Our Lady of Medjugorje Messages containing 'zenu'
Total found:
56
Ujumbe, 25 Aprili 2013
“
W
anangu wapendwa! Salini, salini, mwendelee kusali ili mioyo yenu ifungukie kupokea imani jinsi ua linavyofunguka kuelekea mianga ya joto la jua. Huo ni wakati wa neema ambao Mungu anawajalia kwa njia ya uwepo wangu, lakini ninyi mpo mbali na moyo wangu. Kwa hiyo nawaalikeni kwa uongofu binafsi na kwenye sala katika familia
zenu
. Maandiko matakatifu yawe daima kichocheo chenu. Nawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni kuwa na nguvu na imara katika imani na katika sala, ili sala
zenu
ziwe zenye nguvu za kuweza hata kufungua moyo wa Mwanangu mpendwa Yesu. Salini enyi wanangu wadogo, bila kukoma, ili moyo wenu ujifungue kwa upendo wa Mungu. Mimi nipo pamoja nanyi, nawaombea ninyi nyote nikasali kwa ajili ya uwongofu wenu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Juni 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, katika wakati huu wa wasiwasi nawaalikeni tena kutembea nyuma ya Mwanangu, na kumfuata. Nayajua maumivu, mateso na taabu
zenu
, lakini katika Mwanangu mtapumzika, ndani yake mtapata amani na wokovu. Wanangu, msisahau ya kuwa Mwanangu amewakomboa ninyi kwa msalaba wake akawajalieni kuwa tena wana wa Mungu na kuwafundisha kumwita tena "Baba" yenu, Mungu aliye mbinguni. Ili muwe wapenzi wa Mungu Baba, basi muwe na mapendo na msamaha, kwa kuwa Baba yenu ni upendo na msamaha. Salini na fungeni, kwa maana hii ndiyo njia ya kujua na kumfahamu Baba aliye mbinguni. Mtakapomjua huyo Baba, mtafahamu ya kuwa Yeye tu ni muhimu kwenu (Maria Mtakatifu amenena hayo kwa nguvu na amkazo sana). Mimi, nikiwa Mama, nataka wanangu wawe watu wenye umoja ambamo Neno la Mungu husikilizwa na kutekelezwa. Kwa hiyo, enyi wanangu, mfuateni Mwanangu, muwe kitu kimoja naye, muwe wana wa Mungu. Pendeni wachungaji wenu kama vile Mwanangu alivyowapenda alipowaita kuwatumikia ninyi. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 2 Novemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa moyo wa kimama nawaalikeni tena kupenda, kusali bila kukata tamaa kwa zawadi ya upendo, kumpenda Baba wa Mbinguni zaidi ya yote. Mtakapompenda Yeye, mtajipenda wenyewe na jirani
zenu
. Mambo hayo hayawezi kutengana. Baba wa Mbinguni yumo katika kila mtu, hupenda kila mtu na kumwita kila mtu kwa jina lake. Kwa hiyo, wanangu, kwa njia ya kusali sikilizeni atakalo Baba wa Mbinguni. Ongeeni na Yeye. Muwe na uhusiano wa binafsi pamoja na Baba, atakayeufanya mkubwa zaidi uhusiano wake nanyi, jumuhiya ya wanangu, mitume wangu. Kama Mama napenda kwamba, kwa njia ya upendo kumwelekea Baba wa Mbinguni, inukeni juu ya ubatili wa malimwengu na muwasaidie wengine kujua na kumjongea polepole Baba wa Mbinguni. Wanangu, salini, salini, salini kwa zawadi ya upendo, kwa sababu upendo ndiye Mwanangu. Muwaombee wachungaji wenu, ili wawapende ninyi siku zote, kama vile Mwanangu alivyowapenda ninyi na kuonyesha akitoa maisha yake kwa wokovu wenu. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Januari 2014
“
W
anangu wapendwa! Salini, salini, salini ili mionzi ya sala yenu iwaguse watu wote mnaokutana nao. Wekeni Biblia Takatifu mahali pa kuonekana katika familia
