Our Lady of Medjugorje Messages containing 'yenu'
Total found:
171
Ujumbe, 2 Julai 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, uwepo wangu halisi na wa uhai katikati
yenu
uwafanye kuwa wenye furaha kwani huo ni upendo mkuu wa Mwanangu. Yeye ananituma katikati
yenu
ili, kwa upendo wa kimama, Mimi niwaimarishe; ili muelewe kwamba maumivu na furaha, mateso na mapendo husaidia nafsi
yenu
kuishi kwa bidii zaidi; ili niwaalike tena kuadhimisha Moyo wa Yesu, moyo wa imani: Ekaristi. Mwanangu, siku kwa siku, hurudi hai katikati
yenu
: huwarudia, hata kama hakuwaacha kamwe. Wakati mmoja wenu, wanangu, anamrudia, Moyo wangu wa kimama hushtuka kwa furaha. Kwa hiyo Wanangu, irudieni Ekaristi, mrudieni Mwanangu. Njia ya kumrudia Mwanangu ni ngumu na imejaa kujinyima lakini mwishowe, kuna mwanga siku zote. Naelewa maumivu
yenu
na mateso
yenu
, na kwa upendo wa kimama, ninapangusa machozi
yenu
. Mtumainini Mwanangu, kwa maana Yeye atawafanyieni neno msilojua hata kuomba. Ninyi, wanangu, fikirieni nafsi
yenu
tu, kwani nafsi ni kitu cha pekee mliyo nayo duniani. Chafu ama safi, mtaichukua mbele ya Baba aliye Mbinguni. Kumbukeni: imani katika upendo wa Mwanangu hulipwa siku zote. Nawaambieni kuwaombea hasa wale ambao Mwanangu aliwaita kuishi wakimfuata na kulipenda kundi lao. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Julai 2016
“
W
anangu wapendwa! Ninawaangalia na ninawaona mmepotea, hamna wala sala wala furaha ndani ya mioyo
yenu
. Rudini, wanangu, kusali na wekeni Mungu katika mahali pa kwanza na si mtu. Msipoteze tumaini ninalowaletea. Wanangu, wakati huu uwe kwenu kila siku kumtafuta Mungu katika kimya ya moyo wenu na salini, salini, salini mpaka sala iwe furaha kwenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nimekuja kwenu, katikati
yenu
, ili mnipe mahangaiko
yenu
, niweze kuyaleta mbele ya Mwanangu na kuwaombeeni kwake kwa manufaa
yenu
. Najua kuwa kila mmoja wenu ana mahangaiko yake, majaribu yake. Kwa hiyo kwa moyo wa kimama nawaalikeni: Njooni kwenye Meza ya Mwanangu! Yeye humega mkate kwa ajili
yenu
, huwapa Yeye mwenyewe. Huwapa matumaini. Anawaomba kuwa na imani zaidi, matumaini zaidi, utulivu zaidi. Anawaomba mpigane ndani
yenu
dhidi ya ubinafsi, hukumu na udhaifu wa kibinadamu. Kwa hiyo Mimi, kama Mama, nawaambieni: salini, maana sala huwapa nguvu ya kupigana ndani
yenu
. Mwanangu, alipokuwa mtoto, aliniambia mara nyingi ya kuwa wengi watanipenda na kuniita "Mama". Mimi hapa, katikati
yenu
, nasikia upendo na kuwashukuru! Kwa njia ya upendo huu namwomba Mwanangu ili hakuna hata mmoja wenu, wanangu, arudiye nyumbani jinsi alivyokuja. Ili mlete matumaini, rehema na upendo kadiri muwezavyo; ili muwe mitume wa upendo wangu, wanaoshuhudia kwa maisha yao kwamba Baba aliye Mbinguni ni chemchemi ya uzima si ya mauti. Wanangu wapendwa, nawaomba tena kwa moyo wa kimama: waombeeni wateule wa Mwanangu, kwa ajili ya mikono yao iliyobarikiwa, kwa ajili ya wachungaji wenu, ili waweze kumhubiri Mwanangu kwa upendo mwingi wawezavyo, na hivyo kusababisha wongofu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2016
“
W
