Our Lady of Medjugorje Messages containing 'shetani'
Total found:
23
Ujumbe, 25 Januari 2023
“
W
anangu wapendwa! Ombeni pamoja nami kwa ajili ya amani maana
shetani
anataka vita na chuki katika mioyo na mataifa. Kwa hiyo salini na, katika siku zenu, toeni sadaka kwa kufunga na kutubu ili Mungu awape amani. Wakati ujao uko kwenye njia panda kwa sababu mwanadamu wa kisasa hataki Mungu. Kwa hiyo ubinadamu unaelekea kwenye upotevu. Ninyi, wanangu, ni tumaini langu. Ombeni pamoja nami kwamba niliyoyaanza Fatima na hapa yatimie. Ombeni na mshuhudie amani katika mazingira yenu na muwe watu wa amani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2023
“
W
anangu wapendwa! Ongokeni na mvae mavazi ya toba na maombi ya kina ya kibinafsi na kwa unyenyekevu mwombe Aliye Juu amani. Katika wakati huu wa neema
Shetani
anataka kuwapotosha ninyi, nanyi wanangu, mwangalieni Mwanangu na kumfuata kuelekea Kalvari, kwa kujikana na kufunga. Niko pamoja nanyi kwa sababu Aliye Juu ameniruhusu niwapende ninyi na kuwaongoza kuelekea furaha ya moyo, katika imani inayokua ndani ya wale wote wanaompenda Mungu zaidi ya vitu vyote. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2024
“
W
anangu wapendwa! Nipo pamoja nanyi kuwaambia kuwa nawapenda na ninawasihi sana muombe maana
shetani
ana nguvu na kila siku nguvu zake zinazidi kuimarika kupitia wale waliochagua kifo na chuki. Ninyi, wanangu, muwe maombi na mikono yangu ya upendo iwanyooshee wote walio gizani na kuitafuta nuru ya Mungu wetu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2