Our Lady of Medjugorje Messages containing 'yenu'
Total found:
171
Ujumbe, 25 Desemba 2022
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaletea Mwanangu Yesu ili muwe amani yake na kielelezo cha utulivu na furaha ya Mbinguni. Salini, wanangu, ili muwe wazi kukaribisha amani, kwa sababu mioyo mingi imefungwa kupokea wito ya nuru ibadiliyo mioyo. Niko pamoja nanyi na ninawaombea mjifungue kumkaribisha Mfalme wa Amani anayeijaza mioyo
yenu
joto na baraka. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2023
“
W
anangu wapendwa! Ombeni pamoja nami kwa ajili ya amani maana shetani anataka vita na chuki katika mioyo na mataifa. Kwa hiyo salini na, katika siku zenu, toeni sadaka kwa kufunga na kutubu ili Mungu awape amani. Wakati ujao uko kwenye njia panda kwa sababu mwanadamu wa kisasa hataki Mungu. Kwa hiyo ubinadamu unaelekea kwenye upotevu. Ninyi, wanangu, ni tumaini langu. Ombeni pamoja nami kwamba niliyoyaanza Fatima na hapa yatimie. Ombeni na mshuhudie amani katika mazingira
yenu
na muwe watu wa amani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 18 Machi 2023 - Tokeo la kila mwaka kwa Miriana Dragićević-Soldo
Mwotaji Mirjana Dragićević-Soldo alikuwa na matukio ya kila siku kutoka Juni 24, 1981 hadi Desemba 25, 1982. Katika hafla ya kutokezwa kwake kwa kila siku, akimfunulia siri ya kumi, Bikira alimfunulia kwamba atakuwa na tukio la kila mwaka mnamo Machi 18 na ndivyo ilivyokuwa katika miaka hii yote. Tukio hilo lilianza saa 1.33 jioni na kudumu hadi saa 1.39.
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika mpate kumjua Mwanangu vizuri iwezekanavyo kwa sala na rehema. Ili kwa mioyo safi na iliyo wazi mjifunze kusikiliza. Sikilizeni Mwanangu anachowaambieni ili mpate kuona tena kiroho. Kama watu wamoja wa Mungu, kwa ushirika na Mwanangu, ishuhudieni kweli kwa maisha
yenu
. Ombeni, wanangu, ili kwamba pamoja na Mwanangu muweze kuleta amani, furaha na upendo kwa ndugu zenu wote. Mimi ni pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka zangu za kimama.
”
Ujumbe, 25 Machi 2023
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu uwe wakati wa sala kwa ajili
yenu
.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika ninyi nyote kuwa waletaji wa amani na furaha ya Yesu Mfufuka kwa wale wote walio mbali na maombi ili kwa njia ya maisha
yenu
, upendo wa Yesu uwabadilishe na kuwa katika maisha mapya, maisha ya wongofu na utakatifu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2023
“
W
anangu wapendwa! Aliye Juu ameniruhusu niwe miongoni mwenu, niwaombee, niwe Mama
yenu
na kimbilio lenu. Ninawaalika wanangu, mrudieni Mungu na kwenye maombi na Mungu atawabariki kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika ninyi kwenye maombi kwa moyo. Mioyo
yenu
, wanangu, igeuzwe kuelekea mbinguni kwa maombi, ili mioyo
yenu
ipate kuhisi Mungu wa upendo anayewaponya na kuwapenda kwa upendo mkuu. Mimi niko pamoja nanyi kuwaongoza kwenye njia ya uongofu wa moyo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika kwenye maombi ya nguvu. Umamboleo unataka kuingia katika mawazo
yenu
na kuwaibia furaha ya maombi na kukutana na Yesu. Kwa hiyo, wanangu wapendwa, fanyeni upya sala katika familia zenu ili moyo wangu wa kimama ufurahi kama siku za kwanza nilipowachagua ninyi na jibu lilikuwa ni maombi mchana na usiku na mbingu haikunyamaza bali ilitolea kwa mahali hapa neema, amani na baraka kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu ili aijaze mioyo
yenu
amani kwa sababu Yeye ni amani. Wanangu, mtafuteni Yesu katika ukimya wa mioyo
yenu
ili azaliwe upya. Ulimwengu unamhitaji Yesu, hivyo wanangu, mtafuteni kwa maombi maana anajitoa kila siku kwa kila mmoja wenu.
”
Mama yetu alikuja leo akiwa amevalia mavazi ya heshima akiwa na mtoto Yesu mikononi mwake. Yesu alinyoosha mkono wake kama ishara ya baraka na Mama yetu alituombea kwa lugha ya aramaika.
Karibuni Ujumbe, 18 Machi 2024 - Tokeo la kila mwaka kwa Miriana Dragićević-Soldo
Mwotaji Mirjana Dragićević-Soldo alikuwa na matukio ya kila siku kutoka Juni 24, 1981 hadi Desemba 25, 1982. Katika hafla ya kutokezwa kwake kwa kila siku, akimfunulia siri ya kumi, Bikira alimfunulia kwamba atakuwa na tukio la kila mwaka mnamo Machi 18 na ndivyo ilivyokuwa katika miaka hii yote. Tukio hilo lilianza saa 1.33 jioni na kudumu hadi saa 1.39.
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika mpate kumjua Mwanangu vizuri iwezekanavyo kwa sala na rehema. Ili kwa mioyo safi na iliyo wazi mjifunze kusikiliza. Sikilizeni Mwanangu anachowaambieni ili mpate kuona tena kiroho. Kama watu wamoja wa Mungu, kwa ushirika na Mwanangu, ishuhudieni kweli kwa maisha
yenu
. Ombeni, wanangu, ili kwamba pamoja na Mwanangu muweze kuleta amani, furaha na upendo kwa ndugu zenu wote. Mimi ni pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka zangu za kimama.
”
Ujumbe, 25 Machi 2024
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema, ombeni pamoja nami ili mema yapate kushinda ndani
yenu
na karibu nanyi. Hasa, wanangu, ombeni kwa umoja na Yesu katika njia yake ya msalaba. Wekeni katika maombi
yenu
ubinadamu huu unaotangatanga bila Mungu na bila upendo wake. Muwe maombi, muwe mwanga na mashahidi kwa wale wote mnaokutana nao, enyi wanangu, ili Mungu wa rehema awarehemu.. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9