anangu wapendwa! Leo nataka kushirikiana pamoja nanyi furaha ya mbinguni. Ninyi wanangu fungueni mlango wa moyo ili katika moyo wenu matumaini, amani na mapendo ambazo Mungu peke yake anaweza kutoa ziweze kukua. Wanangu, mnapenda mno dunia na mambo ya dunia, kwa hiyo Shetani huwatikisa kama upepo ufanyavyo na mawimbi ya bahari. Kwa hiyo mnyororo wa maisha
yenu
uwe sala ya moyo na kumwabudu Mwanangu Yesu. Kwake mtolee maisha
yenu
yajayo ili muwe ndani Yake furaha na mfano kwa watu wengine kwa njia ya matendo
yenu
. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kulingana na mapenzi ya Mwanangu na upendo wangu wa kimama naja kwenu, wanangu, hasa kwa wale ambao hawajajua bado upendo wa Mwanangu. Ninakuja kwenu mnaonifikiria, mnaoomba msaada wangu. Ninawapa upendo wangu wa kimama na kuwaletea baraka ya Mwanangu. Mnayo mioyo safi na wazi? Mnaona dalili za uwepo wangu na upendo wangu? Wanangu, katika maisha
yenu
ya dunia igieni moyo na mfano wangu. Maisha yangu yalikuwa maumivu, ukimya, imani na matumaini pasipo mipaka katika Baba wa Mbinguni. Hakuna kitu cha bahati: si maumivu, si furaha, si mateso, si upendo. Hizo zote ni neema ambazo Mwanangu anawapeni na zinazowaongoza kwenye uzima wa milele. Mwanangu anawaomba mapendo na sala ndani yake. Kupenda na kusali ndani yake maana yake — kama Mama nataka kuwafundisha — ni kusali katika ukimya wa nafsi zenu, si kusema kwa midomo tu. Ni tendo dogo zuri litendwalo kwa jina la Mwanangu; ni uvumilivu, rehema, upokeaji wa maumivu na kujitolea kwa ajili ya wengine. Wanangu, Mwanangu huwatazama. Ombeni ili ninyi pia muuone uso wake, na ili uso huo uweze kufunuliwa kwenu. Wanangu, mimi nawafunulia ukweli halisi wa pekee. Salini kwa kuyaelewa na kuweza kueneza mapendo na matumaini, kwa kuweza kuwa mitume wa upendo wangu. Moyo wangu wa kimama hupenda hasa wachungaji. Iombeeni mikono yao iliyobarikiwa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Roho Mtakatifu, kwa njia ya Baba wa Mbinguni, amenifanya Mama: Mama wa Yesu na, kwa hiyo, Mama
yenu
vilivile. Kwa hiyo nawajilia niwasikilize, niwafungulie mikono yangu ya kimama, niwapeni Moyo wangu na kuwaalika kukaa pamoja nami, kwa maana kutoka juu ya msalaba Mwanangu amenikabidhi ninyi. Kwa bahati mbaya wanangu wengi hawakujua upendo wa Mwanangu, wengi hawataka kumjua. Loo, wanangu, mabaya mengi yatoka kwa wale ambao hawana budi ya kuona na kuelewa ili kuamini! Kwa hiyo, wanangu, mitume wangu, katika kimya ya moyo wenu sikilizeni sauti ya Mwanangu, ili moyo wenu uwe makazi yake wala usiwe giza na huzuni, bali uangaziwe na mwanga wa Mwanangu. Tafuteni matumaini kwa imani, maana imani ni maisha ya roho. Ninawaalika tena: salini! Salini ili kuishi imani katika unyenyekevu, katika amani ya kiroho na mkiangaziwa na mwanga. Wanangu, msijaribu kuelewa yote mara moja, maana Mimi nami sikuelewa yote mara moja, lakini niliyaamini maneno ya kimungu aliyoyasema Mwanangu, Yeye aliyekuwa mwanga wa kwanza na mwanzo wa Ukombozi. Enyi mitume wa moyo wangu, ninyi mnaosali, mnaojitolea, mnaopenda wala msiohukumu: ninyi nendeni mkaeneze ukweli, maneno ya Mwanangu, Injili. Ninyi kweli, ni Injili iliyo hai, ninyi ni miali ya mwanga wa Mwanangu. Mwanangu na mimi tutakuwa karibu nanyi, tutawatia moyo na kuwajaribu. Wanangu, ombeeni daima na hasa baraka ya wale ambao Mwanangu amebariki mikono yao, yaani Wachungaji wenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2016