zenu
, mkaisome ili maneno ya amani yatiririke ndani ya mioyo yenu. Nasali pamoja nanyi na kwa ajili yenu, wanangu, ili siku hata siku mzidi kuyapokea mapenzi ya Mungu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Machi 2014
“
W
anangu wapendwa! Nawaalikeni tena: anzeni kupambana na dhambi kama vile katika siku za mwanzo, nendeni kuungama dhambi
zenu
na kateni shauri ya kuwa watakatifu. Kwa njia yenu upendo wa Mungu utaenea ulimwenguni na amani itatawala mioyoni mwenu na baraka ya Mungu itawajaza. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombeeni mbele ya Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2014
“
W
anangu wapendwa! Salini na mfahamu ya kwamba pasipo Mungu ninyi ni mavumbi. Kwa hiyo geuzeni fikira
zenu
na mioyo yenu kwa Mungu na kwa sala. Tegemeeni upendo Wake. Katika Roho ya Mungu ninyi nyote mnaalikwa kuwa mashahidi. Ninyi mna thamani mbele ya Mungu, nami nawaalika, wanangu, kuwa watakatifu, ili mweze kupata uzima wa milele. Kwa hiyo mfahamu ya kwamba maisha haya hupita. Nawapendeni na kuwaalika kwa maisha mapya ya kutubu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2014
“
W
anangu wapendwa! Yeye Aliye Juu ananipa neema ya kuweza kuwa tena pamoja nanyi na kuwaongoza katika sala kuelekea njia ya amani. Mioyo yenu na roho
zenu
zina kiu ya amani na upendo, ya Mungu na ya furaha yake. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini na katika sala mtapata hekima ya kuishi. Nawabarikieni na kukuombeeni mbele ya Mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2014
“
W
anangu wapendwa! Ninyi hamjui neema ya namna gani mnayoishi katika wakati huu ambapo Yeye Aliye Juu awapeni ishara ili mjifungue na kutubu. Mwelekeeni Mungu na kusali; sala itawale katika mioyo yenu, familia na jamaa
zenu
ili Roho Mtakatifu awaongoze na kuhimiza kila siku mjifungue kufanya mapenzi ya Mungu na mpango wake kwa kila mmoja wenu. Mimi nipo pamoja nanyi, na nawaombeeni pamoja na malaika na watakatifu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, mimi, Mama yenu, naja tena katikati yenu kwa upendo usio na mwisho, kutoka upendo usio na kipimo wa Baba wa Mbinguni asiye na mwisho. Na, nikitazama mioyoni mwenu, naona ya kuwa wengi wenu wanipokea kama Mama na, kwa moyo thabiti na safi, wataka kuwa mitume wangu. Lakini Mimi ni Mama pia wa ninyi ambao hamnipokei na, katika ugumu wa moyo wenu, hamtaki kujua upendo wa Mwanangu. Hamjui jinsi moyo wangu ulivyoteseka na jinsi nilivyowaombeeni Mwanangu. Namwomba aponye roho yenu, kwa maana najua Yeye ana uwezo wa kuwaponya. Namwomba awaangaze kwa mwujiza wa mwanga wa Roho Mtakatifu, ili mwache kumsaliti, kumtukana na kumwumiza siku zote kwa kuendelea. Nasali kwa Moyo wote ili muweze kuelewa ya kuwa Mwanangu tu ni wokovu na mwanga wa ulimwengu. Nanyi, wanangu, mitume wangu wapenzi, mbebeni daima Mwanangu katika moyo na fikira
zenu
. Hivyo ninyi mtakuwa mnabeba Upendo. Wale wote wasiomjua watamtambua katika upendo wenu. Mimi nipo sikuzote karibu yenu. Nipo hasa karibu na wachungaji wenu, kwa sababu Mwanangu aliwaita kuwaongozeni katika njia kuelekea milele. Nawashukuru, mitume wangu, kwa sadaka na upendo wenu!
