Our Lady of Medjugorje Messages containing 'wale'
Total found:
73
Ujumbe, 2 Machi 2020 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, upendo wenu safi na wa kweli unavuta Moyo wangu wa kimama. Imani yenu na usadiki wenu katika Baba wa mbinguni ni mawaridi yenye harufu nzuri mnayonitolea: shada la mawaridi mazuri sana, lililotengenezwa kwa sala zenu, kwa matendo ya rehema na ya upendo. Mitume wa upendo wangu, ninyi mnaojaribu kumfuata Mwanangu pasipo unafiki na kwa moyo safi, ninyi ambao pasipo unafiki mnampenda, muwe ninyi wenyewe kusaidia: muwe mfano kwa
wale
ambao hawajajua upendo wa Mwanangu. Lakini, wanangu, siyo kwa maneno tu, bali hata kwa matendo na hisia safi, ambayo kwa njia yake mnamtukuza Baba wa mbinguni. Mitume wa upendo wangu, ni wakati wa kukesha na ninawaombeni upendo; na msihukumu mtu yeyote, kwa maana Baba wa mbinguni atahukumu wote. Ninawaombeni mpende, na mueneze ukweli, kwa maana ukweli ni wa kale: Ukweli siyo mpya, Ukweli ni wa milele, Ukweli ndiyo ukweli! Ukweli unatolea ushuhuda wa umilele wa Mungu. Bebeni mwanga wa Mwanangu na mpasue giza ambalo linataka kuwakandamiza zaidi na zaidi. Msiwe na hofu: kwa ajili ya neema na upendo wa Mwanangu, mimi nipo pamoja nanyi! Ninawashukuru. ”
”
Ujumbe, 25 Mei 2020
“
W
anangu wapendwa, Salini pamoja Nami kwa maisha mapya ya ninyi nyote. Wanangu, katika mioyo yenu mnajua ni nini lazima kibadilike: rudini kwa Mungu na kwa Amri Zake ili Roho Mtakatifu aweze kugeuza maisha yenu na uso wa dunia hii, inayohitaji kufanywa upya katika Roho. Wanangu, muwe sala kwa
wale
wote wasiosali, muwe furaha kwa
wale
wote wasioona njia ya kutokea, muwe waletaji mwanga katika giza za wakati huu wa wasiwasi. Salini na ombeni msaada na ulinzi wa watakatifu ili ninyi pia muweze kutamani mbingu na mambo halisi ya kimbingu. Mimi nipo pamoja nanyi nikiwalinda na kuwabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2021
“
W
anangu wapendwa! Ninawatazama na kuwaalika: mrudieni Mungu maana Yeye ndiye upendo na kwa ajili ya upendo alinituma kwenu ili niwaongoze kwenye njia ya wongofu. Acheni dhambi na maovu, amueni kuwa watakatifu na furaha itatawala; nanyi mtakuwa mikono yangu iliyopanuliwa katika ulimwengu huu uliopotea. Ninatamani ya kuwa muwe sala na matumaini kwa
wale
ambao hawajamjua Mungu wa upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2021
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika kuwa sala kwa
wale
wote wasiosali. Shuhudieni, wanangu, kwa njia ya maisha yenu furaha ya kuwa wangu na Mungu atajibu sala zenu na kuwapa amani katika ulimwengu huu wa wasiwasi ambamo kiburi na ubinafsi hutawala. Wanangu, ninyi muwe wakarimu na upendo wa upendo wangu ili wapagani wahisi ya kuwa ninyi ni wangu na waweze kuugeukia Moyo wangu Usio na dhambi ya asili. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2021
“
W
anangu wapendwa! Kwa furaha ninawaalika ninyi nyote, wanangu, mlioitikia wito wangu, kuwa furaha na amani. Kwa maisha yenu shuhudieni Mbingu ninayowaletea. Ni saa, wanangu, ya kuwa wonyesho wa upendo wangu kwa wote
wale
ambao hawapendi na mioyo yao imeshindwa na machukio. Msisahau: mimi ni pamoja nanyi na ninawaombea ninyi nyote karibu na mwanangu Yesu ili awapeni amani yake. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2021
“
W
anangu wapendwa! Rudieni kusali maana wanaosali hawaogopi wakati ujao.
