Our Lady of Medjugorje Messages containing 'wa'
Total found:
183
Ujumbe, 2 Januari 2020 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, najua kuwepo katika maisha yenu na mioyo yenu. Nahisi upendo wenu, nasikia sala zenu na kuzipeleka kwa Mwanangu. Lakini, wanangu, mimi nataka kwa njia ya upendo
wa
kimama, kuwepo katika maisha ya wanangu wote. Nataka kukusanya karibu yangu wanangu wangu wote, chini ya joho langu la kimama. Kwa hiyo ninawaalika ninyi na kuwaiteni mitume
wa
upendo wangu, il mnisaidie. Wanangu, Mwanangu aliyatamka maneno haya: "Baba yetu”, Baba yetu uliye popote na katika mioyo yetu, kwa sababu ataka kuwafundisha kusali kwa maneno na kwa hisia zenu. Ataka muwe bora zaidi kila siku, muishi upendo wenye rehema ulio sala na sadaka isiyo na mipaka kwa ajili ya wengine. Wanangu mpeni Mwanangu upendo kwa jirani; mpeni jirani wenu maneno ya faraja, ya huruma na matendo ya haki. Yote mliyoyatoa kwa wengine, enyi mitume
wa
upendo wangu, Mwanangu anayapokea kama zawadi. Nami ni pamoja nanyi kwa sababu Mwanangu ataka kwamba upendo wangu, ulio kama mwali
wa
nuru, uzihuishe nafsi zenu, uwasaidie katika kutafuta amani na uheri
wa
milele. Kwa hiyo, wanangu, pendaneni, na muunganishwe kwa njia ya Mwanangu, ili muwe wana
wa
Mungu ambao wote pamoja kwa moyo uliojaa, wazi na safi mkisema kwa pamoja “Baba yetu” pasipo kuogopa! Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2020
“
W
anangu wapendwa, Leo ninawaalika kusali tena zaidi ili msikie katika mioyo yenu utakatifu
wa
msamaha. Katika familia lazima kuwepo utakatifu kwa sababu enyi wanangu, ulimwengu hauna wakati ujao bila upendo na utakatifu, kwa sababu katika utakatifu na katika furaha ninyi mjitolee kwa Mungu Mwumbaji anayewapendeni kwa upendo mkubwa sana. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2020 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nilichaguliwa kuwa mama
wa
Mungu na mama yenu, kwa maamuzi na upendo
wa
Bwana, lakini pia kwa mapenzi yangu, kwa upendo wangu usio na kifani kwake Baba
wa
mbinguni na kwa imani yangu yote Kwake. Mwili wangu ulikuwa kikombe cha Mungu Mtu. Nilikuwa mtumishi
wa
ukweli,
wa
upendo na wokovu kama vile nilivyo sasa katikati yenu, ili kuwaalika, wanangu, mitume
wa
upendo wangu, kuwa waletaji ukweli, ili kuwaalika, kwa njia ya utashi na upendo yenu kumwelekea Mwanangu, ili kueneza maneno Yake, maneno ya wokovu na kuyaonyesha, kwa vitendo vyenu, kwa wale wote ambao hawajamjua mwanangu na upendo Wake. Nguvu mtaipata katika Ekaristi: Mwanangu awalisheni kwa mwili Wake na kuwaimarisha kwa damu Yake. Wanangu, wekeni mikono yenu pamoja kwa sala na tazameni kuelekea msalaba kwa ukimya. Kwa jinsi hii mtapata imani ili muweze kuieneza, mtapata ukweli ili muweze kuupambanua, mtapata upendo ili muweze kuelewa namna ya kupenda kwa uhakika. Wanangu, mitume
