Our Lady of Medjugorje Messages containing 'yesu'
Total found:
53
Ujumbe, 25 Juni 2020
“
W
anangu wapendwa, ninasikiliza maombi yenu na sala zenu na ninawaombea kwa mwanangu
Yesu
aliye njia, kweli na uzima. Wanangu, rudieni kusali na fungueni mioyo yenu katika wakati huu wa neema na shikeni njia ya wongofu. Maisha yenu yanapita na hayana maana bila Mungu. Kwa hiyo mimi ni pamoja nanyi niwaongoze kuelekea utakatifu wa maisha ili kila mmoja wenu agundue furaha ya kuishi. Wanangu, ninawapenda wote na kuwabariki kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2020
“
W
anangu wapendwa, Katika wakati huu wa wasiwasi ambapo ibilisi anavuna nafsi ili kuwavuta kwake, niwaalika kwa sala ya kudumu ili katika sala mtambue Mungu wa upendo na wa matumaini. Wanangu, shikeni msalaba katika mikono yenu. Na uwatie moyo kwa kuwa upendo unashinda sikuzote hasa sasa ambapo msalaba na imani yamekataliwa. Ninyi muwe mwangwi na mfano kwa njia ya maisha yenu ya kuwa imani na matumaini bado hai na ulimwengu mpya wa amani unawezekana. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombea mbele ya mwanangu
Yesu
. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2020
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati wa neema. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaalika tena, wanangu, mrudieni Mungu na kwa kusali ili sala iwe furaha kwenu. Enyi wanangu hamtakuwa na wakati ujao wala amani mpaka katika maisha yenu mtakapoanza kuishi maongezi ya binafsi na badiliko katika mema. Maovu yatakoma na amani itatawala katika mioyo yenu na katika ulimwengu. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombea kwa mwanangu
Yesu
kwa ajili ya kila mmoja wenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Huu ni wakati wa upendo, wa uchangamfu, wa sala na wa furaha. Salini, wanangu, ili Mtoto
Yesu
azaliwe katika mioyo yenu. Fungueni mioyo yenu kwa
Yesu
anayejitoa kwa kila mmoja wenu. Mungu amenialika ili mimi niwe furaha na matumaini katika wakati huu nami ninawaambia: bila Mtoto
Yesu
hamna wala huruma wala hisia ya Mbingu, zinazofichika katika yule Mtoto mchanga. Kwa hiyo, wanangu, fanyeni kazi juu ya nafsi zenu wenyewe. Mkisoma Maandiko Matakatifu, mtagundua kuzaliwa kwa
Yesu
na furaha kama ile ya siku za kwanza ya matokeo ya Medjugorje iliyotolea kwa ubinadamu. Historia itakuwa ukweli, ambao hata leo unajirudia ndani yenu na kuwazunguka. Fanyeni kazi na jengeni amani kwa njia ya sakramenti ya Kitubio. Jipatanisheni na Mungu, wanangu, na mtaona miujiza inawazunguka. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2020
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mtoto
Yesu
anayewaletea amani, Yule aliye wakati uliopita, wakati wa sasa na wakati ujao wa kuishi kwenu. Wanangu, msiruhusu imani yenu na matumaini yenu katika wakati ujao ulio bora yazimike, kwa maana ninyi mmechaguliwa kwa kuwa mashahidi wa matumaini katika kila hali. Kwa ajili hiyo mimi ni hapa pamoja na
Yesu
ili awabariki kwa amani yake. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2021
“
W
anangu wapendwa! Kwa furaha ninawaalika ninyi nyote, wanangu, mlioitikia wito wangu, kuwa furaha na amani. Kwa maisha yenu shuhudieni Mbingu ninayowaletea. Ni saa, wanangu, ya kuwa wonyesho wa upendo wangu kwa wote wale ambao hawapendi na mioyo yao imeshindwa na machukio. Msisahau: mimi ni pamoja nanyi na ninawaombea ninyi nyote karibu na mwanangu
Yesu
ili awapeni amani yake. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2021
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu
Yesu
awapeni amani yake. Wanangu, bila amani hamna wala wakati ujao, wala baraka, kwa hiyo rudieni kusali kwa sababu tunda la sala ni furaha na imani, na bila hiyo hamwezi kuishi. Baraka ya leo tunayowapa, ileteni kwa jamaa zenu na tajirisheni wote wale mnaokuta ili wahisi neema ambayo mnapokea. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2022
“
W
anangu wapendwa! Mungu ananiruhusu niwe pamoja nanyi na kuwaongoza kwenye njia ya amani ili kupitia amani ya kibinafsi, muweze kujenga amani duniani. Nipo pamoja nanyi na ninawaombea kwa Mwanangu
Yesu
ili awape imani thabiti na tumaini ya maisha bora ya baadaye ninayotaka kujenga pamoja nanyi. Ninyi, jipeni moyo na msiogope maana Mungu yu pamoja nanyi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2022
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaletea Mwanangu
Yesu
ili muwe amani yake na kielelezo cha utulivu na furaha ya Mbinguni. Salini, wanangu, ili muwe wazi kukaribisha amani, kwa sababu mioyo mingi imefungwa kupokea wito ya nuru ibadiliyo mioyo. Niko pamoja nanyi na ninawaombea mjifungue kumkaribisha Mfalme wa Amani anayeijaza mioyo yenu joto na baraka. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika ninyi nyote kuwa waletaji wa amani na furaha ya
Yesu
Mfufuka kwa wale wote walio mbali na maombi ili kwa njia ya maisha yenu, upendo wa
Yesu
uwabadilishe na kuwa katika maisha mapya, maisha ya wongofu na utakatifu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaalika kwenye maombi ya nguvu. Umamboleo unataka kuingia katika mawazo yenu na kuwaibia furaha ya maombi na kukutana na
Yesu
. Kwa hiyo, wanangu wapendwa, fanyeni upya sala katika familia zenu ili moyo wangu wa kimama ufurahi kama siku za kwanza nilipowachagua ninyi na jibu lilikuwa ni maombi mchana na usiku na mbingu haikunyamaza bali ilitolea kwa mahali hapa neema, amani na baraka kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2023
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu ili aijaze mioyo yenu amani kwa sababu Yeye ni amani. Wanangu, mtafuteni
Yesu
katika ukimya wa mioyo yenu ili azaliwe upya. Ulimwengu unamhitaji
Yesu
, hivyo wanangu, mtafuteni kwa maombi maana anajitoa kila siku kwa kila mmoja wenu.
”
Mama yetu alikuja leo akiwa amevalia mavazi ya heshima akiwa na mtoto
Yesu
mikononi mwake.
Yesu
alinyoosha mkono wake kama ishara ya baraka na Mama yetu alituombea kwa lugha ya aramaika.
Ujumbe, 25 Machi 2024
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema, ombeni pamoja nami ili mema yapate kushinda ndani yenu na karibu nanyi. Hasa, wanangu, ombeni kwa umoja na
Yesu
katika njia yake ya msalaba. Wekeni katika maombi yenu ubinadamu huu unaotangatanga bila Mungu na bila upendo wake. Muwe maombi, muwe mwanga na mashahidi kwa wale wote mnaokutana nao, enyi wanangu, ili Mungu wa rehema awarehemu.. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3