Our Lady of Medjugorje Messages containing 'upendo'
Total found:
148
Ujumbe, 25 Desemba 2018
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu Yesu ambaye ni Mfalme wa amani. Yeye anawapa amani, basi amani hii isiwe yenu tu, wanangu, lakini wapelekeeni na wengine katika furaha na unyenyekevu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombeeni katika wakati huu wa neema ambayo Mungu anataka kuwapa. Uwepo wangu ni ishara ya
upendo
, wakati nipo hapa pamoja nanyi niwalinde na kuwaongoza kuelekea umilele. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, inasikitisha kwamba katikati yenu, wanangu, yapo mashindano mengi, chuki, masilahi yenu wenyewe na ubinafsi. Wanangu, hivi kwa urahisi mnamsahau Mwanangu, maneno Yake na
upendo
Wake. Imani inazimika katika roho nyingi na mioyo imetekwa na vitu vya ulimwenguni. Lakini moyo wangu wa kimama unajua ya kuwa katikati yenu kuna wale wanaoamini na kupenda, wale ambao wanajaribu kumkaribia Mwanangu zaidi na zaidi, ambao wanamtafuta bila kuchoka na namna hii, wananitafuta hata mimi. Hawa ndio wanyenyekevu na wapole ambao, pamoja na maumivu na mateso wanayoyachukua katika kimya, pamoja na tumaini lao na hasa pamoja na imani yao, ni mitume wa
upendo
wangu. Wanangu, mitume wa
upendo
wangu, ninawafundisha ya kuwa Mwanangu hatafuti sala tu pasipo kuchoka bali hata matendo na hisia. Salini ili katika sala mpate kuzidi katika imani na katika
upendo
. Mpendane wenyewe kwa wenyewe: hilo ndilo analotaka Yeye, hiyo ndiyo ni njia ya uzima wa milele. Wanangu, msisahau ya kuwa Mwanangu ameleta mwanga kwa ulimwengu huu. Ameuleta kwa wale ambao walitaka kuuona na kuupokea. Hawa muwe ninyi, maana huu ndio mwanga wa ukweli, wa amani na wa
upendo
. Mimi ninawaongoza kama mama kumwabudu Mwanangu, kumpenda pamoja nami. Fikira zenu, maneno na matendo yenu yamwelekee Mwanangu, yawe katika jina Lake: hapo tu moyo wangu utajazwa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2019
“
W
anangu wapendwa! kama mama ninawaalika kutubu. Wakati huu ni kwenu, wanangu, wakati wa ukimya na sala. Kwa hiyo, katika joto la moyo wenu iote chembe ya tumaini na imani na hivyo, ninyi nanyi, wanangu, siku kwa siku mtasikia haja ya kusali zaidi. Maisha yenu yatakuwa ya mpangilio na yenye kuwajibika. Mtaelewa, wanangu, ya kuwa sisi ni wa kupita hapa duniani na ya kuwa mtasikia haja ya kuwa karibu zaidi na Mungu na kwa
upendo
mtatoa ushuhuda wa mang'amuzi yenu ya kukutana na Mungu, mtakaoushirikisha pamoja na wengine. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombeeni, lakini siwezi kufanya hivyo bila 'Ndiyo' yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa,
upendo
na wema wa Baba wa mbinguni yanatoa mafunuo ili kwamba imani ikue, iweze kuelezwa, ilete amani, salama na matumaini. Hivi mimi nami, wanangu, kwa ajili ya
upendo
wenye rehema wa Baba wa mbinguni ninawaonyesha sikuzote tena njia ya kwenda kwa Mwanangu, kwa wokovu wa milele; kwa bahati mbaya, lakini, wanangu wengi hawataki kunisikiliza. Wanangu wengi wanasita. Lakini mimi, mimi, katika wakati na zaidi ya wakati, sikuzote nimemtukuza Bwana kwa mambo yale yote aliyoyatenda ndani yangu na kwa njia yangu. Mwanangu anajitolea kwenu, anamega mkate pamoja nanyi, anawaambieni maneno ya uzima wa milele ili muweze kuwaletea watu wote. Nanyi, wanangu, mitume wa