wa
upendo wangu, wekeni mikono yenu pamoja kwa sala na tazameni kuelekea msalaba: katika msalaba tu kuna wokovu. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2020
“
W
anangu wapendwa, Katika kipindi hiki cha neema nataka kuona nyuso zenu zigeuke katika sala. Ninyi mmejaa mahangaiko ya kidunia kiasi kwamba hamuoni hata ujio
wa
majira ya kuchipua kwa mimea. Wanangu, mnaalikwa kwa toba na kwa sala. Kama viumbe vya asili vinapigana katika kimya kwa maisha mapya, hivyo hata ninyi mnaalikwa kujifungua katika sala kwa Mungu ambaye kwake mtapata amani na joto la jua la kipindi cha kuchanua kwa mimea katika mioyo yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2020 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, upendo wenu safi na
wa
kweli unavuta Moyo wangu
wa
kimama. Imani yenu na usadiki wenu katika Baba
wa
mbinguni ni mawaridi yenye harufu nzuri mnayonitolea: shada la mawaridi mazuri sana, lililotengenezwa kwa sala zenu, kwa matendo ya rehema na ya upendo. Mitume
wa
upendo wangu, ninyi mnaojaribu kumfuata Mwanangu pasipo unafiki na kwa moyo safi, ninyi ambao pasipo unafiki mnampenda, muwe ninyi wenyewe kusaidia: muwe mfano kwa wale ambao hawajajua upendo
wa
Mwanangu. Lakini, wanangu, siyo kwa maneno tu, bali hata kwa matendo na hisia safi, ambayo kwa njia yake mnamtukuza Baba
wa
mbinguni. Mitume
wa
upendo wangu, ni wakati
wa
kukesha na ninawaombeni upendo; na msihukumu mtu yeyote, kwa maana Baba
wa
mbinguni atahukumu wote. Ninawaombeni mpende, na mueneze ukweli, kwa maana ukweli ni
wa
kale: Ukweli siyo mpya, Ukweli ni
wa
milele, Ukweli ndiyo ukweli! Ukweli unatolea ushuhuda
wa
umilele
wa
Mungu. Bebeni mwanga
wa
Mwanangu na mpasue giza ambalo linataka kuwakandamiza zaidi na zaidi. Msiwe na hofu: kwa ajili ya neema na upendo
wa
Mwanangu, mimi nipo pamoja nanyi! Ninawashukuru. ”
”
Ujumbe, 25 Aprili 2020
“
W
anangu wapendwa, wakati huu uwe kwenu himizo kwa wongofu wenu binafsi. Wanangu, ombeni katika upweke Roho Mtakatifu ili iwaimarishe katika imani na katika kumsadiki Mungu ili kuweza kuwa mashahidi
wa
upendo ambao Mungu anawapa kupitia uwepo wangu. Wanangu, msiruhusu majaribu yafanye mioyo yenu kuwa migumu na sala kuwa kama jangwa. Muwe mwangi
wa
upendo
wa
Mungu na mshuhudieni Yesu Aliyefufuka kwa njia ya maisha yenu. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawapenda nyote kwa upendo wangu
wa
kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu”.