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalika: ombeni amani! Acheni ubinafsi na ishini ujumbe ninaowapa. Bila hizo ujumbe hamwezi kubadili maisha
yenu
. Mkiwa watu wa sala mtakuwa na amani. Mkiishi katika amani mtaona hitaji la kutoa ushuhuda maana mtamtambua Mungu mnayemhisi sasa kama yu mbali. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini, na mkamwache Mungu aingie mioyoni mwenu. Rudieni kufunga na kuungama, ili muweze kushinda uovu ulio ndani
yenu
na kandokando
yenu
. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Novemba 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kuja na kujifunua kwangu kwenu ni furaha kubwa ya Moyo wangu wa kimama. Ni zawadi ya Mwanangu kwa ajili
yenu
na ya wale watakaokuja. Kama Mama nawaalika: mpendeni Mwanangu kuliko yote! Ili kumpenda kwa moyo wote, yawapaswa kumjua: Mtamjua kwa kusali: Salini kwa moyo na hisia zenu. Kusali maana yake ni kutafakari upendo wake na kujitolea kwake. Kusali maana yake ni kupenda, kutoa, kuteseka na kutolea sadaka. Nawaalika ninyi, wanangu, kuwa mitume ya sala na upendo. Wanangu, ni wakati wa kukesha. Katika kesha hii nawaalika kusali, kupenda na kutumaini. Maadamu Mwanangu ataangalia mioyo
yenu
, Moyo wangu wa kimama unatamani kwamba Yeye aone ndani ya mioyo
yenu
tumaini timilifu na upendo. Upendo wa mitume wangu wote pamoja utaishi, utashinda na utafunua maovu. Wanangu, mimi nilikuwa kalisi ya Mtu - Mungu, nilikuwa chombo cha Mungu. Kwa hiyo nawaalika ninyi, mitume wangu, kuwa kalisi ya upendo mnyofu na safi wa Mwanangu. Nawalika kuwa chombo ambacho kwa njia yake wote wasiojua upendo wa Mungu, wasiopenda kamwe, wataelewa, wataupokea na wakaokolewa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2016
“
W
anangu wapendwa! Leo pia nawaalika kurudi katika sala. Katika wakati huu wa neema, Mungu amenijalia kuwaongoza kuelekea utakatifu na maisha ya unyofu, ili katika mambo madogo muweze kumtambua Mungu Mwumbaji, kumpenda na ili maisha
yenu
yawe shukrani kwa Mungu Mkuu kwa yote aliyowajalia. Wanangu, maisha
yenu
yawe zawadi kwa wengine katika upendo naye Mungu atawabariki. Nanyi, mumshuhudie bila kutafuata faida, kwa ajili ya upendo kwa Mungu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombea ninyi nyote mbele ya Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Moyo wangu wa kimama unalia machozi ninapoyaona yale wanayoyafanya wanangu. Dhambi zinaongezeka, usafi wa moyo unaendelea kupoteza umuhimu wake. Mwanangu amesahauliwa na upendo kwake unaendelea kupunguka na wanangu wanateswa. Kwa hiyo, wanangu, mitume wa moyo wangu, iteni jina la Mwanangu kwa nafsi na kwa moyo: Yeye atakuwa na maneno ya mwanga kwenu. Naye atajionyesha kwenu, anashiriki Mkate pamoja nanyi na anawapa maneno ya upendo, ili myageuze kuwa matendo ya huruma na muwe hivyo mashahidi ya ukweli. Kwa hiyo, wanangu, msiogope! Acheni Mwanangu awe ndani
yenu
