Our Lady of Medjugorje Messages containing 'wa'
Total found:
183
Ujumbe, 25 Januari 2019
“
W
anangu wapendwa! kama mama ninawaalika kutubu. Wakati huu ni kwenu, wanangu, wakati
wa
ukimya na sala. Kwa hiyo, katika joto la moyo wenu iote chembe ya tumaini na imani na hivyo, ninyi nanyi, wanangu, siku kwa siku mtasikia haja ya kusali zaidi. Maisha yenu yatakuwa ya mpangilio na yenye kuwajibika. Mtaelewa, wanangu, ya kuwa sisi ni
wa
kupita hapa duniani na ya kuwa mtasikia haja ya kuwa karibu zaidi na Mungu na kwa upendo mtatoa ushuhuda
wa
mang'amuzi yenu ya kukutana na Mungu, mtakaoushirikisha pamoja na wengine. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombeeni, lakini siwezi kufanya hivyo bila 'Ndiyo' yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, upendo na wema
wa
Baba
wa
mbinguni yanatoa mafunuo ili kwamba imani ikue, iweze kuelezwa, ilete amani, salama na matumaini. Hivi mimi nami, wanangu, kwa ajili ya upendo wenye rehema
wa
Baba
wa
mbinguni ninawaonyesha sikuzote tena njia ya kwenda kwa Mwanangu, kwa wokovu
wa
milele; kwa bahati mbaya, lakini, wanangu wengi hawataki kunisikiliza. Wanangu wengi wanasita. Lakini mimi, mimi, katika wakati na zaidi ya wakati, sikuzote nimemtukuza Bwana kwa mambo yale yote aliyoyatenda ndani yangu na kwa njia yangu. Mwanangu anajitolea kwenu, anamega mkate pamoja nanyi, anawaambieni maneno ya uzima
wa
milele ili muweze kuwaletea watu wote. Nanyi, wanangu, mitume
wa
upendo wangu, mnaogopa nini, ikiwa Mwanangu ni pamoja nanyi? Mwonyesheni nafsi zenu, ili Yeye aweze kuwa ndani yao na aweze kuwafanyeni kuwa vyombo vya imani, vyombo vya upendo. Wanangu, ishini Injili, ishini upendo wenye rehema kuelekea mwenzenu; lakini hasa ishini upendo kuelekea Baba
wa
mbinguni. Wanangu, hamkuungana kwa bahati tu. Baba
wa
mbinguni haunganishi watu kwa bahati tu. Mwanangu anaongea na nafsi zenu, nami ninaongea moyoni mwenu. Kama Mama ninawaambia: tembeeni nami! Pendaneni, na kutoa shuhuda! Hampasi kuogopa kulinda Ukweli, ambao ni Neno la Mungu, lililo la milele na lisilogeuka kamwe, kwa mifano yenu. Wanangu, yule anayetenda kazi katika mwanga
wa
upendo wenye rehema na ukweli, anasaidiwa sikuzote na Mbingu na hayuko peke yake. Mitume
wa
upendo wangu, waweze kuwatambua sikuzote katikati ya wengine wote katika maficho, upendo na utulivu wenu. Mimi nipo pamoja nanyi. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2019
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaalika kwa maisha mapya. Haijalishi miaka yenu ni mingapi, fumbueni mioyo yenu kwa Yesu ambaye atawabadilisha katika wakati huu
wa
neema nanyi, kama nyasi, mtazaliwa katika maisha mapya katika upendo
wa
Mungu na mtafumbua mioyo yenu kwa Mbinguni na kwa vitu vya kimbingu. Mimi nipo bado pamoja nanyi maana Mungu aliniruhusu kwa ajili yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninawaita mitume
wa
upendo wangu. Ninawaonyesha Mwanangu, aliye amani ya kweli na upendo
wa
