Our Lady of Medjugorje Messages containing 'pasipo'
Total found:
22
Ujumbe, 2 Machi 2020 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, upendo wenu safi na wa kweli unavuta Moyo wangu wa kimama. Imani yenu na usadiki wenu katika Baba wa mbinguni ni mawaridi yenye harufu nzuri mnayonitolea: shada la mawaridi mazuri sana, lililotengenezwa kwa sala zenu, kwa matendo ya rehema na ya upendo. Mitume wa upendo wangu, ninyi mnaojaribu kumfuata Mwanangu
pasipo
unafiki na kwa moyo safi, ninyi ambao
pasipo
unafiki mnampenda, muwe ninyi wenyewe kusaidia: muwe mfano kwa wale ambao hawajajua upendo wa Mwanangu. Lakini, wanangu, siyo kwa maneno tu, bali hata kwa matendo na hisia safi, ambayo kwa njia yake mnamtukuza Baba wa mbinguni. Mitume wa upendo wangu, ni wakati wa kukesha na ninawaombeni upendo; na msihukumu mtu yeyote, kwa maana Baba wa mbinguni atahukumu wote. Ninawaombeni mpende, na mueneze ukweli, kwa maana ukweli ni wa kale: Ukweli siyo mpya, Ukweli ni wa milele, Ukweli ndiyo ukweli! Ukweli unatolea ushuhuda wa umilele wa Mungu. Bebeni mwanga wa Mwanangu na mpasue giza ambalo linataka kuwakandamiza zaidi na zaidi. Msiwe na hofu: kwa ajili ya neema na upendo wa Mwanangu, mimi nipo pamoja nanyi! Ninawashukuru. ”
”
Ujumbe, 25 Februari 2022
“
W
anangu wapendwa! Nipo pamoja nanyi na tusali pamoja. Wanangu nisaidieni kwa maombi ili shetani asishinde. Nguvu yake ya mauti, chuki na woga imeitembelea Dunia. Kwa hiyo wanangu, mrudieni Mungu katika maombi na katika kufunga na kuwanyima kwa ajili ya wote waliokanyagwa, maskini na wasio na sauti katika dunia hii
pasipo
Mungu. Watoto wadogo, msipomrudia Mungu na amri zake, hamna wakati ujao. Kwa hiyo amenituma kwenu ili niwaongoze. Leo ninawaalika mrudi kwenye sala ya kibinafsi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2