”
Ujumbe, 2 Novemba 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, mimi nipo pamoja nanyi kwa baraka ya Mwanangu, pamoja nanyi mnaonipenda na mnaotafuta kunifuata. Mimi natamani kuwa pia pamoja nanyi ambao hamtaki kunipokea. Kwenu nyote nafungua moyo wangu wote wa mapendo na kuwabariki kwa mikono yangu ya kimama. Mimi ni Mama ninayewaelewa: nilikuwa nimeishi maisha yenu na kujaribu mateso na furaha yenu. Ninyi mnaoishi katika mateso, mnafahamu maumivu yangu na mateso yangu kwa ajili ya wale wanangu wasiokubali kuangazwa na mwanga wa Mwanangu, kwa wale wanangu wanaoishi gizani. Kwa hiyo nawahitaji ninyi, ninyi mlioangazwa na mwanga na kuufahamu ukweli. Nawaalika kumwabudu Mwanangu, ili moyo wenu ukue na kuyafikia kweli maisha ya kiroho. Basi mitume wangu, natumaini mtaweza kunisaidia. Kunisaidia maana yake ni kuwaombea wale ambao hawajajua upendo wa Mwanangu. Mkiwaombea, mtamwonyesha Mwanangu ya kuwa mnampenda na kumfuata. Mwanangu aliniahidi kwamba uovu hautashinda kamwe, kwa sababu hapo mpo ninyi, roho za wenye haki: ninyi mnaojaribu kusali sala
zenu
kwa moyo wote; ninyi mnaotolea maumivu na mateso yenu kwa Mwanangu; ninyi mnaofahamu ya kuwa maisha ni kufumba na kufumbua tu; ninyi mnaotamani Ufalme wa mbinguni. Hayo yote huwafanya muwe mitume wangu na kuwaongoza kwenye shangwe ya Moyo wangu. Kwa hiyo wanangu, takaseni mioyo yenu mkamwabudu Mwanangu. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 2 Machi 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninyi ni nguvu yangu. Ninyi, mitume wangu, ambao, kwa upendo wenu, unyenyekevu na sala ya kimya kimya, mnamwezesha Mwanangu ajulikane. Ninyi mnaishi ndani yangu. Ninyi mnanibeba mioyoni mwenu. Ninyi mnajua ya kuwa mna Mama awapendaye na aliyekuja kuwaletea upendo. Nawatazama katika Baba wa Mbinguni, natazama fikira
zenu
, maumivu yenu, mateso yenu na kuyaleta kwa Mwanangu. Msiogope! Msipoteze matumaini, maana Mwanangu humsikiliza Mama yake. Yeye hupenda tangu alipozaliwa, na ndio furaha yangu ya kuwa wanangu wote wajue upendo huo; na wote wale ambao, kwa sababu ya maumivu yao na kutoelewa kwao, walimwacha waweze kurudi kwake, na wote wao wasiomjua wamjue. Kwa sababu hiyo ninyi hapa ni mitume wangu, nami pia pamoja nanyi kama Mama yenu. Salini ili kuwa imara katika imani, maana upendo na rehema hutoka katika imani imara. Kwa njia ya upendo na rehema mtawasaidia wale wote wasiofahamu ya kuwa wanachagua giza badala ya nuru. Salini kwa ajili ya wachungaji wenu, maana wao ni nguvu ya Kanisa ambayo Mwanangu aliwaachieni. Kwa njia ya Mwanangu wao ni wachungaji wa roho. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Mei 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, fungueni mioyo yenu mkajaribu kuhisi jinsi ninavyowapenda na kutaka mpendeni Mwanangu. Nataka mpende zaidi kwa kuwa haiwezekani kumjua pasipo kumpenda, maana Yeye ndiye upendo. Wanangu, mimi nawajueni: najua maumivu yenu na mateso yenu maana niliyaishi. Nafurahi pamoja nanyi kwa furaha
zenu
. Nalia machozi pamoja nanyi katika maumivu yenu. Sitawaacheni kamwe. Nitaongea nanyi daima kwa upole wa kimama na, kama mama, nahitaji mioyo yenu ifumbuliwe, ili kwa hekima na unyofu mueneze upendo wa Mwanangu. Nawahitaji ninyi mfumbuliwe na kuwa wepesi kupokea mema na huruma. Nahitaji muungano wenu na Mwanangu, kwa maana nataka mpate kufanikiwa na kumsaidia kuleta heri kwa wanangu wote. Mitume wangu, nawahitaji, ili muwaonyeshe wote ukweli wa Mungu, ili moyo wangu, ulioteswa na kuteswa hata leo kupita kiasi, uweze kushinda katika upendo. Salini kwa ajili ya utakatifu wa wachungaji wenu, ili katika jina la Mwanangu, waweze kutenda maajabu, maana utakatifu hutenda maajabu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2015