”
Ujumbe, 25 Mei 2020
“
W
anangu wapendwa, Salini pamoja Nami kwa maisha mapya ya ninyi nyote. Wanangu, katika mioyo yenu mnajua ni nini lazima kibadilike: rudini kwa Mungu na kwa Amri Zake ili Roho Mtakatifu aweze kugeuza maisha yenu na uso
wa
dunia hii, inayohitaji kufanywa upya katika Roho. Wanangu, muwe sala kwa wale wote wasiosali, muwe furaha kwa wale wote wasioona njia ya kutokea, muwe waletaji mwanga katika giza za wakati huu
wa
wasiwasi. Salini na ombeni msaada na ulinzi
wa
watakatifu ili ninyi pia muweze kutamani mbingu na mambo halisi ya kimbingu. Mimi nipo pamoja nanyi nikiwalinda na kuwabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2020
“
W
anangu wapendwa, ninasikiliza maombi yenu na sala zenu na ninawaombea kwa mwanangu Yesu aliye njia, kweli na uzima. Wanangu, rudieni kusali na fungueni mioyo yenu katika wakati huu
wa
neema na shikeni njia ya wongofu. Maisha yenu yanapita na hayana maana bila Mungu. Kwa hiyo mimi ni pamoja nanyi niwaongoze kuelekea utakatifu
wa
maisha ili kila mmoja wenu agundue furaha ya kuishi. Wanangu, ninawapenda wote na kuwabariki kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2020
“
W
anangu wapendwa, Katika wakati huu
wa
wasiwasi ambapo ibilisi anavuna nafsi ili kuwavuta kwake, niwaalika kwa sala ya kudumu ili katika sala mtambue Mungu
wa
upendo na
wa
matumaini. Wanangu, shikeni msalaba katika mikono yenu. Na uwatie moyo kwa kuwa upendo unashinda sikuzote hasa sasa ambapo msalaba na imani yamekataliwa. Ninyi muwe mwangwi na mfano kwa njia ya maisha yenu ya kuwa imani na matumaini bado hai na ulimwengu mpya
wa
amani unawezekana. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombea mbele ya mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2020
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati
wa
neema. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaalika tena, wanangu, mrudieni Mungu na kwa kusali ili sala iwe furaha kwenu. Enyi wanangu hamtakuwa na wakati ujao wala amani mpaka katika maisha yenu mtakapoanza kuishi maongezi ya binafsi na badiliko katika mema. Maovu yatakoma na amani itatawala katika mioyo yenu na katika ulimwengu. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombea kwa mwanangu Yesu kwa ajili ya kila mmoja wenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Mimi ni pamoja nanyi kwa muda mrefu kwa maana Mungu ni mkuu katika upendo wake na katika uwepo wangu. Wanangu, ninawaalika kurudi kwa Mungu na kwa sala. Kipimo cha kuishi kwenu kiwe upendo na msisahau, wanangu, kwamba maombi na kufunga hufanya miujiza ndani yenu na kuwazunguka. Yote mnayoyafanya yawe kwa ajili ya utukufu
wa
Mungu na hapo Mbingu itajaza moyo wenu na furaha mkahisi ya kuwa Mungu anawapenda na kunituma ili kuokoa ninyi na Dunia ambayo juu yake mnaishi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Huu ni wakati
wa
upendo,
wa
uchangamfu,
wa
sala na
wa
furaha. Salini, wanangu, ili Mtoto Yesu azaliwe katika mioyo yenu. Fungueni mioyo yenu kwa Yesu anayejitoa kwa kila mmoja wenu. Mungu amenialika ili mimi niwe furaha na matumaini katika wakati huu nami ninawaambia: bila Mtoto Yesu hamna wala huruma wala hisia ya Mbingu, zinazofichika katika yule Mtoto mchanga. Kwa hiyo, wanangu, fanyeni kazi juu ya nafsi zenu wenyewe. Mkisoma Maandiko Matakatifu, mtagundua kuzaliwa kwa Yesu na furaha kama ile ya siku za kwanza ya matokeo ya Medjugorje iliyotolea kwa ubinadamu. Historia itakuwa ukweli, ambao hata leo unajirudia ndani yenu na kuwazunguka. Fanyeni kazi na jengeni amani kwa njia ya sakramenti ya Kitubio. Jipatanisheni na Mungu, wanangu, na mtaona miujiza inawazunguka. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mtoto Yesu anayewaletea amani, Yule aliye wakati uliopita, wakati
wa
sasa na wakati ujao
wa