kweli. Kama Mama, kwa ajili ya neema ya kimungu, ninatamani kuwaongoza kwendea Yeye. Wanangu, kwa hiyo ninawaalika kujitazama ninyi wenyewe mkianzia kwa Mwanangu, kumtazama kwa moyo na kuona kwa moyo mahali mlipo na maisha yenu yanakwenda wapi. Wanangu, ninawaalika kuelewa ya kuwa mnaishi kwa ajili ya Mwanangu, kwa njia ya upendo wake na sadaka yake. Ninyi mnamwomba Mwanangu kuwa mwenye rehema nanyi, lakini mimi ninawaalika ninyi kuwa na rehema. Mnamwomba kuwa mwema nanyi na kuwasamehe, lakini tangu lini mimi ninawasihi ninyi, wanangu, kusamehe na kupenda watu wote mnaokutana nao! Mtakapoelewa kwa moyo maneno yangu, mtaelewa na kujua upendo
wa
kweli, na mtaweza kuwa mitume
wa
upendo ule, enyi mitume wangu, wanangu wapendwa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Machi 2019
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati
wa
neema. Kama vile maumbile huhuisha kwa maisha mapya nanyi pia mnaalikwa kugeuka. Kateni shauri kwa ajili ya Mungu. Wanangu, ninyi ni watupu wala hamna furaha maana hamko na Mungu. Kwa hiyo salini ili sala iwe maisha kwenu. Maporini mtafuteni Mungu aliyewaumbeni maana mapori ya asili yanaongea na kupigana kwa ajili ya maisha wala si kwa ajili ya kifo. Vita vinatawala katika mioyo yenu na katika watu maana hamna amani na wala hamuoni, wanangu, ndugu yenu ndani ya jirani yako. Kwa hiyo mrudieni Mungu na kusali. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Aprili 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kama Mama ambaye anajua wana wake, ninajua ya kuwa mnamtamani Mwanangu. Ninajua ya kuwa mnatamani ukweli, amani, na kilicho chema wala si uovu. Kwa sababu hiyo mimi, kama Mama, kwa njia ya upendo
wa
Mungu ninawaita ninyi na kuwaalika ili, mkisali kwa moyo safi na wazi, mmtambue ninyi wenyewe Mwanangu, upendo wake, na Moyo wake wenye rehema. Mwanangu alikuwa akiona uzuri katika vitu vyote. Yeye anatafuta mema, hata yale mema madogo yanayofichika, katika roho zote, ili kusamehe maovu. Kwa hiyo, wanangu, mitume
wa
upendo wangu, ninawaalika kumwabudu, kumshukuru daima na kumstahili. Maana yeye aliwaambieni maneno ya kimungu, maneno ya Mungu, maneno yaliyo kwa watu wote na hata milele. Kwa hiyo, wanangu, ishini uchangamfu, umakini, umoja na muwe na mapenzi baina yenu. Haya mnapaswa kuwa nayo katika ulimwengu
wa
leo: hivyo mtakuwa mitume
wa
upendo wangu, hivyo mtashuhudia Mwanangu kwa jinsi ya haki. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2019
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati
wa
neema, wakati
wa
rehema kwa kila mmoja wenu. Wanangu, msiruhusu upepo
wa
chukio na hofu utawale ndani yenu na karibu nanyi. Ninyi, wanangu, mmealikwa kuwa upendo na sala. Ibilisi ataka hofu na fujo lakini ninyi, wanangu, muwe furaha ya Yesu Mfufuka ambaye amekufa na kufufuka kwa ajili ya kila mmoja wenu. Yeye ameshinda kifo kwa kuwapeni uzima, uzima
wa
milele. Kwa hiyo, wanangu, mshuhudieni na muwe wenye fahari kwa kufufuliwa katika Yeye. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo
wa
kimama ninawaalika ili kwa moyo safi na wazi, kwa imani kabisa, mpokee upendo mkubwa
wa
Mwanangu. Mimi ninajua ukuu
wa
upendo wake, mimi nilimchukua ndani yangu, Hostia moyoni, Mwanga na Upendo
wa
ulimwengu. Wanangu, hata kuelekea kwangu kwenu ninyi ni ishara ya upendo na ya huruma ya Baba
wa
Mbinguni, ni tabasamu kilichojaa upendo
wa
Mwanangu, ni mwaliko kwa uzima
wa
milele. Damu ya Mwanangu ilimwagika kwa ajili yenu kwa upendo. Ile Damu yenye thamani ni kwa wokovu wenu, kwa ajili ya uzima
wa
milele. Baba
wa
mbinguni aliumba mtu kwa ajili ya furaha ya milele. Haiwezekani ninyi kufa, ninyi mnaojua upendo
wa
Mwanangu, ninyi mnaomfuata. Uzima umeshinda: Mwanangu yu hai! Kwa hiyo, wanangu, mitume
wa
upendo wangu, sala iwaonyeshe njia, jinsi ya kueneza upendo
wa
Mwanangu kwa jinsi ilivyo bora zaidi. Wanangu, hata wakati mnapojaribu kuishi maneno ya Mwanangu, ninyi mnasali. Wakati mnapowapenda watu mnaokutana nao, mnaeneza upendo
wa
Mwanangu. Upendo ni neno linalofungua milango ya Uzima. Wanangu, tangu awali nimesali kwa ajili ya Kanisa. Kwa hiyo ninawaalika nanyi, mitume
wa
upendo wangu, kusali kwa ajili ya Kanisa na watumishi wake, kwa wale ambao Mwanangu amewaita. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Mei 2019
“
W
anangu wapendwa, Mungu kwa rehema yake alinijalia kuwa pamoja nanyi, ili kuwaelimisha na kuwaongoza kuelekea katika hatua ya wongofu. Wanangu, ninyi nyote mmeitwa kusali kwa moyo wenu wote ili mpango
wa
wokovu utimilike ndani mwenu na kwa njia yenu. Jueni wanangu, kwamba maisha ni mafupi na uzima
wa
milele unawangoja kwa kadiri ya mastahili yenu. Kwa hiyo salini, salini, salini ili muweze kuwa vyombo vya kufaa mikononi mwa Mungu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Juni 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, moyo safi na wazi tu utawawezesha ninyi kumjua kweli Mwanangu, na wale wote wasiojua upendo wake kuujua kwa njia yenu. Upendo tu utawawezesha kuelewa kuwa ni wenye nguvu kuliko kifo, maana upendo
wa
kweli umeshinda kifo na umefanya hata kifo hakipo tena. Wanangu, msamaha ni mtindo bora
wa
upendo. Ninyi, kama mitume
wa
upendo wangu, yawapasa kusali kwa kuwa wenye nguvu katika roho na kuweza kuelewa na kusamehe. Ninyi, mitume
wa
upendo wangu, kwa njia ya ufahamu na msamaha, mnatoa mfano
wa
upendo na rehema. Kuweza kuelewa na kusamehe ni karama inayotokana na maombi na yatupasa kuitunza. Mkisamehe ninyi mnaonyesha ya kuwa mnajua kupenda. Tazameni, wanangu, kama Baba
wa
mbinguni anavyowapenda kwa upendo mkubwa, kwa ufahamu, kwa uelewa, msamaha na haki. Kama anavyowatolea mimi, Mama
wa
mioyo yenu. Na tazama: mimi nipo katikati yenu ili kuwabariki kwa baraka ya kimama; ili kuwaalika kusali na kufunga; ili kuwasihi kuamini, kutumaini, kusamehe, kuwaombea wachungaji wenu na hasa kupenda bila mipaka. Wanangu, nifuateni! Njia yangu ni njia ya amani na upendo, njia ya Mwanangu. Ndiyo njia ya kuongoza katika ushindi