upendo
wangu, mnaogopa nini, ikiwa Mwanangu ni pamoja nanyi? Mwonyesheni nafsi zenu, ili Yeye aweze kuwa ndani yao na aweze kuwafanyeni kuwa vyombo vya imani, vyombo vya
upendo
. Wanangu, ishini Injili, ishini
upendo
wenye rehema kuelekea mwenzenu; lakini hasa ishini
upendo
kuelekea Baba wa mbinguni. Wanangu, hamkuungana kwa bahati tu. Baba wa mbinguni haunganishi watu kwa bahati tu. Mwanangu anaongea na nafsi zenu, nami ninaongea moyoni mwenu. Kama Mama ninawaambia: tembeeni nami! Pendaneni, na kutoa shuhuda! Hampasi kuogopa kulinda Ukweli, ambao ni Neno la Mungu, lililo la milele na lisilogeuka kamwe, kwa mifano yenu. Wanangu, yule anayetenda kazi katika mwanga wa
upendo
wenye rehema na ukweli, anasaidiwa sikuzote na Mbingu na hayuko peke yake. Mitume wa
upendo
wangu, waweze kuwatambua sikuzote katikati ya wengine wote katika maficho,
upendo
na utulivu wenu. Mimi nipo pamoja nanyi. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2019
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaalika kwa maisha mapya. Haijalishi miaka yenu ni mingapi, fumbueni mioyo yenu kwa Yesu ambaye atawabadilisha katika wakati huu wa neema nanyi, kama nyasi, mtazaliwa katika maisha mapya katika
upendo
wa Mungu na mtafumbua mioyo yenu kwa Mbinguni na kwa vitu vya kimbingu. Mimi nipo bado pamoja nanyi maana Mungu aliniruhusu kwa ajili yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninawaita mitume wa
upendo
wangu. Ninawaonyesha Mwanangu, aliye amani ya kweli na
upendo
wa kweli. Kama Mama, kwa ajili ya neema ya kimungu, ninatamani kuwaongoza kwendea Yeye. Wanangu, kwa hiyo ninawaalika kujitazama ninyi wenyewe mkianzia kwa Mwanangu, kumtazama kwa moyo na kuona kwa moyo mahali mlipo na maisha yenu yanakwenda wapi. Wanangu, ninawaalika kuelewa ya kuwa mnaishi kwa ajili ya Mwanangu, kwa njia ya
upendo
wake na sadaka yake. Ninyi mnamwomba Mwanangu kuwa mwenye rehema nanyi, lakini mimi ninawaalika ninyi kuwa na rehema. Mnamwomba kuwa mwema nanyi na kuwasamehe, lakini tangu lini mimi ninawasihi ninyi, wanangu, kusamehe na kupenda watu wote mnaokutana nao! Mtakapoelewa kwa moyo maneno yangu, mtaelewa na kujua
upendo
wa kweli, na mtaweza kuwa mitume wa
upendo
ule, enyi mitume wangu, wanangu wapendwa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Aprili 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kama Mama ambaye anajua wana wake, ninajua ya kuwa mnamtamani Mwanangu. Ninajua ya kuwa mnatamani ukweli, amani, na kilicho chema wala si uovu. Kwa sababu hiyo mimi, kama Mama, kwa njia ya
upendo
wa Mungu ninawaita ninyi na kuwaalika ili, mkisali kwa moyo safi na wazi, mmtambue ninyi wenyewe Mwanangu,
upendo
wake, na Moyo wake wenye rehema. Mwanangu alikuwa akiona uzuri katika vitu vyote. Yeye anatafuta mema, hata yale mema madogo yanayofichika, katika roho zote, ili kusamehe maovu. Kwa hiyo, wanangu, mitume wa
upendo
wangu, ninawaalika kumwabudu, kumshukuru daima na kumstahili. Maana yeye aliwaambieni maneno ya kimungu, maneno ya Mungu, maneno yaliyo kwa watu wote na hata milele. Kwa hiyo, wanangu, ishini uchangamfu, umakini, umoja na muwe na mapenzi baina yenu. Haya mnapaswa kuwa nayo katika ulimwengu wa leo: hivyo mtakuwa mitume wa