Wale
wanaosali wako wazi kwa uzima na wanaheshimu maisha ya wengine. Yeyote anayesali, wanangu, anahisi uhuru wa wana wa Mungu na kwa moyo wa furaha hutumikia kwa manufaa ya ndugu yake. Kwa sababu Mungu ni upendo na uhuru. Kwa hiyo, wanangu, wanapotaka kuwafunga kwa minyororo na kuwatumia hilo halitoki kwa Mungu maana Mungu ni upendo na humpa kila kiumbe amani yake. Kwa hiyo amenituma niwasaidie ninyi kukua katika njia ya utakatifu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2021
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu Yesu awapeni amani yake. Wanangu, bila amani hamna wala wakati ujao, wala baraka, kwa hiyo rudieni kusali kwa sababu tunda la sala ni furaha na imani, na bila hiyo hamwezi kuishi. Baraka ya leo tunayowapa, ileteni kwa jamaa zenu na tajirisheni wote
wale
mnaokuta ili wahisi neema ambayo mnapokea. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2022
“
W
anangu wapendwa! Aliye juu aliniruhusu niwe pamoja nanyi; kuwa furaha kwenu na njia katika matumaini kwa sababu ubinadamu umeamua kifo. Kwa hiyo amenituma niwaelekeze kwamba bila Mungu hamna wakati ujao. Wanangu, muwe vyombo vya upendo kwa
wale
wote ambao hawajamjua Mungu wa upendo. Kwa furaha toeni ushuhuda wa imani yenu na msipoteze matumaini katika mabadiliko ya moyo wa mwanadamu. Niko pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka yangu ya mama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2023
“
W
anangu wapendwa! Ongokeni na mvae mavazi ya toba na maombi ya kina ya kibinafsi na kwa unyenyekevu mwombe Aliye Juu amani. Katika wakati huu wa neema Shetani anataka kuwapotosha ninyi, nanyi wanangu, mwangalieni Mwanangu na kumfuata kuelekea Kalvari, kwa kujikana na kufunga. Niko pamoja nanyi kwa sababu Aliye Juu ameniruhusu niwapende ninyi na kuwaongoza kuelekea furaha ya moyo, katika imani inayokua ndani ya
wale
wote wanaompenda Mungu zaidi ya vitu vyote. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika ninyi nyote kuwa waletaji wa amani na furaha ya Yesu Mfufuka kwa
wale
wote walio mbali na maombi ili kwa njia ya maisha yenu, upendo wa Yesu uwabadilishe na kuwa katika maisha mapya, maisha ya wongofu na utakatifu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema, ambao Aliye Juu amenituma niwapende ninyi na kuwaongoza katika njia ya uongofu, toeni sala zenu na sadaka zenu kwa ajili ya
wale
wote walio mbali na wasiojua upendo wa Mungu. Ninyi, wanangu, muwe mashahidi wa upendo na amani kwa mioyo yote isiyotulia. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Machi 2024
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema, ombeni pamoja nami ili mema yapate kushinda ndani yenu na karibu nanyi. Hasa, wanangu, ombeni kwa umoja na Yesu katika njia yake ya msalaba. Wekeni katika maombi yenu ubinadamu huu unaotangatanga bila Mungu na bila upendo wake. Muwe maombi, muwe mwanga na mashahidi kwa
wale
wote mnaokutana nao, enyi wanangu, ili Mungu wa rehema awarehemu.. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2024
“
W
anangu wapendwa! Nipo pamoja nanyi kuwaambia kuwa nawapenda na ninawasihi sana muombe maana shetani ana nguvu na kila siku nguvu zake zinazidi kuimarika kupitia
wale
waliochagua kifo na chuki. Ninyi, wanangu, muwe maombi na mikono yangu ya upendo iwanyooshee wote walio gizani na kuitafuta nuru ya Mungu wetu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4