wa
Moyo wangu. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Juni 2019
“
W
anangu wapendwa, Namshukuru Mungu kwa kila mmoja wenu. Hasa, wanangu, asanteni kwa kuitikia wito wangu. Mimi ninawatayarisha kwa nyakati mpya ili muwe imara katika imani na kusali daima, ili Roho Mtakatifu atende kwa njia yenu na afanye upya uso
wa
nchi. Ninasali pamoja nanyi kwa amani, karama ya thamani kuliko zote, hata ingawa shetani hutaka vita na machukio. Ninyi, wanangu, muwe mikono yangu inayonyoshwa na tembeeni katika kujivunia pamoja na Mungu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Julai 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kufuatana na matakwa ya Baba mwenye rehema, nimewapa na tena nitawapa ishara dhahiri za uwepo wangu
wa
kimama. Wanangu, ishara hizo ni kwa hamu yangu ya kimama ya kuziponya roho. Ishara hizo ni kwa hamu ya kuwa kila mwanangu awe na imani ya kweli, aishi mang’amuzi ya ajabu akinywa kwenye chemchemi ya Neno la Mwanangu, Neno la uhai. Wanangu, kwa njia ya upendo wake na sadaka, Mwanangu alichukua ulimwenguni mwanga
wa
imani na aliwaonyesheni njia ya imani. Maana, wanangu, imani huamsha huzuni na maumivu. Imani ya kweli hufanya sala kusisika zaidi, hutimiza matendo ya huruma: mazungumzo na matoleo. Wale wanangu walio na imani, imani ya kweli, ni wenye heri pamoja na yote, maana wanaishi duniani mwanzo
wa
heri ya Mbinguni. Kwa hiyo, wanangu, mitume
wa
upendo wangu, ninawaalika kutoa mfano
wa
imani ya kweli, kupeleka mwanga pale palipo giza, kumwishi Mwanangu. Wanangu, kama Mama ninawaambia: hamwezi kupitia njia ya imani na kumfuata Mwanangu pasipo wachungaji wenu. Salini ili wawe na nguvu na upendo kwa kuwaongoza. Sala zenu ziwe sikuzote pamoja nao. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Julai 2019
“
W
anangu wapendwa, mwaliko wangu kwenu ni sala. Sala iwe kwenu furaha na taji la kuwaunganisha na Mungu. Wanangu, majaribu yatakuja nanyi hamtakuwa na nguvu na dhambi itatawala lakini mkiwa wangu, mtashinda maana kimbilio lenu litakuwa Moyo
wa
Mwanangu Yesu. Kwa hiyo wanangu, rudieni sala ili sala iwe maisha kwenu, mchana na usiku. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Upendo
wa
Mwanangu ni mkubwa. Laiti mngeweza kujua ukuu
wa
upendo Wake, msingeacha kamwe kumwabudu na kumshukuru. Yeye ni sikuzote hai pamoja nanyi katika Ekaristi, maana Ekaristi ni moyo Wake, Ekaristi ni moyo
wa
imani. Yeye hakuwaacha kamwe: hata wakati ninyi mlipojaribu kwenda mbali Naye, Yeye hakuwaacha kamwe.
Kwa hiyo, moyo wangu
wa
kimama unafurahi wakati unapotazama jinsi mlivyojaa upendo mnapomrudia, wakati unapoona ya kuwa mnamrudia kwa njia ya upatanisho, upendo na matumaini. Moyo wangu
wa
kimama unajua ya kuwa ikiwa mngetembea katika njia ya imani, mngekuwa kama machipukizi, kama matumba na kwa njia ya sala na kufunga mngekuwa kama matunda, kama maua, mitume
wa
upendo wangu, mngekuwa waleta mwanga na mngeangaza kwa upendo na hekima pande zote karibu nanyi.
