Our Lady of Medjugorje Messages containing 'wa'
Total found:
183
Ujumbe, 25 Oktoba 2021
“
W
anangu wapendwa! Rudieni kusali maana wanaosali hawaogopi wakati ujao. Wale wanaosali wako wazi kwa uzima na wanaheshimu maisha ya wengine. Yeyote anayesali, wanangu, anahisi uhuru
wa
wana
wa
Mungu na kwa moyo
wa
furaha hutumikia kwa manufaa ya ndugu yake. Kwa sababu Mungu ni upendo na uhuru. Kwa hiyo, wanangu, wanapotaka kuwafunga kwa minyororo na kuwatumia hilo halitoki kwa Mungu maana Mungu ni upendo na humpa kila kiumbe amani yake. Kwa hiyo amenituma niwasaidie ninyi kukua katika njia ya utakatifu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2021
“
W
anangu wapendwa! Niko pamoja nanyi katika wakati huu
wa
rehema na ninawaalika nyote kuwa waleta amani na upendo katika ulimwengu huu, ambapo, wanangu, Mungu anawaalika kupitia Kwangu kuwa sala, upendo na kielelezo cha Paradiso, hapa duniani. Mioyo yenu na ijazwe na furaha na imani katika Mungu ili, wanangu, muwe na imani kamili katika mapenzi yake matakatifu. Hii ndiyo sababu mimi niko pamoja nanyi kwa sababu Yeye, Aliye Juu, ananituma kati yenu ili kuwahimiza ninyi kuwa na matumaini na mtakuwa waleta amani katika ulimwengu huu wenye wasiwasi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2022
“
W
anangu wapendwa! Ninawatazama na ninamshukuru Mungu kwa kila mmoja wenu, kwa sababu ameniruhusu niwe nanyi tena ili kuwasihi katika utakatifu. Wanangu amani inavurugika na shetani anataka mahangaiko. Kwa hiyo maombi yenu yawe na nguvu zaidi ili kila roho chafu ya utengano na vita itulie. Iweni wajenzi
wa
amani na wachukuaji
wa
Aliyefufuka ndani yenu na karibu nanyi ili mema yapate kushinda katika kila mtu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2022
“
W
anangu wapendwa! Ninafurahi pamoja nanyi na kuwashukuru kwa kila sadaka na sala ambayo mlitolea kwa makusudi yangu. Wanangu, msisahau ya kuwa ninyi ni muhimu katika mpango wangu
wa
wokovu
wa
wanadamu. Rudeni kwa Mungu na kwa sala ili Roho Mtakatifu atende kazi ndani yenu na kupitia ninyi. Wanangu, Mimi ni pamoja nanyi hata katika siku hizi ambapo shetani anapiga kwa vita na kwa machukio. Utengano ni wenye nguvu na maovu yatenda kazi katika mwanadamu kama hajatenda bado mpaka leo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2022
“
W
anangu wapendwa! Niko pamoja nanyi kuwaongoza katika njia ya uongofu kwa sababu, wanangu, kwa maisha yenu mnaweza kuleta nafsi nyingi karibu na Mwanangu. Iweni mashahidi wenye furaha
wa
Neno la Mungu na
wa
upendo, mkiwa na matumaini ndani ya mioyo yenu yashindayo uovu wote. Mwasamehe wanaowadhuru na tembeeni katika njia ya utakatifu. Ninawaongoza kwa Mwanangu ili Yeye awe njia, ukweli na uzima kwenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2022
“
W
anangu wapendwa! Salini ili Roho Mtakatifu awaangazie kuwa watafutaji
wa
Mungu wenye furaha na mashahidi
wa
upendo usio na kikomo. Mimi niko pamoja nanyi, wanangu, na ninawaalika ninyi nyote tena: jitieni moyo na mshuhudie matendo mema ambayo Mungu anafanya ndani yenu na kupitia kwenu. Furahini katika Mungu. Mtendeeni mema jirani yenu ili mpate afya njema duniani na ombeeni amani ambayo inatishiwa kwa sababu shetani hutaka vita na mahangaiko. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2022
“
W
anangu wapendwa! Aliye juu aliniruhusu niwe pamoja nanyi; kuwa furaha kwenu na njia katika matumaini kwa sababu ubinadamu umeamua kifo. Kwa hiyo amenituma niwaelekeze kwamba bila Mungu hamna wakati ujao. Wanangu, muwe vyombo vya upendo kwa wale wote ambao hawajamjua Mungu
wa
upendo. Kwa furaha toeni ushuhuda
wa
imani yenu na msipoteze matumaini katika mabadiliko ya moyo
wa
mwanadamu. Niko pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka yangu ya mama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2022
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaletea Mwanangu Yesu ili muwe amani yake na kielelezo cha utulivu na furaha ya Mbinguni. Salini, wanangu, ili muwe wazi kukaribisha amani, kwa sababu mioyo mingi imefungwa kupokea wito ya nuru ibadiliyo mioyo. Niko pamoja nanyi na ninawaombea mjifungue kumkaribisha Mfalme
wa
Amani anayeijaza mioyo yenu joto na baraka. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2023
“
W
anangu wapendwa! Ombeni pamoja nami kwa ajili ya amani maana shetani anataka vita na chuki katika mioyo na mataifa. Kwa hiyo salini na, katika siku zenu, toeni sadaka kwa kufunga na kutubu ili Mungu awape amani. Wakati ujao uko kwenye njia panda kwa sababu mwanadamu
