambue, wanangu, kwamba maisha yenu ni mafupi na umilele unawasubiri ili kwamba
pamoja
na watakatifu wote mmtukuze Mungu kwa nafsi yenu. Msiwe na wasiwasi, wanangu, kwa mambo ya kidunia lakini tamanini Mbingu. Mbingu itakuwa lengo lenu na furaha itatawala moyoni mwenu. Niko
pamoja
nanyi na ninawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2021
“
W
anangu wapendwa! Niko
pamoja
nanyi katika wakati huu wa rehema na ninawaalika nyote kuwa waleta amani na upendo katika ulimwengu huu, ambapo, wanangu, Mungu anawaalika kupitia Kwangu kuwa sala, upendo na kielelezo cha Paradiso, hapa duniani. Mioyo yenu na ijazwe na furaha na imani katika Mungu ili, wanangu, muwe na imani kamili katika mapenzi yake matakatifu. Hii ndiyo sababu mimi niko
pamoja
nanyi kwa sababu Yeye, Aliye Juu, ananituma kati yenu ili kuwahimiza ninyi kuwa na matumaini na mtakuwa waleta amani katika ulimwengu huu wenye wasiwasi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2022
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaalika kurudia sala zenu za binafsi. Wanangu, msisahau ya kuwa shetani ni mwenye nguvu na hutaka kuvuta nafsi nyingi iwezekanavyo kwake. Kwa hivyo, ninyi kesheni katika sala na muwe na azimio katika kutenda mema. Mimi niko
pamoja
nanyi na ninawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2022
“
W
anangu wapendwa! Nipo
pamoja
nanyi na tusali
pamoja
. Wanangu nisaidieni kwa maombi ili shetani asishinde. Nguvu yake ya mauti, chuki na woga imeitembelea Dunia. Kwa hiyo wanangu, mrudieni Mungu katika maombi na katika kufunga na kuwanyima kwa ajili ya wote waliokanyagwa, maskini na wasio na sauti katika dunia hii pasipo Mungu. Watoto wadogo, msipomrudia Mungu na amri zake, hamna wakati ujao. Kwa hiyo amenituma kwenu ili niwaongoze. Leo ninawaalika mrudi kwenye sala ya kibinafsi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2022
“
W
anangu wapendwa! Ninafurahi
pamoja
nanyi na kuwashukuru kwa kila sadaka na sala ambayo mlitolea kwa makusudi yangu. Wanangu, msisahau ya kuwa ninyi ni muhimu katika mpango wangu wa wokovu wa wanadamu. Rudeni kwa Mungu na kwa sala ili Roho Mtakatifu atende kazi ndani yenu na kupitia ninyi. Wanangu, Mimi ni
pamoja
nanyi hata katika siku hizi ambapo shetani anapiga kwa vita na kwa machukio. Utengano ni wenye nguvu na maovu yatenda kazi katika mwanadamu kama hajatenda bado mpaka leo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
Next>>