. Yeye atawatumia ninyi ili kuzitibu nafsi zinazojeruhiwa na kuziongoka zile zinazopotea. Kwa hiyo, wanangu, rudieni kusali Rozari. Mwisali kwa roho ya ukarimu, ya sadaka na ya huruma. Salini si kwa maneno tu, ila kwa matendo ya huruma. Salini kwa upendo kwa watu wote. Mwanangu amekuza kimaadili upendo kwa njia ya sadaka yake. Kwa hiyo isheni pamoja naye mpate nguvu na matumaini, mpate upendo ulio uhai wa kuongoza kwenye uzima wa milele. Kwa njia ya upendo wa Mungu mimi nami ni pamoja nanyi, na nitawaongoza kwa upendo wa kimama. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2016 - Tokeo la Yakobo Kolo la kila mwaka
Katika tokeo la mwisho wa kila siku la tarehe 12 Septemba 1998 Mama Maria alimwambia Yakobo ya kuwa ataona tokeo lake mara moja kila mwaka, tarehe 25 Desemba, siku ya Kristmasi. Hivyo ikatokea na mwaka huu. Mama Maria ametokea pamoja na Mtoto Yesu mikononi mwake. Tokeo likaanza saa nane adhuhuri na dakika ishirini na kudumu dakika kumi. Yakobo, baadaye, akatoa ujumbe ufuatao:
“
W
anangu wapendwa, Leo katika siku hii ya neema nawaalika hasa kusali kwa ajili ya amani. Wanangu, nimekuja hapa kama Malkia wa Amani na mara nyingi nimewaalika kusali kwa ajili ya amani. Lakini wanangu, mioyo
yenu
imefadhaika. Dhambi inawazuia kufunguliwa kabisa kwa neema na amani ambayo Mungu ataka kuwapeni. Ili kuishi amani, wanangu, yawapasa kuwa kwanza na amani mioyoni mwenu na kujiachia kabisa kwa Mungu na mapenzi Yake. Msitafute amani na furaha katika mambo ya dunia hii maana haya yote hupita. Muelekee rehema ya kweli, amani itokayo kwa Mungu tu na hivyo mioyo wenu hivyo tu itajaa furaha ya kweli; hivyo tu mtaweza kuwa mashahidi wa amani katika dunia hii ya hofu. Mimi ni mama
yenu
na ninawaombea kila mmoja wenu mbele ya Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2016
“
W
anangu wapendwa! Kwa furaha kubwa leo nawaletea Mwanangu Yesu ili Yeye awapeni amani Yake. Wanangu, fungueni mioyo
yenu
na muwe wafurahivu, ili muweze kuipokea. Mbingu ni pamoja nanyi na zinapambana kwa ajili ya amani mioyoni mwenu, katika jamaa na ulimwenguni na ninyi, wanangu, msaidieni kwa sala zenu ili iwe hivyo. Ninawabariki pamoja na Mwanangu Yesu na kuwaomba msikose matumaini, na mtazamo wenu na moyo wenu yaelekee daima mbinguni na uzima wa milele. Hivyo mtafunguliwa kwa Mungu na mipango Yake. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Mwanangu alikuwa chemchemi ya upendo na mwanga alipoongea na watu wa mataifa yote. Mitume wangu, fuateni mwanga wake, si rahisi, yawapasa kuwa wadogo, yawapasa kuwa wadogo kuliko wengine wote na kwa msaada wa imani kujazwa na upendo wake. Hakuna mtu duniani, pasipo imani, awezaye kuwa na uzoefu wa mwujiza. Mimi nipo pamoja nanyi, ninajionyesha kwa matokeo hayo, kwa maneno hayo, nataka kuwashuhudia upendo wangu na utunzaji wangu wa kimama. Wanangu, msipoteze wakati mkiweka maswali ambayo hamtapata kamwe majibu, maisha
yenu
duniani yatakapomalizika Baba wa Mbinguni atawajibu. Mjue daima ya kuwa Mungu hujua yote, Mungu huona, Mungu hupenda. Mwanangu mpenzi sana huangaza maisha na kupasua giza. Upendo wa kimama unaonileta kwenu hauelezeki, umefichwa lakini ni halisi, ninawaonyesheni hisia zangu, upendo, hisani na ukarimu wangu wa kimama. Kutoka kwenu, mitume wangu, ninatafuta sala zenu: mawaridi yaliyo matendo ya upendo, hizo ndizo kwa moyo wangu wa kimama sala za kunipendeza sana, haya ninayaletea Mwanangu aliyezaliwa kwa ajili