“
W
anangu wapendwa, hata leo ninamwomba Roho Mtakatifu ili ajaze mioyo yenu kwa imani thabiti. Sala na imani zitajaza mioyo yenu kwa upendo na furaha, nanyi mtakuwa ishara kwa wale walio mbali na Mungu. Wanangu, mpeane moyo wenyewe kwa wenyewe ili kufanya sala ya moyo, ili sala iweze kujaza maisha yenu na ninyi, wanangu, kila siku muwe mashahidi wa utumishi: kwa Mungu katika kuabudu na kwa majirani
zenu
katika mahitaji yao. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombea ninyi nyote. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nipo hapa katikati yenu kuwatieni moyo, kuwajaza kwa upendo wangu, kuwaalika tena kuwa mashahidi wa upendo wa Mwanangu. Wanangu wengi hawana tumaini, hawana amani, hawana upendo. Wao wanatafuta Mwanangu lakini hawajui jinsi wala wapi ya kumpata. Mwanangu awafungulia mikono Yake, nanyi wasaidieni ili waje mikononi Mwake. Wanangu, kwa hiyo ni lazima msali kwa upendo, lazima msali sana, sana, ili kupata upendo zaidi na zaidi, kwa maana upendo hushinda mauti na hudumisha maisha. Watume wa upendo wangu, wanangu wenye moyo mnyofu na safi, jiungeni zaidi na zaidi katika kusali. Mnatengana sana! Jipeni moyo katika kukua kiroho, kama vile Mimi ninawapeni moyo. Ninawaangalia na nipo karibu nanyi kila mnaponifikiria. Waombeeni wachungaji wenu, wale walioacha yote kwa ajili ya Mwanangu. Wapendeni na waombeeni, Baba wa Mbinguni husikiliza sala
zenu
. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kulingana na mapenzi ya Mwanangu na upendo wangu wa kimama naja kwenu, wanangu, hasa kwa wale ambao hawajajua bado upendo wa Mwanangu. Ninakuja kwenu mnaonifikiria, mnaoomba msaada wangu. Ninawapa upendo wangu wa kimama na kuwaletea baraka ya Mwanangu. Mnayo mioyo safi na wazi? Mnaona dalili za uwepo wangu na upendo wangu? Wanangu, katika maisha yenu ya dunia igieni moyo na mfano wangu. Maisha yangu yalikuwa maumivu, ukimya, imani na matumaini pasipo mipaka katika Baba wa Mbinguni. Hakuna kitu cha bahati: si maumivu, si furaha, si mateso, si upendo. Hizo zote ni neema ambazo Mwanangu anawapeni na zinazowaongoza kwenye uzima wa milele. Mwanangu anawaomba mapendo na sala ndani yake. Kupenda na kusali ndani yake maana yake — kama Mama nataka kuwafundisha — ni kusali katika ukimya wa nafsi
zenu
, si kusema kwa midomo tu. Ni tendo dogo zuri litendwalo kwa jina la Mwanangu; ni uvumilivu, rehema, upokeaji wa maumivu na kujitolea kwa ajili ya wengine. Wanangu, Mwanangu huwatazama. Ombeni ili ninyi pia muuone uso wake, na ili uso huo uweze kufunuliwa kwenu. Wanangu, mimi nawafunulia ukweli halisi wa pekee. Salini kwa kuyaelewa na kuweza kueneza mapendo na matumaini, kwa kuweza kuwa mitume wa upendo wangu. Moyo wangu wa kimama hupenda hasa wachungaji. Iombeeni mikono yao iliyobarikiwa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Novemba 2016 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kuja na kujifunua kwangu kwenu ni furaha kubwa ya Moyo wangu wa kimama. Ni zawadi ya Mwanangu kwa ajili yenu na ya wale watakaokuja. Kama Mama nawaalika: mpendeni Mwanangu kuliko yote! Ili kumpenda kwa moyo wote, yawapaswa kumjua: Mtamjua kwa kusali: Salini kwa moyo na hisia
zenu