upendo
wangu, hivyo mtashuhudia Mwanangu kwa jinsi ya haki. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2019
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati wa neema, wakati wa rehema kwa kila mmoja wenu. Wanangu, msiruhusu upepo wa chukio na hofu utawale ndani yenu na karibu nanyi. Ninyi, wanangu, mmealikwa kuwa
upendo
na sala. Ibilisi ataka hofu na fujo lakini ninyi, wanangu, muwe furaha ya Yesu Mfufuka ambaye amekufa na kufufuka kwa ajili ya kila mmoja wenu. Yeye ameshinda kifo kwa kuwapeni uzima, uzima wa milele. Kwa hiyo, wanangu, mshuhudieni na muwe wenye fahari kwa kufufuliwa katika Yeye. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa
upendo
wa kimama ninawaalika ili kwa moyo safi na wazi, kwa imani kabisa, mpokee
upendo
mkubwa wa Mwanangu. Mimi ninajua ukuu wa
upendo
wake, mimi nilimchukua ndani yangu, Hostia moyoni, Mwanga na
Upendo
wa ulimwengu. Wanangu, hata kuelekea kwangu kwenu ninyi ni ishara ya
upendo
na ya huruma ya Baba wa Mbinguni, ni tabasamu kilichojaa
upendo
wa Mwanangu, ni mwaliko kwa uzima wa milele. Damu ya Mwanangu ilimwagika kwa ajili yenu kwa
upendo
. Ile Damu yenye thamani ni kwa wokovu wenu, kwa ajili ya uzima wa milele. Baba wa mbinguni aliumba mtu kwa ajili ya furaha ya milele. Haiwezekani ninyi kufa, ninyi mnaojua
upendo
wa Mwanangu, ninyi mnaomfuata. Uzima umeshinda: Mwanangu yu hai! Kwa hiyo, wanangu, mitume wa
upendo
wangu, sala iwaonyeshe njia, jinsi ya kueneza
upendo
wa Mwanangu kwa jinsi ilivyo bora zaidi. Wanangu, hata wakati mnapojaribu kuishi maneno ya Mwanangu, ninyi mnasali. Wakati mnapowapenda watu mnaokutana nao, mnaeneza
upendo
wa Mwanangu.
Upendo
ni neno linalofungua milango ya Uzima. Wanangu, tangu awali nimesali kwa ajili ya Kanisa. Kwa hiyo ninawaalika nanyi, mitume wa
upendo
wangu, kusali kwa ajili ya Kanisa na watumishi wake, kwa wale ambao Mwanangu amewaita. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Juni 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, moyo safi na wazi tu utawawezesha ninyi kumjua kweli Mwanangu, na wale wote wasiojua
upendo
wake kuujua kwa njia yenu.
Upendo
tu utawawezesha kuelewa kuwa ni wenye nguvu kuliko kifo, maana
upendo
wa kweli umeshinda kifo na umefanya hata kifo hakipo tena. Wanangu, msamaha ni mtindo bora wa
upendo
. Ninyi, kama mitume wa
upendo
wangu, yawapasa kusali kwa kuwa wenye nguvu katika roho na kuweza kuelewa na kusamehe. Ninyi, mitume wa
upendo
wangu, kwa njia ya ufahamu na msamaha, mnatoa mfano wa
upendo
na rehema. Kuweza kuelewa na kusamehe ni karama inayotokana na maombi na yatupasa kuitunza. Mkisamehe ninyi mnaonyesha ya kuwa mnajua kupenda. Tazameni, wanangu, kama Baba wa mbinguni anavyowapenda kwa
upendo
mkubwa, kwa ufahamu, kwa uelewa, msamaha na haki. Kama anavyowatolea mimi, Mama wa mioyo yenu. Na tazama: mimi nipo katikati yenu ili kuwabariki kwa baraka ya kimama; ili kuwaalika kusali na kufunga; ili kuwasihi kuamini, kutumaini, kusamehe, kuwaombea wachungaji wenu na hasa kupenda bila mipaka. Wanangu, nifuateni! Njia yangu ni njia ya amani na
upendo