kuishi kwenu. Wanangu, msiruhusu imani yenu na matumaini yenu katika wakati ujao ulio bora yazimike, kwa maana ninyi mmechaguliwa kwa kuwa mashahidi
wa
matumaini katika kila hali. Kwa ajili hiyo mimi ni hapa pamoja na Yesu ili awabariki kwa amani yake. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2021
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huo ninawaalika kusali, kufunga na kujikana ili muweze kuwa wenye nguvu zaidi katika imani. Huu ni wakati
wa
mwamko na
wa
kuzaliwa upya. Kama vitu vya asili vinavyojitoa nanyi wanangu, fikirini juu ya mambo mliyopokea. Muwe waletaji
wa
amani na
wa
upendo wenye furaha ili kuishi vizuri duniani. Tamanini Mbingu kwa sababu Mbinguni hakuna wala huzuni wala machukio. Kwa hiyo, wanangu, amueni tena kuongoka, na utakatifu utawale katika maisha yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2021
“
W
anangu wapendwa! Mungu ameniruhusu kuwa pamoja nanyi leo pia kwa kuwaalika kusali na kufunga. Ishini wakati huu
wa
neema na muwe mashahidi
wa
tumaini maana, ninawaambia tena wanangu, kwa kusali na kufunga hata vita vinaweza kuisha. Wanangu, aminini na kuishi katika imani na kwa imani wakati huu
wa
neema na Moyo wangu usio na dhambi ya asili haumwachi yeyote kati yenu katika wasiwasi ikiwa ananikimbilia. Ninawaombea mbele ya Yeye aliye juu na ninasali ili amani iwepo katika mioyo yenu na kwa ajili ya tumaini katika wakati ujao. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Machi 2021
“
W
anangu wapendwa! Hata leo mimi ni pamoja nanyi ili kuwaambieni: wanangu, yule anayesali hana hofu ya wakati ujao wala hapotezi tumaini. Mmechaguliwa kwa kuleta furaha na amani, kwa maana ni wangu. Nimekuja hapa pamoja na jina: Malkia
wa
Amani kwa sababu ibilisi anataka kuleta wasiwasi na vita, anataka kuijaza mioyo yenu kwa hofu ya wakati ujao na wakati ujao ni
wa
Mungu. Kwa hiyo muwe wanyenyekevu, salini na acheni yote katika mikono ya Yeye aliye Juu aliyewaumba. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2021
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaalika kushuhudia imani yenu katika rangi za majira ya kuchipua, na iwe imani ya matumaini na ya ujasiri. Wanangu, imani yenu isitindike katika hali yoyote na hata katika wakati huu
wa
majaribio. Tembeeni kwa ujasiri pamoja na Kristo Mfufuka kuelekea Mbingu iliyo lengo lenu. Mimi ninaandamana nanyi katika mwendo huu
wa
utakatifu na kuweka ninyi nyote katika Moyo wangu Usio na dhambi ya asili. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2021
“
W
anangu wapendwa! Ninawatazama na kuwaalika: mrudieni Mungu maana Yeye ndiye upendo na kwa ajili ya upendo alinituma kwenu ili niwaongoze kwenye njia ya wongofu. Acheni dhambi na maovu, amueni kuwa watakatifu na furaha itatawala; nanyi mtakuwa mikono yangu iliyopanuliwa katika ulimwengu huu uliopotea. Ninatamani ya kuwa muwe sala na matumaini kwa wale ambao hawajamjua Mungu
wa
upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2021
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika kuwa sala kwa wale wote wasiosali. Shuhudieni, wanangu, kwa njia ya maisha yenu furaha ya kuwa wangu na Mungu atajibu sala zenu na kuwapa amani katika ulimwengu huu
wa
wasiwasi ambamo kiburi na ubinafsi hutawala. Wanangu, ninyi muwe wakarimu na upendo
wa
upendo wangu ili wapagani wahisi ya kuwa ninyi ni wangu na waweze kuugeukia Moyo wangu Usio na dhambi ya asili. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2021
“
W
anangu wapendwa! Kwa furaha ninawaalika ninyi nyote, wanangu, mlioitikia wito wangu, kuwa furaha na amani. Kwa maisha yenu shuhudieni Mbingu ninayowaletea. Ni saa, wanangu, ya kuwa wonyesho
wa
upendo wangu kwa wote wale ambao hawapendi na mioyo yao imeshindwa na machukio. Msisahau: mimi ni pamoja nanyi na ninawaombea ninyi nyote karibu na mwanangu Yesu ili awapeni amani yake. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
Next>>