Wanangu, kama mama, ninawaomba: salini, fikirini na kutafakari. Yote yanayowatokea, mazuri, ya kuumiza na ya kufurahisha, hayo yote yawasababisha kukua kiroho, yawafanya kuwa Mwanangu akue ndani yenu. Wanangu mkabidhi kwake. Mumwamini na mtumainie upendo Wake. Na Yeye awaongoze. Na Ekaristi iwe mahali mtakapolisha roho zenu ili kueneza upendo na ukweli. Shuhudieni Mwanangu. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2019
“
W
anangu wapendwa, Fanyeni kazi na shuhudieni kwa upendo Ufalme
wa
Mbinguni ili muweze kuwa hamjambo hapa duniani. Wanangu, Mungu atabariki mara mia zaidi juhudi yenu na mtakuwa mashahidi katikati ya watu, roho za wale wasioamini zitahisi neema ya wongofu na Mbingu itazipokea taabu zenu na sadaka zenu. Wanangu, shuhudieni kwa tasbihi mkononi ili muwe wangu na kateni shauri kuwa watakatifu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Salini kila siku Tasbihi, taji lile la maua linaloniungana moja kwa moja kama Mama kwa maumivu yenu, mateso, mahitaji na matumaini. Mitume
wa
upendo wangu, Mimi nipo pamoja nanyi kwa njia ya neema na upendo
wa
Mwanangu, nanyi ninawaombeni sala. Sala zenu zinahitajika sana ulimwenguni, ili roho ziongoke! Fungueni wazi kwa imani timilifu mioyo yenu kwa Mwanangu, na yeye ataandika ndani yao muhtasari
wa
Neno lake, yaani upendo. Ishini muungano usiotenganika na Moyo Mtakatifu sana
wa
Mwanangu! Wanangu, kama Mama nawaambieni ya kwamba hakuna wakati
wa
kupoteza ili kupiga magoti mbele ya Mwanangu, kumkiri kama Mungu wenu, aliye kitovu cha maisha yenu. Mtoeni karama, zile anazozipenda zaidi, yaani upendo kwa jirani yako, rehema na mioyo safi. Mitume
wa
upendo wangu, wanangu wengi bado hawajamkiri Mwanangu kama Mungu wao, bado hawajajua upendo wake. Lakini ninyi, kwa njia ya sala yenu inayosema kwa moyo safi na wazi, pamoja na karama mnazotoa kwa Mwanangu, mtasababisha kwamba hata mioyo migumu zaidi ifunguke. Mitume
wa
upendo wangu, nguvu ya sala inayosemwa kutokana na moyo, ya sala yenye nguvu na iliyojaa upendo, hugeuza ulimwengu. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini! Mimi nipo pamoja nanyi.. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, mapenzi na upendo
wa
Baba
wa
mbinguni hufanya mimi niwe katikati yenu, ili kusaidia kwa upendo
wa
kimama ukuaji
wa
imani katika mioyo yenu, ili kwamba muweze hakika kuelewa lengo la maisha ya kidunia na ukuu
wa
yale ya kimbingu. Wanangu, maisha ya kidunia ndiyo njia kuelekea umilele, kuelekea ukweli na uzima: kuelekea kwa Mwanangu. Kwa njia hii nataka kuwaongoza. Ninyi, wanangu, ninyi wenye sikuzote kiu ya upendo mkubwa zaidi, ukweli na imani, mjue ya kuwa moja tu ni chemchemi mnakoweza kunywa: imani katika Baba
wa
mbinguni, imani katika upendo wake. Mtegemee kabisa mapenzi yake wala msiogope: kila lililo bora kwa ajili yenu, kila linalowachukua kwenye uzima
wa
milele, mtapewa! Mtaelewa ya kuwa lengo la maisha si sikuzote kutaka na kutwaa, lakini kupenda na kutoa; mtakuwa na amani ya kweli na upendo
wa
kweli, mtakuwa mitume
wa
upendo. Kwa mfano wenu, mtawafanya wale wanangu wasiomjua Mwanangu na upendo wake watake kumjua. Wanangu, mitume
wa
upendo wangu, mwabuduni Mwanangu pamoja nami, na mpendeni juu ya vyote. Jaribuni sikuzote kuishi katika ukweli wake. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Novemba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Mwanangu mpenzi alimwomba sikuzote na kumtukuza Baba