yenu
. Yeye anawatazama ninyi na kuwasikia. Sisi tupo kila siku karibu nanyi kwa upendo wenu ambao huita, huunga, huongoa, hutia moyo na kujaza. Kwa hiyo mitume wangu pendaneni daima, lakini hasa mpende Mwanangu, hii ni njia ya pekee ya wokovu kuelekea uzima wa milele, hiyo ni sala ya kunipendeza ambayo kama harufu nzuri ajabu ya mawaridi, hujaa moyo wangu. Ombeni daima, waombeeni wachungaji wenu ili wapate nguvu ya kuwa mwanga wa Mwanangu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Februari 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninyi mnaojaribu kumtolea Mwanangu kila siku ya maisha
yenu
, ninyi mnaojaribu kuishi pamoja naye, ninyi mnaosali na kujitolea, ninyi ni matumaini katika ulimwengu huu wenye udhia. Ninyi ni miali ya mwanga wa Mwanangu, Injili iliyo hai, na ninyi ni mitume wangu wapenzi wa upendo. Mwanangu ni pamoja nanyi. Vili vile, lakini, Yeye anawangojea kwa uvumilivu wale wasiomjua. Kwa hiyo ninyi, mitume wa upendo wangu, salini kwa moyo na onyesheni kwa matendo upendo wa Mwanangu. Kwenu ninyi hiyo ni matumaini ya pekee, na njia ya pekee kuelekea uzima wa milele. Mimi, kama Mama, ni hapa pamoja nanyi. Sala zenu mnazoniomba ni kwangu mawaridi ya upendo mazuri kuliko yote, Siwezi kutokuwapo pale ninapohisi harufu ya mawaridi. Kuna matumaini! Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2017
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalika kuishi kwa kina imani
yenu
na kumwomba Aliye juu ili aiimarishe, hivyo upepo na dhoruba yasije yakaivunja. Mizizi ya imani
yenu
iwe sala na tumaini katika uzima wa milele. Tokea sasa, wanangu, jijengeni wenyewe, katika wakati huu wa neema ambapo Mungu anawapeni neema ili kwa njia ya kujinyima na mwito wa kuongoka muwe watu wenye imani na tumaini safi na ya kuvumilia. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo wa kimama naja kuwasaidieni kuwa na upendo zaidi, maana yake imani zaidi. Naja kuwasaidieni kuishi kwa upendo maneno ya Mwanangu, ili ulimwengu uwe tofauti. Kwa sababu hiyo nawakusanya, mitume wa mapendo yangu, karibu nami. Niangalieni kwa upendo, ongeeni nami kama vile na Mama kuhusu mateso
yenu
, maumivu
yenu
, furaha zenu. Ombeni ili nisali Mwanangu kwa ajili
yenu
. Mwanangu ni mwenye rehema na haki. Moyo wangu wa kimama ungependa ninyi pia muwe hivyo. Moyo wangu wa kimama ungependa ya kuwa ninyi, mitume wa mapendo yangu, mngeongea kwa maisha yetu juu ya Mwanangu na juu yangu pamoja na watu wote walio karibu nanyi, ili ulimwengu uwe tofauti, ili wairudie imani na tumaini. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini kwa moyo. Salini kwa upendo, salini kwa matendo mema. Salini ili wote wamjue Mwanangu, ili ulimwengu ugeuke, ulimwengu uokoke. Ishini kwa upendo maneno ya Mwanangu. Msihukumu, lakini mpendaneni, ili Moyo wangu uweze kushinda. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Machi 2017
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema nawaalika nyote kufungua mioyo
yenu