wa
kisasa hataki Mungu. Kwa hiyo ubinadamu unaelekea kwenye upotevu. Ninyi, wanangu, ni tumaini langu. Ombeni pamoja nami kwamba niliyoyaanza Fatima na hapa yatimie. Ombeni na mshuhudie amani katika mazingira yenu na muwe watu
wa
amani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2023
“
W
anangu wapendwa! Ongokeni na mvae mavazi ya toba na maombi ya kina ya kibinafsi na kwa unyenyekevu mwombe Aliye Juu amani. Katika wakati huu
wa
neema Shetani anataka kuwapotosha ninyi, nanyi wanangu, mwangalieni Mwanangu na kumfuata kuelekea Kalvari, kwa kujikana na kufunga. Niko pamoja nanyi kwa sababu Aliye Juu ameniruhusu niwapende ninyi na kuwaongoza kuelekea furaha ya moyo, katika imani inayokua ndani ya wale wote wanaompenda Mungu zaidi ya vitu vyote. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 18 Machi 2023 - Tokeo la kila mwaka kwa Miriana Dragićević-Soldo
Mwotaji Mirjana Dragićević-Soldo alikuwa na matukio ya kila siku kutoka Juni 24, 1981 hadi Desemba 25, 1982. Katika hafla ya kutokezwa kwake kwa kila siku, akimfunulia siri ya kumi, Bikira alimfunulia kwamba atakuwa na tukio la kila mwaka mnamo Machi 18 na ndivyo ilivyokuwa katika miaka hii yote. Tukio hilo lilianza saa 1.33 jioni na kudumu hadi saa 1.39.
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika mpate kumjua Mwanangu vizuri iwezekanavyo kwa sala na rehema. Ili kwa mioyo safi na iliyo wazi mjifunze kusikiliza. Sikilizeni Mwanangu anachowaambieni ili mpate kuona tena kiroho. Kama watu wamoja
wa
Mungu, kwa ushirika na Mwanangu, ishuhudieni kweli kwa maisha yenu. Ombeni, wanangu, ili kwamba pamoja na Mwanangu muweze kuleta amani, furaha na upendo kwa ndugu zenu wote. Mimi ni pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka zangu za kimama.
”
Ujumbe, 25 Machi 2023
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu uwe wakati
wa
sala kwa ajili yenu.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika ninyi nyote kuwa waletaji
wa
amani na furaha ya Yesu Mfufuka kwa wale wote walio mbali na maombi ili kwa njia ya maisha yenu, upendo
wa
Yesu uwabadilishe na kuwa katika maisha mapya, maisha ya wongofu na utakatifu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika ninyi mwende katika mazingira ya asili na kusali ili kwamba Aliye Juu Sana aseme na moyo wenu na kwamba muweze kuhisi uwezo
wa
Roho Mtakatifu kushuhudia upendo ambao Mungu anao kwa kila kiumbe. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu
wa
neema, ambao Aliye Juu amenituma niwapende ninyi na kuwaongoza katika njia ya uongofu, toeni sala zenu na sadaka zenu kwa ajili ya wale wote walio mbali na wasiojua upendo
wa
Mungu. Ninyi, wanangu, muwe mashahidi
wa
upendo na amani kwa mioyo yote isiyotulia. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu
wa
neema ninawaalika ninyi kwenye maombi kwa moyo. Mioyo yenu, wanangu, igeuzwe kuelekea mbinguni kwa maombi, ili mioyo yenu ipate kuhisi Mungu
wa
upendo anayewaponya na kuwapenda kwa upendo mkuu. Mimi niko pamoja nanyi kuwaongoza kwenye njia ya uongofu
wa
moyo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika kwenye maombi ya nguvu. Umamboleo unataka kuingia katika mawazo yenu na kuwaibia furaha ya maombi na kukutana na Yesu. Kwa hiyo, wanangu wapendwa, fanyeni upya sala katika familia zenu ili moyo wangu
wa
kimama ufurahi kama siku za kwanza nilipowachagua ninyi na jibu lilikuwa ni maombi mchana na usiku na mbingu haikunyamaza bali ilitolea kwa mahali hapa neema, amani na baraka kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu na uunganishwe na sala kwa ajili ya amani na kwa matendo mema ili kusudi ionekane furaha ya kumngoja Mfalme
wa
amani mioyoni mwenu, ndani ya familia zenu na katika ulimwengu ambao hauna matumaini. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu ili aijaze mioyo yenu amani kwa sababu Yeye ni amani. Wanangu, mtafuteni Yesu katika ukimya
wa
mioyo yenu ili azaliwe upya. Ulimwengu unamhitaji Yesu, hivyo wanangu, mtafuteni kwa maombi maana anajitoa kila siku kwa kila mmoja wenu.
”
Mama yetu alikuja leo akiwa amevalia mavazi ya heshima akiwa na mtoto Yesu mikononi mwake. Yesu alinyoosha mkono wake kama ishara ya baraka na Mama yetu alituombea kwa lugha ya aramaika.
Ujumbe, 25 Januari 2024
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu uwe wakati
wa
maombi.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
Next>>