, njia ya Mwanangu. Ndiyo njia ya kuongoza katika ushindi wa Moyo wangu. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 2 Julai 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kufuatana na matakwa ya Baba mwenye rehema, nimewapa na tena nitawapa ishara dhahiri za uwepo wangu wa kimama. Wanangu, ishara hizo ni kwa hamu yangu ya kimama ya kuziponya roho. Ishara hizo ni kwa hamu ya kuwa kila mwanangu awe na imani ya kweli, aishi mang’amuzi ya ajabu akinywa kwenye chemchemi ya Neno la Mwanangu, Neno la uhai. Wanangu, kwa njia ya
upendo
wake na sadaka, Mwanangu alichukua ulimwenguni mwanga wa imani na aliwaonyesheni njia ya imani. Maana, wanangu, imani huamsha huzuni na maumivu. Imani ya kweli hufanya sala kusisika zaidi, hutimiza matendo ya huruma: mazungumzo na matoleo. Wale wanangu walio na imani, imani ya kweli, ni wenye heri pamoja na yote, maana wanaishi duniani mwanzo wa heri ya Mbinguni. Kwa hiyo, wanangu, mitume wa
upendo
wangu, ninawaalika kutoa mfano wa imani ya kweli, kupeleka mwanga pale palipo giza, kumwishi Mwanangu. Wanangu, kama Mama ninawaambia: hamwezi kupitia njia ya imani na kumfuata Mwanangu pasipo wachungaji wenu. Salini ili wawe na nguvu na
upendo
kwa kuwaongoza. Sala zenu ziwe sikuzote pamoja nao. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 2 Agosti 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa,
Upendo
wa Mwanangu ni mkubwa. Laiti mngeweza kujua ukuu wa
upendo
Wake, msingeacha kamwe kumwabudu na kumshukuru. Yeye ni sikuzote hai pamoja nanyi katika Ekaristi, maana Ekaristi ni moyo Wake, Ekaristi ni moyo wa imani. Yeye hakuwaacha kamwe: hata wakati ninyi mlipojaribu kwenda mbali Naye, Yeye hakuwaacha kamwe.
Kwa hiyo, moyo wangu wa kimama unafurahi wakati unapotazama jinsi mlivyojaa
upendo
mnapomrudia, wakati unapoona ya kuwa mnamrudia kwa njia ya upatanisho,
upendo
na matumaini. Moyo wangu wa kimama unajua ya kuwa ikiwa mngetembea katika njia ya imani, mngekuwa kama machipukizi, kama matumba na kwa njia ya sala na kufunga mngekuwa kama matunda, kama maua, mitume wa
upendo
wangu, mngekuwa waleta mwanga na mngeangaza kwa
upendo
na hekima pande zote karibu nanyi.
Wanangu, kama mama, ninawaomba: salini, fikirini na kutafakari. Yote yanayowatokea, mazuri, ya kuumiza na ya kufurahisha, hayo yote yawasababisha kukua kiroho, yawafanya kuwa Mwanangu akue ndani yenu. Wanangu mkabidhi kwake. Mumwamini na mtumainie
upendo
Wake. Na Yeye awaongoze. Na Ekaristi iwe mahali mtakapolisha roho zenu ili kueneza
upendo
na ukweli. Shuhudieni Mwanangu. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2019
“
W
anangu wapendwa, Fanyeni kazi na shuhudieni kwa
upendo
Ufalme wa Mbinguni ili muweze kuwa hamjambo hapa duniani. Wanangu, Mungu atabariki mara mia zaidi juhudi yenu na mtakuwa mashahidi katikati ya watu, roho za wale wasioamini zitahisi neema ya wongofu na Mbingu itazipokea taabu zenu na sadaka zenu. Wanangu, shuhudieni kwa tasbihi mkononi ili muwe wangu na kateni shauri kuwa watakatifu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Salini kila siku Tasbihi, taji lile la maua linaloniungana moja kwa moja kama Mama kwa maumivu yenu, mateso, mahitaji na matumaini. Mitume wa
upendo
wangu, Mimi nipo pamoja nanyi kwa njia ya neema na
upendo
wa Mwanangu, nanyi ninawaombeni sala. Sala zenu zinahitajika sana ulimwenguni, ili roho ziongoke! Fungueni wazi kwa imani timilifu mioyo yenu kwa Mwanangu, na yeye ataandika ndani yao muhtasari wa Neno lake, yaani