kwa huruma ya Mungu ili kwa ajili ya sala, toba na maamuzi kwa ajili ya utakatifu muanze maisha mapya. Majira haya ya kuchipua yanawaita, katika mawazo
yenu
na mioyo
yenu
, kuishi maisha mapya, kujifanya upya. Kwa hiyo, wanangu, mimi nipo pamoja nanyi niwasaidie ili mkatakati wa kukata shauri muweze kusema NDIYO kwa Mungu na amri za Mungu. Ninyi si peke
yenu
, mimi nipo pamoja nanyi kwa njia ya neema ambayo Yeye Aliye juu hunijalia kwa ajili
yenu
na kwa uzao wenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Aprili 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, mitume wa upendo wangu, inawapasa ninyi kuujulisha upendo wa Mwanangu kwa wale wote ambao hawakumjua. Inawapasa ninyi, mianga midogo ya ulimwengu, ambao mimi ninaifunza kwa upendo wa kimama ili ing'ae waziwazi kwa mwangaza kamili. Sala itawasaidia, maana sala huwaokoa ninyi, sala huuokoa ulimwengu. Kwa hiyo, wanangu, salini kwa maneno, kwa moyo, kwa upendo wenye huruma na kwa sadaka. Mwanangu aliwaonyesha njia: Yeye aliyejimwilisha na kunifanya kuwa kalisi ya kwanza; Yeye ambaye kwa sadaka yake isiyo na kifani aliwaonyesha kama inavyopaswa kupenda. Kwa hiyo, wanangu, msiogope kusema kweli. Msiogope kujigeuza wenyewe na ulimwengu ili kueneza mapendo, mkitenda kila jinsi kusudi Mwanangu aweze kujulikana na kupendwa kwa kuwapenda wengine kwa ajili yake. Mimi, kama mama, nipo daima pamoja nanyi. Namwomba Mwanangu awasaidie ili katika maisha
yenu
upendo utawale: upendo uishio, upendo uvutao, upendo utoao uzima. Huo ndio upendo ninaowafundisha, upendo safi. Inawapasa ninyi, mitume wangu, kuutambua, kuuishi, kuueneza. Waombeeni wachungaji wenu kwa moyo, ili waweze kumshuhudia Mwanangu kwa upendo. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Mei 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawaalika kusali pasipo kuomba, bali mkitoa sadaka, mkijitolea wenyewe. Nawaalika kuleta habari ya ukweli na upendo wenye rehema. Ninamwomba Mwanangu kwa ajili
yenu
, kwa imani
yenu
, inayoendelea kupunguka katika mioyo
yenu
. Ninamwomba awasaidieni kwa Roho ya Mungu, kama vile mimi nami ninavyotaka kuwasaidieni kwa roho ya kimama. Wanangu, itawabidi kujiboresha! Wale tu walio safi, wanyenyekevu na wamliojaa upendo wanautegemeza ulimwengu, wanaokoa ulimwengu na wao wenyewe. Wanangu, Mwanangu ndiye moyo wa ulimwengu: lazima kumpenda na kumwomba, na si kumsaliti daima tena. Kwa hiyo ninyi, mitume wa upendo wangu, mstawishe imani katika mioyo ya watu kwa mfano wenu, kwa sala
yenu
na kwa upendo wenye rehema. Mimi nipo karibu nanyi na nitawasaidia. Salini ili wachungaji wenu wapate mwanga zaidi kadiri wawezavyo, ili waweze kuangaza wale wote wanaoishi gizani. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Mei 2017
“
W
anangu wapendwa! Yeye Aliye juu ameniruhusu kuwaalikeni tena kwa uongofu. Wanangu, fungueni mioyo
yenu
kwa neema ambayo wote mnaalikwa. Muwe mashahidi wa amani na wa upendo katika ulimwengu huu wa wasiwasi. Maisha
yenu
hapa duniani ni ya mpito. Salini ili kwa njia ya sala muweze kutamani mbingu na mambo ya mbinguni na mioyo
yenu
itaona yote kwa njia tofauti. Ninyi si peke
yenu
, Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombeeni kwa Mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
Next>>