Our Lady of Medjugorje Messages containing 'wenu'

Total found: 102
Wanangu wapendwa! Salini na mfanye upya moyo wenu ili lile jema mlilopanda lizae matunda ya furaha na ushirika na Mungu. Magugu yamechukua mioyo mingi na imekuwa tasa. Kwa hiyo ninyi, wanangu, muwe mwanga, upendo na mikono yangu iliyonyoshwa katika ulimwengu huu unaomtamani Mungu ambaye ni upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika ninyi kuomba kwa moyo wenu. Wanangu, tengenezeni vikundi vya maombi ambavyo ndani yake mtahimizana kutenda mema na kukua katika furaha. Wanangu, bado mko mbali. Kwa hiyo, daima ongokeni upya na mchague njia ya utakatifu na matumaini ili Mungu awape amani kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
   




To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous  1 2 3 4 5 6
Medjugorje WebSite