upendo
. Ishini muungano usiotenganika na Moyo Mtakatifu sana wa Mwanangu! Wanangu, kama Mama nawaambieni ya kwamba hakuna wakati wa kupoteza ili kupiga magoti mbele ya Mwanangu, kumkiri kama Mungu wenu, aliye kitovu cha maisha yenu. Mtoeni karama, zile anazozipenda zaidi, yaani
upendo
kwa jirani yako, rehema na mioyo safi. Mitume wa
upendo
wangu, wanangu wengi bado hawajamkiri Mwanangu kama Mungu wao, bado hawajajua
upendo
wake. Lakini ninyi, kwa njia ya sala yenu inayosema kwa moyo safi na wazi, pamoja na karama mnazotoa kwa Mwanangu, mtasababisha kwamba hata mioyo migumu zaidi ifunguke. Mitume wa
upendo
wangu, nguvu ya sala inayosemwa kutokana na moyo, ya sala yenye nguvu na iliyojaa
upendo
, hugeuza ulimwengu. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini! Mimi nipo pamoja nanyi.. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2019
“
W
anangu wapendwa, Leo ninawaalika kusali kwa ajili ya makusudi yangu ili niweze kuwasaidia. Wanangu, salini Rosari mkitafakari mafumbo ya Rosari maana hata ninyi katika maisha yenu mnapitia furaha na maumivu. Kwa njia hii mtageuza mafumbo katika maisha yenu maana maisha ni fumbo hadi mtakapoyaweka katika mikono ya Mungu. Hivyo mtakuwa na mang'amuzi ya imani kama Petro aliyemkuta Yesu na Roho Mtakatifu aliyoijaza roho yake. Hata ninyi, wanangu, mnaalikwa kushuhudia mkiishi
upendo
ambao kwao siku kwa siku Mungu anawajaza kwa njia ya uwepo wangu. Kwa hiyo, wanangu, muwe wazi na salini kwa moyo katika imani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, mapenzi na
upendo
wa Baba wa mbinguni hufanya mimi niwe katikati yenu, ili kusaidia kwa
upendo
wa kimama ukuaji wa imani katika mioyo yenu, ili kwamba muweze hakika kuelewa lengo la maisha ya kidunia na ukuu wa yale ya kimbingu. Wanangu, maisha ya kidunia ndiyo njia kuelekea umilele, kuelekea ukweli na uzima: kuelekea kwa Mwanangu. Kwa njia hii nataka kuwaongoza. Ninyi, wanangu, ninyi wenye sikuzote kiu ya
upendo
mkubwa zaidi, ukweli na imani, mjue ya kuwa moja tu ni chemchemi mnakoweza kunywa: imani katika Baba wa mbinguni, imani katika
upendo
wake. Mtegemee kabisa mapenzi yake wala msiogope: kila lililo bora kwa ajili yenu, kila linalowachukua kwenye uzima wa milele, mtapewa! Mtaelewa ya kuwa lengo la maisha si sikuzote kutaka na kutwaa, lakini kupenda na kutoa; mtakuwa na amani ya kweli na
upendo
wa kweli, mtakuwa mitume wa
upendo
. Kwa mfano wenu, mtawafanya wale wanangu wasiomjua Mwanangu na
upendo
wake watake kumjua. Wanangu, mitume wa
upendo
wangu, mwabuduni Mwanangu pamoja nami, na mpendeni juu ya vyote. Jaribuni sikuzote kuishi katika ukweli wake. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Novemba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Mwanangu mpenzi alimwomba sikuzote na kumtukuza Baba wa Mbinguni. Sikuzote alikuwa amemwambia yote na kujiachia katika mapenzi yake. Hivyo mnapaswa kufanya hata ninyi, wanangu, maana Baba wa Mbinguni anawasikiliza sikuzote wanawe. Moyo wa umoja katika moyo mmoja:
upendo
, mwanga na uhai. Baba wa Mbinguni amejitolea kwa njia ya sura ya kibinadamu, na sura ile ndiyo sura ya Mwanangu. Ninyi, mitume wa
upendo