. Kusali maana yake ni kutafakari upendo wake na kujitolea kwake. Kusali maana yake ni kupenda, kutoa, kuteseka na kutolea sadaka. Nawaalika ninyi, wanangu, kuwa mitume ya sala na upendo. Wanangu, ni wakati wa kukesha. Katika kesha hii nawaalika kusali, kupenda na kutumaini. Maadamu Mwanangu ataangalia mioyo yenu, Moyo wangu wa kimama unatamani kwamba Yeye aone ndani ya mioyo yenu tumaini timilifu na upendo. Upendo wa mitume wangu wote pamoja utaishi, utashinda na utafunua maovu. Wanangu, mimi nilikuwa kalisi ya Mtu - Mungu, nilikuwa chombo cha Mungu. Kwa hiyo nawaalika ninyi, mitume wangu, kuwa kalisi ya upendo mnyofu na safi wa Mwanangu. Nawalika kuwa chombo ambacho kwa njia yake wote wasiojua upendo wa Mungu, wasiopenda kamwe, wataelewa, wataupokea na wakaokolewa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2016
“
W
anangu wapendwa! Kwa furaha kubwa leo nawaletea Mwanangu Yesu ili Yeye awapeni amani Yake. Wanangu, fungueni mioyo yenu na muwe wafurahivu, ili muweze kuipokea. Mbingu ni pamoja nanyi na zinapambana kwa ajili ya amani mioyoni mwenu, katika jamaa na ulimwenguni na ninyi, wanangu, msaidieni kwa sala
zenu
ili iwe hivyo. Ninawabariki pamoja na Mwanangu Yesu na kuwaomba msikose matumaini, na mtazamo wenu na moyo wenu yaelekee daima mbinguni na uzima wa milele. Hivyo mtafunguliwa kwa Mungu na mipango Yake. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Mwanangu alikuwa chemchemi ya upendo na mwanga alipoongea na watu wa mataifa yote. Mitume wangu, fuateni mwanga wake, si rahisi, yawapasa kuwa wadogo, yawapasa kuwa wadogo kuliko wengine wote na kwa msaada wa imani kujazwa na upendo wake. Hakuna mtu duniani, pasipo imani, awezaye kuwa na uzoefu wa mwujiza. Mimi nipo pamoja nanyi, ninajionyesha kwa matokeo hayo, kwa maneno hayo, nataka kuwashuhudia upendo wangu na utunzaji wangu wa kimama. Wanangu, msipoteze wakati mkiweka maswali ambayo hamtapata kamwe majibu, maisha yenu duniani yatakapomalizika Baba wa Mbinguni atawajibu. Mjue daima ya kuwa Mungu hujua yote, Mungu huona, Mungu hupenda. Mwanangu mpenzi sana huangaza maisha na kupasua giza. Upendo wa kimama unaonileta kwenu hauelezeki, umefichwa lakini ni halisi, ninawaonyesheni hisia zangu, upendo, hisani na ukarimu wangu wa kimama. Kutoka kwenu, mitume wangu, ninatafuta sala
zenu
: mawaridi yaliyo matendo ya upendo, hizo ndizo kwa moyo wangu wa kimama sala za kunipendeza sana, haya ninayaletea Mwanangu aliyezaliwa kwa ajili yenu. Yeye anawatazama ninyi na kuwasikia. Sisi tupo kila siku karibu nanyi kwa upendo wenu ambao huita, huunga, huongoa, hutia moyo na kujaza. Kwa hiyo mitume wangu pendaneni daima, lakini hasa mpende Mwanangu, hii ni njia ya pekee ya wokovu kuelekea uzima wa milele, hiyo ni sala ya kunipendeza ambayo kama harufu nzuri ajabu ya mawaridi, hujaa moyo wangu. Ombeni daima, waombeeni wachungaji wenu ili wapate nguvu ya kuwa mwanga wa Mwanangu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Februari 2017 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninyi mnaojaribu kumtolea Mwanangu kila siku ya maisha yenu, ninyi mnaojaribu kuishi pamoja naye, ninyi mnaosali na kujitolea, ninyi ni matumaini katika ulimwengu huu wenye udhia. Ninyi ni miali ya mwanga wa Mwanangu, Injili iliyo hai, na ninyi ni mitume wangu wapenzi wa upendo. Mwanangu ni pamoja nanyi. Vili vile, lakini, Yeye anawangojea kwa uvumilivu wale wasiomjua. Kwa hiyo ninyi, mitume wa upendo wangu, salini kwa moyo na onyesheni kwa matendo upendo wa Mwanangu. Kwenu ninyi hiyo ni matumaini ya pekee, na njia ya pekee kuelekea uzima wa milele. Mimi, kama Mama, ni hapa pamoja nanyi. Sala
zenu
mnazoniomba ni kwangu mawaridi ya upendo mazuri kuliko yote, Siwezi kutokuwapo pale ninapohisi harufu ya mawaridi. Kuna matumaini! Nawashukuru.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
1
2
3
Next>>