wa
Mbinguni. Sikuzote alikuwa amemwambia yote na kujiachia katika mapenzi yake. Hivyo mnapaswa kufanya hata ninyi, wanangu, maana Baba
wa
Mbinguni anawasikiliza sikuzote wanawe. Moyo
wa
umoja katika moyo mmoja: upendo, mwanga na uhai. Baba
wa
Mbinguni amejitolea kwa njia ya sura ya kibinadamu, na sura ile ndiyo sura ya Mwanangu. Ninyi, mitume
wa
upendo wangu, ninyi mnapaswa sikuzote kupokea sura ya Mwanangu katika mioyo yenu na katika fikira zenu. Ninyi mnapaswa sikuzote kuufikiria upendo wake na sadaka yake. Mnapaswa kusali ili kusudi mwone uwepo wake sikuzote. Maana, enyi mitume
wa
upendo wangu, hii ni jinsi ya kuwasaidia wale wote wasiomjua Mwanangu, wale ambao hawajajua upendo wake. Wanangu, someni kitabu cha Injili: ni sikuzote kitu kipya, ni kinachowaunganisha na Mwanangu, aliyezaliwa kwa kuwaletea maneno ya uzima wanangu wote na kwa kujitoa sadaka kwa ajili ya wote. Mitume
wa
upendo wangu, mkisukumwa na upendo kumwelekea Mwanangu, leteni upendo na amani kwa ndugu zenu wote. Msimhukumu mtu, pendeni kila mtu kwa njia ya upendo kwa kumwelekea Mwanangu. Hivyo mtashughulika hata na roho zenu, nayo ni yenye thamani kuliko kitu chochote mlicho nacho. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2019
“
W
anangu wapendwa, wakati huu uwe kwenu wakati
wa
sala. Bila Mungu hamwezi kuwa na amani. Kwa hiyo, wanangu, salini kwa ajili ya amani katika mioyo yenu na katika familia zenu ili Yesu aweze kuzaliwa ndani yenu na kuwapeni upendo wake na baraka yake. Ulimwengu uko katika vita kwa sababu mioyo imejaa machukio na wivu. Wanangu, wasiwasi unaonekana katika macho yenu kwa sababu hamkuruhusu Yesu kuzaliwa katika maisha yenu. Mtafuteni, ombeni na Yeye atajitoa kwenu katika yule Mtoto aliye furaha na amani. Mimi niko pamoja nanyi na ninasali pamoja nanyi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninapowatazama ninyi mnaopenda Mwanangu, furaha inajaza Moyo wangu. Ninawabariki kwa baraka ya kimama. Pamoja na baraka ya kimama ninawabariki hata wachungaji wenu: ninyi mnaotangaza maneno ya Mwanangu, mnaobariki kwa mikono yake na mnaompenda hata kuwa tayari kufanya kwa furaha kila sadaka kwa ajili yake. Ninyi mfuateni Yeye, aliyekuwa Mchungaji
wa
kwanza, Mmisionari
wa
kwanza. Wanangu, mitume
wa
upendo wangu, kuishi na kufanya kazi kwa ajili ya wengine, kwa wale wote mnaopenda kwa njia ya Mwanangu, ni furaha na faraja ya maisha ya kidunia. Ikiwa kwa njia ya sala, upendo na sadaka Ufalme
wa
Mungu ni katika mioyo yenu, hapo kwa ninyi maisha ni yenye furaha na matulivu. Katikati ya wale wanaompenda Mwanangu na wanaopendana kwa ajili yake, maneno si ya lazima. Kutazamana kwatosha ili kusikia maneno yasiyonenwa na hisia zisizoonyeshwa. Pale panapotawala upendo, wakati hauna maana tena. Sisi ni pamoja nanyi! Mwanangu anawajua na kuwapenda. Upendo ni kilichowaongoza kwangu na, kwa njia ya upendo huu, mimi nitakuja kwenu na nitawaambieni kazi za wokovu. Ninataka ya kuwa wana wangu wote wawe na imani na wahisi upendo wangu
wa
kimama unaowaongoza kwa Yesu. Kwa hiyo ninyi, wanangu, ko kote mwendako angazeni kwa upendo na kwa imani, kama mitume
wa
upendo. Ninawashukuru.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
Next>>