wangu, ninyi mnapaswa sikuzote kupokea sura ya Mwanangu katika mioyo yenu na katika fikira zenu. Ninyi mnapaswa sikuzote kuufikiria
upendo
wake na sadaka yake. Mnapaswa kusali ili kusudi mwone uwepo wake sikuzote. Maana, enyi mitume wa
upendo
wangu, hii ni jinsi ya kuwasaidia wale wote wasiomjua Mwanangu, wale ambao hawajajua
upendo
wake. Wanangu, someni kitabu cha Injili: ni sikuzote kitu kipya, ni kinachowaunganisha na Mwanangu, aliyezaliwa kwa kuwaletea maneno ya uzima wanangu wote na kwa kujitoa sadaka kwa ajili ya wote. Mitume wa
upendo
wangu, mkisukumwa na
upendo
kumwelekea Mwanangu, leteni
upendo
na amani kwa ndugu zenu wote. Msimhukumu mtu, pendeni kila mtu kwa njia ya
upendo
kwa kumwelekea Mwanangu. Hivyo mtashughulika hata na roho zenu, nayo ni yenye thamani kuliko kitu chochote mlicho nacho. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2019
“
W
anangu wapendwa, wakati huu uwe kwenu wakati wa sala. Bila Mungu hamwezi kuwa na amani. Kwa hiyo, wanangu, salini kwa ajili ya amani katika mioyo yenu na katika familia zenu ili Yesu aweze kuzaliwa ndani yenu na kuwapeni
upendo
wake na baraka yake. Ulimwengu uko katika vita kwa sababu mioyo imejaa machukio na wivu. Wanangu, wasiwasi unaonekana katika macho yenu kwa sababu hamkuruhusu Yesu kuzaliwa katika maisha yenu. Mtafuteni, ombeni na Yeye atajitoa kwenu katika yule Mtoto aliye furaha na amani. Mimi niko pamoja nanyi na ninasali pamoja nanyi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninapowatazama ninyi mnaopenda Mwanangu, furaha inajaza Moyo wangu. Ninawabariki kwa baraka ya kimama. Pamoja na baraka ya kimama ninawabariki hata wachungaji wenu: ninyi mnaotangaza maneno ya Mwanangu, mnaobariki kwa mikono yake na mnaompenda hata kuwa tayari kufanya kwa furaha kila sadaka kwa ajili yake. Ninyi mfuateni Yeye, aliyekuwa Mchungaji wa kwanza, Mmisionari wa kwanza. Wanangu, mitume wa
upendo
wangu, kuishi na kufanya kazi kwa ajili ya wengine, kwa wale wote mnaopenda kwa njia ya Mwanangu, ni furaha na faraja ya maisha ya kidunia. Ikiwa kwa njia ya sala,
upendo
na sadaka Ufalme wa Mungu ni katika mioyo yenu, hapo kwa ninyi maisha ni yenye furaha na matulivu. Katikati ya wale wanaompenda Mwanangu na wanaopendana kwa ajili yake, maneno si ya lazima. Kutazamana kwatosha ili kusikia maneno yasiyonenwa na hisia zisizoonyeshwa. Pale panapotawala
upendo
, wakati hauna maana tena. Sisi ni pamoja nanyi! Mwanangu anawajua na kuwapenda.
Upendo
ni kilichowaongoza kwangu na, kwa njia ya
upendo
huu, mimi nitakuja kwenu na nitawaambieni kazi za wokovu. Ninataka ya kuwa wana wangu wote wawe na imani na wahisi
upendo
wangu wa kimama unaowaongoza kwa Yesu. Kwa hiyo ninyi, wanangu, ko kote mwendako angazeni kwa
upendo
na kwa imani, kama mitume wa
upendo
. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2019
“
W
anangu wapendwa, Nawaletea ninyi Mwanangu Yesu ili awabariki na kuwafunulia
Upendo
wake utokao mbinguni. Moyo wenu unatamani amani inayopungua zaidi na zaidi duniani. Kwa sababu hiyo watu wako mbali na Mungu, nafsi zinaumwa na zinaelekea kifo cha kiroho. Mimi nipo pamoja nanyi, wanangu, niwaongoze kwenye njia hii ya wokovu ambayo Mungu anawaiteni. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
Next>>