Search this website | ||||
Our Lady of Medjugorje Messages containing 'kuangazwa'“Wanangu wapendwa, mimi nipo pamoja nanyi kwa baraka ya Mwanangu, pamoja nanyi mnaonipenda na mnaotafuta kunifuata. Mimi natamani kuwa pia pamoja nanyi ambao hamtaki kunipokea. Kwenu nyote nafungua moyo wangu wote wa mapendo na kuwabariki kwa mikono yangu ya kimama. Mimi ni Mama ninayewaelewa: nilikuwa nimeishi maisha yenu na kujaribu mateso na furaha yenu. Ninyi mnaoishi katika mateso, mnafahamu maumivu yangu na mateso yangu kwa ajili ya wale wanangu wasiokubali kuangazwa na mwanga wa Mwanangu, kwa wale wanangu wanaoishi gizani. Kwa hiyo nawahitaji ninyi, ninyi mlioangazwa na mwanga na kuufahamu ukweli. Nawaalika kumwabudu Mwanangu, ili moyo wenu ukue na kuyafikia kweli maisha ya kiroho. Basi mitume wangu, natumaini mtaweza kunisaidia. Kunisaidia maana yake ni kuwaombea wale ambao hawajajua upendo wa Mwanangu. Mkiwaombea, mtamwonyesha Mwanangu ya kuwa mnampenda na kumfuata. Mwanangu aliniahidi kwamba uovu hautashinda kamwe, kwa sababu hapo mpo ninyi, roho za wenye haki: ninyi mnaojaribu kusali sala zenu kwa moyo wote; ninyi mnaotolea maumivu na mateso yenu kwa Mwanangu; ninyi mnaofahamu ya kuwa maisha ni kufumba na kufumbua tu; ninyi mnaotamani Ufalme wa mbinguni. Hayo yote huwafanya muwe mitume wangu na kuwaongoza kwenye shangwe ya Moyo wangu. Kwa hiyo wanangu, takaseni mioyo yenu mkamwabudu Mwanangu. Nawashukuru! ” To compare Medjugorje messages with another language versions choose | | |||
Our Lady of Medjugorje Messages Find messages Enter words or phrase Random Messages “I am with you and I guide you into a new time, a time which God gives you as grace so that you may get to know him more.” ( From message, 25 Januari 1993 ) | Medjugorje Live Current time in Medjugorje (CET): Deep concern & disturbing information: Latest news & articles 15 Aprili 2017 24 Septemba 2016 5 Aprili 2016 2 Oktoba 2015 Latest videos 11 Juni 2018 10 Mei 2018 13 Aprili 2018 31 Machi 2018 16 Machi 2018 Most read articles Most watched videos Most watched Medjugorje Photos Gallery albums Favorite content related to Medjugorje" | |||
Our Lady of Medjugorje Messages Medjugorje Videos Medjugorje News & Articles Medjugorje Web Sites Links Picture & Photo Galleries The Polls | Copyright © 2005-2024 Medjugorje WebSite medjugorje.ws medjugorie.ws medugorje.ws ourlady.eu and content contributors | |||